Sunday, March 18, 2012

CHEKA TARATIBU...

Katika ziara yake nchini Zimbabwe, Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa njiani kutoka Uwanja wa Ndege muda wote macho yake yalikuwa nje akishangaa ufupi wa maghorofa ya nchini humo. Mwishowe uzalendo ukamshinda na kumuuliza mwenyeji wake, “Hivi hakuna majengo marefu zaidi ya haya niliyoyaona?” Rais Mugabe akageuka na kumtazama tu. Baada ya kumaliza ziara, miezi michache baadaye Rais Putin akamualika Mugabe kutembelea Urusi. Siku ikafika safari ikaanza na ndege ikatua salama mjini Moscow. Mara baada ya kuingia kwenye gari maalumu kuelekea hotelini, kazi ya kwanza kwa Mugabe ilikuwa kutazama majengo. Kila aliloliona lilikuwa refu mno kuanzia ghorofa mia na kuendelea, akabaki kimyaa. Baada ya kitambo kidogo hatimaye akaona ghorofa fupi na kupiga kelele, “Enhe Putin ulijifanya kushangaa maghorofa mafupi Harare kumbe hata huku yapo, tazama lile pale.” Bila kuchelewa Putin akamjibu, “Lile ni jingo la Ubalozi wa Zimbabwe.” Duh, Mugabe akabaki mdomo wazi.

No comments: