MAPACHA WAISHI TANGU 1934 BILA KUTENGANA!!


Paul (kushoto) na Peter enzi za utoto wao.
Paul na Peter Walipokuwa Jeshi la Kujenga Taifa.
Paul na Peter walivyo hivi sasa.
Mapacha Peter na Paul Kingston wamesisimua wengi duniani baada ya kuweza kuishi pamoja bila kutengana tangu walipozaliwa Juni  23, 1934. 

"Tulizaliwa tukipishana masaa mawili kila mmoja," anasimulia Paul. "Baba alipofika hospitali nesi alimwambia, "Umepata mtoto wa kiume. Nenda na urudi baada ya masaa kadhaa."

"Aliporejea, nesi akamwambia tena, "Umepata mtoto wa kiume," ndipo baba akamjibu, "Ulishaniambia." Nesi akamwambia, "Huyu sasa ni mwingine."

Tangu hapo, Peter na Paul wamekuwa wakiambatana kila kona huku wakichangia vyumba vya madarasa, kambi za jeshi, likizo na hata kazi. Haikushangaza hata pale miaka 40 iliyopita walipoamua kuhama kutoka London kwenda West Sussex ambako walichangia nyumba.

Peter na mkewe Kari wao wanaishi ghorofa ya chini kwenye nyumba yao iliyoko East Wittering karibu na Chichester wakati Paul na mkewe, Mavis wao wanaishi ghorofa ya juu. Mapacha hawa wanachangia majadiliano kiasi kwamba Peter akianza sentensi, Paul anamalizia.

Wakiwa na umri wa miaka 18, walijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria huku wakati mwingine wakitumia bahati ya kufanana kwao kuwachanganya maofisa na hata wachumba zao.

Peter anasimulia, ""Kuna wakati nilitakiwa kwenda sinema na mchumba wangu, lakini sikuwa nikijisikia kutoka. Nilimwambia Paul aende badala yangu, na mchumba wangu hakuweza kugundua tofauti."

Baada ya kumaliza Jeshi, mapacha hao walikwenda mapumzikoni  Raymond Electric huko Hanger Lane pamoja na wazazi wao, Henry na Ivy.

Bahati ilioje!!

No comments: