Friday, February 17, 2012

BOBBY BROWN AALIKWA MAZISHI YA WHITNEY

IMERIPOTIWA kwamba familia ya Whitney Houston hatimaye imeamua kumualika Bobby Brown kuhudhuria mazishi ya mkewe, Whitney kesho (leo) Jumamosi.

Vyanzo vya habari kutoka familia ya Houston vimeeleza kwamba, "Katika dakika za mwisho, familia imeona kwamba uamuzi huo (kumwalika Bobby) utaleta amani kwenye mazishi hayo, japo baadhi ya wanafamilia wanapingana na uamuzi huo".

Kama ilivyoripotiwa awali, wanafamilia kadhaa wa Houston walipinga vikali kumualika Bobby kwenye mazishi kutokana na kumtuhumu kuwa chanzo cha sababu za kuporomoka kwa Whitney.

Vyanzo vya habari vilivyo karibu na Bobby vilieleza kwamba marafiki wa familia walimwonya Bobby kutokanyaga kwenye mazishi hayo, lakini sasa baada ya kulegeza msimamo wao, ni wazi Bobby atahudhuria mazishi.

Bobby amekubali kutumbuiza kwenye tamasha litakalofanyika kwenye Casino ya Indian iliyoko Connecticut saa chache baada ya mazishi. Imeelezwa pia Bobby ana mpango wa kuondoka mara tu baada ya mazishi kwa ndege yake binafsi ili kuwahi tamasha hilo.

Imetafsiriwa kutoka mtandaoni

No comments: