Friday, October 26, 2012

'JUMUIYA YA UAMSHO INATUMIWA NA WAHUNI ZANZIBAR'...

Polisi wakikabiliana na wafuasi wa kundi la Uamsho katika moja ya mitaa ya mjini Unguja.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesema wakati kuna madai kwamba Jumuiya ya Uamsho ni ya kidini (Kiislamu), lakini imekuwa ikitumiwa na makundi ya wahuni ambayo yamejipachika majina tofauti.
Taarifa ya Tume hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana ikiwa imesainiwa na Kamishna wake, Zahor  Khamis, imetaja baadhi ya majina ya makundi hayo kuwa ni Mbwa mwitu, Simba mkali,  Ubaya ubaya na Toto tundu na kuongeza kuwa yamekuwa yakitumika kufanikisha azma yao.
Mbali na jumuiya hiyo kutumiwa na wahuni, Tume pia imesema kutekwa kwa kiongozi wa jumuiya hiyo, Shekhe Farid Hadi Ahmed, kuna utata mkubwa ambao unahitaji uchunguzi na ufafanuzi kufahamu huko alikotekwa na kutoa mfano wa madai ya kunyimwa kula kwa siku tatu bila kuathirika kiafya.
Tume hiyo imehoji kama kweli alikuwa ametekwa, aliwezaje  kufika msalani ambako alikuwa akinywa maji, wakati alikuwa amefungwa kitambaa usoni na mikononi akiwa na pingu na ilikuwa nyumba ambayo haijui!
Kutokana na utata huo, Tume imemtaka Shekhe Farid  kutoa maelezo yanayothibitisha pasipo shaka ili kuwathibitishia Wazanzibari, Watanzania na ulimwengu kwa jumla, juu ya kutoweka kwake.
“Shekhe Farid amedai alitekwa na watu wasiojulikana tarehe 16 mwezi huu na kuonekana siku tatu baadaye akiwa katika hali ya uzima na salama, jambo ambalo lilisababisha vurugu kubwa Zanzibar na kusimama kwa shughuli zote za kiuchumi na kijamii,” ilieleza taarifa hiyo ya Tume.
Kwa mujibu wa Tume, kutokana na fujo hizo zilizotokea, hasara ilitokea ambayo mpaka sasa haijajulikana thamani, askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Said Abdulrahman kuuawa.
Kutokana na matukio hayo, Tume imeishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuwatafuta na kuwakamata wote walioshiriki katika vurugu hizo na kuvunja vikundi vyote vya kihalifu vilivyoanza kushamiri Zanzibar.
“Tunalaani mauaji ya askari Abdulrahman kwani ni uvunjaji wa haki za binadamu, inapingana na sheria za nchi na ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 14 inayozungumzia haki ya kuishi na Katiba ya Zanzibar ibara ya 13 inayozungumzia haki ya kuwa hai,” taarifa hiyo ilifafanua.
Tume pia imelaani kitendo  alichofanyiwa Diwani wa CCM Wadi ya Chumbuni kwa kushambuliwa na kujeruhiwa, kitendo ambacho kinakwenda kinyume na haki za binadamu na Katiba ya Tanzania  inayopiga marufuku mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au adhabu za kumdhalilisha.
“Kuna uhusiano gani wa kutekwa kwa kiongozi wa Uamsho na  hujuma za mali za watu na CCM?” Taarifa hiyo ilihoji.
Kwa mujibu wa Kamishina wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa Polisi inafanya uchunguzi wa kina kubaini kama Shekhe Farid anahusika na mtandao hatari wa ugaidi wa Al-Qaeda.
Akizungumza kwa simu jana, Mussa alisema Polisi nchini inafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa ikiwamo Polisi - Interpol.
“Jeshi la Polisi nchini kwa sasa linafuatilia kwa karibu sana nyendo zote za kiongozi wa Uamsho Shekhe Farid ikiwamo kuhusishwa kwake na mtandao wa Al-Qaeda,” alisema.

KATIBU WA BAKWATA ARUSHA ALIPULIWA KWA 'BOMU'...

Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) wa Mkoa huo, Shekhe Abdulkarim Jonjo, amejeruhiwa na mlipuko unaosadikiwa kuwa wa bomu lililotegwa nyumbani kwake katika eneo la Esso.
Shekhe Jonjo alijeruhiwa na mlipuko huo saa 6.30 usiku wa kuamkia jana chumbani kwake eneo la Sokoni One,  Esso, jijini humo ambapo pia chumba hicho kiliharibiwa baada ya kupata tundu kubwa ukutani.
Akisimulia kisa hicho katika wadi ya majeruhi ya Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru alikolazwa, Shekhe Jonjo alisema alifika nyumbani kwake juzi saa moja usiku umeme ukiwa umekatika.
Alisema aliingia ndani na baada ya muda mfupi, alipitiwa na usingizi lakini ilipotimu saa 4 usiku umeme ulirudi ndipo aliposhituka na kuamka kuchaji simu yake ya mkononi.
Baada ya kuacha simu hiyo, alisema aliendelea na usingizi na ilipotimu saa 6 usiku, ghafla aliona kitu kinawaka chumbani mwake.
Shekhe Jonjo alisema alishituka na kujiuliza ni nini akaenda kukishika ndipo kilipomlipukia na kumsababishia majeraha  usoni, machoni, mkononi na kifuani.
Alisema baada ya mlipuko huo, alipoteza fahamu kwa muda na alipozinduka kwa sababu alikuwa peke yake kwa kuwa familia yake ilikwenda Tabora msibani, alipata akili ya kwenda kufungua mlango na kuomba msaada kwa majirani ambao walimwahisha hospitalini kupata matibabu zaidi.
"Nilikuwa peke yangu usingizini na niliposhituka niliona kitu kinawaka kama utambi nikajiuliza ni kitu gani ndipo nilipokwenda kukishika, kikanilipukia, ukweli nimepoteza damu nyingi na ninasikia maumivu," alisema.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mount Meru, Dk Ijosia Mlay  alisema walimpokea Katibu huyo juzi usiku akiwa na maumivu ingawa si makubwa sana na hakuvunjika sehemu yoyote.
"Tunaendelea kumpa huduma lakini hajapata majeraha makubwa ni ya kawaida ila ameumia usoni, kifuani na baadhi ya sehemu za mwili lakini majeraha ni ya kawaida na si makubwa," alisema Dk Mlay.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo jana alifika hospitalini  kumjulia hali na kumpa pole  na kwenda nyumbani kwa Katibu huyo na kuwasihi wakazi wa Arusha kuacha kuingiza tukio hilo na masuala ya dini kwani ni mapema kutoa majibu.
Alisema tayari timu ya wataalamu wa milipuko ya Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imeundwa kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na watakapomaliza kuchunguza, majibu yao yatatoa taswira ya tukio hilo lililogubikwa utata.
"Tukio hili ni la utata kwani kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa wataalamu wa JWTZ na Polisi mlipuko wa bomu ulitokea ndani ya chumba cha Shekhe Jonjo na si nje hivyo ni mapema kusema aina ya bomu au aliyefanya hivyo, tusubiri uchunguzi," alisema.
Mmoja wa wataalamu wa JWTZ ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema mlipuko unavyotokea kama ungekuwa   nje lazima moshi ungeonekana kwa nje lakini ulitokea ndani ndio maana chumbani kwa Shekhe Jonjo kulikutwa na moshi na nyufa.
“Kama mlipuko huu ungetokea nje lazima shimo lingekuwa dogo na kwa ndani likawa kubwa, lakini hili lina utata kwani kwa jinsi tunavyoona, mlipuko huu umeanzia ndani kwa kuwa kuna shimo dogo na nje ya dirisha lake katika chumba anacholala kunaonekana shimo kubwa," alisema mtaalamu huyo.
Mmoja wa majirani wanaoishi karibu na nyumba anayoishi Shekhe huyo, Mama Husna alikiri kusikia mtikisiko saa 6:30 usiku kwenye nyumba yao wakahisi ni majambazi.
Alidai wakati wanapigiana simu, ndipo walipogundua kuwa nyumba anayoishi Shekhe Jonjo pametokea mlipuko huo ingawa hawajui bomu hilo ni la aina gani.
Mpangaji anayeishi na Jonjo,  Hillary Musa alisema alisikia mtikisiko katika nyumba wanayoishi yeye na wapangaji wenzake akiwamo Shekhe huyo na alipotoka nje alidhani ni shoti ya umeme, lakini ghafla alimwona Shekhe Jonjo akihitaji msaada  ndipo walipomwuliza kulikoni, naye aliwaeleza ilibidi waombe msaada kwa majirani na kumkimbiza hospitalini.

HAWA NDIO WANAODAIWA KUMUUA KAMANDA BARLOW...

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewatia mbaroni watu watano kutoka Dar es Salaam wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow akiwemo anayedaiwa kuwa kinara wa mauaji hayo.
Aidha linawashikilia watu wengine watano wa jijini hapa ambao wanahojiwa juu ya mauaji ya kamanda huyo.
Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba aliwataja watuhumiwa  hao ambao wanadaiwa na Polisi kuwa kabla ya mauaji hayo walifanya uporaji katika maeneo mengine ni pamoja na Muganizi Michael Peter (36) mkazi wa Isamilo ambaye alikiri mwenyewe kumuua kwa risasi.
Wengine ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward kusota na Bhoke Mara Mwita (42) ambao walikamatwa jijini Dar es salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada wa wananchi.
Manumba alisema majambazi hao kabla ya kufanya mauaji hayo jijini mwanza walifanya uporaji katika maeneo mbalimbali majira ya saa 4 na 6 na kwamba wakiwa Dar es Salaam pia walifanya matukio ya uporaji,
Manumba ambaye alikuwa akitoa taarifa katika kikao kilichomshirikisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Said Mwema alisema baada ya kuwakamata wauaji hayo pia wamefanikiwa kukamata bunduki mbili ikiwemo shotgun iliyotumika katika mauaji ya RPC pamoja na
ya aina Pump action ambazo zote zilipatikana jijini Dar es salaam zikiwa zimechimbiwa.
Alisema kupatikana kwa wauaji hao kunatokana na jeshi hilo kujipanga katika makundi yakiwemo intelijinsia, mahojiano na watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ambavyo vilisambaa katika mikoa yote ya kanda ya ziwa na mingineyo ili wasitoe nafasi kwa wahalifu kukimbia.
Manumba alisema bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ambapo watu wawili waliohusika katika tukio hilo bado wanasakwa.
Wanaoshikiliwa jijini Mwanza kwa mahojiano ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na RPC wakati mauaji yakitokea, Felix Felician Minde (50), Philemon Felician (46) maarufu kama Fumo, Bahati Agustino Lazaro (28) na Amos Magoto (30) maarufu kama Bonge.
Naye IGP, Mwema alisema jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote anayefanya uhalifu, hujuma na uchochezi kwa kisingizio chochote ili kupunguza uhalifu hapa nchini.
Alisema kifo cha RPC Barlow kimewafanya kuwa imara na kukuza uweezo wao wa kulinda wananchi na viongozi mbalimbali serikali.
Hata hivyo alisema uchunguzi wa kifo cha RPC Barlow bado unaendelea kutokana na taarifa mbalimbali wanazoendelea kuzipokea kutoka kwa raia wema na kuwashukuru wananchi na vyombo vya habari kwa ushirikiano waliounyesha tangu mauaji hayo yatokee.
IGP Mwema aliwasili jijini Mwanza jana mchana na kukutana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, kisha alizungumza na askari polisi wapata 500 katika ukumbi wa halmashauri ya jiji na kisha alizungumza na vyombo vya habari ambapo alisema madhumuni ya ujio wake ni pamoja na kukagua na kufanya tathmini ya tukio la kuuawa kwa kamanda Barlow pamoja na kuangalia hali ya usalama ya mkoa.
Marehemu Kamanda Barlow aliuawa  usiku wa Oktoba 12 majira ya kati ya saa 7 na 8 usiku katika eneo la Kitangiri, kona ya Bwiru baada ya kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja kaenda zake Uarabuni. Njiani akakutana na Mwarabu akivuta sigara. Jamaa akapiga hesabu jinsi ya kumwomba moto lakini atamuanzaje? Mwishowe akapata mbinu na kumwendea kwa kujiamini, "Give me JEHANAM!" Kasheshe...

JICHO LA TATU...


KIPINDI CHA FAMILIA YA HOUSTON CHAANZA KWA VITIMBI...


Kwamba kifo cha ghafla cha Whitney Houston kimeiacha familia yake ikipepesuka, kwenda bila kuongea, lakini uamuzi wao wa kukabiliana na mshituko huu kwa  kutengeneza kipindi cha televisheni kumesababisha macho kufunguka kwa mshangao.
Mbaya zaidi, ni kwamba mwanzo wa mfululizo huo wa vipindi anaonekana kwenye vipande kadhaa Bobbi Kristina mwenye miaka 19, binti wa Whitney Houston aliyezaa na Bobby Brown, akitembelea kaburi la mama yake kwa mara ya kwanza kabisa.
Kama hiyo haitoshi kuvuta hisia zako, vipande vingine vimekwenda mbali zaidi kwa kumuonesha Bobbi akinywa pombe huku umri wake ukiwa hauruhusu.
"Hajafikisha umri anaoruhusiwa kunywa pombe," analalamika shangazi yake.
Bobbi Kristina anaonekana akinywa kidogo kidogo kinywaji chenye kilevi na kumgeukia kaka yake aliyeasiliwa isivyo rasmi ambaye sasa amegeuka kuwa mchumba wake, Nick Gordon.
Vipande hivyo vya kutisha vinamhusisha pia Mama wa Whitney, Cissy, na kaka yake, Gary.
Angalau kufikia hapa, sauti nzuri na za kuvutia za Whitney vinatawala ...na kukipa kipande hiki uchungu na hali ya kuogofya.
Japo ilikuwa vigumu mno kumtazama Bobbi Kristina akiwa kaweka mikono yake kichwani mbele ya kaburi la mama yake, licha ya ukweli kwamba wifi yake Whitney, Pat alijaribu kuelekea kwenye tukio.
Cissy anaonekana akimwambia mjukuu wake aendelee na kazi hiyo.
"Alikuwa ni mama yangu tu," Bobbi alimweleza Nick kwa unyonge. "Sijali kitu chochote kile kingine."
Mapema katika mfululizo wa matukio, alionesha hadharani pete ya mama yake ambayo aliielezea familia yake iliyopatwa na mshituko kwamba inawakilisha uchumba kati ya wawili hao.
Nick alisema mbele ya kamera: "Kila mmoja anachukulia visivyo, haikuwa kisheria ...si kosa la kujamiiana."
Pat anafikiri kwamba Bobbi anahitaji kujikita zaidi kwenye kazi kusaidia kufikia malengo, badala ya mahusiano yake ya karibu na Nick.
Anamhamasisha kuonana na mwalimu wa uigizaji, baada ya kukiri kwenye kamera kwamba Bobbi alikuwa mwenye furaha kufanya kazi na Tyler Perry katika 'For Better of Worse'.
"Kuigiza ni utumwa kwangu," anakiri Bobbi.
Katika kipande cha video kupromoti shoo hiyo mwishoni kimedokeza kwamba uhusiano wa Bobbi na baba yake Bobby Brown - ambaye hivi karibuni alikamatwa mjini Los Angeles kwa kuendesha gari huku akiwa amelewa - utachunguzwa kwa kina.

Thursday, October 25, 2012

POLISI ANASWA KATIKA HARAKATI ZA KUWANIA UONGOZI UVCCM...

