Thursday, July 31, 2014

FEMALE BOMBER KILLS 6 IN NIGERIA, GIRL WITH EXPLOSIVES HELD

A female suicide bomber killed six people at a college campus in Nigeria's Kano city on Wednesday, the fourth time Boko Haram Islamists were suspected of using a female attacker in as many days.
The latest violence came as the government announced the arrest of a 10-year-old girl with explosives strapped to her chest in a neighbouring area.
Boko Haram is blamed for killing more than 10,000 people since 2009, and their extreme tactics have been denounced worldwide, including on some jihadi websites.
But what appears to be a new tactic of deploying young women and girls as bombers will spur further outrage as Nigeria seems unable to contain the violence.
At about 2:30 pm (1330 GMT) on Wednesday, an assailant blew herself up at a noticeboard on the campus of the Kano Polytechnic College while students were crowded around it.
Witness Isyaku Adamu said the explosion came from within the crush of students and left blood splattered on the ground, as soldiers and police scrambled to secure the area.
Government spokesman Mike Omeri put the casualties at six dead and six wounded and confirmed that a female, whose age was not immediately known, was responsible for the bloodshed.
It was the fourth attack by a female bomber in Nigeria's second city since the weekend.
On Sunday, a young woman injured five police officers as she blew herself up at a another campus in the city.
The next day, two young women believed to be in their late teens or early 20s separately attacked a petrol station and a shopping centre, suicide blasts that killed at least three people and injured 13.
Omeri said security forces on Tuesday stopped a car in Kano's neighbouring state of Katsina and arrested three suspected Boko Haram members.
The group included one male and two girls, aged 18 and 10.
The older two tried to flee, according to Omeri's statement.
The "10-year-old ... was discovered to have been strapped with an explosive belt," he said.
National police spokesman Frank Mba said established international "terrorist organisations" use female suicide bombers mainly because "women generally raise fewer suspicions."
The chilling trend of deploying young women and girls as bombers comes three-and-a-half months after Boko Haram kidnapped more than 200 schoolgirls from the remote town of Chibok in the northeast.
Boko Haram leader Abubakar Shekau boasted about the mass abductions in a video during which he threatened to sell the girls as slaves.
The Chibok abductions prompted a social media campaign that went viral and drew unprecedented global attention to Boko Haram's extremist uprising, which the group says is aimed at creating a strict Islamic state in the mainly Muslim north.
In the weeks following the kidnappings, some prominent jihadi websites had posts condemning the Nigerian group's extreme tactics.
Nigeria has repeatedly insisted that it knows where the girls are, while President Goodluck Jonathan and top military officials have suggested they will be brought home safely soon.
But little progress has been made in securing their release while the violence appears to be escalating across the north and centre of the country.
On Thursday in the capital Abuja, Jonathan is set to launch a fund in support of "all those who have been adversely affected by terrorism and insurgency in the country," a statement from his office said.
He hopes to raise $500 million (370 million euros) over a 12-month period from the private sector and international donors, the statement said.
More than 2,000 civilians have been killed this year, making the first half of 2014 one of the deadliest stretches of the insurgency.
Attacks had been concentrated in the remote northeast, Boko Haram's stronghold, but waves of strikes since April in major cities including Abuja have underscored the grave threat the Islamists pose to Nigeria, Africa's most populous country and top oil producer.

WALIOFARIKI, MAJERUHI AJALI YA BASI LA MOROBEST HAWA HAPA

Ajali  ya watu 19 wamekufa katika ajali mbili tofauti zilizotokea mkoa wa  Dodoma na Arusha jana.
Ajali hizo mbili zimesababisha majeruhi zaidi ya 70.
Ajali ya kwanza mbaya ilihusisha basi la abiria na lori ambapo watu 17 walikufa na wengine 56 kujeruhiwa. Katika ajali hiyo basi la abiria na lori yaligongana uso kwa uso.
Aidha,  katika ajali ya Arusha, madereva wa magari mawili yaliyogongana maeneo ya Sadeki wilayani Arumeru, walikufa na wakati huo huo watu 14 wamejeruhiwa.
Ajali ya mkoani Dodoma ilihusisha basi la Morobest lililokuwa likitoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam, na ilitokea eneo la Pandambili, Wilaya ya Kongwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David  Misime alisema ajali hiyo ilitokea saa 2 asubuhi jana. Kati ya 17 waliopoteza maisha,  wanaume ni 12.
Basi hilo lenye namba za usajili T258 AHV likiendeshwa na Said Lusogo, liligongana na lori namba T820CKU/ T390CKT likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma,  likiendeshwa na Gilbert  Nemanya. Madereva wote wawili wamekufa.
Kwa mujibu wa Kamanda Misime, kufikia jana mchana miili  11 ilikwishatambuliwa.
Waliotambuliwa ni  dereva wa lori hilo, Nemanya  pamoja na utingo wake, Mikidadi Zuberi.
Wengine ni dereva wa basi la Morobest, Lusogo na kondakta wake, Omary Mkubwa.
Marehemu wengine waliotambuliwa ni Merina Malikeli, Nasib Machenje, Wilson Suda, Gabriel Mejachiwipe, Justine Makasi na mwanamke aliyetambuliwa kwa jina moja la Christina.
Kwa mujibu wa Misime, watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na hadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita gari lingine.
Majeruhi 23 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Majina yao ni Frank Raymond, Patricia Ngamwai, Amos Chiwaga, Mary Mateo, Safari Jonas, Suzan Charles, Gasper Shao,Felician Rite, Felister Mathias, Amos Jonas, Edina Lwande, Seleman Kaseni, Nazareth Kasua, Saimon Msoloka, Juma Mtezi  na   Swalehe Bakari.
Wengine ni Naseria John, Getruba Kombo, George Njelewa, Manase Makuja, Chibago Mchiwa, Nicholous Roger na Michael Chibwela.
Kwa upande wa ajali ya mkoani Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema ilitokea juzi saa 3 usiku maeneo ya Sadeki kwa Fundi.
Alisema gari aina ya Subaru lenye namba za usajili T842 CCP lililokuwa likiendeshwa na David Natal (35) liligongana na gari ya Nissan Mini Bus lenye namba za usajili T355 CGA lililokuwa likiendeshwa na aliyetambuliwa kwa jina moja la Joshua.
Alisema ajali hiyo ilitokea wakati Natal aliyekuwa anatoka Arusha mjini kwenda Makumira, alipojaribu kupita  gari lililokuwa mbele yake ndipo lilipogongana na gari lililokuwa linatoka Usa River kwenda Arusha mjini.
Mbali na vifo vya madereva hao, ajali hiyo ilisababisha majeruhi 14 waliokuwa kwenye gari aina ya Nissan Mini Bus.
Majeruhi hao ni Frida Joseph (18), Elisante Mungure (45), Lilian Mathias (29), Juma Mohamed (42), Silvia Kelvin (26), Charles Massawe (40), Kelvin Charles (29), Emmanuel Adedia (29), Zainabu Issa (40), Regard Joseph (30), Elirehema  Abrod (29),  Alfred Lucas (21), Gipson Tackson (3) na Salma Abdallah (44).
Kamanda alisema majeruhi hao wanatibiwa katika Hospitali ya Tengeru na Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

ZITTO KABWE AKANA KUWA MWANACHAMA WA UKAWA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) amesisitiza hajawahi kuwa katika kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wala kundi lolote ndani ya Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa, yuko kwenye linalotaka maridhiano.
Hata hivyo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, Zitto alisema msimamo wake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba mpya ni  kutohudhuria Mkutano wa Bunge Maalumu unaotarajiwa kuanza wiki ijayo, kama makundi hasimu hayatafikia maridhiano.
Alisisitiza msimamo wake kuhusu Muungano kuwa ni serikali tatu zilizoboreshwa kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa washirika wake.
Mbunge huyo alikuwa akitoa kile alichosema ni ufafanuzi kuhusu msimamo wake kulingana na mahojiano aliyofanyiwa katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM na hatimaye, mahojiano hayo kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Alisema Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yoyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua dawa vijijini.
Hata hivyo, Zitto alisema anaunga mkono mgomo wa baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mikutano.
Pia alisema anaunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni iliyotokana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Zitto alisema kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba bora, unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana.
“Ukawa hawataki mazungumzo na viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza Ukawa, jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka.
“Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache,”  alisema katika taarifa yake. 
Kwa mujibu wa Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), aliyataja marekebisho yanayotakiwa kufanywa kwenye Katiba ya sasa kuwa ni pamoja na Tume ya Uchaguzi kuwa huru kwa kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi.
Marekebisho mengine ni,kuruhusu mgombea binafsi na kuondoa mafuta na gesi kama jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano.

POLISI ALIYETIMULIWA KAZI ADAKWA AKIJIANDAA KUFANYA UHALIFU

Askari Polisi aliyefukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu mwaka 2012 baada ya kukutwa na silaha katika ukumbi wa disko mkoani Kilimanjaro, James Marwa (26) amekamatwa na Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime-Rorya akidaiwa kuwa katika harakati za kwenda kufanya uhalifu eneo la mgodi wa Nyamongo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime-Rorya, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kukamatwa kwa Marwa.
Mambosasa alisema kwa sasa anashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya riffle ikiwa na risasi tano ya kampuni ya ulinzi ya Paroma Security na kukiri kwamba alikuwa anaenda kuungana na wenzake kwenda kufanya uhalifu mgodi wa Nyamongo.
Akifafanua Kamanda Mambosasa alisema Julai 29 walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuonekana mtuhumiwa maeneo ya Mtaa wa Magamaga, kata ya Sabasaba, Tarime, akiwa na bunduki aina ya riffle yenye namba 58368 TZCAR 5963 ikiwa na risasi tano.
“Tulifuatilia na kumkamata mtuhumiwa akiwa na silaha hiyo, tumemhoji na kubaini kuwa kwa hivi sasa alikuwa akifanya kazi ya ulinzi katika kampuni ya ulinzi ya Paroma Security eneo la ujenzi wa Mizani huko Sirari na alipohojiwa zaidi alidai alikuwa akienda Nyamongo mgodini kuungana na wenzake kufanya Uhalifu,” alisema Kamanda.
Alisema watamfikisha mtuhumiwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

JICHO LA TATU


UBORA HAFIFU WAKWAMISHA AJIRA KWA WAHITIMU VYUO VIKUU

Ubora hafifu wa wahitimu wa vyuo vikuu kiasi cha kusababisha wengine kutoajirika, vimeigusa serikali na sasa inatarajia kuja na mpango wa kukabili hali hiyo.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekiri kwamba rejea mbalimbali za waajiri zinaonesha upo  upungufu katika ubora wa wahitimu kiasi cha kutoajirika, jambo ambalo imesema haiwezi kulinyamazia.
“Rejea mbalimbali za waajiri zinaonesha kuna upungufu katika ubora wa wahitimu wa vyuo vikuu na kuwa hawaajiriki,” alisema  Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu.
Katika mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Temu aliendelea kusema, “...ni jambo ambalo hatuwezi kulinyamazia kama watunga sera,  huwezi kujadili peke yako bali na wadau ili kupata mawazo chanya.”
Serikali katika kuhakikisha suala hilo linapata utatuzi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Kamati ya Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vishiriki zinatarajia kuja na mpango kuhakikisha vyuo vinatoa wahitimu bora wenye ujuzi wa kuajirika na kujiajiri.
Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Magishi Mgasa katika mkutano huo, alisema suala hilo ni miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa kwa kina kwenye kongamano la elimu ya juu, mjini Arusha.
Mgasa alisema kwa sasa kumekuwapo na mjadala wa kuwepo wahitimu wa elimu ya juu wasio na ujuzi na ambao wamekuwa hawaajiriki na hawawezi kujiajiri.
Kuhusu kongamano, Mgasa alisema litakakwenda sanjari na maonesho ya huduma za vyuo vikuu mbalimbali, yanafanyika kuanzia Agosti 13 hadi 15 chini ya kauli mbiu ‘Elimu ya Juu baada ya Mpango wa Maendeleo wa Milenia baada ya 2015.’
 Mgasa alisema wadau watajadili na kutafakari juu ya maendeleo ya ujuzi kwa kutambua uwezo wa kiuchumi nchini.
“Tutaamua wajibu wa taasisi za elimu ya juu katika kusaidia maendeleo endelevu kupitia maendeleo ya ujuzi katika nchi, tukitilia mkazo aina ya maarifa na ujuzi unaotolewa na taasisi za elimu ya juu na mahitaji halisi ya taifa katika elimu, ujuzi na ushindani,” alisema Mgasa.
Alisema pia kongamano hilo litatambua fursa muhimu ambayo taasisi za elimu ya juu zinaweza kuchagiza wajibu wa maendeleo endelevu ya nchi kwa kulenga kujenga ajira ya wahitimu.
“ Pia tutatumia fursa hiyo kuweka mikakati ya uwezeshaji wa mtandao mkubwa kati ya taasisi za elimu ya juu, sekta binafsi na viwanda na baadhi ya wadau muhimu wa elimu ya juu,” alisema.
Akizungumzia mafanikio ya makongamano yaliyopita,  Temu alisema kupitia jukwaa hilo, wadau wa elimu walikuja na mpango wa miaka mitano (2010-2015) uliolenga kuongeza udahili wa wanafunzi, uwekezaji katika elimu ya juu na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Alisema kupitia mpango huo, Serikali imepunguza tatizo la walimu kwa kusomesha walimu 400 na kati ya hao, wenye Shahada ya Uzamivu ni zaidi ya walimu 120.
 “Nchi ina mabadiliko makubwa, sasa tunazungumza uchumi wa gesi, kuzalisha wataalamu katika sekta za vipaumbele kama utalii, usafiri, hivyo tunataka kushirikiana na sekta binafsi ili kupata fikra chanya,” alisema.

MAJINA YA WANAOPIGA MABOMU ARUSHA KUANIKWA HADHARANI

Watuhumiwa wa mabomu katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha, watawekwa hadharani hivi karibuni ikiwa ni pamoja na umma kuelezwa kilichotokea na waliowatuma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema hayo juzi alipokuwa akihutubia sherehe za Baraza la Idd jijini Dar es Salaam.
Alisema ingawa hatua za kisheria zinaendelea kwa baadhi ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi, serikali pia itaweka wazi juu ya matukio hayo ya mabomu, ikiwemo wanaowatuma.
Alisema kinachosubiriwa ni kukamatwa watuhumiwa wengine kama wawili, ambapo aliomba wananchi kushirikiana na Serikali  watiwe mbaroni.
“Serikali haikulala tangu tukio la kurushwa kwa bomu pale  Olasiti, tuliongeza nguvu ya wataalamu wa upelelezi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na dalili nzuri zimeanza kuonekana.
“Napongeza vyombo vya ulinzi na usalama, tumekamata kundi kubwa na baadhi  yao wamekiri kushiriki mambo kadhaa na tutakuja kuwashirikisha,” alisema Pinda.
Alitaka jamii kufichua watu wote wenye  nia ovu ya uhalifu ili wananchi na jamii nzima iishi kwa amani. Alitaka viongozi wa dini kuepuka mifarakano ndani ya dini kwa kuwa inasababisha chuki zisizo na msingi.
Alisema mifarakano ndani ya dini ni mibaya na inapotoka nje na kuwa kati ya dini moja na dini nyingine, inakuwa mbaya zaidi na kuwasisitizia viongozi wa dini, kuhakikisha kila dini waumini wanakuwa na amani, utulivu na mshikamano.
Pinda alisema  anaamini amani na utulivu wa Tanzania, msingi wake ni mafundisho ya dini. Alisisitiza taifa lolote ambalo halina msingi huo wa dini, watu wake hawana tofauti na wanyama , kwa kuwa hawana hofu ya Mungu na hivyo hawaogopi lolote.
Alipongeza viongozi wa dini wa Dar es Salaam kwa kuunda Kamati ya Amani, inayohusisha viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo  ambayo hukutana na kujadili  namna ya kuboresha amani bila kujali tofauti zao.
Kutokana na ubunifu huo wa viongozi wa Dar es Salaam,  Pinda alisema kila mkoa anaokwenda, amekuwa akiwahamasisha wakuu wa mikoa kusaidia kuandaa kamati kama hizo kwa kuwa ni msingi wa amani.
Baraza la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) wilayani   Arumeru,  limeahidi  kushirikiana na  polisi mkoani kuhakikisha linafichua watu ambao wamekuwa wakijihusisha na uvunjifu wa amani mkoani Arusha.
Kiongozi wa Baraza la Wazee, Wilaya ya Arumeru, Shehe Haruna Husein  alisema hayo jana akizungumza na waandishi wa habari kulaani vikali vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyoendelea mkoani humo.
Alisema, “Bakwata wilayani Arumeru inalaani vikali vitendo hivyo vya uhalifu vinavyoendelea mkoani hapa.” Alisisitiza watashirikiana na polisi kufichua wahilifu.
Alipongeza Polisi kwa jitihada zao kudhibiti uhalifu. Alitoa mwito kwa wahisani wengine kuhakikisha wanashirikiana na jeshi hilo kuwezesha wahalifu wakamatwe.
“Kwa kweli sisi kama Bakwata tunalaani vikali sana hivi vitendo vya uhalifu vinavyoendelea mkoani hapa, huku tukiahidi kushirikiana na jeshi la polisi katika kudhibiti matukio ya uhalifu yanayoendelea mkoani hapa ili wahalifu wote wanaojihusisha na matukio hayo wachukuliwe hatua kali za kisheria,” alisema.
Miongoni mwa matukio ya ulipuaji mabomu ni pamoja na kwenye Kanisa Katoliki, Parokia ya Joseph Mfanyakazi, Olasiti. Katika tukio hilo, watu wawili walipoteza maisha na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
Tukio lingine la ulipuaji bomu, ni kwenye mkutano wa wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa Madiwani wa Chadema katika eneo la Soweto, ambalo pia watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Hivi karibuni, mlipuko mwingine ulitokea katika mgahawa wa Vama Traditional Indian Cuisine na kusababisha majeruhi. Baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika katika ulipuaji wameshafikishwa mahakamani.
Tukio lingine la hivi karibuni ni la Katibu wa Bakwata, mkoani Arusha, AbdulKarim Jonjo aliyejeruhiwa na mgeni wake baada ya kurushiwa bomu nyumbani kwake, eneo la Esso wakati akipata daku na mgeni wake.

'MVUA ZINAZONYESHA NI MABADILIKO YA HALI YA HEWA'

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua zilizonyesha kuanzia alfajiri ya jana zinatokana na mabadiliko ya hali ya hewa baharini na zinatarajia kuendelea leo katika maeneo yote ya pwani.
Imesema hali hiyo pia imesababisha kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi katika Pwani ya Kusini hivyo kuwatahadharisha wananchi wa maeneo hayo kutotumia vyombo vya baharini.
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Dk Agness Kijazi alisema kwa sasa hakuna msimu wa mvua hivyo mvua hizo ni za kawaida kutokana na kuwepo kwa mgandamizo mdogo wa hewa baharini na kusababisha mvua kwa baadhi ya maeneo.
Alisema ingawa mvua hizo ni za kawaida lakini pia kutakuwa na  upepo mkali wa kilometa 40 kwa saa na mawimbi yenye ukubwa wa mita mbili katika maeneo ya Pwani ya Kusini.
“Tutaendelea kutoa tahadhari lakini hali hiyo itadumu kwa  usiku wa leo mpaka kesho (leo), hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua hatua stahili hasa kwa wale wanaotumia vyombo vya baharini,” alisema Dk Kijazi.
Dk Kijazi alisema mabadiliko hayo yatasababisha mvua kidogo katika maeneo yote ya Pwani  mpaka Mkoa wa Mtwara  huku upepo na mawimbi ukiathiri mikoa ya Lindi na Mtwara.

ONYO!! SIMU ZA MKONONI, KOMPYUTA HUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME

Watanzania wametakiwa kuwa makini wanapotumia simu na kompyuta, kwani ndio chanzo cha matatizo mbalimbali yakiwemo ya kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.
Mshauri wa masuala ya teknolojia, Alex Mpompo aliyasema hayo juzi kwenye semina inayohusu teknolojia katika Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Mpompo alisema matatizo yanayochangiwa na teknolojia yapo mengi ikiwamo kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.
Alisema vijana wengi nchini wana upungufu wa nguvu za kiume jambo linalochangiwa na matumizi mabaya ya teknolojia hivyo kuchangia familia kusambaratika.
Aliwaasa Watanzania kutotumia kompyuta kwa muda mrefu kwa kuipakata kwenye mapaja, kwani mionzi inapenya kwa urahisi katika maeneo hayo na kuathiri mbegu za kiume na kusababisha ugumba.
"Watu wengi hawaelewi kama ukiweka simu karibu na jiko la gesi unaweza kuunguza nyumba, pia unapogandamiza simu na ngozi inasababisha saratani ya matiti na ugonjwa wa moyo," alisema Mpompo.
Alisema vijana wanaoongea na simu kwa muda mrefu wapo kwenye hatari zaidi ya kupoteza kumbukumbu na kutosikia.

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO ALHAMISI - JULAI 31

UJENZI MUHAS KUONGEZA UDAHILI WA WANAFUNZI

Kukamilika kwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) na ujenzi wa hospitali ya kisasa katika Kijiji cha Mloganzila, kunatarajiwa kuongeza mara tano ya udahili wa sasa wa  wanafunzi.
Akizungumza jana, Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Profesa Ephata Kaaya alisema kwa sasa chuo kinadahili wanafunzi 3,000. Ujenzi ukikamilika, kitadahili wanafunzi 15,000 watakaosoma taaluma mbalimbali za afya.
Alisema kukamilika kwa ujenzi huo pia kutatoa fursa kwa wanafunzi kupata sehemu za kusomea kwa ufanisi kama vile ya maabara za kisasa, madarasa, na sehemu za ufanyaji mazoezi.
Hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete aliweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa hospitali ya kisasa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili.
Naye Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu alisema ndani ya miaka mitano serikali imewekeza katika elimu ya juu kwa kuboresha miundombinu ya vyuo vya umma.
Temu alitolea mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo wameweza kujenga maabara za sayansi, kuboresha miundombinu katika Kitivo cha Uhandisi na kujenga majengo mapya.
“Ukiangalia vyuo vya umma vilikuwa katika hali mbaya lakini sasa miundombinu yake imeboreshwa na hata Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kilizidiwa na ndio maana serikali inajenga chuo kikubwa,” alisema.

YATIMA 500 WASHEREHEKEA PAMOJA IDD EL FITRI

Zaidi ya watoto yatima 500 wanaoishi katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam na wilayani Kondoa, Singida wameungana na Waislamu wengine duniani kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitr.
Sherehe hizo zilizofanyika juzi, jijini Dar es Salaam, zilitokana na kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Watoto hao kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima, walipata fursa ya kula na kufurahi pamoja na wengine wakati wa chakula kilichoandaliwa kwa ajili yao na taasisi ya Al-Madinah Social Service Trust.
Karamu hiyo ilidhaminiwa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Meneja Rasilimali Watu wa IPTL, Aidan Kaude, aliyejumuika na watoto hao katika sherehe hizo, alisema kampuni yake imeona haja ya kuisaidia Al-Madinah katika kuhakikisha kuwa watoto hao wanapata haki ya kusherehekea wakati huu muhimu katika maisha ya waislamu wote duniani.
"Tulipopata maombi kutoka Al-Madinah kusaidia kufanikisha karamu hii, Mwenyekiti wetu Mtendaji Harbinder Sethi aliidhinisha haraka ombi hilo na kusema kuwa ni jambo la heri sababu watoto hao ni yatima na wanahitaji msaada kutoka kwa kila mtu waweze kuishi maisha ya kawaida kama wengine wanavyoishi licha ya kupoteza wazazi wao," alisema.
Mkurugenzi wa Al-Madinah Social Service Trust, Sheikh Ally Mubaraki, alisema kuwa baada ya kufanya kazi karibu na kwa muda mrefu na makundi mengi na taasisi mbali mbali za Kiislamu, taasisi yake imegundua kuwa yatima wengi wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na ukosefu wa mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi.
Alisema taasisi yake iliomba msaada wa kifedha kutoka IPTL  kuwapatia msaada watoto waishio katika mazingira magumu nao wapate nafasi ya kusherehekea na Waislamu wenzao katika sikukuu hiyo.
Sherehe hizo zinahimiza Waislamu duniani kufanya yale yaliyoagizwa na Mtume Muhammad.

MADIWANI WAMLAUMU MKUU WA WILAYA KWA KUWADHALILISHA

Madiwani wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida waliokuwa wamewekwa mahabusu kwa amri ya Mkuu wa Wilaya, Queen Mlozi (pichani), wamesema kitendo hicho kimewadhalilisha na kuwaondolea heshima mbele ya jamii.
Madiwani hao, Hinga Mnyawi wa kata ya Ikhanoda na Ntandu Seleman wa kata ya Mwasauya, walituhumiwa kukwamisha ujenzi wa vyumba vya maabara.
Aidha, kwa nyakati tofauti mbele ya kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo juzi, madiwani hao walidai kuwa kuwekwa kwao korokoroni hakukuwa na uhalali wowote.
Akichangia kwenye taarifa ya kamati ya huduma za kijamii, Mnyawi alisema kuwa anasikitishwa mno na kitendo cha Mlozi kumweka ndani kwa kile alichodai yeye kushindwa kuhamasisha wananchi kuchangia Sh milioni 5 za ujenzi wa maabara kwenye shule iliyopo kwenye kata yake.
“Hivi ina maana mimi sijui kazi yangu hadi DC (mkuu wa wilaya) aje kunikumbusha wajibu wangu kwa kuniweka ndani?” alihoji Mnyawi.
Naye Seleman alisema kuwa anashangazwa na kitendo cha mkuu huyo kumkejeli kuwa analala Singida mjini ‘kwa raha zake’ badala ya kusaidia kusukuma mbele ujenzi wa maabara kwenye eneo lake kijijini.
Akichangia suala hilo, diwani wa kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni alisema kuwa kitendo cha Mlozi kuwaweka ndani madiwani wenzake ni kuwadhalilisha mbele ya jamii iliyowachagua.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Eliya Digha alihitimisha mjadala huo kwa kusema kuna umuhimu wa madiwani wa halmashauri hiyo kukutana na Mlozi kurejesha uhusiano ambao unaelekea kupotea.
Julai 8 mwaka huu, Mlozi alitumia madaraka aliyonayo kisheria kuwakamata na kuwaweka ndani kwa saa mbili madiwani wa kata hizo mbili kwa tuhuma mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa maabara.

WAKATA MAPANGA NG'OMBE NA KUCHOMA MTUMBWI WA WAVUVI

Wananchi katika Kijiji cha Mugara, Kata ya Iramba wilayani hapa wamewakatakata kwa mapanga ng’ombe wawili wa wavuvi waliodaiwa kufanya uvuvi haramu na kuteketeza kwa moto mtumbwi wao.
Imeelezwa kuwa wananchi hao walijichukulia sheria mkononi kwa kile walichodai kuwa, waliwakuta wavuvi hao wakitumia sumu kuvua samaki katika Ziwa Victoria. Pia waligawana nyama baada ya kuwachinja ng’ombe hao.
Mwenyeiti wa kijiji cha Mugara, Ngajeni Bituro pamoja na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Wilibard Marea walisema kwa nyakati tofauti kuwa, tukio hilo ni la juzi saa 8 mchana kijijini hapo.
 Walisema kuwa wavuvi hao Ngarya Musimu, jina maarufu ‘Kajee’, mkazi wa kijiji cha Nyakatuba na Kengera Gagi, mkazi wa kijiji Mugara, wilayani hapa, walikamatwa na wananchi hao wakivua kwa kutumia sumu na walishavua samaki zaidi 200 aina ya sato.
 Aidha, walisema kuwa kulingana na sheria ndogo walizojiwekea kijijini hapo, kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu mtu yeyote anayekamatwa akifanya kosa hilo, adhabu yake ni zana zake zote za uvuvi huo kuteketezwa kwa moto na kuchukuliwa ng’ombe wawili ama kulipa faini ya Sh 300,000.
Marea alisema wakazi hao baada ya kuwakamata wavuvi hao wenzao wawili walikimbia na kutokomea kusikojulikana.
Alisema kuwa wavuvi waliotoroka ni pamoja na Doi Wiliam Buriro na Kileo Kwibyira  ‘Rasi’, wote ni wakazi wa kijiji cha Kasahunga wilayani hapa.
Mtendaji huyo alisema wananchi wenye hasira walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa mmoja na kuwakatakata kwa mapanga ng’ombe wawili na kugawana nyama, ikiwa ni pamoja na kuuteketeza kwa moto mtumbwi mmoja uliohusika katika uvuvi huo.
Alisema kuwa wavuvi hao walikutwa wakivua samaki kwa sumu katika eneo la kisiwa cha Hilera katika Ziwa Vistoria na walipelekwa Kituo kidogo cha Polisi Kibara.
Viongozi hao wakiwemo wa Vikundi vya Ulinzi wa rasilimali za Ziwa Victoria (BMU) walisema kuwa wavuvi hao ni wazoefu kwenye uvuvi haramu.
 Hata hivyo walidai wavuvi haramu wamekuwa wakikamatwa na kuachiwa na vyombo vya dola, jambo linalowakatisha wananchi tamaa na kuamua kuchukua sheria mkononi wanapowakamata.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philipo Kirangi, alisema jana kuwa bado hajapata taarifa kamili kuhusu tukio hilo, na kwamba atafuatilia na kulitolea ufafanuzi.

Wednesday, July 30, 2014

Miili ya abiria waliokufa kwenye ajali ya basi la Morobest lililokuwa likitokea Mpwapwa ikiwa imelazwa kando ya basi hilo baada ya kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo asubuhi na kusababisha vifo vya watu 17 wakiwamo madereva wa magari yote mawili pamoja na kondakta na utingo wa lori hilo.

Wasamaria wakihangaika kunasua majeruhi na miili ya marehemu kutoka kwenye basi la Morobest lenye namba za usajili T 258 AHV lililogongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi. Watu 17 wamethibitishwa kufariki na wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa vibaya.

Basi la Morobest lenye namba za usajili T 258 AHV likiwa eneo la tukio baada ya kugongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi.

Majeruhi wa ajali ya basi la Morobest lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam, wakiwa wamelazwa chini kusubiria huduma ya matibabu hospitalini. Watu 17 wamethibitishwa kufariki dunia mpaka sasa katika ajali hiyo ambayo basi hilo lenye namba za usajili T 258 AHV liligongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi.

Tuesday, July 29, 2014

AJIRA 200 ZA KONSTEBO, KOPLO ZAPIGWA 'STOP' UHAMIAJI

Ajira za washindi 200, walioitwa kufanya usaili wa nafasi za ajira za Konstebo na Koplo wa Uhamiaji, zimesitishwa kupisha uchunguzi wa utaratibu wa uteuzi wa washindi hao.
Hatua hiyo imekuja katika siku chache, tangu kulipoibuka utata, uliotokana na kuitwa kwa watu zaidi ya 10,000 wenye shahada za kwanza, kufanya usaili wa nafasi 70 tu za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, zilizokuwa wazi katika Idara hiyo.
Taarifa ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa hatua hiyo ya kusitisha ajira hizo, imechukuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Kwa mujibu wa Nantanga, hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuibuka tuhuma kuwa kati ya washindi hao 200, ambao walishatangazwa na kutakiwa kuanza kazi Jumatano ya wiki ijayo, sehemu kubwa ni ndugu na jamaa za wafanyakazi wa Uhamiaji.
“Kutokana na kusitishwa kwa ajira hizi, waombaji wote walioitwa na kutakiwa kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji tarehe 6, Agosti 2014, sasa wanatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa tena baada ya uchunguzi huu kukamilika na uamuzi kufanyika,” alieleza Nantanga katika taarifa yake.
Tayari Katibu Mkuu, Abdulwakil, ameshaunda Kamati Ndogo ya Uchunguzi wa suala hilo. Taarifa zilizofikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa kuna uwezekano muda wa uchunguzi huo na hadidu za rejea, vitajulikana leo.
Sifa za wasailiwa 100 katika nafasi ya Koplo wa Uhamiaji, zilikuwa awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu, bila kutaja kiwango cha ufaulu ; na ya pili ni umri usiozidi miaka 30.
Kwa nafasi 100 za Konstebo wa Uhamiaji, sifa zilikuwa awe amehitimu Kidato cha Nne na kufaulu, bila kutaja kiwango cha ufaulu, na awe na umri usiozidi miaka 25.
Majukumu na kazi zao, zilikuwa kufungua, kupanga na kutunza majalada ya huduma mbalimbali za Uhamiaji, kuandika hati mbalimbali za Uhamiaji, kufanya doria sehemu za mipakani, bandarini, vituo vya mabasi, treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini, vikiwemo vya majini.
Nyingine ni kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini, kufanya ukaguzi kwenye mahoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara, kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila siku za Uhamiaji, kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji na kuandaa na kutunza takwimu za huduma mbalimbali za uhamiaji.
Tuhuma hizo zilizosambaa katika mitandao ya jamii, zilidai kuwa matokeo ya usaili wa nafasi za kazi Uhamiaji, yaliyotolewa katika magazeti, yameonesha kuwa katika Idara hiyo Watanzania wengine, mbali ya watoto au ndugu wa wafanyakazi wa Idara hiyo, hawawezi kupata ajira ndani ya Idara hiyo ya Serikali kirahisi. 
“Majina ya wengi walioitwa kazini ni watoto au ndugu wa wafanyakazi wa idara hiyo,” ilieleza taarifa hiyo, iliyosambazwa katika mitandao na kutaja majina ya wanaodaiwa kuwa ni washindi wa usaili huo na uhusiano wao na maofisa wa Uhamiaji.
“Hii ni sampuli tu, ila zaidi ya asilimia tisini ni watoto na ndugu wa maofisa Uhamiaji. Nadhani ingekuwa vyema wasingekuwa wanatangaza nafasi hizi, bali wawe wanagawiana ndani kwa ndani. Alamsiki,” ilieleza taarifa hiyo.
Hivi karibuni Idara ya Uhamiaji ilipotangaza majina ya wasailiwa zaidi ya 10,000, waliotakiwa kushindania nafasi 70 za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji. Hatua hiyo ilisababisha utata, kutokana na uchache wa nafasi, ikilinganishwa na wasailiwa walioitwa.
Utata huo ulisababisha kuibuka kwa hisia za usaili huo, kugubikwa na rushwa, kiasi kwamba Nantanga alilazimika kutoa taarifa, kukanusha kuwepo kwa tuhuma hizo.
“Tuhuma za rushwa zinazoambatanishwa na kazi hii, ni hisia tu za wahusika, kwani kwanza hazina ushahidi, na pia usaili ulifanywa kufuatana na kanuni na sheria zinazosimamia ajira za watumishi wa umma,” ilieleza taarifa hiyo ya Nantanga, kuhusu usaili wa watu zaidi ya 10,000.
Nantanga alifafanua kuwa nafasi za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, zilitangazwa katika magazeti na Tovuti ya Wizara na Idara ya Uhamiaji, kufuatana na taratibu za Serikali, zinazosimamia ujazaji wa nafasi za kazi katika utumishi wa umma, kwa lengo la kuiweka wazi kwa umma wa Watanzania na matokeo yake wahitimu zaidi ya 20,000, walitumia haki yao ya msingi kuomba nafasi hizo.   
Kufuatana na wingi wa waombaji, Wizara ilifanya zoezi la mchujo wa awali, ambao hatimaye ulibakiza kiasi cha maombi 10,000 yenye waombaji wenye sifa zinazohitajika.
Aidha, kutokana na wingi huo, na haki ya kila mwombaji ya kupatiwa nafasi ya kushindania nafasi hizo, ilibidi Wizara ifanye utaratibu wa kutafuta eneo lenye nafasi ya kutosha ya kuweza kuwapokea wasailiwa, ambalo hatimaye ilionekana iwe Uwanja mpya wa Taifa.
Tayari katika usaili huo wa wasailiwa zaidi ya 10,000, walishinda wasailiwa 1,281  ambao walikuwa wakiwania nafasi hizo 70.
Nantanga alitangaza kuwa washindi hao, walitarajiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha mwisho cha usaili uliofanyika Juni 30 hadi Julai 3 mwaka huu katika Bwalo la Maofisa wa Magereza, Ukonga.
Mwandishi alielezwa jana kuwa usaili wa watahiniwa wa nafasi hizo 70 za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji pamoja na Uhamiaji kuita katika usaili watu zaidi ya 10,000, haukuleta matatizo na washindi wameshapatikana. 
Wasailiwa walitakiwa kuwa na Shahada au Stashahada ya Juu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani za Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa Habari, Ualimu, Usafirishaji, Rasilimali Watu, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi Majengo na Uhandisi Mitambo.

BABA ACHARAZA VIBOKO WALIMU WAWILI TABORA

Vitendo vya baadhi ya wazazi, kudhalilisha walimu vinaendelea, ambapo mzazi mmoja Selemani Juma, amewashambulia walimu wawili kwa viboko.
Amefanya hivyo kupinga mwanawe kurudishwa nyumbani, akashone kaptura. Alifanya hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Taarifa zilizomfikia mwandishi zilibainisha kuwa Juma alidhalilisha walimu wawili wa Shule ya Msingi Nzogimlole iliyopo wilayani Nzega mkoani Tabora.
Aliwashambulia kwa viboko, akipinga kitendo cha mwalimu mmojawapo, kumrudisha nyumbani mwanawe.
Mwandishi alifika katika shule hiyo, yenye walimu tisa tu na kuzungumza na Mwalimu Mkuu Msaidizi, Emmanuel Josephat, ambaye alisema mwanafunzi huyo, Shaaban Maziku anayesoma darasa la pili, alipeleka ujumbe tofauti na alioagizwa na walimu kwa baba yake, hivyo kusababisha kadhia hiyo.
Kwa mujibu wa Mwalimu Josephat, mwalimu aliyedhalilishwa (jina limehifadhiwa), alikuwa akifundisha katika darasa hilo na alipomuona mwanafunzi huyo kavaa kaptura iliyochanika vibaya, kiasi cha sehemu za siri kuonekana, alimrudisha nyumbani kwenda kurekebisha sare yake.
Mwalimu Josephat alisema mwalimu huyo wa kiume wa darasa la pili, alimwagiza mwanafunzi wake aende kwa baba yake, akamuombe amsaidie kushona kaptura hiyo.
‘’Mwalimu hana kosa, kwani mtoto kaptura  yake ilikuwa imechanika vibaya kiasi cha sehemu zake za siri kuonekana… walimu hatupaswi tuwaache hivi watoto, mwalimu alichofanya ni kumwambia akamwambie baba yake aishone ile sare, lakini mambo hayakuwa hivyo,’’ alisema Mwalimu Josephat.
Akizungumza kwa majonzi, Mwalimu Josephat alisema mtoto huyo alipofika nyumbani, alimweleza baba yake kuwa mwalimu huyo, amechana kaptura hiyo na amemwagiza arudi nyumbani kwenda kumwambia baba huyo aishone.
Ujumbe huo unadaiwa kusababisha mzazi huyo, kufika shuleni na kuanza kutoa lugha chafu dhidi ya mwalimu huyo na baadaye baba huyo alianza kutoa kipigo.
Mwalimu Josephat alidai kuwa baba huyo, alianza kutumia mawe kurusha kwa walimu hao. Baadaye alitumia fimbo, kumchapa mwalimu huyo wa darasa la pili.
Hatua hiyo inadaiwa ilisababisha mwalimu huyo, kupiga mayowe kuomba msaada. Wananafunzi waliokuwa darasani, walitoka na kuanza kumsaidia kupiga kelele za kuomba msaada.
Mayowe hayo yalisaidia mwalimu mwenzake, Elias Kafiku kutoka ofisini kwa nia ya kuamua ugomvi huo ili wazungumze kiofisi na kufikia muafaka. Lakini, mwalimu huyo pia aliambulia kipigo.
Kutokana na kipigo hicho, mwalimu huyo wa darasa la pili alipata majeraha na kupelekwa zahanati ya kijiji, ambako alipatiwa huduma na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Akizungumza na mwandishi, mwalimu huyo wa darasa la pili alisema hali yake inaendelea vizuri. Alisema sababu ya kupigwa na mzazi huyo, hazijui kwa kuwa alitekeleza majukumu yake kama kawaida.
 Akitoa maoni yake kuhusu tukio hilo, Mwalimu Elizabeth Kafulila wa shule hiyo, alisema tukio hilo limewatia hofu katika utendaji kazi, kutokana na mzazi kuingilia majukumu ya walimu.
Mwalimu Elizabeth aliwataka wazazi kujirekebisha na kushirikiana na walimu katika kulea watoto wao, na wanapokuwa na malalamiko, wafuate taratibu za kiofisi.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Suzan Kaganda alisema   mzazi huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kupiga na kujeruhi vibaya na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika. 
Tukio hilo limekumbushia tukio la mwaka 2009 ambapo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Albert Mnali, aliamuru askari kucharaza bakora walimu wa shule za msingi wa wilaya hiyo.
Mnali anadaiwa aliwaamrisha askari Polisi kuwacharaza viboko walimu hao, kutokana na kusababisha wanafunzi kufeli mitihani pamoja na pia kuchelewa kazini.
Walimu walioripotiwa kuchapwa viboko na Mkuu huyo wa Wilaya ni wa shule za msingi za Katerero, Kanazi na Kasenene mkoani Kagera.
Walimu karibu nchi nzima, walilaani kitendo hicho, wakisema kimewadhalilisha na kimekiuka haki za binadamu.
Baadaye, Serikali ilichukua hatua ya kumstaafisha kazi Mkuu huyo wa Wilaya.

