Monday, July 28, 2014

MFUKO WA RAIS WAELEZA SABABU ZA MIKOPO KUTOTOLEWA

Mfuko wa Rais (PTF) Kanda ya Morogoro umeshindwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali pamoja na Vyama vya Kuweka na Kukopa  (Saccos) kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na baadhi  kushindwa kurejesha mikopo.
Mikopo hiyo iliyotolewa mwaka  2009/2010 hali iliyosababisha kuwanyima fursa wajasiriamali pamoja na Saccos zilizorejesha kushindwa kupata fedha hizo.
Meneja wa PTF Kanda ya Morogoro, Christopher Peter alisema hata hivyo juhudi zimefanyika kuhakikisha madeni yanalipwa.
Kutokana na juhudi hizo,  hivi sasa Saccos moja pekee ndiyo inadaiwa kutokana na kushindwa kurudisha hata nusu ya deni.
Meneja huyo alitaja Saccos hiyo kuwa ni Ushirikiano inayodaiwa Sh milioni  22.1 walizozichukua katika kipindi cha mwaka 2009/2010.
Peter alisema  fedha hizo ni za wananchi na anashangaa kuona taasisi husika zikishindwa kurejesha fedha hizo ambazo kila mwananchi mwenye uhitaji aliyeidhinishwa na Mfuko anapaswa kukopa na kurejesha kwa wakati.
Hata hivyo alisema mpango wa kuendelea kutoa mikopo kwa Saccos uko palepale. Alisisitiza kabla ya kutoa mikopo hiyo, watazichambua na kuzifanyia usaili.
Kwa mujibu wa Peter, Sh milioni 424.9 zilikopeshwa kwa Saccos katika kipindi hicho cha mwaka 2009/2010.

SHULE KUTIMUA WATUMIA VIPODOZI NA WAVAA MLEGEZO

Shule ya Sekondari Mwadui iliyopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, imetangaza kufukuza wanafunzi wote wanaotumia vipodozi, wanaovaa sketi fupi, milegezo na wanaotumia simu za mkononi shuleni.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Yohana Nzelu, alisema hayo jana katika kikao cha Bodi ya Shule na Wazazi.
Mwalimu Nzelu alisema moja ya chachu ya mafanikio ya wanafunzi shuleni, ni nidhamu ya kutosha na maadili mema na kuongeza kuwa Bodi hiyo ilikaa na kujadili namna ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wake na kuweka mikakati, ikiwemo hatua hizo.
Akisoma taarifa kwa wazazi na walezi wa wanafunzi walio katika shule hiyo, Mwalimu Nzelu alisema hatua hizo zinalenga kuzuia wanafunzi kujiingiza katika makundi mabaya na kuboresha taaluma.
‘’Shule hii katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012, wanafunzi 61 waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu na mwanafunzi mmoja alichaguliwa kwenda kidato cha tano.”
‘’Mwaka jana (2013) wanafunzi 76 walifanya mtihani wa kidato cha nne, waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu 33, waliochaguliwa na Serikali kujiunga kidato cha tano wanafunzi 24, na waliokwenda shule binafsi walikuwa saba.
 “Tumepiga hatua hivyo mikakati iliyopo ni kusisitiza maadili na kuondoa changamoto zilizokuwepo za wanafunzi kukosa nidhamu,“ alieleza Mwalimu Nzelu.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Askofu Mkuu wa KKKT  Dayosisi hiyo, Emmanuel Makala, ambaye ndiye msimamizi wa shule hiyo, alisema suala hilo si la kupuuzwa na hawatakuwa na msamaha kwa mwanafuzi atakayekiuka sheria hizo huku akitoa mwito kwa wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja.
Askofu Makala alisema wazazi na walezi wakishirikiana ipasavyo na walimu kwa kufuatilia taarifa za watoto wao shuleni, itasaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza taaluma ya wanafunzi na kupata ufaulu mzuri.

MAKANISA YANAYOENDEKEZA VURUGU KUFUTILIWA MBALI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amesema yeye mwenyewe atayafuta makanisa yote yanayoleta vurugu na uvunjifu wa amani kwa kuwa hayatoi taswira ya kile wanachopaswa kufanya na ni aibu kwa Mungu  wanayemtumikia.
Amesema ni aibu kwa viongozi wa makanisa kupigana hadharani wakati wa Ibada na kupishana katika vituo vya Polisi wakishtakiana jambo alilosema linachochea shari na kuharibu nchi.
Amelitaja kanisa mojawapo ambalo lina vurugu kuwa ni Kanisa la Moravian, Jimbo la Misheni Mashariki ambalo kwa zaidi ya miaka miwili sasa sharika zake zimekuwa na vurugu inayohusisha uongozi na ubadhirifu wa mali.
"Serikali haitavumilia vitendo vya vurugu katika makanisa na ikibidi mimi mwenyewe nitayafuta usajili wa hayo makanisa yenye migogoro kuepusha shari," alisema Chikawe jana katika ibada maalumu ya kuombea Taifa amani, utulivu na uzalendo wa kweli.
Hivi karibuni kanisa hilo wilayani Kinondoni, waumini walipigana na sasa kuna kesi kuhusu ugomvi huo katika vyombo vya Sheria.
Maombi hayo yaliandaliwa na Chama cha Kitume cha Karismatiki Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Kituo cha Maombi na Maombezi cha Emaus, kilichopo Ubungo, jijini humo.
Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi akiwakilisha viongozi wa Serikali na kisiasa katika maombi hayo yaliohusisha pia kuombea mchakato wa Katiba, vita dhidi ya rushwa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani, alisema viongozi wa dini wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kuchochea amani ya Taifa, lakini inashangaza baadhi yao wanaongoza kwa kuleta vurugu.
"Kwa bahati mbaya migogoro katika makanisa na madhehebu mbalimbali imekuwa mingi wakati huu na sababu za migogoro hiyo ni pamoja na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na ubadhirifu wa mali za kanisa, mathalani Kanisa la Moravian Tanzania, lipo katika mgogoro mkubwa hivi sasa kiasi cha watu kupigana hadharani.
"Wanapigana wakati wa ibada, tujiulize ni mfano gani tunawaonesha Watanzania wasio na dini, kwa utaratibu huo nani atatamani kuwa Mkristo, natumia fursa hii kuwakumbusha viongozi kuwa mfano wa kuigwa, viongozi ni  lazima  tuwe na hofu ya Mungu na tutumie nafasi zetu kujenga umoja, amani na mshikamano," alisema Chikawe.

WASSIRA AMTAKA LISSU AWAOMBE RADHI MAASKOFU NA MASHEHE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uratibu na Sera), Stephen Wassira ameshauri wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kurejea bungeni na kama maoni yao ni ya wananchi, wasubiri wakati wa kura za maoni.
Aidha, Wasira pia amemtaka msemaji wa Ukawa, Tundu Lissu kuwaomba radhi mashehe na maaskofu ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kwa kudai ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wamekuwa wakihongwa chakula, chai na fedha katika nyumba za viongozi.
Alitoa maoni hayo jana kwenye mdahalo wa Tanzania Tuitakayo uliolenga kuangalia ‘Nani anataka kuwazuia Watanzania kupata Katiba Mpya,” akiwa sambamba na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Profesa Ibrahim Lipumba na Lissu.
Alisema kama Ukawa wanaungwa mkono na wananchi, ni vyema watumie nafasi hiyo kurejea bungeni na kujadili rasimu ndani ya Bunge na baadaye wasubiri wananchi waamue.
 “Kama wanachokiamini Ukawa kuwa wako pamoja na wananchi, kwanini wanakwenda kwa wananchi kabla hawajamaliza kazi. Warejee bungeni tujadiliane na kumaliza kazi halafu wakatushitaki kwa wananchi, tuone Ukawa watapata ngapi…  kwanini tuandikie mate na wino upo?”
Aliongeza: “Kama ni muundo wa serikali mbili au tatu utajulikana bungeni.”
Wasira alisema Ukawa wanatakiwa kujua kuwa sheria inataka Katiba kuandikwa ndani ya Bunge na si sehemu nyingine na kushindwa kufanya hivyo ni kukwamisha mchakato huo ambao umefikia hatua ya tatu.
Alisema watu waliokataa kurudi bungeni ndio wanaowazuia Watanzania kupata Katiba mpya sababu Katiba haiwezi kuandikwa nje ya Bunge.
“Wanaokataa kwenda bungeni ndio wavurugaji, Katiba haiwezi kuandikwa Kibanda Maiti au Ubungo, inaandikwa ndani ya Bunge Maalumu.”
Awali, Lisu alisema kati ya wajumbe 201 walioteuliwa na Rais kama wajumbe wa Bunge, 169 ni wanachama wa CCM wakiwamo mashehe na maaskofu na wamekuwa wakihongwa katika nyumba za mawaziri.
Katika hatua nyingine, Wasira amewataka wanasiasa kuacha kusemea wananchi masuala ya mchakato wa Katiba kwa kuweka mawazo yao na kuwa CCM haipingi mawazo ya wananchi.
“Wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wanadai kuwa tunapinga mawazo ya wananchi kama yaliyowekwa kwenye rasimu ya Katiba, lakini wamekuwa wakiweka mawazo yao kwa kisingizio kuwa ni mawazo ya wananchi.
Naye Profesa Lipumba, alisema rasimu inapaswa kuboreshwa na kujadiliwa kulingana na rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba na kutuhumu CCM kuwa ndio wanaovuruga mchakato kwa kutaka kupitisha mfumo wa serikali mbili.
Kwa upande wa Lissu alidai kuwa machakato wa Katiba umekuwa ukiendeshwa kwa kupendelea wajumbe wengi wa CCM.

