Wednesday, March 4, 2015

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATANO

Kama kawaida tunakuletea muonekano wa habari zilizomo kwenye magazeti ya leo Jumatano Machi 4, 2015. Kusoma vichwa vya habari kwenye kurasa za mbele na nyuma za magazeti hayo bofya kwenye picha hapo kushoto. Kupata yaliyoandikwa kwenye magazeti usikose kuperuzi blogu hii kila siku.

Tuesday, March 3, 2015

MAMBO MAGUMU KWA NGELEJA BARAZA LA MAADILI YA VIONGOZI


Mbunge wa Sengerema,  William Ngeleja amekiri mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kwamba, aliomba na kupokea Sh milioni 40.4 kutoka kwa James Rugemalira, kwa kujitetea alifanya hivyo kama ilivyo kawaida pia kwa wabunge wengine.

MAPACHA WALIOUNGANA KUINGIA KIDATO CHA TANO


Mapacha  walioungana kiwiliwili, Consolata na Maria Mwakikuti (18), wa Kijiji cha Ikonda wilayani Makete mkoani Njombe, wamefaulu mtihani wao wa kuhitimu kidato cha nne kwa alama sawa isipokuwa masomo mawili. 

RAIS KIKWETE AMWAGA CHOZI MAZIKO YA KAPTENI KOMBA


Rais Jakaya Kikwete jana alishindwa kujizuia kutoa machozi, wakati mwili wa Mbunge wa Mbinga Magharibi wilaya ya Nyasa mkoa wa  Ruvuma,  Kapteni John Komba ukishushwa kaburini,  kwenye maziko  yaliyofanyika kijijini  Lituhi.

BEI YA MAFUTA YAENDELEA KUPOROMOKA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kuendelea kushuka kwa bei ya mafuta bei ambazo zinaanza kutumika Jumatano hii.

TMA YATAHADHARISHA UKAME MWAKA HUU

Hali ya ukame inatarajiwa kukabili nchi kutokana na upungufu wa mvua utakaoathiri pia upatikanaji wa nishati ya umeme.

MBARONI KWA KUUA WAZEE WATATU KWA MADAI WANAZUIA MVUA

Watu wanne akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihanda na wazee wawili wa kimila wa kijiji  hicho wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusu kuuawa kwa  wazee wawili mtu na mkewe.

MAITI WATATU WENYE MAJERAHA WATELEKEZWA MJOHORONI


Watu watatu  wanaume wasiofahamika, wamekutwa wamekufa na kutelekezwa maeneo ya Mjohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, huku miili yao ikionesha majeraha maeneo tofauti pamoja na kuvuja damu nyingi puani.

WATANO KORTINI KWA KUMDHALILISHA ASKARI POLISI


Wafanyabiashara watatu na wanachuo watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  Singida wakikabiliwa na mashitaka ya kumdhalilisha kupindukia askari polisi wa kike  na kumsababishia maumivu makali mwilini.

SHERIA YATUNGWA KUDHIBITI OMBAOMBA

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam inakusudia kutunga sheria kadhaa ndogo, ikiwemo ya kudhibiti ombaomba na uendeshaji wa soko la samaki Feri.

SERIKALI YASITISHA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI UWANJA WA TAIFA

Serikali imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.

AZAM FC YAMALIZANA NA MAKOCHA WAKE

Uongozi wa Azam FC umesema umemalizana na makocha wake Joseph Omog (pichani) na Ibrahim Shikanda na wako huru kuondoka muda wowote kwani hawana wanachodai.

10 WAYS PATRICE LUMUMBA PAID FOR HIS BELIEFS


Patrice Lumumba was the first prime minister of the Republic of Congo and is credited with making great strides to free the region from Belgian colonization. Many of his tactics were questioned and some say he caused unrest in the Congo. Lumumba endured criticism, several arrests and torture. Here are 10 ways Patrice Lumumba paid for his beliefs.

12 CLUBS THAT COULD WIN THE 2015 CAF CHAMPIONS LEAGUE


In two weeks, the First Round of the 2015 CAF Champions League will be played. Thirty-two teams from all around Africa will take part, and we at AFKSports have compiled a slideshow of 12 teams we believe can lift the cup later on in the year.

10 BREAKFAST FOODS THAT BOOST YOUR METABOLISM ALL DAY


We all love to blame our weight on a slow metabolism, and want to boost ours, but what is metabolism anyway? Metabolism is the process by which your body converts what you eat and drink into energy. Metabolism influences your energy needs, but it isn’t really the culprit in weight gain. One way to make your metabolism work for you is to start at the beginning of the day. Here are 10 breakfast foods that boost your metabolism all day.

12 THINGS ISABEL DOS SANTOS HAS THAT YOU DO NOT


Let’s start by listing the one thing she has and that you will never have, which has allowed her to have everything else on this list. Isabel dos Santos is the daughter of a president, the first known female billionaire on the African continent, and she has a lifetime membership in the so-called cryptocracy, or shadow government, where real economic-political power resides. She can have anything she wants — even if she professes to have a humble lifestyle. Here are 12 things Isabel dos Santos has that you do not, bearing in mind that best things in life are usually not even things.

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU

Kama kawaida tunakuletea muonekano wa habari zilizomo kwenye magazeti ya leo Jumatatu Machi 3, 2015. Kusoma vichwa vya habari kwenye kurasa za mbele na nyuma za magazeti hayo bofya kwenye picha hapo kushoto. Kupata yaliyoandikwa kwenye magazeti usikose kuperuzi blogu hii kila siku.

NAMIBIAN PRESIDENT WINS $5M MO IBRAHIM AFRICAN LEADERSHIP PRIZE



Outgoing Namibian President Hifikepunye Pohamba has won the Mo Ibrahim Foundation’s $5 million African leadership prize, an award that recognizes good governance and has been given just five times in eight years, Reuters reports.

VILIO, SIMANZI VYATAWALA MAZISHI YA KAPTENI KOMBA



Rais  Jakaya Kikwete jana ameongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kuaga mwili wa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba aliyefariki Jumamosi jioni katika Hospitali ya TMJ ikielezwa kuwa  kaondoka kama moto wa kiberiti.

WAUAJI WA ALBINO SASA WATANGAZIWA HALI YA HATARI



Rais Jakaya Kikwete amezungumzia hali ya usalama wa nchi, ikiwemo  uvamizi wa vituo vya Polisi,  uporaji wa silaha ulioambatana na vifo vya askari na kusema matukio hayo, baadhi yake yana dalili za ugaidi. 

MKE NA MUME WASOTA RUMANDE KWA KUMWOZESHA BINTI WA MIAKA 10



Mke na Mume wanaotuhumiwa kumuoza binti wa miaka 10 jana walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini huku Mahakama ikifunga dhamana yao hadi kesi hiyo itakapomalizika.

TANESCO YAKIRI ‘MADUDU’ KATIKA MFUMO WA KUUZA LUKU



Shirika la Ugavi na Usambazaji wa Umeme nchini (TANESCO), limekiri kuwepo na matatizo ya mfumo wa kununua Luku, ulioanza Ijumaa jioni wiki iliyopita  hadi jana na kuwa matatizo hayo yanatokana na mfumo wa kuuza umeme wa Luku.

UPELELEZI KESI YA LWAKATARE NA MWENZAKE BADO KUKAMILIKA



Upelelezi wa kesi ya kula njama ya kudhuru kwa sumu, inayomkabili Mkurugenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilfred Lwakatare na mwenzake bado haujakamilika.

TAZARA SASA KUSUKWA UPYA KIMFUMO NA UTENDAJI



Serikali ya Tanzania na Zambia zimekubali kulisuka upya Shirika la Reli la nchi hizo (Tazara), kwa kufanya marekebisho ya kimfumo na kiutendaji ili kutatua matatizo ya kimuundo na kimenejimenti yanayochangia kuzorota kwa ufanisi wa shirikia hilo.

Monday, March 2, 2015

OIL & GAS AFRICA: DISPUTES SIMMER OVER EXPLORATION RIGHTS IN EASTERN AFRICA



The discovery of large reserves of oil and gas has raised the profile of eastern Africa countries, with the potential of joining world’s energy producers. But  the new found reserves have brought a bigger problem and triggered escalating disputes among the soon to be new oil states in Africa.

Sunday, March 1, 2015

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMAPILI

Kama kawaida tunakuletea muonekano wa habari zilizomo kwenye magazeti ya leo Jumapili Machi 1, 2015. Kusoma vichwa vya habari kwenye kurasa za mbele na nyuma za magazeti hayo bofya kwenye picha hapo kushoto. Kupata yaliyoandikwa kwenye magazeti usikose kuperuzi blogu hii kila siku.

TIBAIJUKA, CHENGE, NGELEJA WASIMAMISHWA CCM


Kamati Kuu ya CCM (CC) imewasimamisha uongozi wa vikao vya chama, vigogo watatu wa chama hicho, akiwemo Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kutokana na kuhusishwa na sakata la Escrow.

HIVI NDIVYO MAUTI YALIVYOMKUTA KAPTENI JOHN KOMBA


Ni huzuni kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jimbo la Mbinga Magharibi, Taifa, marafiki na familia, baada ya kufikwa na msiba mkubwa wa kiongozi, Mbunge, Kapteni wa Jeshi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na msanii mashuhuri wa Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT), Kapteni John Komba.

VIONGOZI WA DINI KUCHUNGUZWA MIENENDO YA UTUME WAO


Serikali imetakiwa ichunguze viongozi wa madhehebu ya dini ya Kikristo na Kiislamu nchini, ili ijiridhishe na mienendo ya utume wao wa kuhubiri injili na sala kwa wananchi.