VIGOGO WANNE IMTU KORTINI SAKATA LA MABAKI YA MIILI

Vigogo wanne wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Cha Tiba na Teknolojia (IMTU),  wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, wakikabiliwa na mashitaka ya kutupa mifuko 83 yenye miili ya binadamu  kinyume cha sheria.
Washitakiwa hao ambao ni wataalamu na walimu wa IMTU ni Venlat Subbaiah (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (69) na Dinnesh Kumar (27).
Walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mawili na Wakili wa Serikali, Magoma Mtani  mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kwey Rusema.
Ilidaiwa kuwa Julai 20 mwaka huu, katika eneo la Mpiga Majohe washitakiwa wakiwa wataalamu na walimu wa IMTU, walishindwa kufukia miili ya binadamu ambayo ni  mifuko 83 kinyume na sheria, miili hiyo ilitumiwa na wanafunzi kwa ajili ya kufanya mafunzo ya vitendo.
Katika mashitaka mengine, vigogo hao wanadaiwa tarehe hiyo hiyo, walishindwa kupeleka hati kwa Ofisa Mchunguzi wa Vifo, kuonesha kuwa wamefukia miili mingapi ya binadamu  na sehemu gani.
Washitakiwa hao walikana mashitaka, ambapo Hakimu Rusema alisema ili washitakiwa wawe nje kwa dhamana, wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili  Watanzania wanaotambulika na Serikali.
Hata hivyo, wakati mchakato wa dhamana unaendelea, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salum Mohamed aliwasilisha hati ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuwafutia mashitaka washitakiwa hao.
Wakili Mohamed alidai DPP hana nia ya kuwashitaki vigogo hao kwa sasa. Pia,   alidai mashitaka hayo yameletwa mahakamani hapo kimakosa.
Kutokana na hati hiyo ya DPP, Rusema alikubali kuondoa mashitaka hayo na washitakiwa wakaachiwa. Hata hivyo, Jeshi la Polisi liliwachukua tena washitakiwa hao na kuondoka nao.
Nje ya Mahakama, Wakili wa washitakiwa hao, Gaudiosus Ishengoma alisema kitendo hicho cha kuwaachia na kuwakamata tena, kinaashiria kwamba wanataka kuwashitaki wateja wake kwa makosa, ambayo hayana dhamana.

JICHO LA TATU


WALIMU WANNE WATIMULIWA KAZI KWA MAPENZI NA WANAFUNZI

Walimu wanne wa kiume wa Shule ya Sekondari Mwembetogwa ya mjini Iringa, wamefukuzwa kazi baada ya kubainika wakijihusisha na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi.
Walimu  hao walifukuzwa  kazi takribani miezi mitatu iliyopita.
Pia,  shule hiyo ya Jumuiya ya Wazazi,  imefukuza wanafunzi wawili wa kike, kwa madai kukubuhu katika ngono. 
Mkuu wa Shule hiyo, Kevin Mlengule alisema walimu na wanafunzi hao, walibainika kujihusisha na vitendo vinavyobomoa maadili ya watumishi na wanafunzi, baada ya kupigiwa kura ya siri.
“Katika kuboresha nidhamu kwa watumishi na wanafunzi wawapo shuleni, jambo lililokuwa linatusumbua na tukaamua kulitafutia dawa kali ni la mahusiano ya mapenzi kati ya walimu na wanafunzi, na wanafunzi na watu wa mitaani,” alisema.
Alisema miaka mitatu iliyopita, lilikuwa ni jambo la kawaida kwa wanafunzi wa kike, kujihusisha katika mapenzi na walimu wao pamoja na watu wengine kutoka mitaani.
 Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wanafunzi wenye tabia hiyo, kufuatwa na wanaume shuleni muda wowote na kutoroshwa; vitendo vilivyoporomosha taaluma.
Mlengule alisema matokeo hayo, yaliwafanya baadhi ya wazazi kuwahamisha watoto wao kutoka shule hiyo.
“Shule ilikuwa na wastani wa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita 2,500 kila mwaka, matatizo hayo na mengine yaliyokuwepo, yaliifanya ibakiwe na wanafunzi wasiozidi 600,” alisema.
 Alisisitiza “hatuna mzaha hata kidogo, mwalimu na mwanafunzi atakayebainika akijihusisha na ngono katika mazingira yoyote yale, wote kwa pamoja tunawafukuza.”
 Alisema udhibiti huo, umewezesha ufaulu katika shule hiyo kuongezeka. Alisema matokeo ya kidato cha sita mwaka 2012, 2013 na 2014 ni kielelezo tosha.
 Alisema katika matokeo ya mwaka huu, hakuna mwanafunzi aliyefeli kati ya wanafunzi 156 waliofanya mtihani wa kidato cha sita.
Matokeo hayo yamefanya shule hiyo kuwa ya kwanza kati ya shule sita za kidato cha sita zilizo katika Manispaa ya Iringa. Imekuwa ya sita kimkoa kati ya shule 22. Kitaifa ni ya 47 kati ya shule 268.
Baadhi ya wazazi walipongeza uamuzi huo wa shule. “Tunataka shule nyingine ziige mfano wa shule hii, tumefarijika kusikia imechukua uamuzi huo na kwa kufanya hivyo, tunaamini shule hiyo itakuwa salama kwa watoto wetu wa kike,” alisema mmoja wa wazazi, Joachim Mwaikambo.

ATUHUMIWA KUKUTWA NA MTAMBO WA KUZALISHA DOLA FEKI

Raia wa Kongo,  Ambanipo Siva (33) aliyekiri kuishi nchini bila kuwa na kibali  amedaiwa kukutwa na mitambo ya kutengezea dola bandia za Marekani.
Wakili  kutoka Idara ya Uhamiaji,  Patrick Ngayomela alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Frank Moshi baada ya kumsomea mshitakiwa mashitaka.
Awali,  Ngayomela alidai  Julai 24 mwaka huu katika eneo la Mbezi Beach Wilaya ya Kinondoni, Siva alikutwa akiishi nchini bila kuwa na kibali. Mshitakiwa alikiri kosa hilo.
Hata hivyo  Wakili Ngayomela alishindwa kumsomea maelezo ya awali, kwa  kuwa alidai mshitakiwa huyo alipokamatwa, alikutwa akiwa na mitambo ya kutengenezea dola bandia za  Marekani.
Wakili Ngayomela aliiomba Mahakama, iruhusu mshitakiwa arudishwe Polisi ili ahojiwe waone kama watamuongezea mashitaka au la.
Hakimu Moshi aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 12 mwaka huu, kesi itakapotajwa tena. Mshitakiwa alirudishwa rumande.