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU - JULAI 28

MTANDAO WA TAASISI ZA WAKURUGENZI AFRIKA WAPANUKA

Mtandao wa Taasisi za Wakurugenzi Afrika (ACGN) umezidi kukua kwa kupata wajumbe wapya wawili katika mkutano wake jijini Dar es Salaam.
Wajumbe waliosaini makubaliano na mtandao huo ni Taasisi ya Wakurugenzi kutoka Tunisia na Kituo cha Utawala Bora cha Misri.
Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano wa mtandao huo uliomalizika jijini hivi karibuni.
Kituo cha Utawala Bora wa Mashirika Taasisi ya Wakurugenzi Ethiopia nayo iko katika mchakato wa kujiunga na ilihudhuria mkutano huo kama mtazamaji tu.
Pia mtandao huo ulifikia makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Maadili ya Afrika ya Kusini pamoja na Taasisi ya Kimataifa ya Uhasibu, ACCA.
“Tunazidi kukua lakini bado kazi ni kubwa...tunahitaji wanachama wengine zaidi,” alisema Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania na Makamu Mwenyekiti wa ACGN, Said Kambi.
Mtandao huo kwa sasa  una wanachama ambao ni taasisi kutoka nchi 13 na washirika wengine saba huku Kambi akisema ushirikiano na Taasisi ya Maadili ya Afrika ya Kusini utasaidia kuimarisha maadili katika uendeshaji wa mashirika Afrika wakati ushirika na ACCA utasaidia kutoa mafunzo ya kitaalamu, utafiti na kubadilishana taarifa.
Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Wakurugenzi Kenya, Meshack Jerome alisema utawala bora wa mashirika ni kitu muhimu kwa maendeleo ya nchi za Afrika ya Mashariki.
Alitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuhakikisha zinazingatia uongozi bora wa mashirika ili kufikia maendeleo endelevu.
“Taasisi hii iliyoanza mwaka 2004 imesaidia kwa kiwango kikubwa nchi yetu kupambana na ufisadi na kuimarisha maadili katika nchi yetu,” alisema.
Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Maadili Afrika ya Kusini, Profesa Deon Rossouw alisema utawala bora wa mashirika unahusu kuendesha mashirika kwa mafanikio na kwa uwazi.
Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa ACGN,  Jane Valls alishauri serikali za Afrika  kufikiria kuwa na mwongozo thabiti utakaoweka viwango, na maadili yatakayopaswa kufuatwa na mashirika.
Valls ambaye pia ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Wakurugenzi Mauritius (MIoD) alisema uendeshaji wa mashirika na kampuni ni jambo la muhimu kwa maendeleo endelevu ya nchi yoyote.
Alisema kuwa uendeshaji bora wa mashirika barani Afrika ni muhimu kwa sasa ambapo biashara miongoni mwa mataifa ya Afrika inakuwa  pia na  mitaji ya uwekezaji barani humo inazidi kuongezeka.
Waanzilishi wa mtandao huo walikuwa ni Taasisi za Wakurugenzi kutoka Kenya, Malawi, Mauritius, Morocco, Msumbiji, Afrika ya Kusini na Tanzania. Wengine ni taasisi za Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Mtandao huu unalenga kujenga uwezo wa taasisi wanachama na kuendeleza uendeshaji bora wa mashirika katika sekta binafsi na umma barani Afrika.
 ACGN iliundwa kujenga uwezo wa wanachama wake kuimarisha uendeshaji wa mashirika, na kujenga mashirika bora barani Afrika miongoni mwa mambo mengine.
Mtandao huo pia unatoa fursa kwa watunga sera na wadau wengine kujadiliana kuhusu masuala  mbalimbali yanayohusu changamoto mbalimbali  na uendeshaji wa mashirika na kampuni barani Afrika.

WASIFU USHIRIKIANO WA MZUMBE, CHUO KIKUU AFRIKA KUSINI

Serikali na sekta binafsi nchini zimesifu ushirikiano wa kitaaluma uliozinduliwa kati ya vyuo vikuu vya Mzumbe na Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Stellenbosch cha Afrika ya Kusini.
Taasisi hizo zimeingia makubaliano ya kutoa mafunzo ya Menejimenti kwa maofisa wa Serikali na sekta binafsi nchini na Afrika ya Mashariki kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema ushirikiano huo ni hatua nyingine ya maendeleo kwa taifa.
Naibu Waziri huyo aliyewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Adolph Mkenda alisema Serikali inakaribisha ushirikiano huo ambao alisema unaendana na mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa.
“Watanzania watafaidika na mpango huu ambao masomo yake yatakuwa yanatayarishwa na wataalamu kutoka vyuo hivi viwili,” alisema na kuongeza kuwa Serikali ingependa kuona ushirikiano kama huu zaidi nchini.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni, Dk Elisante Gabriel alisema ushirikiano huo umekuja wakati mwafaka.
“Nawatakia mafanikio na nashauri kampuni hapa nchini kupeleka maofisa wake kusoma programu hizo zitakazokuwa zinatolewa Mzumbe,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye alisifu uhusiano huo na kusema wadau wa sekta wanahitaji mafunzo kama hayo.
Ofisa Mkuu Mtendaji wa Kitengo kinachotoa mafunzo hayo katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Profesa Frik Landman alisema kama sekta binafsi na Serikali wataona umuhimu, uhusiano huo utakuwa chachu ya maendeleo ya Tanzania na Afrika Kusini.
Alisema ni muhimu na ni jambo la thamani kwa taasisi katika nchi zikawa na mameneja wenye ufanisi kuzalisha na kuleta tofauti.
Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Fedha na Utawala, Profesa Faustin Kamuzora alisema uhusiano huo unatokana na mpango mkakati wa chuo hicho unaolenga kushirikiana na taasisi toka sekta za umma na binafsi.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Mafunzo hayo hapa nchini, Profesa Shiv Tripathi awamu ya kwanza ya mafunzo hayo itatolewa jijini katika chuo hicho kwa siku mbili.

PINDA ATAKA WANAOTAKA UONGOZI KWA RUSHWA WATOSWE

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameonya Watanzania kuwa makini na watu wanaotumia rushwa, ili kupata nafasi za uongozi na hasa kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015.
Ametoa onyo hilo jana wakati akizungumza na mamia ya waumini na viongozi mbalimbali waliohudhuria ibada ya uzinduzi wa Dayosisi mpya ya Ruvuma ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kuwekwa wakfu kwa Askofu Amon Mwenda, aliyeteuliwa kuongoza dayosisi hiyo.
“Ninawasihi wananchi wawe makini na viongozi wanaopenda kutoa rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Kama mtu ana nia ya kweli ya kuongoza ni kwa nini atumie fedha ili kupata nafasi ya uongozi?”
“Tatizo ni kwamba hata wananchi hivi sasa wanakubali kupokea kile kinachotolewa na wagombea. Atakuja huyu atakupa hiki na mwingine naye atakupa kile, lakini ujue akiingia madarakani anaanza kurudisha haraka vile alivyowagawia,” alisema.
Aliwaonya wananchi kuwa makini ili wasije wakageuzwa mtaji wa kuwanufaisha watu binafsi. “Tukikubali kutumika ni sawa tutapata viongozi wakati wa uchaguzi, lakini watakuwa ni wale wasio na hofu ya Mungu, wenye kujali maslahi yao kuliko ya wananchi waliowachagua,” aliongeza.
Aliwaomba viongozi wote wa dini waliohudhuria sherehe hizo pamoja na waumini wote waendelee kuliombea Taifa ili Mungu aliepushe na janga hilo la watu kupenda rushwa.
Alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wazidi kuuombea mchakato wa kupata Katiba mpya ili wajumbe wote warejee ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na kuikamilisha kazi waliyoianza.
Alimuomba Askofu huyo mpya apokee jukumu hilo kwa mikono miwili na kumuahidi kuwa kama Serikali watakuwa naye bega kwa bega kuwaongoza Watanzania walioko kwenye dayosisi yake.
Dayosisi hiyo mpya inahusisha Mkoa wote wa Ruvuma na Wilaya ya Ludewa eneo ambalo lina ukubwa wa kilometa za mraba 72,630. Kati ya hizo kilometa za mraba 64,233 ni za Mkoa wa Ruvuma na kilometa za mraba 8,397 ni za Wilaya ya Ludewa.
Akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kusimikwa rasmi,
Askofu Mwenda alisema Dayosisi mpya ya Ruvuma imezaliwa katika kipindi chenye changamoto nyingi za kidunia na utandawazi ukiwemo mmomonyoko mkubwa wa maadili.
Hata hivyo, akiainisha malengo ya dayosisi hiyo ambayo anakuwa Askofu wake wa kwanza, alisema mbali ya kufundisha neno la Mungu, dayosisi hiyo itahimiza ufanyaji kazi ili wakazi wake wawe na akiba ya chakula cha kutosha.
Alisema watashirikiana na Serikali na wadau wa ndani na nje katika kutoa huduma za kijamii hasa elimu na afya. Aidha, alisema atakabiliana na changamoto za sasa ambazo alizitaja kuwa ni mmomonyoko wa maadili, rushwa, mauaji ya albino, unajisi wa watoto na ubakaji wa wanawake.
Akitoa shukrani kwa niaba ya waumini wa kanisa hilo, Askofu Mkuu wa KKKT, Dk Alex Malasusa alisema Kanisa lingependa kupata viongozi ambao ni wacha Mungu.
Akirejea mahubiri yake, Askofu Malasusa alisema inashangaza kuona kuna baadhi ya watu wanagombea nafasi za uongozi lakini hawana mapenzi na Mungu aliyewaumba watu anaotaka kuwaongoza.

KAMPUNI YA NAKUMATT KUNUFAISHA WAFANYABIASHARA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nakumatt Holdings Limited, Atul Shah amewahakikishia Watanzania kunufaika na duka jipya la vyakula na vifaa kwa kupata fursa mbalimbali ikiwamo kununua bidhaa za wafanyabiashara wa hapa nchini.
Shah aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi wa duka hilo lililopo Mlimani City, ambapo alihakikisha kuwa duka hilo halijaja kuwa maadui wa Watanzania kwa kuwanyang'anya fursa zao ikiwemo ajira.
Alisema duka hilo litahakikisha linanunua bidhaa zake kwa wafanyabiashara wa hapa nchini kusaidia kuleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa bidhaa zitakazokuwa na viwango vya kimataifa zitapata fursa za kuuzwa katika maduka yao mengine yaliyopo nchi za Afrika Mashariki.
Alisema walikuwa na ndoto za muda mrefu za kufungua duka hilo jijini hapa na kwa sasa imekamilika, ambapo alisema kuwa mikakati waliyojiwekea ni kuwa na matawi 50 Afrika Mashariki kufikia mwaka 2015.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene ametaka wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo nchini kuhakikisha wanatumia vizuri fursa zilizopo ili kurasimisha biashara zao na kuongeza kipato.
Mbene alisema, wajasiriamali wadogo wana uwezo mkubwa wa kutengeneza bidhaa bora lakini wamekuwa wakiangushwa na utafutaji wa masoko.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka la vyakula na vifaa la Nakumatt,  Mbene alipongeza uamuzi wa duka hilo wa kuhakikisha linanunua bidhaa zake hapa nchini kwa lengo la kuongeza maendeleo.
Alisema tofauti na maduka mengine ambayo asilimia kubwa ni ya nchi za mbali, duka hilo ni kutoka ndani ya Afrika Mashariki hivyo ujio wa duka hilo ni fursa nzuri kwa Watanzania.
Alitaka wajasiriamali kuhakikisha wanatengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa kama walivyofanya katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' waweze kupata soko kubwa na kufanya kutoka katika sekta isiyo rasmi kwenda katika sekta rasmi.

Sunday, July 27, 2014

BOKO HARAM MILITANTS SEIZE CAMEROON VICE PM'S WIFE

Boko Haram militants attacked Kolofata, a town in Cameroon's Far North Region near Nigeria, on Sunday and seized several people including the wife of Cameroon's Vice Prime Minister Amadou Ali, a military commander in the region said.
"The situation is very critical here now, and as I am talking to you the Boko Haram elements are still in Kolofata town in a clash with our soldiers," said Colonel Felix Nji Formekong, the second commander of Cameroon's third inter-army military region (RMIA3) based in the regional headquarters Maroua.
"Some of them have already taken away the wife of Vice Prime Minister Ahmadou Ali and her house help while the bodyguards of the Vice Prime Minister have succeeded in taking him out of the town to Mora," Formekong said, adding that there could be more casualties.

REMY FAILS MEDICAL, LIVERPOOL MOVE OFF

Loic Remy's move from QPR to Liverpool has fallen through after the Frenchman failed a medical.
The striker's transfer has been cancelled following his examination, which he underwent in Boston on Tuesday.
The results took longer than usual to come through as the medical took place away from Merseyside. Neither club has commented officially, and the specific issue is not known.
A possible heart defect was revealed in 2010, when Remy joined Marseille from Nice, but the transfer went through after further tests saw doctors give Remy the all-clear.
Back then, it was decided that Remy was still suitable for a career in professional football. However, it is unknown whether the latest problem is related to his cardiovascular, or another issue.
Liverpool had agreed an £8.5m deal to sign Remy from QPR after he impressed on loan at Newcastle last season, earning himself a place in France's World Cup squad.
Brendan Rodgers must look elsewhere to replace Luis Suarez, who has joined Barcelona, though Rickie Lambert arrived before the World Cup.
Liverpool are reportedly close to signing Belgian striker Divock Origi for £12.5m - they had originally planned to loan him back to Lille for the 2014/15 season but may now wish to press the 19-year-old into immediate service.

ARUSHA'S TEMDO HAS SOLUTION TO DISPOSAL OF HOSPITAL WASTE

Other than death itself, nothing gets more frightening than the sight of dead bodies and especially when they also appear in form of butchered pieces of human anatomies.
But that was exactly what happened in Dar es Salaam last week; horror was the word when freshly dumped human organs were discovered at a local dumpsite in the city. It was as if the gory scenes from the ‘Hostel,’ ‘Saw,’ and ‘Texas Chainsaw Massacre,’ had just come to life.
As usual, urban legend speculations opened the first chapter; the prologue rumours was that ‘Jack the ripper,’ had moved into Dar and was busy slicing up the residents, the second rounds of gossips were deeply etched in supernatural beliefs, somebody must be busy offering human sacrifice to some sadistic gods.
Eventually, however when the truth came out, the parts of dead bodies were linked to a medical facility which as it happens did not have the proper equipment to dispose of remains of human tissues, organs and even chemicals.
The human organs scandal in the end was tightly shrouding the International Medical and Technological University in Dar es Salaam after the latter was discovered to have carelessly disposed of those pieces of dead human beings from their training laboratories.
But the IMTU saga was not to be an isolated incident; following the human-organs saga, more skeletons eventually started coming from other medical facilities’ closets.
“Many dispensaries, hospitals and health centres in the country do not have appropriate facilities to destroy their waste products,” stated Dr Edwin Kuzwa, the in-charge at the SOS Hospital in Ngaramtoni area on the outskirts of Arusha City.
Dr Kuzwa revealed another shocking revelation; “There are some hospitals that of late have been instructing expectant mothers reporting for maternity services at their facilities to bring along large plastic containers; you know what  that is for?” he asked.
The answer was revolting; apparently, immediately after delivering their babies, those women are expected to collect any waste they would produce in the plastic containers for disposal.
“And that is because most health centres for some reason, do not have waste and tissue burning equipment at their facilities,” pointed out the medical expert. That should also explain why dogs love to frequent hospital environments; it is not just for left over foods.
So how does Dr Kuzwa’s hospital deal with the situation? “Very simple, we have a properly constructed incinerator capable of totally destroying human tissues, chemicals and other forms of medical wastes from our treatment centre,” he explained.
But maybe most hospitals find incinerators expensive additions to their already overwhelming costs of medical facilities that need to be frequently upgraded and maintained; besides, others figure that the machines even have to be imported.
“Not exactly, because we have a government-run engineering outfit in Arusha which designs and manufacture these incinerators on tailor made basis, they make the equipment depending with particular needs and size of pocket,” said the medical official.
The state-owned Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organisation (TEMDO), has been around since time in history, producing practically all types of locally designed machinery as well as repairing most of the imported ones.
“Installing incinerators at medical facilities is as important as treatment itself,” explained the Director General of TEMDO, Dr Kalutu Koshuma, adding that if there is a place where dangerous garbage are produced then it should be at hospitals and dispensaries.
“Health centres churn out various types of medical wastes including chemicals that could be dangerous upon contact with people or animals; human tissues and organs that may be infectious to others and discarded surgical tools equally lethal,” pointed out Dr Koshuma.
He warned that, some medical facilities let their waste products enter the main public drainage or solid waste management system, which can spread deadly diseases to the mass. “Hospital wastes must not be let out of the compound,” he insisted.
And that was why TEMDO which is located in Njiro Area, south of the Arusha City, came up with own designs of incinerators, capable of destroying such medical waste products without trace within an hour of intensive heat application inside their closed chambers.
The organisation produces and undertakes the task of fixing such equipment for clients rather cheaply, they claimed. Well at least, more affordable than facing the costs as well as consequences of having your facility closed down as it was the case with IMTU.
TEMDO Engineer, Richard Eliamringi, said their incinerators can handle waste products of more than 50 kilogrammes per single intake and reduce the latter to soft ash within 50 minutes of 1000 degrees centigrade burning, without puffing out destructive fumes or in other words, they are ‘environmentally friendly.’
But should the whole country start sending in requests for the incinerators, can TEMDO handle the demand? “We are capable of producing 50 such equipment per year,” said the engineer, adding that ten local hospitals are already using their incinerators.
And what about those who want to know how they should describe ‘incinerators’ in Kiswahili? “Simple, the singular name is ‘Kiteketezi,’ or ‘Viteketezi’ in plural,” they defined!
Written by MARC  INKWAME  in Arusha.

CHUO KINGINE CHA TIBA MATATANI, CHAPIGWA MARUFUKU

Siku moja baada ya Serikali kuifungia kwa muda usiojulikana Hospitali ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU), kinachohusishwa na utupaji wa viungo vya binadamu mithili ya takataka, Serikali mkoani Rukwa nayo imekifungia chuo kingine cha  Rukwa College of Health and Allied Sciences.
Moja ya sababu ya kukifungia chuo hicho ni kutokuwa na kibali cha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii huku mitaala ya kozi zake ikiwa haipo, kwa maana ya kupitwa na wakati.
Kutokana na kasoro hizo, Serikali ya mkoa kupitia Idara yake ya Afya imezuia wanafunzi wa chuo hicho kufanya mazoezi ya vitendo katika Hospitali ya Mkoa na nyingine mkoani hapa.
Chuo  hicho kinachomilikiwa  na Umoja wa Kuendeleza Wanawake Mkoani Rukwa (RWAA)  ambacho kipo  Kanondo, nje kidogo  ya Mji wa Sumbawanga, kwa sasa wanafunzi  wake wa mwaka  wa mwisho wako katika maandalizi ya mitihani yao  ya  kuhitimu  masomo. Mitihani hiyo inatarajia kuanzia Agosti 25, mwaka  huu.
Mganga Mkuu  wa Mkoa wa Rukwa, Dk John Gurisha  amelithibitishia gazeti hili juu ya uamuzi huo wa serikali ya mkoa kwa kile alichosema chuo hicho kinaendeshwa  kinyemela,  ikiwa ni  kinyume cha utaratibu  kwani hata  mitaala ya kozi  zinazofundishwa haipo katika mfumo wa masomo Tanzania,  hivyo si  rahisi kupata  viwango  vya ubora  wa  wanafunzi.
Akifafanua,  Dk Gurisha  alisema  usajili  wa muda   uliotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NACTE) haukipi chuo hicho  uhalali  wa kutoa  mafunzo ya tiba,  bali  kinatoa  ruhusa ya kufungua  chuo ili kiweze kutoa  kozi  za  tiba.
Alisema baada ya kupata usajili huo, chuo kilitakiwa kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu  Wizara ya Afya  na Ustawi  wa Jamii  na si vinginevyo.
 Aliongeza kuwa   chuo hicho hakifuati  mitaala  ya Wizara ya Afya kwa kuwa  kozi ya  wahudumu wa afya   inayotolewa  chuoni  hapo ilishasitishwa na wizara husika.
“Awali  kabla Wizara  ya Afya na Ustawi  wa Jamii  kusitisha  kozi  ya  wahudumu wa  afya  ilikuwa ikitolewa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa pekee  kwa mantiki hii  kozi  zinazofundishwa  chuoni  hapo ni batili,  pia hakina  baraka za Katibu Mkuu  wa Wizara ya Afya  ambaye  ndiye  pekee  mwenye mamlaka  ya kutoa  vibali vinavyowezesha vyuo  vya afya  kufundisha  kozi mbalimbali.
“Hivyo chuo  hiki  akitambuliwi,  nimezuia pia  wanafunzi  wa chuo hicho kufanya  mazoezi ya vitendo  katika hospitali  hii ya mkoa na zinginezo  zilizopo  mkoani hapa;  sasa  kutokana  na hili  chuo hicho kinawapeleka wanafunzi wake Mpanda  mkoani Katavi  kwa  mafunzo  ya  mazoezi kwa  vitendo …. Niwe wazi wanaosoma katika chuo hicho wanajipotezea muda wao,“ alisema.
Aliongeza kuwa  atahakikisha  chuo  hicho  kinafuata utaratibu   ili kiweze kutambuliwa na kwamba haogopi  licha  ya kauli kali  zinazomshutumu  kuwa  yeye (Dk Gurisha)  anakipiga vita kwa kuwa  si mzawa  wa  mkoa huo.
“Huwezi  kuchezea  maisha na afya za watu kwa  sura ya uzawa …kwanza kama  kweli  kingekuwa  ni halali  ilikuwa ni jambo jema  kwetu kwa kuwa  baadhi ya wahitimu  wake  wangeweza kuajiriwa hospitalini hapa na kwingineko   ili kupunguza  upungufu wa wahudumu  wa afya wenye ujuzi,“ anaeleza.
Naye Katibu  wa Hospitali  ya Mkoa wa Rukwa, Dorice Nzingilwa  anasema  wanafunzi wa chuo hicho  wanasoma  kwa  miezi  mitatu kisha wanapelekwa  kufanya  mazoezi  ya vitendo  na kuanza  kuwatibu wagonjwa,  jambo  ambalo linahatarisha  maisha ya wagonjwa.
Aidha alisema hata walimu wanaofundisha  katika  chuo hicho hawana  sifa  kwa kuwa baadhi yao  ni  matabibu wasaidizi.
Kwa mujibu  wa  barua  ya Agosti 20, 2013  iliyosainiwa na Dk Gurisha kwenda  kwa Katibu Mkuu  Wizara ya Afya  na Ustawi wa Jamii yenye kumbukumbu namba GHS /T 40/15/4,  licha ya kuainisha mapungufu lukuki yanachokikabili  chuo  hicho  pia  kimebainisha kuwa  kinaendeshwa kinyume cha utaratibu  kwa vile hata mitaala  ya kozi  zinazofundishwa  haipo .
“Hivyo  si rahisi kupata  viwango  na ubora wa wanafunzi,“ inaeleza sehemu ya  barua  hiyo.
Pia imebainisha kuwa Kaimu Mkuu  wa Chuo  hicho ni Ofisa  Tabibu mstaafu  na wengine watatu ambao  ni walimu wa kudumu  ni  wauguzi wastaafu  huku mwingine  cheo chake pia makazi  yake halali hayafahamiki. 
Pia kwa mujibu wa barua  hiyo  walimu  wa muda ambao ni watano hawafai kufundisha kwani mmoja wao ni muuguzi mstaafu, wengine tabibu wasaidizi  watatu na daktari mmoja kutoka Hospitali ya Rufaa  ya Mkoa  wa Rukwa.
“Timu ya usimamizi wa huduma  za afya  Mkoa RHMT na ile ya wilaya CHMT  tunapendekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  iwe inafanya ukaguzi wa vyuo  vinavyotaka kuanzishwa  kabla ya Nacte ili wajiridhishe;  na wakati wa  kufanya  ukaguzi  washirikishe timu ya mkoa  na wilaya ili  kuondoa  au kuepuka  migongano isiyo ya lazima  kati ya Wizara  ya Afya na Nacte  wataarifiwe  kwa ajili ya kukamilisha  usajili. Aidha Nacte  wafahamishwe  kwamba  wanapotoa usajili  msimamizi mkuu  na mtoa mitaala  ni Wizara  husika …
“Na ukaguzi wanaoufanya Nacte  uzingatie  vigezo  vilivyopo  kwani hatutegemei  kama Rukwa College  of Health Sciences  wangepewa  namba ya usajili  kwa hali  tuliyoikuta  wakati wa  ziara yetu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.
Akizungumzia hayo, Mwenyekiti  wa Asasi  hiyo ya RWAA  inayomikili chuo hicho, Annastela Malaji  anasititiza kuwa  chuo  hicho  ni halali kwa kuwa  kimepata usajili  wa muda  kutoka Nacte uliotolewa Januari 31,2014  na kitakoma Januari 30,2015 ambapo  kilishaanza kuchukua wanafunzi tangu mwaka  jana.
“Tuko kihalali  isitoshe tuna usajili wa Nacte  kama kweli  tungekuwa hatuna uhalali  mbona Agosti 25 mwaka  huu  wanafunzi  watafanya mitihani yao  ya kuhitimu  tena wataifanyi katika hospitali  ya mkoa kwa  maelekezo ya Wizara  husika …. Lipo jambo  hapa,“  alisema Malaji.
 Katika hatua nyingine, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kimepongeza uamuzi wa Serikali wa kuifungia Hospitali ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU) na kuiomba kufanya ukaguzi kwa hospitali nyingine nchini za serikali na binafsi.
Hayo yamesema na Rais wa MAT, Dk Primus Saidia aliyeongeza kuwa, hatua ya serikali inalinda watu wake na kuhakikisha watoa huduma wanakuwa na sifa stahili, huku wakitoa huduma bora.
Alisema kutokana na taaluma ya afya kuingiliwa na matatizo mbalimbali, ikiwemo kuwepo kwa watoa huduma wasio na sifa huku wengine wakiwa hawana vifa vya kutosha hivyo ukaguzi uendele na hospitali nyingine.
“Tunaipongeza serikali kwa hatua hii ya kumlinda mlaji, lakini tunawasihi isiwe kwa IMTU pekee kwani kuna hospitali za binafsi na za serikali zenye matatizo kama ya IMTU na zinatakiwa kuchukuliwa hatua,“ alisema Dk Saidia.
Alisisitiza kuwa pia inatakiwa kuzingatia hospitali zote zinakuwa na namna ya kutupa na kuteketeza taka za hospitalini kwa ajili ya kulinda afya za wananchi wake kwani uchafu kama damu au mabomba yaliyotumika yana madhara mbalimbali.
Rais huyo wa MAT, aliwataka wananchi wanaopatiwa huduma zisizoridhisha katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya nchini kupeleka malalamiko yao ili hatua ziweze kuchukuliwa, jambo litakalosaidia kuleta mabadiliko kwenye sekta hiyo muhimu.

MAASKOFU WANAWAKE TANZANIA 'BADO KWANZA'

Pamoja na majimbo mawili ya kanisa la Anglikana nchini kuruhusu wachungaji wanawake, uamuzi wa kuwapa au kutowapa Uaskofu wanawake unategemea makubaliano ya mkutano wa Sinodi ya Anglikana nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Kanisa hilo nchini, Dk Dickson Chilongani  wakati alipoulizwa na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu kama lipo tamko lolote kuhusu maamuzi ya Kanisa la Anglikana Uingereza la kutoa daraja la Uaskofu kwa wanawake.
Alisema kanisa la Anglikana nchini linabaki na utamaduni wake hadi hapo Sinodi itakapoketi na kuona kama ipo sababu ya kubadili desturi iliyopo.
Hata hivyo, amesema hakuna kikao cha Sinodi kilichoitishwa kujadili maamuzi ya kanisa la Uingereza na athari yake kwa kanisa la Tanzania. Makao makuu ya kanisa la Anglikana yapo Uingereza.
Katibu huyo alisema maamuzi ya Kanisa la Uingereza hayana uhusiano na kanisa la Tanzania kutokana na ukweli kuwa mfumo wa maamuzi wa kanisa la Anglikana iko tofauti na Wakatoliki, wao upo kwa majimbo husika.
Alisema kwa utaratibu kila jimbo katika kanisa hilo linajitegemea na kwamba uamuzi wa kanisa la Uingereza la kuruhusu kuwapo kwa maaskofu wanawake hakuna uhusiano na msimamo wa kanisa la Tanzania.
Hivi karibuni Baraza Kuu la kanisa la Kianglikana Uingereza, (The General Synod), liliidhinisha wanawake kuwa maaskofu. Uamuzi huo wa kutoa daraja la uaskofu kwa wanawake kunafanya kanisa hilo la Uingereza kuungana na majimbo mengine 20 ambayo yanatoa daraja la uaskofu kwa wanawake.
Majimbo hayo yapo katika nchi za New Zealand, Australia, Marekani, Canada na Afrika Kusini.
“Sinodi ya Tanzania bado hatujadili suala la wanawake kuwa maaskofu mpaka hapo tutakapojadili, msimamo wetu hauwezi kulazimishwa na msimamo wa kanisa la Uingereza,” alisema Dk Chilongani.
Majimbo ya Tanzania ambayo yana wachungaji wa kike ni Dayosisi ya Central Tanganyika Dodoma na Mara.
“Pamoja na majimbo hayo kuwa na wachungaji wa kike, wachungaji hawa hawawezi kuwa maaskofu kwa kuwa maamuzi ya kisinodi hayajafikiwa,” alisema Dk Chilongani.
Hivi karibuni Kasisi Moses Bushendich kutoka kanisa la Kianglikana Uganda akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza ( BBC) alisema kuwa kanisa la Afrika limegawanyika juu ya maaskofu wanawake kutokana na mafundisho ya Biblia.
''Kanisa la Afrika halina uamuzi wa pamoja juu ya suala hili. Kila tawi limechukua msimamo wake baadhi wanapinga na wengine wanaunga mkono,'' amesema Kasisi Bushendich.

MAWAKILI KWENDA MAREKANI KUSOMEA SHERIA ZA MAFUTA, GESI

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wakishirikiana na The Colom Foundation INC na Nashera Hotel wanakusudia kuwapeleka mawakili 20 wa Tanzania katika Chuo Kikuu cha Mississippi nchini Marekani kujifunza zaidi juu ya elimu ya nadharia na vitendo katika sheria, hususan ya gesi na mafuta.
Hayo yalisemwa jana na makamu wa rais wa chama cha wanasheria Tanganyika, Flaviana Charles wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema chama hicho pamoja na majukumu mengine, kina jukumu la kusimamia upatikanaji wa elimu ya sheria hivyo ushirikiano huo wa kuwapatia mawakili mafunzo ni njia mojawapo ya kuboresha, kusimamia na kuwaongezea mawakili ujuzi na uwezo wa kulinda haki na usawa katika jamii.
Alisema mafunzo hayo yatakuwa ni ya miezi mitano yatakayoanza Septemba mosi mwaka huu na kutarajiwa kumalizika Januari mwakani na watasoma masomo matatu ambapo somo mojawapo la lazima kusoma ni somo la mafuta, na gesi na madini.
Rais wa The Colom Foundation INC na Nashera Hotel, Wilbur Colom ambaye ni mwekezaji hapa nchini, alisema  mafunzo hayo hadi kumalizika yatagharimu kiasi cha dola 12,500 (Sh milioni 20.3) kwa kila mwanafunzi, hivyo wao kama wawekezaji watahusika moja kwa moja katika kuleta maendeleo katika nchi waliyowekeza na kuwa wanajiona ni sehemu ya Taifa.

JICHO LA TATU


RAIS KIKWETE AWAPA IDD EL FITRI WAZEE WASIOJIWEZA

Rais Jakaya Kikwete ametoa msaada wa chakula kwa kambi ya wazee wasiojiweza ya Bukumbi, wilayani Misungwi mkoani hapa kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitr.
Msaada huo ulikabidhiwa jana kwa Mwenyekiti wa wazee hao na Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Mwanza, Jalia Mtani.
Alisema mwaka huu kwa niaba ya Rais Kikwete amekabidhi mchele  kilo 240, mbuzi wanne, mafuta ya kupikia lita 40 pamoja na chumvi vyote vikiwa na thamani ya Sh 665,000.
Alisema kituo hicho kina wazee wasiojiweza 114 ambao wengine waliugua ugonjwa wa ukoma na kutunzwa kwenye kambi hiyo.
Akizungumzia mkakati walionao katika kuhakikisha wazee hao wanapata huduma muda wote, Mtani alisema ni pamoja na kuhamasisha watu binafsi, taasisi za umma na NGOs kujitokeza na kuwasaidia.
Naye Mwenyekiti wa wazee hao, Richard Bushasha alimshukuru Rais kwa msaada huo wa chakula na kwamba na wao watafurahia sherehe hiyo pamoja na wenzao.

LEO NI SIKU YA KULIOMBEA TAIFA

Watanzania bila kujali imani zao wameombwa kujitokeza kwa wingi leo katika maombi maalumu ya kuliombea Taifa amani, utulivu na uzalendo wa kweli na kuliepusha na vurugu na matukio ya kigaidi.
Aidha, suala la mchakato wa Katiba mpya litaombewa pia na imeelezwa kuwa, bila amani, uzalendo na amani ya kweli, maridhiano hayataweza kupatikana kwa kuwa kila upande utakuwa unajali maslahi binafsi na si ya Taifa.
Katika maombi hayo yatakayofanyika kwenye Kituo cha Sala na Maombezi cha Emaus kilichopo Ubungo kinachoratibiwa na Chama cha Kitume cha Karismatiki Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Katibu wa Karismatiki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Merdad Banzi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, maombi hayo kwa Taifa ni maalumu kuuombea mchakato wa Katiba mpya, amani na utulivu, Uchaguzi Mkuu ujao na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Banzi alisema kabla ya maombi hayo yatakayofanyika leo mchana katika viwanja vya kituo hicho cha sala kilichopo nyuma ya stendi ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, pia watatembelea vituo vya watoto yatima, magereza ya Ukonga, Keko na Segerea pamoja na vituo vya wazee wasiojiweza.
Alisema pia watatembelea hospitali za Mwananyamala, Temeke, Amana,  Muhimbili na Ocean Road ambako kote huko watatoa misaada mbalimbali kulingana na mahitaji wa walengwa pamoja na kuomba nao kuwatia moyo kwamba Mungu hajawaacha na anawapenda.

POLISI YAAHIDI SIKUKUU TULIVU YA IDDI EL FITRI

Jeshi la Polisi nchini limejipanga kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu ya Idd el Fitr kwa amani na utulivu.
Jeshi hilo limesema kwamba limeweka mikakati thabiti ya kuimarishwa ulinzi katika maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine.
Aidha, inakusudia kuwabana madereva walevi na wazembe watakaokiuka sheria za usalama barabarani.
Hayo yameelezwa na msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso (pichani) katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu mikakati ya jeshi lake katika kipindi hiki cha sikukuu za Idd el Fitr zinazoashiria kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Alisema  katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo, badala ya  kujaza watu kupita kiasi, kwa tama ya fedha .
Aidha aliwataka wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao kwa kuhakikisha hawaachi nyumba wazi ama bila mtu na watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu.
Aliwataka  wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao au kwa namba ya simu 0754 785 557, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.

KAYA MASKINI KUOKOLEWA NA TASAF III

Mpango wa awamu ya tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii nchini (Tasaf), unatarajia kutumia Sh bilioni 408, kwa ajili ya kunusuru kaya masikini milioni 1.2 zinazoishi kwenye hali duni, imeelezwa. 
Asilimia kubwa ya fedha hizo za Tasaf ni mkopo ikiwemo Sh bilioni 330 za Benki ya Dunia, Sh bilioni 45 zimetolewa na Serikali ya Tanzania, Sh bilioni 24 zimetolewa na Uingereza, Hispania imetoa Sh bilioni 9 na Sh bilioni 1.4 zimetolewa na Marekani.
Akizungumza juzi wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga, Wambura alisema: “Aina ya miradi itakayotekelezwa ni ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi na sekondari, nyumba za walimu, vyoo, maji, ofisi za walimu, maktaba, maabara, miundombinu ya maji na mabweni”.
Alitaja miradi mingine itakayotekelezwa ni ujenzi wa madaraja ya waendao kwa miguu, karavati, umwagiliaji kwa njia ya mifereji, visima vilivyochimbwa kwa mkono, uvunaji wa maji ya mvua, ujenzi wa malambo na kilimo mseto.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Elias Ntiruhungwa alisema kutakuwa na ugumu wa kupata walengwa wa kunufaika na miradi hiyo endapo wanasiasa wataingiza itikadi zao na kuweka ndugu zao.
Alisema Serikali imejipanga kikamilifu kwa ajili ya kunufaisha kaya hizo masikini .

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMAPILI - JULAI 27

UTUMISHI KUWAINGIZA WATANZANIA HISTORIA YA MASHUJAA

Wananchi mkoani Mbeya wametakiwa kuingia katika historia ya mashujaa kwa kulitumikia taifa la Tanzania kiuadilifu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro wakati akizungumza na wakazi jijini Mbeya waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mashujaa zilizofanyika katika maeneo ya Mnara wa Mwenge jijini hapa.
Kandoro alisema uwepo wa siku ya kuwakumbuka mashujaa kunaikumbusha jamii kutambua kuwa kuna watu waliojitolea kumwaga damu yao kwa ajili ya taifa lao.
Alisema wakati umefika sasa kwa wanajamii kujiuliza kizazi kijacho kitawakumbuka kwa mazuri yapi waliyoyatenda kwa taifa lao huku wenzao wakiwakumbuka kwa kumwaga damu kutetea taifa hili.

MANISPAA YA KINONDONI YATIMUA KAZI WATUMISHI WAKE

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imewafukuza kazi watumishi tisa wa idara mbalimbali kutokana na makosa ya utoro kazini pamoja na matumizi mabaya ya madaraka ya ofisi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Uhusiano wa Manispaa hiyo, Sebastian Mhowera mbali na hatua hiyo pia imewapa karipio watumishi wengine wawili kutokana na makosa hayo.
Alisema hatua hiyo ilifikiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo kilichokaa Julai 22 mwaka huu chini ya Mstahiki Meya Yusuph Mwenda ambacho mbali na mambo mengine kilijadili na kutoa maamuzi ya mashitaka ya nidhamu yaliyofunguliwa kwa watumishi 11.
“Baraza limefikia uamuzi wa kuwafukuza kazi watumishi 9 na kuwapa karipio watumishi wawili, kati ya watumishi waliofukuzwa kazi wanatoka idara za afya, utawala na utumishi, wamo maofisa watendaji wa mitaa, walimu kutoka idara ya elimu ya sekondari na polisi msaidizi mmoja,” alisema Mhowera.
Aidha alisema watumishi wawili waliopewa karipio kutoka Idara ya afya wametakiwa kujirekebisha na watakuwa katika uangalizi kwa muda kuona kama watajirekebisha mienendo yao.

SHULE ZA GREEN ACRES ZADAIWA KUTIRIRISHA MAJITAKA

Shule za Msingi na Sekondari za Green Acres zilizopo Tegeta Salasala, jijini Dar es Salaam, zinadaiwa kutiririsha maji ya kinyesi kupitia mkondo wa maji ya mvua.
Imeelezwa kuwa tabia hiyo inaathiri makazi ya wananchi waishio eneo jirani na shule hizo.
Mkondo huo wa maji ya mvua, ulichimbwa wananchi wa Salasala, kwa lengo la kuondoa adha ya maji ya mvua na mazalia ya mbu.
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Wazo, Atilio Maginga alisema kufuatia tatizo hilo, waliuandikia uongozi wa shule hizo barua na kutoa agizo la siku 14, kuacha kutiririsha maji machafu ya kinyesi, kwani mtaro huo haukuchimbwa kwa ajili hiyo.
 “Nilishatembelea eneo hilo mara mbili, na kukuta maji hayo yakitiririka katika chemchemi, kama hatambui kuwa kuna wakazi wanatumia maji hayo,”alisema Maginga.
Alisema muda waliopewa wa siku 14, haujaisha na kwamba wataendelea kufuatilia suala hilo na kuchukua hatua zaidi, ili kuhakikisha uharibifu huo wa mazingira unasitishwa.
Ofisa Afya wa kata hiyo ambaye alizungumza kwa masharti ya kutotaja jina, alisema walitembelea shule hizo kupulizia dawa ya ugonjwa wa Dengue na kukuta chemba za maji taka zimejaa na kutiririka katika makazi ya watu na kutoa maelekezo kuhusu suala hilo.
Hata hivyo, Mjumbe wa mtaa wa Salasala, aliyejitambulisha kwa jina moja la Mussa alisema Uongozi wa Serikali ya Mtaa ulimuandikia barua Mkurugenzi wa shule hiyo na kwamba hakuna hatua alizochukua.
 Alisema tatizo hilo ni la muda mrefu na wananchi wa maeneo hayo wanaendelea kuteseka na harufu ya kinyesi na pia wanahofia usalama wa watoto wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule hiyo, Edger Rushaigo alisema tatizo lililopo ni kwamba ujenzi wa mabomba ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) katika maeneo hayo, yamechangia kuzuia maji ya mvua ambayo yalikuwa yakitoka katika mto Salasala ambao umepita katika shule yao na kusababisha maji hayo kukwama.
Aliongeza kuwa wasingekubali kuona maji taka yanatiririka wakati kuna wanafunzi wa bweni ambao wanaishi shuleni hapo hivyo wangehatarisha afya zao.
Hata hivyo, Rushaigo alikataa kuwapeleka waandishi wa habari katika maeneo ya ndani ya shule hizo na kudai kuwa tatizo lipo nje ya shule.
Naye mkazi wa maeneo hayo, maarufu kama mama Jack alisema maji hayo hayaambatani na maji ya mvua na kwamba chemba walizozijenga zimebomoka na kuruhusu maji taka kupita katika makazi ya watu.
Alisema Dawasa iliwaita waathirika wa maeneo hayo, Mkurugenzi wa shule hiyo, na wafugaji wa kuku kiwanda cha Interchick na kuambiwa kuwa waondoe maji hayo kwani mabomba yanayopita ni ya maji safi.
‘’Majirani wote tulikutana kutafuta suluhisho kwa kuwasaidia kuondoa maji hayo, lakini hawakutuelewa, Dawasa pia waliingilia kati na kuwapa saa tano za kuondoa maji yaliyokuwa yametuama, lakini kama hawasikii,’’alisema Mama Jack.
Aliongeza kuwa walijenga kwa makusudi chemba hizo katika mkondo wa maji ili wapate kisingizio kwamba maji hayo ni ya mvua jambo ambalo si kweli.

BENKI YA UCHUMI YAZIDI KUCHANJA MBUGA

Benki ya Uchumi (UCB) iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, imetangaza faida ya Sh milioni 599.2, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14, ikilinganishwa na faida ya Sh milioni 524.2 kwa mwaka jana.
Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika ukumbi wa Hosteli za Uhuru mjini hapa jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Uchumi, Wilson Ndesanjo, alisema faida ya taasisi hiyo imetokana na kutanua wigo na kuimarisha mtandao wa wateja.
Alisema mbali na faida hiyo, pia ongezeko la thamani kwa mwanahisa limefikia asilimia 16.25, ikiwa ni ongezeko la juu la lengo lililowekwa katika mpango mkakati wa kufikia asilimia 14.
Alisema benki hiyo katika kufanikisha malengo yake imejipanga kuongeza mtaji kutoka Sh biloni 2.5 hadi kufikia Sh bilioni 7 ifikapo mwaka 2017, ili kuimarisha ukwasi, utoaji mikopo,  kupanua huduma na kukidhi sheria za Benki kuu (BoT).

Saturday, July 26, 2014

NICE BOSS SAYS WORLD CUP KEEPER OSPINA TO JOIN ARSENAL

Arsenal are on the brink of signing Colombia World Cup star David Ospina after Nice boss Claude Puel confirmed his goalkeeper will join the Gunners.
Ospina, who has 44 caps for Colombia, rose to prominence with some impressive performances at the World Cup, where his team lost to hosts Brazil in the quarter-finals.
And following Nice’s 3-2 friendly defeat to Brentford in London on Saturday, Nice manager Puel told Sky Sports that Ospina, 25, had agreed to join the North London club.
"It is confirmed, yes," Puel told Sky Sports News. "At 25 years old it is important for him to experience another championship, so it is a fantastic move for him.
"I think he can take the number one spot at Arsenal because his qualities are very, very strong.
"He is very good with his feet, with his arms, and he knows football. He is a very, very good player."
There is no word from Arsenal but Ospina, available at a cut-price £3million, had looked to be on the brink of moving to the Emirates Stadium after Arsene Wenger let slip that the player would be number two to Wojciech Szczesny.
"You know at the start Szczesny will be the number one, then again we'll be down to performances and, if Ospina shows that he is better, he will play," the Frenchman had told ESPN on Friday.
Ospina will be the third World Cup star to arrive at Arsenal this summer, joining Chile’s Alexis Sanchez and France’s Mathieu Debuchy, who left Barcelona and Newcastle United respectively.
Wenger's side, who won the FA Cup and qualified for the Champions League last season, have also been linked with Southampton duo Morgan Schneiderlin and Calum Chambers, although a move for Real Madrid's Germany midfielder Sami Khedira appears to have stalled.

BREAKING NEWS!! MWIMBAJI BAHATI BUKUKU APATA AJALI MBAYA YA GARI

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba, mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini, Bahati Bukuku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali mbaya katika eneo la Kongwa, mkoani Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwimbaji huyo alipata majeraha makubwa sehemu mbalimbali mwilini na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinadhaniwa kuwa ni mwendokasi.
Chanzo hicho hakijaweza kueleza zaidi kwamba Bukuku alikuwa akielekea ama kutoka mkoani Dodoma na kama ndani ya gari hilo kulikuwamo na abiria wengine.
Pia haikuweza kufahamika mara moja kama mwimbaji huyo alikuwa akiendesha mwenyewe gari hilo, ingawa kilithibishwa ajali hiyo na kwamba Bukuku alijeruhiwa vibaya.
Endelea kuperuzi blogu hii kwa habari zaidi ya tukio hilo.

DIDIER DROGBA RE-SIGNS FOR CHELSEA

Chelsea have announced the return of Champions League hero Didier Drogba on a one-year deal.
Drogba, now 36, left Stamford Bridge in 2012 after scoring the winning penalty in the Champions League final against Bayern Munich after a 1-1 draw over 90 minutes and extra-time.
Drogba told Chelsea's official website: "It was an easy decision - I couldn't turn down the opportunity to work with Jose again. Everyone knows the special relationship I have with this club and it has always felt like home to me.
"My desire to win is still the same and I look forward to the opportunity to help this team. I am excited for this next chapter of my career."
Chelsea announced the deal and welcomed the player back to the club in a Tweet.
He had a spell with Shanghai Shenhua in China before turning out last term for Turkish side Galatasaray, and faced Jose Mourinho's side in the Champions League last 16 where Gala suffered defeat.
He remains a firm fans favourite among the Chelsea diehards with the Stamford Bridge club expected to announce his return before the weekend.
He will sign as a player with a view to becoming part of the coaching staff at the club where he spent eight seasons between 2004-2012 scoring 157 goals.
Jose Mourinho said: "He’s coming because he’s one of the best strikers in Europe.
"I know his personality very well and I know if he comes back he’s not protected by history or what he’s done for this club previously. He is coming with the mentality to make more history.
"His 34 goals in European competition remains a Chelsea record, as do his nine strikes in nine cup finals."
Drogba joined the Blues from Olympique Marseille for £24 million in 2004, at the start of Mourinho's first spell in charge, and scored 157 goals in 342 appearances, hoovering up silverware along the way.
He won three Premier League titles, four FA Cups, two League Cups as well as the Champions League before leaving in 2012.
While Chelsea's billionaire owner Roman Abramovich seemed determined to bring more glamorous centre forwards to the club, with Andriy Shevchenko and Fernando Torres all arriving with lofty reputations, the Ivorian proved immovable.
He remains their record scorer in European competition with 34 goals while his nine strikes in nine cup finals is also a record.
When he left Stamford Bridge two years ago to play for Shanghai Shenhua in China, many thought his career was on the wane with his performances in that final season fluctuating between brilliant and largely ineffective.
Mourinho has decided to bring him back, however, after a successful year in Turkey playing for Galatasaray that showed he still had something to offer at the highest level.
The Portuguese predicted in March, when Galatasaray played Chelsea in the Champions League, that Drogba would one day return to the Chelsea family and said on Friday that there was no emotion or sentiment involved in the decision.

SERIKALI YAIFUNGA HOSPITALI YA IMTU SAKATA LA MABAKI YA MIILI

Hospitali ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU) kinachohusishwa na utupaji wa viungo vya binadamu mithili ya takataka, imefungiwa kwa muda usiojulikana baada ya kugundulika kutokidhi viwango na maadili ya utoaji huduma za hospitali nchini.
Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imechukua jukumu la kuifungia hospitali hiyo baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza na kubaini uwepo wa mapungufu kadhaa.
Mapungufu yaliyobainika kuwepo katika hospitali hiyo ni pamoja na kutokuwa na wauguzi wa kutosha, kutokuwa na vifaa vya kutosha ikiwemo kifaa cha kuchomea taka ngumu, kuchanganya dawa zilizokwisha muda na ambazo hazijaisha muda wake na pia wauguzi kufanya kazi ambazo si za kwao.
Akizungumza wakati wa kufunga hospitali hiyo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Gunini Kamba alisema, hospitali hiyo inastahili kufungiwa kutokana na kutokidhi viwango hivyo.
"Baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza tumebaini kuwepo kwa mapungufu haya, kwa hiyo tunaifungia hospitali hii mpaka pale watakaporekebisha," alisema Dk Kamba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Profesa Yassin Mgonda alikiri kuwepo kwa mapungufu hayo ambayo aliahidi kuyafanyia kazi.
Hata hivyo, Profesa Mgonda aliiomba Manispaa na Wizara ya Afya kuangalia adhabu hiyo waliyoitoa .
Baadhi ya wagonjwa waliokuwa hospitalini hapo wakipata huduma walishtushwa na kusikitishwa na kitendo hicho, lakini walikipongeza na kutaka kuwa endelevu.
Mmoja kati ya wagonjwa hao aliyejitambulisha kwa jina la Neema Kiwalo alisema, ukaguzi huo unatakiwa kuwa endelevu ili kuendelea kufichua madudu yaliyopo katika hospitali mbalimbali nchini.
Aidha, Msemaji Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema, endapo hospitali hiyo watatimiza masharti waliyopewa na Mganga Mkuu wa Manispaa wao kama wizara watafanya ukaguzi kuona kama wamekamilisha.
Alisema ikiwa watakuwa wamerekebisha kasoro hizo zilizopelekea kufungiwa hospitali hiyo itaruhusiwa kutoa huduma zake kama kawaida.
Hospitali hiyo imefungiwa wakati kukiwa kuna sakata linalolihusisha chuo chake, kinachodaiwa kutupa viungo vya binadamu jalalani.
Katika sakata hilo lililovuta hisia za watu na kuzua mjadala mitaani, katika vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii, watu wanane wakiwemo madaktari wa IMTU, walikamatwa na Polisi kwa mahojiano wakituhumiwa kuhusika katika utupaji viungo vya binadamu jalalani.
Serikali wakati ikiendelea kuchunguza tukio hilo ikiwemo kuunda tume nyingine ya watu 15 chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kujiridhisha kabla ya hatua kuchukuliwa iliyopewa siku saba kukamilisha kazi yake, tume hiyo imeundwa kukiwa na tume nyingine iliyoundwa na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Tume iliyoundwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,  imejielekeza kuja na majibu kadhaa,  ikiwa ni pamoja na kufahamu idadi kamili ya watu wenye viungo hivyo.
Ikiwa na watu saba akiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali, Tume hiyo itakuja na majibu yanayofafanua viungo hivyo ni vya muda gani na zilitumika kemikali gani kuvikausha.
Pia, jopo hilo litabaini kama ipo sheria na ni ipi  inavunjwa. Wataalamu hao wanalenga kubaini, pia kama upo uzembe katika kulinda viungo vya binadamu na vinapatikanaje kwa ajili ya mazoezi.
Kwa mujibu wa Polisi, mifuko ipatayo 85 yenye vichwa, miguu, mikono, moyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu, ilikutwa maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji  eneo la Bunju jijini Dar es Salaam.

BUNGE LA KATIBA 'RUKSA' KUENDELEA BILA WAJUMBE WA UKAWA

Kamati ya Mashauriano ya Bunge Maalumu la Katiba imetoa mapendekezo kwa Kamati ya Uongozi kwamba Bunge Maalumu liendelee na mkutano wake wa pili wa Bunge hilo kuanzia Agosti 5 mwaka huu.
Katika ngwe hiyo ya pili mkutano huo uzingatie upya baadhi ya kanuni za Bunge hilo ambazo ni kikwazo katika kuhakikisha kazi ya kujadili na kupitisha katiba inayopendekezwa inakamilika kwa siku 63 zilizosalia kisheria.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alisema kamati hiyo imetoa sababu za kuendelea na ngwe ya pili ya bunge hilo inatokana na kuwepo masuala mengi muhimu ya kikatiba ambayo yanawaunganisha.
Alitaja mambo hayo kuwa ni kama usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi, kuikarabati Tume ya Uchaguzi, kurekebisha kikatiba masuala  ya Muungano, haki za wakulima, wafugaji, wasanii, ukomo wa vipindi vya uongozi na mengineyo.
Akitoa maoni na ushauri wa kamati hiyo kwa wananchi katika taarifa yake iliyosomwa jana na Katibu wake, Yahya Khamis Hamad alisema  ngwe ya pili imebakiwa na siku 60 kisheria na nyongeza tatu zilizokuwa pungufu kufika 70 za awali na kueleza kuwa wajumbe wa kamati hiyo wameshangazwa na wenzao kugomea hata  kikao cha mashauriano.
Alisema kuanzia sasa bunge litaanza kujibu upotoshwaji kuhusu mchakato wa Katiba kadri utakavyojitokeza kutokana na  baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kwenda kwa wananchi na kuwapotosha wananchi.
Sitta alisema kamati imegundua mapungufu yaliyochangia kukuza tatizo lililopo  la baadhi ya wajumbe kugomea vikao kuwa ni pamoja na wajumbe wanaosusia mchakato huo kutambuliwa kama kundi rasmi  la bunge hilo wakati makundi rasmi ni wabunge, wawakilishi na lile la wajumbe 201.
“Lazima ielewekwe kuwa wakati wa kura za maamuzi makundi rasmi ni kundi la wajumbe kutoka Tanzania bara na wa Tanzania Zanzibar na siyo kundi hilo, ”alisema.
Sitta alisema sababu nyingine ni Sheria ya mabadiliko ya Katiba hata kanuni za bunge kutokuwa na vipengele vinavyozuia utoro, ukosefu wa nidhamu na matendo mengine yanayolenga kuvuruga mchakato huo.
Alisema kamati inaona kwamba kitendo cha kuendelea kususia bunge na kupuuza mwito wa jamii kupitia makundi mbalimbali pamoja na madhehebu ya dini inatia shaka dhamira halisi ya viongozi wa kundi hilo la wasusiaji.
“Kupuuzia juhudi zote za usuluhishi kunazua  mashaka kuhusu lengo la wasusiaji kwamba pengine agenda ya viongozi hao ni nyingine na sio upatikanaji wa Katiba,” alisema Sitta.
Alisema pia  kamati inahoji utamaduni mpya unaoanza kujengeka wa kuendesha mambo kwa kususa, kwani ni  vigumu muafaka wa jambo lolote ukapatikana kwa kususia majadiliano na kuendesha kampeni ya maneno nje ya vikao rasmi.
Mwenyekiti huyo alisema kamati inarejea kuwa wajumbe 629 wamekabidhiwa jukumu adhimu na la kihistoria kwa niaba ya Watanzania ambalo hutokea baada ya miongo kadhaa ya uhai wa taifa lolote haitakuwa haki kwa Watanzania  ikiwa hakutakuwa na maridhiano yatakayowezesha kukamilisha kazi waliyopewa.
“Pamoja na yote, kamati ya mashauriano inaendelea kutoa mwito kwa wajumbe waliosusa mikutano ya bunge hili kurejea kwani ndilo lenye uwezo wa kutatua matatizo yaliyopo,” alisisitiza.
Sitta alisema mapema mwezi huu wajumbe 30 wa kamati ya mashuriano waliteuliwa lakini kikao kilichofanyika juzi wajumbe wa vyama vya CUF, Chadema na NCCR- Mageuzi walisusia kikao licha ya jitihada za Mwenyekiti na Sekretarieti kuwashawishi kwa siku nzima.
Alisema wajumbe waliohudhuria kikao cha kamati hiyo walikuwa zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wote waliendelea na kikao na kufikia maazimio hayo.
Wakati Bunge Maalumu la Katiba kilitarajiwa kuendelea wiki ijayo, Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) limependekeza kuahirishwa kwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya hadi baada ya uchaguzi mkuu kumalizika mwakani, kutokana na wanasiasa kupandwa na joto la uchaguzi.
Hatua hiyo inatokana na sababu zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Hebron Mwakagenda ambaye alisema, inatokana na michakato mikubwa sita ya kitaifa katika kipindi kifupi cha miezi 15.
Mwakagenda alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, kutokana na kuwepo kwa michakato hiyo, wanapendekeza pia kuahirishwa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa ili ufanyike pamoja na uchaguzi mkuu mwakani  na kusimamiwa na tume huru ya uchaguzi kwa kutumia daftari la kudumu la mpiga kura litakaloandaliwa mwaka huu.
Alisema pia wanapendekeza kuahirishwa kwa mchakato wa kuandika Katiba mpya hadi baada ya uchaguzi mkuu, ambapo alisema lengo ni kufupisha mkutano ujao wa Bunge Maalumu la Katiba utakaoanza Agosti 5 kutoka siku 60 walizowekewa  hadi wiki mbili ili kufanya kazi ya kujadili, kuridhia na kupendekeza ratiba mpya ya mchakato huo.
Akifafanua juu ya kuahirishwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba alisema, kwa sasa wanasiasa waliomo ndani ya bunge hilo wamepandwa na joto la uchaguzi na wengi wao wanaangalia zaidi mwakani hivyo ni ngumu kupata katiba ya muda mrefu.
Alisema hata chanzo cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutoka nje ya bunge sio matusi pekee, bali  ni joto la uchaguzi limewapanda jambo linalofanywa na makundi yote ya vyama yaliyomo ndani ya katiba hiyo.
Alifafanua kuwa jukwaa hilo limebaini hata ufa uliopo wa mchakati kati ya wanaopendekeza serikali mbili na tatu ni sehemu ya mivutano ya kisiasa inayotokana na wanasiasa wanaoendelea kujipima umarufu wao wa kisiasa kwa kutumia katiba mpya.
"Kosa lilifanyika tangu mwanzo katika sheria ya mabadiliko ya katiba kwa kuwaingiza wanasiasa wote ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, wanasiasa wamepandwa na joto la uchaguzi na ndio sababu ya malumbano kuibuka kule bungen.
"Hao Ukawa au Ukiwa kama watu wanavyowaita na Tanzania Kwanza ambalo ni kundi la CCM wasingeweza kugombana kama ingekuwa ni 2006, kwa hiyo ni heri tukaachana na mchakato wa Katiba Mpya kwa sasa," alisema Kibamba.