Monday, June 15, 2015

WALIOFARIKI AJALI YA BASI LA ANOTHER G NA KUUA ABIRIA 23 WATAMBULIWA

Watu 23 wamekufa katika ajali iliyohusisha basi na lori mjini Mafinga, Iringa huku wengine 34 hali zao zikiwa mbaya.

MUFTI SIMBA KUZIKWA LEO JUMANNE SHINYANGA

Wakati mwili wa  Mufti na Shehe  Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Shaaban Simba (78) aliyefariki dunia jana asubuhi ukitarajiwa kuzikwa leo jioni mkoani Shinyanga, Rais Jakaya Kikwete ameungana na Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) kuomboleza kifo cha kiongozi huyo wa juu wa kiroho nchini.

MIGIRO, MWANAFUNZI WACHUKUA FOMU ZA URAIS

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro jana alichukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, hivyo kufikisha idadi ya makada 36 wa chama hicho wanaowania urais, lakini pia akiwa mwanamke wa nne kuthubutu kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu.