Thursday, February 16, 2012

WHITNEY HOUSTON ALIJIUA?

Mwili wa Whitney ukitolewa kwenye chumba cha hoteli alimokutwa amekufa mjini Los Angeles, Jumamosi iliyopita.
Whitney na binti yake, Bobbi Kristina.

Whitney Houston aliwaambia rafiki zake "wakati wangu umefika" na kusema "namwona Yesu" masaa machache kabla ya kifo chake, limeandika gazeti la The Sun.

Mwanamuziki huyo aliendelea kuzungumza mambo ya kiroho huku akinukuu mistari ya Biblia huku akisisitiza mwisho wake u-karibu.

Ijumaa ya wiki iliyopita, siku moja kabla ya kukutwa amekufa bafuni kwenye Hoteli mjini Los Angeles, alimweleza mmoja wa rafiki zake, "Nitamwona Yesu. Nataka kumwona Yesu."

Na siku ya Jumamosi muda mfupi kabla ya kufikwa na umauti aliripotiwa kusema: "Unajua, ni mkarimu mno. Hakika nataka kumwona Yesu."

Taarifa hizo zinaashiria kwamba Whitney pengine alijua nini kitakachomtokea kesho yake.

Lakini Whitney ambaye alikuwa akikabiliana na ulevi na utumiaji wa dawa za kulevya, alidai kwenye moja na mahojiano yake ya mwisho kwamba ameridhika na maisha yake.

Gwiji huyo wa miondoko ya soul mwenye umri wa miaka 48 alidai kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya na kwamba sasa anaelekeza nguvu zake katika malezi ya bintiye, Bobbi Kristina mwenye miaka 18.

Akizungumza wakati we maandalizi ya filamu yake mpya ya Sparkle, Whitney alifafanua: "Sasa mimi ni mtu mzima, na ninafikiria mbali. Uzoefu wangu wa maisha unaongezeka. Hii inashabihiana na maisha yangu ya kila siku kama mama.

Sitazami filamu hii mpya kama kurejea kwenye fani. Nadhani hii ni zawadi niliyopewa na Mungu. Sio kama vile nilivyowahi kusema, "Oh, nataka kuburudisha'. Hii inaanzia kwenye historia ya familia, siwezi kukwepa. Ni asilia".

Whitney alijipambanua kama mama madhubuti, mwenye wajibu wa kuhakikisha kwamba Bobbi Kristina hafanyi makosa aliyoyafanya yeye siku za nyuma.

Alifafanua: "Ni mama mwenye msaada na mwenye nidhamu".

"Nina vipaumbele. Kuhakikisha binti yangu ni chaguo la kwanza".

"Binti yangu ana damu ya uigizaji, anahudhuria darasa la kuimba na kuigiza".

"Namfanya awe bize na hakika anafuraha sana na hali hiyo".

"Ana miaka 18 na siku si nyingi atakuwa mwanamke. Mungu ashukuriwe". - THE SUN

No comments: