Thursday, March 29, 2012

MKONGWE WA MIELEKA WWE KUKATWA MGUU WA PILI...

Imefahamika hivi punde kuwa Mwanamieleka mkongwe wa WWE, Kamala anakabiliwa na hatari ya kukatwa mguu wake wa pili kutokana na maradhi ya sukari na shinikizo la damu yanayomkabili.
Mwanamieleka huyo alikatwa mguu wa kushoto mwaka jana kutokana na matatizo hayo, lakini kwa bahati mbaya tatizo hilo halijaisha na limeendelea kuwa kubwa.
Mtoto wa mwanamieleka huyo, Kamala Junior ameeleza kwenye kipindi cha runinga cha "The Roman Show" leo kuwa: "Baba yangu anasumbuliwa na mguu wake wa kulia kwa sasa…kesho Ijumaa ndio tutajua kama utalazimika nao kukatwa."
Kwa wakati huu, mtoto wa mwanamieleka huyo amesema Kamala anaendelea kuperuzi ukurasa wake wa Facebook…na hakika anashukuru kwa meseji mbalimbali za kumtakia afya njema kutoka kwa mashabiki wake.

No comments: