Richard Remes akikatiza mitaa kabla ya kuachwa. Picha ndogo kushoto ni Patricia alivyokuwa kabla ya shambulio na kulia ni alivyo sasa baada ya shambulio.
Mwanamke mmoja ambaye sura yake imeharibiwa vibaya kwa kumwagiwa tindikali na mpenzi wake ambaye ni mume wa mtu, jana ametinga mahakamani ambako amemshitaki mpenzi wake huyo wa zamani kwa kumbadili sura kuwa kama 'mdudu'.
Akizungumza katika siku yake ya kwanza ya kusikilizwa kesi dhidi ya Richard Remes ya kujaribu kuua nchini Ubelgiji, mwanamke huyo Patricia Lefranc amesema "nataka anitazame machoni na kutathmini madhara aliyonisababishia kwa kitendo chake hicho".
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 48 ambaye amefanyiwa upasuaji mara 86 kufuatia dhahma hiyo, amesema, "Naamini nitaishawishi mahakama kuona kwamba alidhamiria kuniua."
Remes mwenye miaka 57 inasemekana aliamua kushambulia kwa tindikali baada ya Patricia kuvunja mahusiano yao miaka miwili tu iliyopita.
Patricia akisimulia kwa huzuni mkasa huo anasema, "Desemba 1, 2009 ni siku ambayo Remes "hatimaye aliangamiza maisha yangu."
Aliendelea kusimulia kwamba mkasa huo ulimkumba wakati akishuka kwenye lifti akitokea kitongoji cha Molenbeek-Saint-Jean, Ubelgiji ambapo alikuta Remes akimsubiria kufanya alichokusudia.
"Alinifukizia tindikali ambayo ilifahamika kama 'oil of vitriol' ambayo hutumika zaidi kwenye viwanda vya kemikali, kichwa kizima hadi kifuani," Patricia aliiambia mahakama.
Anasema aliamini kwamba atakufa tu, lakini majirani zangu walisikia kelele na kufanikiwa kumuwahisha kitengo cha kuhudumia majeraha ya moto kwenye hospitali ya karibu ambako ambako alilazwa kwa miezi mitatu akiwa mahututi.
Patricia anasema, "Naamini Remes atatiwa hatiani, hakutaka kunidhuru tu bali alitaka kunipoteza kabisa kwenye sura ya dunia. Nataka kuielezea mahakama hali ninayopitia na machungu yake."
"Nitamtafuta mkewe pia. Kwa sasa ananiona kama msaliti niliyempora mume. Nafikiri haya ni matusi kwangu na ni kama mzimu unaonitafuna."
Aliendelea kusema, "Tuiachie mahakama, lakini wakati tukisubiri uamuzi wa mahakama tusisahamu machungu ya milele aliyonisababishia kimwili na hata kimaumbile."
Patricia ameendelea kusimulia kwamba hata marafiki wa mwanaye wamekuwa wakihoji sura yake ya sasa na kuongeza, "Remes ameharibu kabisa maisha yangu kama mwanamke."
"Nimekuwa kituko mitaani. Mbaya zaidi nimekuwa kielelezo cha kinachoweza kumpata mwanamke ambaye anataka kusitisha mahusiano ya kimapenzi," anasema Patricia.
Binti mmoja mwenye miaka 22 ameeleza kuwa amekuwa akitishiwa na rafiki yake wa kiume akisema" "Unakumbuka kilichompata Patricia Lefranc?", anasimulia Patricia.
Mbali ya athari za kisaikolojia, Patricia amekuwa akipata maumizu ya mara kwa mara kutoka kwenye majeraha yake ambayo yanakumbushia shambulio hilo la kutisha lililompata.
Anasimulia, "Nikijitazama kwenye kioo, kila mshipa wa fahamu mwilini unasisimka na kukumbuka shambulio lile."
"Nimepofuka jicho langu la kushoto na kwenye sikio. Wakati nikifanyiwa upasuaji kwa mara ya nane, niliacha kuhesabu. Lakini nilitambua kwamba nitapasuliwa zaidi ya mara ishirini."
Anaendelea, "Tindikali aliyonimwagia ni hatari zaidi kuliko silaha za kivita, bado inaendelea kunishambulia mwilini."
"Pua yangu inaning'inia na siku si nyingi itabidi kubadilishwa. Huo utakuwa upasuaji wa mwisho na nadhani utakuwa mgumu kuliko yote," anasema Patricia.
Anasema, "Kwa miezi mitatu nitalazimika kuvaa sura ya bandia kuficha matundu usoni mwangu."
"Sura hii bandia inabidi kuivua kila siku kwa ajili ya kuisafisha. Hapana, siwezi kuisafisha, nesi amekuwa akinisaidia."
Remes ameomba rashi kwa shambulio hilo huku akikanusha kutaka kumuangamiza. Utetezi wake ni kwamba hakujua tindikali aliyofukiza kama ingekuwa na madhara kiasi hicho.
Baba huyo aliieleza mahakama jinsi alivyoanza mahusiano na Patricia ambaye alikuwa mtunza jengo wa ghorofa analoishi, mwaka 2009.
Aliendelea, "Tulihamia kwenye ghorofa hilo lililopo Mtaa wa Sippelberg mimi na familia yangu mwaka 2006. Patricia tayari alikuwa akiishi hapo. Alikuwa mtunza jengo. Mwanzoni tulisalimiana tu, iliishia hapo."
"Baadaye mahusiano yake na mchumba wake za zamani yakafa. Na, mwaka 2008 akanitaka kumsaidia baadhi ya kazi ndani mwake ambazo hakuweza kufanya mwenyewe," aliendelea Remes.
Alieleza, "Siku moja mwanzoni mwa mwaka 2009 nilimtaka twende naye kupata kahawa. Tukaenda naye hoteli na hapo mahusiano yetu ndipo yakaanza."
Kesi hiyo inaendelea na panapo majaliwa tutawaletea muendelezo na hatma yake hapa hapa ziro99blog.

2 comments:
Huwezi kuamini, machoni kama watu lakini mioyoni ni wanyama kabisa. Mungu atusamehe kwa kweli!
HILI BALAA JAMANI!
Post a Comment