Kamanda wa Polisi, Faustine Shilogile.
Wakati Mkutano  Mkuu wa Nane wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) ukimalizika, mmoja wa wagombea wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho nafasi sita Tanzania Bara, Stanley Mdoe,  ametiwa mbaroni na Polisi akibainika kuwa askari Polisi. 
Askari huyo mwenye namba F 7961 wa cheo cha Konstebo, anatoka kituo cha  Polisi  Mvomero, Morogoro  ambaye alibainika jana  akijihusisha  na  siasa hata kuingia  kinyang’anyiro cha kuwania   ujumbe wa NEC  kupitia  Vijana.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana Morogoro, askari huyo alijitambulisha  kwa baadhi ya wajumbe kuwa  yeye ni mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera,  akijiita Stanley Bendera.
Wapambe waliofuatana naye kutoka Morogoro wakiwa Dodoma waliarifu kuwa mgombea huyo  alikamatwa  juzi jioni akiwa amevalia  sare za chama hicho akiomba kura kwa wajumbe ili wamchague kwa nafasi hiyo.
Hata hivyo, ilielezwa na baadhi ya wanachama waliofuatana naye na wengine wanaotambua kazi yake uaskari, waliwajulisha maofisa usalama  waliokuwa eneo hilo nao kufikisha taarifa hizo Polisi na kukamatwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari,  askari huyo alikuwa ameomba likizo isiyo na malipo, wakati wengine  wakidai kuwa  ameacha kazi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro,  Faustine Shilogile  akizungumzia tukio hilo alisema alipata taarifa ya kukamatwa kwa askari huyo Dodoma  na kwamba wakati huo alikuwa akimtafuta kwa siku mbili kwa ajili ya shughuli za kikazi bila mafanikio.
“Sina  uhakika kama  askari huyu amejiingiza katika siasa ... nimetuma askari wengine kwenda Dodoma   kufanya uchunguzi wa suala hilo,” alisema Kamanda Shilogile na kuongeza:
“Iwapo itabainika kuwa kweli,  atachukuliwa hatua stahiki na kinidhamu kulingana na taratibu za kijeshi.
Hata hivyo siwezi kuzungumzia suala la ugombeaji wake, sijathibitisha ukweli wake, isipokuwa hakuwa kazini kwa siku mbili na  ni utovu wa nidhamu kwa Jeshi letu kutoonekana eneo la kazi,” alisema Kamanda Shilogile.
Kwa mujibu wa Kamanda, sheria za nchi na Katiba kuna vifungu vinavyohusu majeshi ya ulinzi na usalama vikitamka kuzuia na kupiga marufuku mwanajeshi kujihusisha na siasa.
Alisema iwapo jambo hilo litabainika, litakuwa limefanyika  kinyume na kanuni na taratibu za kazi ya uaskari.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bendera, hakupatikana ofisini kwake wala kwa njia ya simu ya mkononi ili kufafanua kadhia hiyo. Hata hivyo wasaidizi wake walidai kuwa yuko  nje ya nchi kwa shughuli za kikazi.

KIONGOZI WA KUNDI LA UAMSHO ZANZIBAR AHUSISHWA NA AL QAEDA...

Shekhe Farid Hadi Ahmed.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema Polisi inafanya uchunguzi wa kina kubaini kama kiongozi wa Uamsho, Shekhe Farid Hadi Ahmed anahusika na mtandao hatari wa ugaidi wa Al-Qaeda.
Akizungumza jana, Mussa alisema Polisi nchini inafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa ikiwamo Polisi - Interpol.
“Jeshi la Polisi nchini kwa sasa linafuatilia kwa karibu sana nyendo zote za kiongozi wa Uamsho, Shekhe Farid ikiwamo kuhusishwa kwake na mtandao wa Al-Qaeda,” alisema.
Alisema licha ya kiongozi huyo na wenzake sita kuwa rumande, lakini uchunguzi wa kujua nyendo zao pamoja na uhusiano wake na taasisi za nje ya nchi kwa sasa unafanywa.
Aidha, alisema kiongozi huyo na wenzake wanatazamiwa kufikishwa tena katika Mahakama ya Mwanakwerekwe mjini hapa kwa ajili ya kusikilizwa shauri lao la dhamana kuhusu tuhuma za kufanya fujo na uchochezi.
“Maandalizi ya Polisi kufikishwa mahakamani kwa kiongozi wa Uamsho na wenzake yamekamilika na kusisitiza ulinzi mkali umewekwa katika maeneo yote jirani na mahakama hiyo,” alisema.
Viongozi saba wa Uamsho walifikishwa katika Mahakama ya Mwanakwerekwe Jumatatu   wakituhumiwa kufanya fujo na uchochezi na kuhatarisha amani.
Viongozi hao ni Mselem Ali Mselem, Khamis S. Khamis, Mussa Juma Issa, Shekhe Azan Khalid Hamdani, Suleiman Juma na Hassan Bakari.
Mapema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imevitaka vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi wa kina kujua sababu zilizosababisha Shekhe Farid kutoweka huku akidai kutekwa nyara na kusababisha kuibuka kwa fujo.
Akitoa tamko la SMZ kuhusu suala la madai ya kutekwa nyara kwa Shekhe Farid na baadaye kuibuka kwa fujo zilizosababisha vifo vya wananchi na askari Polisi katika Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud alisema uchunguzi wa kina unahitajika kufanywa ili kujua sababu zote.
“Tumeviagiza vyombo vya Dola kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha fujo zilizosababisha hasara kubwa na upotevu wa maisha ya wananchi,” alisema.
Alisema SMZ kamwe haitavumilia aina zozote za vitendo vinavyohatarisha amani na utulivu kiasi ya kutishia kuvurugika kwa uchumi wa nchi.
Aidha, aliviagiza vyombo vya ulinzi kudhibiti vitendo vya fujo vinavyofanywa na baadhi ya vikundi vya watu ikiwamo vijana wanaovamia wananchi na kupora mali zao.
Alisema kama Serikali itaendelea kuvumilia na kulea vitendo vya aina hiyo vinavyosababisha vurugu,  uchumi wa Zanzibar na amali iliyopo utavurugika moja kwa moja na kutoweka.
“Serikali kamwe haitavumilia vurugu za aina hii ambazo zinahatarisha maendeleo ya sekta ya utalii huku sekta hiyo ikiwa kiongozi wa uchumi wa nchi,” alisema Aboud.
Hivi karibuni kulijitokeza uvunjifu wa amani visiwani hapa baada ya kuibuka vikundi vinavyovamia makanisa na kufanya uharibifu kwa kuvunja na kuchoma moto mali kwa kisingizio cha  kulipiza kisasi kidini.
Kwa visiwani hapa hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya wafuasi wa Uamsho kusababisha ghasia kubwa wakidai kuwa Shekhe Farid  ‘ametekwa na Polisi’, wakitaka aachiwe. Polisi ilikanusha  madai hayo.
Ilifafanua kuwa kiongozi huyo wa Uamsho hakutekwa na wala vyombo vya usalama nchini havina sababu yoyote ya kumteka au kumkamata kisiri, kwani vinafanya kazi zake kwa uwazi, weledi na kwa mujibu wa sheria. Kama wangetaka kumkamata wasingemvizia na kumkamata kisiri.
Vurugu za wafuasi wa Uamsho zilisababisha kifo cha askari wa Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) F.2501 Koplo Saidi Abdrahamani Juma (41) ambaye alivamiwa na kupigwa. Chanzo cha vurugu hizi ni uchochezi mkubwa uliofanywa na viongozi wa  kundi hilo, akiwamo Shekhe Farid.
Farid ambaye yuko rumande anadaiwa kuendesha mihadhara yenye kupandikiza mbegu za chuki, uhasama na uchochezi  baina ya Watanzania wa Bara na Visiwani, na baina ya Wakristo na Waislamu.
Amekuwa akifanya hivyo katika misikiti na sehemu mbalimbali za Zanzibar.   
Kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari jana, Shekhe Farid ana asili ya Yemen, ambako wazazi wake walizaliwa kabla ya kuingia nchini na haijathibitika kama alikana uraia wa Yemen kama sheria ya Uhamiaji inavyotaka ili awe raia wa Tanzania.
Madai zaidi yaliyopo ni kwamba Shekhe Farid alipata kuajiriwa na Jeshi la Qatar lakini akafukuzwa kwa sababu za kiafya.
Hatua ya Polisi Zanzibar kumchunguza Shekhe Farid kwa tuhuma za kuhusiana na al Qaeda zinato-kana na madai kuwa alipata kushiriki mafunzo ya mtandao huo katika nchi tatu Arabuni ikiwamo Yemen.
"Huyu ana ujuzi wa kigaidi na hata kitendo chake cha kujificha na kudai katekwa, ni uongo na mbinu zake za kigaidi ili kuchochea ghasia na machafuko nchini," kilisisitiza chanzo cha habari kilichokaririwa na vyombo hivyo vya habari.
Shekhe Farid  alikamatwa na kufikishwa mahakamani Oktoba 22 na viongozi wenzake wengine wa Uamsho baada ya kujitokeza kutoka mafichoni alikokuwa. 
Wakati kukiwa na habari hizo kumhusu Shekhe Farid, ziko pia taarifa kwamba miongoni mwa wanaotuhumiwa sambamba naye kuna mmoja ambaye anadaiwa kuwa mwakilishi wa kikundi cha kiislamu cha Boko Haram cha Nigeria, akikiwakilisha katika Afrika Mashariki, kutokea Mombasa, Kenya.
Nchini wafuasi wake wanadaiwa kutumia jina la Hizb Tahrir na alipata kutambulishwa jijini katika viwanja vya Magomeni miaka takriban miwili iliyopita na wamekuwa na mkakati wa kuchoma makanisa na baa.
Kikundi cha Boko Haram kimekuwa ‘mwiba’ kwa Serikali ya Nigeria ambako kimekuwa kikishiriki kuchafua hali ya amani nchini humo kwa kushambulia makanisa na shule kwa mabomu.
Hata hivyo vikosi vya Serikali vimekuwa vikiendesha msako dhidi ya wapiganaji wa kikundi hicho na kufanikiwa kuua baadhi ya viongozi wake na wengine kuwatia mbaroni.
Boko Haram mbali na mashambulizi hayo, imekuwa ikipiga vita elimu ya Magharibi na kusisitiza matumizi ya sharia.

BAADA YA KIMYA KIREFU, DECI YAIBUKIA MAHAKAMANI KISUTU...

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kusimamia na Kuendesha Upatu (Deci), Mchungaji Jackson Mtares amekiri kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliwakataza kupokea fedha kutoka kwa mwanachama yeyote wa taaasisi hiyo.
Mtares alieleza hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi katika kesi ya kuendesha shughuli za upatu bila kibali inayomkabili pamoja na wakurugenzi wenzake wanne.
Akihojiwa na Wakili wa Serikali Prosper Mwangamila, Mtares alidai katika barua ya majibu ya kuomba leseni ya kufanya shughuli za taasisi hiyo, BOT iliwatakaza kupokea fedha kutoka kwa mwanachama yeyote iwe kwa hiari au kwa lazima.
Hata hivyo alipoendelea kuhojiwa na kupewa barua hiyo ambayo imepokelewa mahakamani hapo kama kielelezo cha upande wa mashitaka, Mtares alidai kuwa Mkurugenzi mwenziye ambaye pia ni mshitakiwa ndiye atakayetoa maelezo zaidi.
Awali Mtares aliwasilisha kielelezo ambacho ni barua ya maombi waliyoandika kwa Gavana wa Benki Kuu (BOT) kuomba leseni ya kufanya shughuli za taasisi ambazo ni kusaidia watu wenye kipato cha chini kujikimu kimaisha.
Akiongozwa na Wakili wake wa utetezi Hudson Ndusyepo, Mtares alidai hakuhusika kupokea fedha wala kutoa risiti kwa wanachama na hata katika ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa mashitaka hakuna shahidi aliyedai yeye alipokea fedha.
Mtares aliendelea kudai kuwa,  Benki ya Afrika (BOA) ilikataa kuhifadhi fedha za taasisi hiyo hivyo walizihamishia katika akaunti ya kanisa lake la Jesus Christ  deliverance iliyopo katika Benki ya Wananchi Dar es salaam (DCB) ambayo ilikutwa na zaidi ya Sh bilioni 1.3 baada ya shughuli za Deci kusimama.
Alipoulizwa sababu za benki hiyo kukataa kuhifadhi fedha hizo alidai hajui bali walipewa taarifa kuwa wanatakiwa watoe fedha hizo haraka ndipo bodi ya wakurugenzi ilipoamua fedha hizo ziwekwe kwenye akaunti ya kanisa lake.
Aliendelea kudai kuwa wanachama walikuwa wanalipa kiingilio cha Sh 30,000 na baadaye wanaweka fedha na kupata uwezeshwaji (riba) ya asilimia 150 ya fedha ambayo mwanachama ameweka.
Alipobanwa kwa maswali na upande wa mashitaka, Mtares alidai fedha za riba  zilitokana na fedha walizokuwa wanaweka wanachama kwasababu Deci ilikuwa haijishughulishi na biashara yeyote zaidi ya kuwasaidia watu wenye kipato cha chini.
Hakimu Stewart Sanga aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 8 mwaka huu, wakatakapoendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Wachungaji wa makanisa tofauti ya Pentecoste ni, Dominic Kigendi, Samuel Mtares, Timotheo Ole Loitingye na  Arbogast Francis.
Wanadaiwa katika tarehe tofauti mwaka  2007 na  Machi 2009 katika Makao Makuu ya Deci, Mabibo Dar es Salaam walikusanya fedha kutoka kwa wananchi  wakiwaahidi kuwa watapata faida ya riba kubwa, katika mpango huo waliouita kupanda na kuvuna pia walifanya shughuli hiyo bila leseni.

ZIRO PLUS...


CHEKA TARATIBU...

Trafiki kamsimamisha dereva mmoja aliyekuwa akiendesha gari lenye matatizo. Trafiki akamuuliza, "Mbona namba za mbele za gari lako ni tofauti na za nyuma?" Baada ya sekunde kadhaa dereva akajibu kwa ukali, "Unashangaa nini? Wewe Sura yako na Makalio vinafanana?" Duh...

MIFUPA YA MTU ALIYEKUFA ZAIDI YA MIAKA 15 YAKUTWA KITANDANI...

Mifupa ya mitupu ya binadamu akiwa bado kavalia nguo zake za kulalia kitandani inaaminika imekuwa hapo bila kugundulika kwa zaidi ya miaka 15 kwenye nyumba moja iliyotelekezwa.
Polisi wa Ufaransa wanajaribu kuutambua mwili huo, uliokutwa kaskazini mwa jiji la Lille, ambao unadhaniwa kuwa ni wa mtu mzima aliyekuwa mmiliki wa nyumba hiyo.
Mwanaume huyo alikuwa akiishi mwenyewe na inaonekana hakuwa na ndugu. Mamlaka husika zimekuta lundo la barua ambazo hazijafunguliwa za tangu mwaka 1996 ndani ya nyumba hiyo.
Alikuwa na asili ya Hispania na kwamba alizaliwa mwaka 1921, kwa mujibu wa ripoti za Ufaransa.
"Mazingira ya nyumbani hapo yanaashiria kwamba kilikuwa kifo cha kawaida cha mtu aliyefia kwenye kitanda chake," ofisa wa usalama wa raia Didier Perroudon alisema.
Aliongeza kwamba hakuna ripoti zozote zilizotolewa hapo kabla kuhusu kupotea kwa mtu huyo, na kueleza: "Alikuwa kitandani kwake, akiwa kavalia nguo zake za kulalia."
Didier alisema: "Hakukuwa na chochote, Nyumba ilikuwa imefungwa kwa nje. Hakuna kinachoashiria kitendo chochote cha jinai."
Mwili wa mtu huyo ambaye hakufahamika uliondolewa mahali hapo kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi zaidi.
Alikutwa amekufa Ijumaa iliyopita wakati wakaguzi wa afya wanaofanya kazi hiyo kwa niaba ya jiji hilo kutembelea nyumba hiyo.
Didier aliongeza: "Kwa sasa, hatufahamu zaidi.
"Uchunguzi umeanza. Itachukua muda kugundua mahali anakotokea, alikuwa akifanya nini na waliko jamaa zake."

ZIRO PLUS...


BOBBY BROWN AKAMATWA TENA AKIENDESHA GARI HUKU KALEWA...

Bobby Brown.
Bobby Brown amekamatwa kwa kosa la kuendesha gari huku akiwa amelewa chakari hii ikiwa ni mara yake ya pili mwaka huu, imefahamika.
Vyanzo vya habari vimeeleza, Bobby alikamatwa majira ya Saa 7 usiku wa manane baada ya polisi kugundua mwimbaji huyo akiendesha gari visivyo katika mitaa ya jiji la Los Angeles.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, maofisa wa polisi walilifuata gari la Bobby na kukuta pombe kali na hivyo kumwamuru ashuke kutoka katika gari lake.
Imeelezwa Bobby alifanyiwa jaribio la kupima kilevi, lakini hakufanikiwa kunasuka kutoka katika mikono ya polisi, hivyokushitakiwa kwa kuendesha gari huku akiwa kalewa.
Bobby hapo kabla alikamatwa kwa kosa kama hilo Machi, mwaka huu na kujiunga na tiba maalumu ya kuacha pombe na vurugu zinazohusiana na ulevi. Pia amekuwa na rekodi ya kuhusika na makosa kama hayo tangu mwaka 1996.

JICHO LA TATU...


Wednesday, October 24, 2012

SIKU NAIBU WAZIRI 'ALIPOWAKOROGA VICHWA' WATANZANIA...


Hii kwakweli ni zaidi ya kuboronga. Sijui tuiite vipi. Msikilize Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo kisha ututumie maoni yako. Bofya COMMENTS hapo chini kisha tujuze unachofikiria.

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU KUUNDWA UPYA...


Serikali imesema inatarajia kuunda upya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) ili ijiendeshe yenyewe na kupunguza utegemezi wa Serikali na kuwezesha kurejesha Sh trilioni 1.1 zilizokopwa na wanafunzi. 
Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, hivi sasa Bodi hiyo inapata asilimia 75.5 ya bajeti yote ya wizara hiyo huku asilimia 25.5 pekee ikibaki wizarani.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Celestine Gesimba aliyasema hayo jana alipo kuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotaka ufafanuzi kuhusu utegemezi wa Bodi hiyo kwa Serikali utakwisha lini.
Hoja ya wajumbe wa kamati hiyo, iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Cheyo, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP) ilitokana na utegemezi wa asilimia 75.5 kwa bajeti ya Serikali na namna ya kulipa madeni kwa wanafunzi waliokopa.
Akifafanua kuhusu hoja hizo na kiasi cha deni lililopo mpaka sasa na kilicholipwa baada ya ripoti ya CAG kuonesha upungufu, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Onesmas Laizer alisema mpaka Juni Bodi imekopesha Sh trilioni 1.087.
“Hata hivyo, Bodi ina miaka saba sasa tangu ianzishwe na kabla haijaanza bodi, serikali ilishakopesha wanafunzi Sh bilioni 51.1, jumla ni Sh trilioni 1.138 zilizokopwa. Mikopo iliyoiva tayari kurejeshwa ni Sh bilioni 160.7,” alieleza Laizer.
Hata hivyo, alisema kati ya hizo Sh bilioni 160.7 ambazo marejesho hufanywa kwa awamu, fedha zilizopaswa kuwa zimerejeshwa ni Sh bilioni 39.54 lakini mpaka Juni wameshakusanya Sh bilioni 20.15 pekee huku Sh bilioni 19 zikiwa mikononi mwa wakopaji.
Cheyo alihoji kwa nini Bodi iendelee kiutendaji wa namna hiyo na kueleza kuwa tatizo la wizara na Bodi ni mfumo wa kumbukumbu (Data Base) na upungufu wa vyanzo mbadala vya mapato, unaorudisha nyuma ubora wa elimu nchini.
Akifafanua hilo, Kaimu Katibu Gesimba alikiri kuwepo kwa tatizo kubwa katika utegemezi wa Bodi na kueleza kamati kuwa tayari Waziri mwenye dhamana aliliona hilo na aliunda timu kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha vyanzo vya mapato vya Bodi.
“Ni kweli tatizo lipo, asilimia 75.5 ya bajeti inakwenda Bodi lakini siku zinavyokwenda na mahitaji ya mikopo kwa wanafunzi yanaongezeka, ila tayari mapendekezo ya awali yanaonesha kuwa Bodi itaundwa upya ili kupata vyanzo vya mapato, utendaji na kuongeza ufanisi,” alisema Gesimba.
Ingawa hakusema timu itafanya kazi lini, Gesimba aliwambia waandishi wa habari nje ya kikao kuwa, tayari mapendekezo ya awali ya timu yamemfikia Waziri na yanachambuliwa ili kufikisha serikalini, na Serikali ikibariki, maboresho yatafanyika.

KAPTENI WA JWTZ AFA KATIKA AJALI YA NDEGE...


Rubani mwanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kapteni Deo Mangushi amekufa huku mwenzake Kapteni F. Kwidika akijeruhiwa wakati wakijiokoa katika ajali ya ndege waliyokuwa wakiitumia kufanya mazoezi ya mafunzo.
Marubani hao wanafunzi walikuwa katika mafunzo na ndege hiyo na walipoona hatari, walitumia mfumo wa kujiokoa wa ndege hiyo wa kurushwa angani wakiwa na viti umbali wa meta 100 kwa kasi ya risasi kutoka ndege hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema ajali hiyo ilitokea saa 4.25 asubuhi katika Kikosi cha Anga cha Airwing, Ukonga  ndege hiyo ikiwa imeruka meta 100  kutoka ardhini.
Alifafanua kuwa waliporushwa angani, wakati wa kutua, Kapteni Kwidika parachuti lake lilifunguka na kujaa upepo akashuka ardhini salama, lakini Kapteni Mangushi la kwake halikufunguka vizuri ndipo alipojibamiza kwenye paa la hanga (karakana ya ndege) na kufa papo hapo.
Hata hivyo,  pamoja na Kapteni Kwidika kutua na parachuti, alijeruhiwa na amelazwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam ambako hali yake ya afya inaendelea vizuri. 
Mgawe alisema ndege iliyopata ajali imeharibika kiasi kwenye bawa na eneo linaloonesha kasi ya ndege, lakini inaweza kutengenezeka na taarifa zaidi wanatarajia kuzipata kutoka kwa Kapteni Kwidika mara akipata nafuu.

HANDAKI LA AJABU LA WAKOLONI LAGUNDULIKA MKOANI IRINGA...



Mamia ya wakazi wa mjini Iringa wakiwa wamekusanyika eneo la Kitanzini kushuhudia handaki hilo (kulia).
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba handaki linaloaminika kutumiwa na Wakoloni wa Kijerumani limegunduliwa jana katika eneo la Kitanzini, mkoani Iringa kwenye Mtaa wa Sokoni na kuibua gumzo kubwa na hofu miongoni mwa wakazi wa mkoa huo.
Kugundulika kwa handaki hilo linalokadiriwa kufikia ukubwa wa futi 6 kwa 6, kumekuja wakati wafanyakazi wa Kampuni ya JR wanaoshugulika na uboreshaji wa miundombinu ya maji mjini humo wakiendelea na kazi ya uchimbaji mitaro kwa ajili ya kusimika mabomba mapya ya maji safi.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, mmoja wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Abdukareem, amesema kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa hizo alifika akiwa na mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Salehe na kukubaliana kuingia ndani ili kujionea wenyewe kwa macho.
Amesema kutokana na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa kwani ngazi hiyo ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi na kamba na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani.
Aliendelea kusema kwamba walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama futi tatu na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa zege na kubainisha kulikuwa na vyumba vingine zaidi ambavyo hawakuweza kuingia kutokana na kuwa vimezibwa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk Leticia Warioba alifika katika eneo la tukio huku akiwa ameongozana na wafanyakazi wa  Kampuni ya JR pamoja na Ofisa wa Usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo kwa nje bila kuingia ndani ya handaki hilo.
Inadhaniwa kwamba mahandaki hayo yalikuwa yakitumiwa enzi za ukoloni wa Wajerumani, na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kugundulika mahandaki zaidi katika siku za usoni kwenye maeneo mbalimbali mkoani humo.

WANAWAKE WANUSURIKA KIFO KWA KUNASA CHINI YA BOTI MASAA MANNE...

Wanawake wawili wa Uingereza wamestahimili masaa manne ya kutisha wakiwa wamenasa chini ya boti ya kitalii baada ya kupinduka kwenye maji yaliyojaa papa karibu na Cape Town.
Lynette Hartman mwenye miaka 55, na Bronwyn Armstrong walinasa chini ya moja ya maganda mawili na wakisaidiwa na mifuko ya kupumulia ya hewa.
Watalii mwenzao Peter Hyett mwenye miaka 64 wa Vale of Glamorgan, huko Wales ya kusini, alikufa baada ya boti ndogo, ambayo ilikuwa imebeba watu 40 kupinduka majira ya Saa 8 mchana Jumamosi.
Wanawake hao wawili wa Uingereza walikutwa wakiwa wamening'inia pembeni ya boti hiyo wakati wazamiaji wakitafuta miili na waokoaji waliwasiliana kwa kunasa maganda hayo.
Huku joto la bahari likiwa chini ya nyuzijoto 10, isingekuwa rahisi kwao kuweza kuendelea kuwa hai kwa muda wa saa moja zaidi kama wangekuwa kwenye maji ya wazi.
Wazamiaji wa polisi waliwapatia vifaa vya kuwasaidia kupumua kabla ya kuwashawishi wavue majaketi yao ya kujiokolea hivyo kuweza kuogelea na kujinasua kwenye kina cha futi 36.
Craig Lambinon, kutoka Taasisi ya Taifa ya Bahari na Ukoaji, alisema abiria karibu wote waliokolewa kwa kutumia boti ndogo zilizokuwa maeneo ya jirani.
Lakini alisema wanawake hao wawili 'walikuwa wamenaswa wakati boti yao ilipopinduka na kupata mfuko wa hewa uliowasaidia kuweza kupumua', alisema Craig.
"Walikuwa wameganda kwa ubaridi huku wakiwa wamevalia majaketi yao ya kujiokolea na nguo zao za kawaida tu.
"Waokoaji walifanikiwa kuwakuta lakini walikuwa wamejawa hofu mno na ilichukua muda mrefu kuweza kuwashawishi wavue majaketi yao na kuogelea kutoka eneo hilo.
"Wanawake hao walilazimika kupewa mafunzo ya kutumia vifaa vya kusaidia kupumua na hatimaye waliweza kuokolewa majira ya Saa 11:50 jioni."
Hyett aliopolewa na kupelekwa ufukweni, ambako ilitangazwa baadaye kwamba amefariki dunia.
Mke wa Mwingereza huyo aliyekufa Suzanne, mwenye miaka 63 na binti yake Helen mwenye miaka 37 wakazi wa Bournemouth, walinusurika katika ajali hiyo na walikuwa wakiendelea na matibabu hospitalini.

JICHO LA TATU...


ABAMIZA GARI LAKE LA PAUNI 75,000 KWENYE BASI NA KUFA PAPO HAPO...

Hali ilivyokuwa muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea.
Mtu mmoja amekufa baada ya gari lake la michezo lenye thamani ya Pauni za Uingereza 75,000 alilokuwa akiendesha kujibamiza kwenye basi.
Kifusi kilisambaa barabarani baada ya gari aina ya Audi R8 nyeupe kugongana uso kwa uso na basi la Arriva mjini Newcastle juzi usiku.
Dereva huyo mwenye miaka 39 alilazimika kutolewa kwa kukatwa sehemu ya gari lake na wafanyakazi wa dharura, lakini alithibitika kufa katika eneo la tukio. Dereva wa basi hilo mwenye miaka 61, alikimbizwa hospitali kufuatia kupata majeraha madogo.
Hakukuwa na abiria kwenye basi hilo wakati ilipotokea ajali hiyo karibu na Mtaa wa Gosforth High.
Wageni waliopanga katika hoteli ya jirani ya Gosforth waliokuwa wakirejea kutoka kwenye baa walishuhudia ajali hiyo mbaya, alisema Mfanyakazi wa Hoteli ya Gosforth.
"Tulikuwa na wateja kadhaa ndani ambao walikuwa wanakunywa kwenye baa nyingine na kushuhudia ajali hiyo. Walisema dereva alitolewa baada ya kukatwa sehemu ya gari lake lakini madaktari hawakuwa na la kufanya zaidi kuokoa maisha yake," alisema mfanyakazi wa kike.
Tony Batty, Mkuu wa Huduma wa Arriva alisema: "Tunazo taarifa za tukio hilo kati ya gari dogo na basi la Arriva huko Mtaa wa Gosforth High.
"Dereva wa gari dogo alifariki. Tunazipa pole familia za dereva wa basi na dereva wa gari dogo. Tukio limehusisha basi ambalo halikuwa kwenye huduma na dereva amepelekwa hospitali kwa matibabu."
Polisi wa Northumbria walithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya Saa 3:00 usiku wa Jumapili pale magari mawili yaliyokuwa yakisafiri kutumia njia moja, ambapo yalisababisha barabara hiyo kufungwa kwa  kwa masaa matano.

CHEKA TARATIBU...

Mlokole mmoja kakutana na Mlevi njiani na kuanza kumsema, "Hivi wewe ndugu yangu unamjua Mungu na Yesu?" Kwa kujiamini huku akiyumba Mlevi akajibu, "Mie mwenyewe mgeni mitaa hii, labda ulizia mtaa wa pili umaweza kuwapata wote wawili!" Duh...

KWA WANAOJUA KIMOMBO! MDAHALO WA URAIS MAREKANI...

Tuesday, October 23, 2012

JICHO LA TATU...


WAWAKILISHI WAIKATAA RIPOTI YA UBADHIRIFU SERIKALINI...

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika moja ya vikao vyao, mjini Unguja.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekataa taarifa iliyotolewa na Serikali kuhusu Kamati teule ya Baraza hilo ya kuchunguza matukio mbalimbali ukiwamo ubadhirifu wa mali za Serikali.
Wakichangia ripoti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud jana, wawakilishi walisema ripoti hiyo imeshindwa kugusa na kuwatia hatiani watendaji waliohusika na ubadhirifu na ufujaji wa mali za umma.
Mwakilishi wa Wawi, Saleh Nassor Juma (CUF) akichangia alisema anaikataa ripoti hiyo kwa sababu imekwepa watendaji waliotajwa na ripoti wakihusika na ubadhirifu wa mali za umma wakiwamo wengine kujigeuza madalali wa mali za Serikali.
“Sikubaliani na taarifa ya Serikali kuhusu ripoti ya ubadhirifu wa mali za umma ... ripoti hii haikutia hatiani wahusika wakiwamo watendaji wa Serikali kama mawaziri na makatibu wakuu,” alisema Juma.
Mwakilishi wa Chaani, Jecha Ussi Simai (CCM), alisema anapinga taarifa ya Serikali ambayo haikutia hatiani watendaji wa Serikali wanaojishughulisha na ubadhirifu.
“Mimi nikiwa Mwakilishi pamoja na wananchi wa Chaani tunaikataa ripoti hii kwa sababu inalinda watendaji wa Serikali waliohusika moja kwa moja na ubadhirifu,” alisema Simai ambaye kitaaluma ni mwanasheria.
Mwakilishi wa Viti Maalumu Wanawake, Mwanajuma Faki Mdachi (CUF), alisema Serikali imeidharau ripoti ya Kamati Teule na kusema hakuna makosa yaliyofanywa kwa watendaji wake, kitendo ambacho kinalidhalilisha Baraza la Wawakilishi na kuonekana kuwa waongo.
“Mimi napinga taarifa ya Serikali kuhusu Kamati Teule ambayo inaonesha kwamba hakuna ubadhirifu uliofanywa na watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),” alisema.
Mwakilishi wa Konde, Suleiman Hemed Khamis (CUF), alisema hivi karibuni Serikali iliunda Tume ya kupambana na rushwa ikiwa na lengo la kudhibiti tatizo hilo, lakini haoni kama kutakuwa na mafanikio katika mapambano hayo kutokana na tabia ya kuoneana chuki katika utekelezaji wa vita dhidi ya vitendo vya ubadhirifu.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi 24 walichangia taarifa ya Serikali kuhusu ripoti ya Kamati Teule ya kuhusu ubadhirifu na tuhuma za watendaji wa Serikali na wote kuikataa ripoti hiyo.
Agosti 9 mwaka jana, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho alikubaliana na uamuzi wa wajumbe wa Baraza kuunda Kamati kuchunguza vitendo vya ubadhirifu serikalini katika taasisi mbalimbali kwa watendaji wake, baada ya wajumbe kuonesha wasiwasi mkubwa.
Ripoti iliyosomwa na Waziri Aboud iliwasafisha kwa kutowahusisha na makosa yoyote aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi katika awamu iliyopita, Machano Othman Said na tuhuma mbalimbali ikiwamo kuuza viwanja vya Serikali.
Machano ambaye kwa sasa ni Waziri wa Nchi asiye na Wizara Maalumu na pia Mwakilishi wa Chumbuni, alihusishwa na tuhuma katika wizara hiyo pamoja na Katibu Mkuu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya Serikali inayotokana na ripoti ya Baraza la Wawakilishi, Aboud alikiri kuwapo ukiukwaji wa taratibu za kazi na utumishi ambapo baadhi ya wakurugenzi wamekuwa wakiunda kampuni zao binafsi katika sehemu za kazi na kufanya biashara.
“Taarifa ya Serikali imegundua kuwapo wakurugenzi wanaofanya biashara katika sehemu za kazi na kutaka wachague moja.,” alisema Aboud na kuongeza:
“Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga, Said Iddi Ndobugani anayemiliki kampuni ya Aero Tech, Serikali inamtaka ajiondoe kama anataka kubaki kuendelea na wadhifa wa ukurugenzi serikalini.”

MWAKYEMBE ASHUGHULIKIA RIPOTI YA BANDARI 'NENO KWA NENO'...

Dk. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema anaipitia kwa umakini ripoti ya chanzo cha kutofanya vizuri kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na atakuwa akitoa msimamo wake kuhusu maagizo ya ripoti hiyo kila wiki.
Dk Mwakyembe alikabidhiwa matokeo ya uchunguzi huo na Mwenyekiti wa Kamati maalumu aliyoiunda mwishoni mwa Agosti, Bernard Mbakileki juzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea ripoti hiyo juzi, alisema kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, wataisoma mstari kwa mstari na kuyafanyia kazi mapendekezo ya kamati hiyo kuhusu utendaji wa bandari.
“Kama mnavyoiona ripoti hii ni kubwa hii inaonesha kuwa kazi iliyofanyika pia ni kubwa, sasa sisi tunachowaahidi ni kuipitia mstari kwa mstari hakuna kitu tutakachokiacha na tutawataarifu wananchi kila wiki hatua tulizochukua kuhusu maagizo ya ripoti hii,” alisema Dk Mwakyembe.
Kuhusu waliokwepa kuhojiwa na kamati hiyo kwa visingizio mbalimbali, Waziri huyo alisema kamwe hawawezi kuepuka kwa kuwa sasa watahojiwa mbele yake na kama polisi itahusika watahojiwa pia Polisi.
Awali Mbakileki wakati akiwasilisha ripoti, pamoja na kukamilisha kazi ya uchunguzi, alisema walikabiliwa na matatizo ya hujuma kutoka kwa baadhi ya watu waliostahili kuhojiwa, lakini walikwepa kwa visingizio mbalimbali bila kuwataja majina watu hao.
Hata hivyo, Dk Mwakyembe hakutaka kuwataja pia majina watu hao wanaotajwa kukwepa kuhojiwa wakisingizia misiba, kuugua na wengine kuzima simu zao zaidi ya kuihakikishia kamati hiyo lazima watahojiwa mbele yake na mbele ya polisi pale itakapowezekana.

KIKWETE AKIRI RUSHWA INAIPELEKA CCM 'KUZIMU'...

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya  Kikwete amesema vitendo vya rushwa na ununuaji kura vinavyoendelea katika kutafuta uongozi ndani ya chama hicho visipodhibitiwa vitakipeleka pabaya.
Akifunga Mkutano wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) juzi mjini hapa, Rais Kikwete alifafanua kuwa vitendo hivyo vitaendelea kuleta makundi ndani ya CCM ambayo yatakifikisha pabaya.
Huku akionesha kusikitishwa na vitendo vya rushwa kwa wanawake ambao wamekuwa wakitumia fedha kununua uongozi ndani ya CCM na hata jumuiya zake, Rais Kikwete alitaka viongozi waliochaguliwa kufanya jitihada za kupunguza mgawanyiko uliotokea baada ya uchaguzi huo.
“Ninasikitika sana kusikia hata wanawake sasa wanajihusisha na utoaji rushwa ili kununua nafasi za uongozi, kitu ambacho ni hatari sana,” alisema Rais Kiwete na kusisitiza kuwa chama kinakoelekea si kuzuri na ni lazima zifanyike jitihada za mabadiliko. 
Katika kupunguza mgawanyiko uliotokea baada ya uchaguzi, Rais Kikwete alitaka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi UWT walioshindwa wasiweke visasi na walioshinda kutowapiga vijembe walioshindwa na kuwakumbusha kuwa kazi iliyo mbele yao ni kubwa, kwa kuwa CCM hivi sasa inakabiliwa na hali ngumu ya ushindani wa kisiasa.
Alisema demokrasia ya uchaguzi ina athari zake, kwani baada ya uchaguzi kumalizika kuna kazi kubwa ya kujenga umoja na mshikamano ambao kazi ya kwanza ni kuziba nyufa na mipasuko iliyotokea wakati wa uchaguzi
“Ukomavu wa kisiasa na ustahmilivu unahitajika sana. Jambo la kufahamu ni kwamba kugombea ni haki ya mwanachama na pia kila mwanachama ambaye ni mjumbe ana haki ya kumuunga mkono mjumbe anayemwona anafaa.
“Mnaweza kuchukiana kwa mtu kugombea, kwa nini kagombea nafasi yangu, Katiba inasema utakuwa kiongozi miaka mitano nafasi yako ilishakwisha, sasa unaomba upya,” alisema.
Alisema mwanachama hapaswi kumchukia mwenzake kwa vile ameomba nafasi anayoitaka wakati nafasi hiyo ni haki ya kila mwanachama. Pia alitaka walioshinda au kushindwa  wasichukie ambao hawakuwaunga mkono. 
“Ukimchukia mtu aliyetumia haki ya demokrasia kugombea au asiyekuunga mkono utakuwa umeonesha udhaifu wa hali ya juu sana, utakuwa hujiamini, utakuwa kiongozi ambaye daima utaongoza kwa makundi … hawa wangu, hawa si wangu, hakuna mtu wa binafsi, wote ni wa chama”,
“… lazima wote wapewe fursa ya kutumikia jumuiya kwa uwezo wao, sifa yao isiwe hakuniunga mkono, mkifanya hivyo mtaua jumuiya,” alionya.
Alisema uchaguzi una mifarakano lakini kiongozi akipatikana ni lazima aungwe mkono na wa kuonesha mfano ni wale walioshinda, hawapaswi kuwabeza walioshindwa kwa kuwaambia kiko wapi.
Rais Kikwete alisema madhumuni ya CCM yaliyotamkwa katika Katiba ya Chama hicho ni kushinda uchaguzi wa Serikali Kuu na serikali za mitaa, Tanzania Bara na Zanzibar ili kuunda Serikali Kuu na  za mitaa.
“Madhumuni ya msingi ya kuundwa kwa CCM ni kushinda uchaguzi, sisi si chama cha mpira, riadha,  ama utamaduni sisi ni chama cha siasa kazi yetu ni kukamata Dola, tunataka Serikali ya Mtaa na Kijiji iwe CCM na halmashauri iwe mikononi mwa CCM, wabunge na serikali zote mbili ziwe za
CCM,” alisema.
Rais Kikwete alisema Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ya vyama vingi, inapozungumziwa kushinda Dola ni kushinda uchaguzi na maana yake ni kupigiwa kura nyingi kuliko wenzao.
Alisema ushindi wa CCM unapatikana kwa kukubaliwa na kuungwa mkono na wananchi wengi zaidi watakaojitokeza kupiga kura na jumuiya za chama zimeundwa kwa ajili ya kusaidia CCM na kila jumuiya ina kazi zake.
“Kwa vile mmemaliza uchaguzi, jipangeni sawa sawa ili mtimize wajibu wenu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama,” alisema.
Aliwapongeza kwa kukamilisha uchaguzi wa viongozi watakaoongoza Jumuiya hiyo kwa miaka mitano na hata waliojitokeza kugombea, kwani kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi … uchaguzi si kazi ndogo kuna mambo mengi husemwa.
Aliwataka kushughulikia masuala ya uchumi ya kinamama na si kuhuburi tu maneno ya CCM bila kuwa na msaada wowote.
Awali Mwenyekiti wa UWT, Sofia Simba alisema  wamefanya mengi ikiwamo kuongeza wanachama na wamejipanga kuhakikisha wanaleta ushindi katika uchaguzi mkuu 2015.
Alisema UWT imepiga hatua kubwa na kufanikiwa kupata hatimiliki ya viwanja na mashamba ambayo ni mali ya jumuiya. Alimshukuru Rais Kikwete kwa kutambua uwezo wa wanawake tangu alipoingia madarakani ambapo viongozi wanawake wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka.
Simba alisema hata katika CCM hivyo hivyo idadi ya wanawake katika uongozi imekuwa ikiongezeka na ameendelea kulea Jumuiya hiyo na sasa wamefanikiwa kupata magari matano makao makuu na pikipiki kwa kila wilaya.
Licha ya kuwapa vitendea kazi kwa nyakati tofauti, Simba alisema Rais Kikwete pia amekuwa akitoa msaada wa hali na mali jambo linalochangia mafanikio yao.
Katika uchaguzi uliomalizika juzi UWT, Simba alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UWT kwa mara nyingine baada ya kupata kura 715 na kumshinda Anne Kilango-Malecela  aliyepata kura 310 na May Rose Majinge aliyepata kura saba.
Akitangaza matokeo hayo Jumamosi saa 7 usiku, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Abdul-rahman Kinana, alitaja walioshinda kuwa wajumbe wa Baraza Kuu la UWT na kura zao kwenye mabano kuwa ni  Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene (610), Pindi Chana (734), Diana Chilolo (555), Zainab Kawawa (580) na  Betty Machangu (516).
Wengine ni Mbunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa (600) Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Mary Mwanjelwa (517), Shamsa Mwangunga (606) na Subira Mgalu (603).
Aliyechaguliwa Makamu Mwenyekiti wa umoja huo ni Asha Bakari Makame (559) na kumshinda mshindani wake  Asha Abdalah  Juma (403).
Kwa upande wa viti sita vya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM ni Panya Alli  Abdallah (472), Fatma Said Ally (580), Maulide Castico (614), Mbunge wa Koani, Amina Andrew Clement (456), Waride Bakari Jabu (416), na Tauhida Cassian Nyimbo (620).
Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT ni  Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Halima Dendegu (585),
Juliana Manyerere (548), Amina Masenza ( 441), Mbungwa wa Nkenge, Assumpter Mshama (442) na Shamsa Mwangunga (488).
Wengine kutoka Zanzibar ni Mwanajuma Majid Abdallah (433), Khadija Hassan Aboud (442),  Elizabeth Lazaro Mayala (419),  Catherine Peter Nao (666) na Zainab Hamis Shomari (486).
Uwakilishi UVCCM Taifa ni Esther Mambali (682) uwakilishi Wazazi ni Namelok Sokoine (740) aliyemwangusha Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata.

KINARA WA KUNDI UAMSHO ZANZIBAR APANDISHWA KIZIMBANI...

Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Shekhe Farid Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana kusomewa mashitaka yanayomkabili ikiwemo kusababisha vurugu na uchochezi.
Baada ya uvumi wa kutoweka na kusababisha ghasia visiwani hapa na kisha kuonekana, jana kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu(JUMIKI) maarufu kama Uamsho, Shekhe Farid Hadi Ahmed na wenzake saba walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za uchochezi na kusababisha fujo.
Hata hivyo, Mahakama ya Mwanakwerekwe ilikataa kutoa dhamana kwa viongozi hao hadi keshokutwa shauri lao litakaposikilizwa katika mahakama hiyo, kwa madai kwamba uchunguzi zaidi unahitajika katika matukio hayo.
Shekhe Farid na viongozi hao saba, walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mjini saa nne asubuhi katika msafara wa magari sita ya Polisi.
Wengine waliofikishwa katika Mahakama ya Mwanakwerekwe ni  kiongozi mwandamizi wa Uamsho, Shekhe Azan Khalid Hamdani (43), Mussa Juma Issa (37), Suleiman Juma (50), Hassan Bakari Suleiman (39), Mselem Ali Mselem (52) na Khamis S. Khamis.
Akisoma mashitaka yanayowakabili washitakiwa hao, Mwendesha Mashitaka wa Serikali Mohamed Ame, alidai washitakiwa hao walikwenda kinyume na kifungu 45(a) na (b) cha Sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar namba 6 ya mwaka 2004.
Akifafanua, Ame alidai Agosti 17 saa 11 jioni Magogoni mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, washitakiwa hao wakiongoza Jumuiya ya Uamsho walitoa matamko ya uchochezi yanayoashiria uvunjifu wa amani na kusababisha fujo na mtafaruku kwa Serikali katika sehemu ya mihadhara yao.
Wakili wa Washitakiwa, Abdalla Juma aliomba Hakimu kuwapa hati ya mashitaka na dhamana  washitakiwa hao, kitendo ambacho kilipingwa na Wakili wa Serikali.
Awali Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ame Msaraka Pinja alisema baada ya kupitia hoja za kila upande,  Mahakama iliona isikurupuke kutoa dhamana ili kulifanyia kazi zaidi shauri hilo.
“Mahakama imepitia maombi yote mawili kutoka kwa upande wa mashitaka na Wakili wa washitakiwa na kuona isikurupuke na ni bora kulifanyia uchunguzi zaidi shauri la dhamana,” alisema Msaraka.
Kabla ya hapo, wafuasi wa Uamsho walijazana katika eneo la mahakama hiyo ambapo ulinzi uliimarishwa katika maeneo mbalimbali ikiwamo jirani na jengo hilo.
Aidha, ulinzi uliimarishwa pia katika maeneo na barabara zinazokwenda na kuingia katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe kwa ajili ya kudhibiti fujo za wafuasi wa Uamsho.
Hali ya usalama katika mji wa Unguja na maeneo mengine ya mitaa kwa sasa ni shwari huku vikosi vya SMZ vikifanya doria na kutawanya makundi mbalimbali ya vijana.
Shekhe Farid  alitoweka ghafla wiki iliyopita na kudaiwa na wafuasi wake kuwa alikuwa ametekwa na vyombo vya usalama jambo lililosababisha vurugu.
Katika vurugu hizo za Zanzibar, maskani mbili za CCM za Kisonge na Mwembeladu zilichomwa moto na pia baadhi ya wafuasi wa Uamsho kudaiwa kumwua Koplo Said Abdul-rahman wa Polisi kwa kumkata mapanga.
Wakati hali ikiwa hivyo  na kusababisha Polisi kuongeza ulinzi Zanzibar, Shekhe Farid  aliibuka ghafla na kudai kuwa alikuwa ameshikiliwa na watu wasiojulikana ambao walikuwa wakimhoji kuhusu harakati za jumuiya hiyo lakini hawakumdhuru.
Hata hivyo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havikuwa vimemshikilia Shekhe Farid, alisema walilazimika kumkamata na viongozi wenzake  ili kufahamu wapi alikuwa na kuthibitisha kama kweli alitekwa au la kabla ya kumfikisha mahakamani jana.

CHEKA TARATIBU...

Wabwia dawa za kulevya aka 'mateja' wawili wamekaa kichochoroni wakivuta 'unga'. Mara ndege ikapita angani na Teja moja likasema, "Ile ndege lazima itakuwa imembeba Rais." Mwenzake akajibu kwa kujiamini, "Hapana imebeba Wazungu. Kama ile ingekuwa imembeba Rais lazima ungeona pikipiki mbele!" Balaa...