Wednesday, April 18, 2012

AJIFUNGUA MTOTO KWA SIRI CHUMBANI NA KUMWACHA AFE...

Mama mmoja ambaye alijifungua mtoto kwa siri kufuatia kuwa na mahusiano ya kimapenzi, amemwacha mwanae huyo afe kabla ya kufukia mwili wake ardhini.
Fatima Ali wa eneo la Bury, Greater Manchester alihofia kuleta aibu katika familia yake ya Kiislamu kwa kuzaa kabla ya ndoa.
Baada ya kuzaa kwa siri peke yake kitandani, alimkata kitovu mtoto huyo na kumwachia afe.
Ijumaa iliyopita katika Mahakama Kuu ya Bolton, Fatima alibubujikwa machozi wakati alipohukumiwa kifungo cha wiki 26 jela, kutengwa kwa miaka miwili na mwaka mmoja kuishi chini ya uangalizi maalumu.
Alitoa hukumu hiyo, Jaji John Appleby alisema, "Umeshindwa kuomba msaada wa kitabibu baada ya kujifungua binti yako.
"Kitendo hicho cha kinyama kimepelekea maangamizi ya mtoto. Alikufa masaa mawili tu baada ya kuzaliwa, na umehusika kikamilifu, maisha yake yangeweza kuokolewa.
"Hakuna ushahidi kwamba hukumpatia huduma ama kumdhuru mtoto na itabaki kuwa siri, japo inabaki kuwa uzembe wako baada ya kujifungua ndio chanzo cha kifo."
"Janga hili na maamuzi uliyochukua yataandamana nawe katika maisha yako yote."
Mapema, Mahakama iliambiwa kuwa Fatima alikuwa akiishi na mjomba na shangazi yake.
Familia yake ilipinga mahusiano yake na Kazi Mohammed Dilwar Hussein, na alipopata ujauzito mpenzi wake huyo alimpatia fedha kwa ajili ya kutolea mimba hiyo mjini Birmingham mwaka 2009.
Nazi Afzal, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama Kuu ya Greater Manchester alisema: "Vyovyote ambavyo jamii au familia kufedheheka au kupata aibu, uhakika au hisia, kwamba Fatima alifikiri hatokuwa na hatia kuondoa maisha ya mtoto asiye na hatia awe wa kiume au kike.
"Maisha ni tunu ya ajabu na si kitu cha kupotezwa kirahisi tu kwenye bustani ya jirani."
Amkitetea, Wakili Lisa Roberts alisema mteja wake alichukua uamuzi mbaya na hakika alipata mshituko mkubwa wa kimwili na kisaikolojia kwa kipindi fulani baada ya kujifungua.
Wakili huyo aliendelea, akiwa amelelewa na shangazi yake, hakika alikuwa na familia mbili ambazo angezivunjia heshima kwa kuzaa kabla ya ndoa kulingana na utamaduni wao.
Wakili Lisa amenukuu: "Alitoka kwa matembezi na familia yake jioni ya siku hiyo. Kipi kingine angefanya? Aliwataarifu kuhusu mimba yake watu wake wa karibu.
"Alichelewa kidogo kuwaambia kwamba kajifungua mtoto kitandani kwake, na kusema kuwa hawezi kutoka nje."
Wakili huyo aliongeza kuwa ilikuwa vigumu kujua mazingira aliyopitia Fatima.
"Anajua vizuri alichofanya na sababu za kufanya hivyo."
Wakili alisema Fatima alikuja kujigundua ni mpumbavu kujihusisha na mwanaume aliyemuahidi kumuoa na kumsaidia, lakini badala yake kakimbia.
"Katika simu yake zimekutwa meseji za majibizano kati yake na mpenzi wake ambaye alikuwa nje ya nchi ambapo mojawapo ilikuwa imeambatana na picha ya mtoto wake.

No comments: