PICHA NDOGO JUU: Elton John (kushoto) na Whitney Houston. CHINI: Elton John na David Furnish wakiwa na mtoto wao, Zachary. KULIA: Elton John akiwa amembeba mwanae Zachary.
Elton John ameweka bayana kuwa ametumia sana dawa za kulevya na kwamba ni kama muujiza tu kuepuka kifo tofauti na ilivyotokea kwa Whitney Houston.Mwanamuziki huyo mwenye miaka 65 amekiri kuwa kama asingepambana na dawa hizo na kufikia kuacha mwaka 1990, basi angekuwa ameshakufa kitambo huku tetesi zikizagaa kuwa hivi karibuni wanatarajia kupata mtoto mwingine na mumewe David Furnish."Ningekuwa nimekufa," amekiri hivyo. "Sikutaka kabisa kuacha kama ilivyokuwa kwa Whitney Houston na pengine ningeishia kufa kama yeye.""Ni miujiza sikuendelea kwani nina hakika kwamba nilitumia dawa hizo kwa kiasi kikubwa mno kushinda Whitney alivyotumia."Kukiri huko kwa Elton kumekuja wiki sita tu baada ya Whitney kukutwa amekufa bafuni chumbani kwake kwenye Hoteli ya Beverly Hills akiwa na umri wa miaka 48.Wiki iliyopita, ripoti mpya ya dawa za kulevya ilionesha kuwa Whitney alikuwa na chembechembe za dawa hizo mwilini mwake wakati wa kifo chake.Msemaji wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Los Angeles alieleza kuwa vipimo vimeonyesha kuwa Whitney alikuwa 'mtumiaji sugu' wa dawa za kulevya.Elton, ambaye ameolewa na David Furnish mwaka 2005, siku zote amekuwa wazi katika vita dhidi ya dawa za kulevya na pombe.Tetesi zilianza kusambaa kwenye mtandao kwamba wapenzi hao wanatarajia kupata mtoto wa pili. Tayari wana mtoto wa mwaka mmoja Zachary, lakini taarifa hizi mpya bado hazijathibitishwa.Mwimbaji huyo mkongwe aliwahi kusema kuwa alikuwa amepotea katika maisha yake ya nyuma na kubainisha kuwa kubadilika na kuwa msafi mwaka 1990 yalikuwa ni 'mafanikio makubwa' kabisa maishani mwake.Jana katika mahojiano, alisema kuwa maisha yake yasingekuwa hivi kama asingepambana na matumizi ya dawa hizo."Nisingekuwa hivi nilivyo leo. Nisingempata na Zachary, nisingekuwa na David, nisingekuwa na chochote," anasema Elton.Akielezea kuhusu mtoto wake mwenye mwaka mmoja, ambaye alizaliwa na mwanamke asiye na uwezo Siku ya Krismasi mwaka 2010, Elton anasema: "Ilikuwa ni furaha kubwa ambayo haina mfano.""Nafikiri nimepata uzoefu mkubwa wa kupendwa tangu nilipokuwa na David kwa miaka 18, na ni upendo usiyo wa kawaida, lakini David pia ataelezea kitu hiki hiki, hakuna upendo mpaka utakapopata mtoto."Elton amesema amekuwa akishirikiana bega kwa bega na mama wa ubatizo wa Zachary, Lady Gaga, katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya."Watu wengi sana wamekufa. Vijana wengi sana wamejiua kwa sababu wamekuwa wakitumia, unajua, janga hili limewakumba wenye umri wa miaka 15 au 16," alisema."Inaelekea kukoma na inaweza kukomeshwa. Lakini tunaweza kukomesha kwa kuwaeleza watu athari zake na kuwaadhibu."

No comments:
Post a Comment