POLISI KUTUMIA MAGARI YA WASHAWASHA KUDHIBITI VURUGU IDD EL FITRI

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya Ulinzi na Usalama imeimarisha ulinzi ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea Sikukuu ya Idd el Fitr kwa amani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alisema zitafanyika doria za miguu, pikipiki na magari ya washawasha, askari wa mbwa na farasi ili kuhakikisha usalama.
“Tutashirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, kampuni binafsi za ulinzi, vikosi vya uokoaji wakati wa majanga na vikundi vya ulinzi shirikishi kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza,” alisema.
Aidha, alisema kuwa kutokana na sababu za kiusalama na matishio mbalimbali katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki, jeshi hilo limepiga marufuku disko toto katika kumbi mbalimbali kutokana na sifa za kumbi hizo kutokidhi viwango vya kiusalama.
“Wananchi wanapoona dalili zozote au maandalizi ya uvunjifu wa amani watoe taarifa mapema iwezekanavyo katika vituo vya Polisi vya karibu ili hatua zichukuliwe haraka,” alisema Kova.
Alisema madereva wote wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi na kutokutumia kilevi.
Pia alisema Kikosi cha Polisi Wanamaji kitafanya doria kwenye fukwe za bahari na maeneo yote ya bahari jijini humo ambapo pia helikopta ya Jeshi la Polisi itafanya doria kuzunguka jiji hilo.
“Polisi watatoa ulinzi maalumu katika fukwe za bahari kwa kuweka vituo vya Polisi vya muda vinavyohamishika ili kutoa msaada wa haraka pindi unapohitajika. Pia askari wa kutosha watakuwepo kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani,” alisema Kamanda Kova.

KESI YA ARV'S FEKI YAPIGWA KALENDA HADI SEPTEMBA 3

Kesi ya kusambaza dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) inayomkabili Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha Tanzania Pharmacentical Ltd ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, inatarajiwa kuendelea kusikilizwa Septemba 3 mwaka huu.
Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka ambaye aliahirisha hadi Septemba 3 kwa ajili ya kusikiliza mashahidi wa upande wa mashitaka, kwa kuwa Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba  anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo mahakamani.
Mbali na kushitakiwa kwa kusambaza dawa hizo, Madabida na wenzake wanadaiwa kusababisha hasara ya Sh milioni 148 baada ya kusambaza dawa hizo kupitia kiwanda chake cha TPL kwa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD).
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni wafanyakazi wa kiwanda hicho Mkurugenzi Uendeshaji, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msoffe na Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango, pamoja na wafanyakazi wa MSD, Meneja Udhibiti Ubora, Sadick Materu na Ofisa Udhibiti Ubora, Evans Mwemezi.
Inadaiwa Aprili 5 mwaka 2011, Madabida, Shamte, Msoffe na Fatma walisambazia MSD makopo 12,252 ya dawa bandia za Antiretroviral, ikionesha zimetengenezwa Machi 2011 na mwisho wa matumizi Februari mwaka jana pia walijipatia Sh milioni 148.35 kwa madai ni malipo halali ya dawa hizo.
Materu na Mwemezi wanadaiwa, kati ya Aprili 5 na 13, 2011, Dar es Salaam, wakiwa waajiriwa wa MSD, kwa nia ya kutenda kosa la kusambaza dawa hizo, walishindwa kutumia uwezo wao wote kuzuia kutendeka kwa kosa hilo.
Katika mashitaka mengine, washitakiwa wote wanadaiwa kati ya Aprili 5 na 30, mwaka 2011, kwa nia ovu au sababu za kutotekeleza majukumu yao vizuri, waliisababishia MSD hasara ya kiasi hicho cha fedha, kutokana na kuwasambazia dawa bandia.

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMANNE - JULAI 29

MBOWE, SLAA KUTETEA NAFASI ZAO UCHAGUZI WA CHADEMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa rasmi ratiba yake ya uchaguzi wa ndani, ambapo viongozi wa taifa wa chama hicho, akiwemo mwenyekiti na katibu mkuu wapya wanatarajiwa kutangazwa Septemba 11, mwaka huu.
Pia chama hicho kimesema Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe na Katibu wake Mkuu, Dk Wilbroad Slaa, wanayo haki ya kuendelea kutetea nafasi zao hizo kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi huo, Mkurugenzi wa Kampeni za Uchaguzi wa chama hicho, Singo Kigaila, alisema ratiba hiyo, ilitolewa na kuthibitishwa na Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi Julai 18 hadi 20, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
 “Tunafahamu kuwa Dk Slaa alishatangaza ratiba nyingine ya uchaguzi wa ndani na kubainisha kuwa uchaguzi wa ngazi ya taifa utafanyika Agosti 30, mwaka huu, lakini kutokana na wageni wetu tuliowaalika na mipango kuingiliana tumeahirisha uchaguzi huo, hadi Septemba 14,” alisema Kigaila.
Alisema kwa mujibu wa kamati hiyo, pia iliidhinisha ratiba ya chaguzi zingine za ndani za chama hicho, ambapo iliazimia kuwa uchaguzi wa Baraza la Wazee Taifa utafanyika mapema zaidi  kuwezesha kusimamia uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya taifa kama Katiba ya chama hicho inavyotaka.
“Kamati pia imeazimia uchaguzi ngazi ya Kanda utafanyika baada ya uchaguzi wa ngazi ya taifa, ili kuwezesha mkutano mkuu kufanya maboresho ya Katiba ya chama hicho, kwa ajili ya kuwezesha ngazi hiyo kufanya uchaguzi kwa ufanisi zaidi,” alisema.
Alisema ratiba hiyo mpya inaonesha kuwa uchaguzi wa kata wa chama hicho utakamilika keshokutwa, uchaguzi wa majimbo na wilaya utakamilika Agosti 15, mwaka huu na uchaguzi wa Baraza la Wazee wa chama hicho utakamilika Septemba 6, mwaka huu.
Aidha alisema Ratiba hiyo pia inaonesha kuwa uchaguzi wa Baraza la Vijana wa Chadema utakamilika Septemba 10 na kufuatiwa na uchaguzi wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), Septemba 11, mwaka huu.
Uchaguzi wa Kamati Kuu ya chama hicho utakamilika Septemba 12 na kufuatiwa na uchaguzi wa Baraza Kuu Septemba 13 huku uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa chama hicho ukifuatia Septemba 14, mwaka huu na uchaguzi wa Baraza Kuu utakamilika Septemba 15 na kumalizia na uchaguzi wa Kamati Kuu mpya Septemba 16, mwaka huu.
Kigaila alisema  Kamati Kuu ya chama hicho, imeagiza kuundwa kwa kamati ya kusimamia uchaguzi wa ndani wa chama hicho ngazi ya mikoa, wilaya na majimbo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.
Alisema tayari fomu za kuwania nafasi hizo zimeanza kusambazwa kwenye ngazi husika ambapo fomu za kuwania nafasi za ngazi ya taifa zitatolewa kwa Sh 50,000, ngazi ya mikoa Sh 20,000 na ngazi ya jimbo na ngazi nyingine za chini Sh 10,000.
Kaimu Mwenyekiti wa Bawacha,  Susan Lyimo, alitaka wanawake wanachama wa chama hicho, kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo ya uchaguzi wa ndani wa Chadema kuwania nafasi mbalimbali na kuachana na tabia ya kuwa wasindikizaji.

BARABARA 12 ZANZIBAR ZAKARABATIWA

Bodi ya Mfuko wa Barabara Zanzibar umezifanyia ukarabati barabara 12 za mjini na vijijini, kwa lengo la kuimarisha huduma za usafiri kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bodi hiyo, Shomari Omar alisema barabara zilizopo Mji Mkongwe za Mkunazini na Kikwajuni, zimefanyiwa ukarabati kwa kuwekewa kifusi.
Aidha alisema barabara za Mbweni hadi Chukwani na Buyu zimefanyiwa ukarabati na sasa zinapitika kwa urahisi kiasi ya kuimarisha huduma za usafiri kwa wananchi wa maeneo hayo.
“Bodi ya Mfuko wa Barabara imeweka malengo ya kuzifanyia ukarabati barabara za mjini na vijijini kwa kiwango kikubwa kinachoelekea baadaye kuwekwa lami,” alisema Omar.
Omar alisema malengo ya pili ya bodi hiyo ni kuzifanyia ukarabati barabara za vijijini zaidi katika maeneo ya sekta ya utalii.
Alitaja barabara za vijijini zilizofanyiwa ukarabati kuwa ni Cheju hadi Unguja Ukuu, ambayo hadi kumalizika kwake itasaidia kuimarisha huduma na shughuli za kilimo.
Ofisa wa bodi hiyo, Mohamed Said alisema  Sh bilioni saba zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara hizo.
Said alisema katika awamu ya kwanza, bodi imeweka malengo ya kuzifanyia ukarabati barabara zote za Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwamo ya Mji Mkongwe ambako ni kitovu cha sekta ya utalii.

RAIS SHEIN KUHUTUBIA BARAZA LA EID

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein atalihutubia Taifa katika Baraza la Eid katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini hapa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Wakfu na Mali ya Amana, sala ya Idd kitaifa itafanyika katika Msikiti Mkuu wa Mwembe Shauri.
Taarifa hiyo ilisema Baraza la Idd , litahudhuriwa na viongozi wa juu wa nchi na litafanyika katika Hoteli ya Bwawani.
Ofisa wa Wakfu na Mali ya Amana, aliyejitambulisha kwa jina moja la Haji alisema maandalizi ya Baraza la Idd yamekamilika, ambapo Waislamu mbalimbali kutoka mikoa mitano ya Unguja wamealikwa.
Kwa kawaida hotuba ya Baraza la Idd, hutumiwa na viongozi wakuu kuelezea masuala mbalimbali, ikiwemo hali ya nchi na ustawi wa jamii.
Kwa wiki moja sasa, baadhi ya wananchi  walikuwa katika maandalizi ya Sikukuu ya Idd huku wazazi wakitafuta bidhaa mbali mbali ikiwemo chakula na nguo kwa ajili ya watoto.
Mwandishi aligundua kwamba bidhaa za nguo, zimepanda maradufu mwaka huu, kiasi baadhi ya wananchi kulazimika kufunga safari kwenda Tanzania Bara kununua bidhaa hizo.
“Bidhaa za nguo za watoto zimepanda bei zaidi mwaka huu na wazazi wengi wameenda Dar es Salaam kwa ajili ya kununua nguo ambazo zinapatikana kwa bei nafuu,” alisema Fatuma Haji, mkazi wa Zanzibar.
Bei ya nguo za watoto zimepanda na kufikia Sh 40,000 kwa kuanzia, hadi Sh 100,000. Hata hivyo bidhaa za nguo za mitumba zimekuwa zikipatikana kwa wingi na kwa bei nafuu.

SUMATRA YABARIKI UKATISHAJI TIKETI KWENYE MITANDAO

Mamlaka ya Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra) imesema haina pingamizi kwa kampuni zinazotoa huduma ya usafiri wa mabasi kwenda mikoani kutumia mfumo wa kuuza tiketi kwa njia ya mtandao.
Meneja Mawasiliano kwa Umma wa Sumatra, David Mziray  alisema hayo akijibu hoja iliyotolewa na Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua) kuwa mamlaka hiyo imekuwa kikwazo cha kutumia mfumo wa kukata tiketi kwa njia ya mtandao.
Mziray alisema  kampuni ambayo iko tayari kutumia mfumo huo inaruhusiwa ili mradi itoe tiketi halali na kwa bei halali.
“ Sisi hatuna tatizo, mmiliki anayetaka kutumia afanye hivyo. Sheria haitulazimishi kusimamia mfumo upi utumike kukata tiketi ila tunachotakiwa ni kuhakikisha tiketi inayotolewa ni halali kwa bei halali,” alisema.
Awali, Mwenyekiti wa Chakua, Hassan Mchanjama alisema: “Tumefuatilia utekelezaji wa ukataji wa tiketi za mabasi ya kwenda mikoani kwa njia ya ya mtandao ikiwamo simu na mkononi kwa muda mrefu bila mafanikio,” alisema.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) Enea Mrutu alisema pamoja na wanachama wao kuruhusiwa kutumia mfumo, utekelezaji wake ni mgumu.
“Lakini utekelezaji wake umekuwa ni mgumu kutokana na baadhi ya watoa huduma, kutokuwa wanachama wetu na pia wengine wanaogopa uharamia,” alisema.

Monday, July 28, 2014

ASKOFU ATAKA USHAURI WA RAIS KIKWETE BUNGE LA KATIBA UHESHIMIWE

Watanzania wameshauriwa kuendelea kuheshimu hadhi na mamlaka aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania, Jakaya Kikwete, kwa kuthamini na kuzingatia mwongozo na ushauri mbalimbali anaoutoa kwa wananchi, kwani mamlaka hayo yanatoka kwa Mungu.
Askofu mstaafu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Dodoma, Mhashamu Mathias Isuja, amesema hayo jana katika mahubiri yake maalumu wakati wa Misa ya Jumapili katika Parokia ya Makole, Jimbo Katoliki la Dodoma.
Misa hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiaskofu Jimbo la Kondoa.
Askofu Isuja, ambaye ni Askofu wa kwanza Mtanzania katika jimbo hilo, aliwataka Watanzania waombe Mungu, ili ajalie busara na hekima katika kutenda na kuamua mambo mbalimbali yahusuyo nchi, hasa kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya.
Alisema hafurahishwi na jinsi makundi mbalimbali ya Watanzania wanavyolumbana na kubeza hata miongozo inayotolewa na Rais Kikwete.
 “Imekuwa ni tabia kwa Watanzania kubeza na kudharau ushauri wake pasipo kujua kuwa yeye ameteuliwa na Mungu kuwaongoza Watanzania,” alisema Askofu Isuja.
Alisema ili nchi iwe na amani na upendo bila kugombana, hakuna budi kuitegemea sana busara na hekima ya Mungu, ili kusiwe na kutumbukia katika mizozo itakayohatarisha amani.
Ushauri wa Rais Kikwete alioutoa wakati akizindua Bunge Maalumu la Katiba, ambao umekuwa ukibezwa na Ukawa, ulihusu maoni yake kuhusu hatari ya muundo wa Muungano wa serikali tatu, unaopendekezwa katika Rasimu ya Katiba mpya, kwa Tanzania na Watanzania.
Katika ushauri huo, Rais Kikwete alinukuu Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, ambayo pamoja na kupendekeza muundo huo wa serikali tatu, ilieleza wazi athari zake kuwa ni pamoja na kuibuka kwa misuguano na mikwamo katika kujadili na kufanya uamuzi kuhusu mambo muhimu ya Muungano.
Athari ya pili ya muundo huo ambayo Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilieleza na ambayo Rais Kikwete aliinukuu, ni kuibuka kwa hisia za utaifa wa zamani kwa nchi washirika. 
“Nawaomba myatafakari kwa makini sana mambo haya, kwa
sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuhatarisha siyo tu ustawi na uhai wa Muungano, bali hata  usalama wa raia na mali zao. 
“Naona hata Tume haikuweza kupata ufumbuzi ulio mwafaka kabisa kwa changamoto hizi. Bila ya shaka katika mijadala yenu Waheshimiwa Wajumbe mnaweza kusaidia,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete aliwashauri wajumbe hao kuwa ni lazima lifanyike kila linalowezekana, kuhakikisha kuwa uamuzi wakati wa uendeshaji wa serikali hizo, haukwami kwani ukikwama maana yake shughuli za Muungano zitakuwa zimekwama.
“Kama hazitakwamuliwa kwa wakati ustawi wa Muungano utaathirika. Ikishindikana kabisa kupatikana ufumbuzi, Muungano unaweza kuvunjika,” aliasa Rais Kikwete.
Akizungumzia hatari ya Serikali tatu, ya kuibua na kukuza hisia za utaifa kwa nchi washirika, yaani Utanganyika na Uzanzibari, Rais Kikwete alisema hatari hiyo ni tishio kubwa sana kwa uhai wa Muungano.
“Hebu fikiria, watu walioishi pamoja kindugu na kwa kushirikiana, kama watu wamoja  na raia wa nchi moja yaani Watanzania kwa miaka 50, kuja kujikuta uhusiano wao kuwa ni kati ya Watanganyika na Wazanzibari na siyo kati ya Watanzania,” alisema.
Alikumbusha kuwa sensa iliyopita ya 2012, imebaini kuwa takribani asilimia 90 ya Watanzania waliopo sasa, wamezaliwa baada ya mwaka 1964 na nchi wanayoijua ni Tanzania.
Rais Kikwete alionya kuwa litakuwa ni jambo lenye mshituko mkubwa na athari zisizoweza kutabirika, ikiwa watu hao watajikuta ni wageni wanaotakiwa kutengenezewa utaratibu maalumu wa kusafiri na kuishi wakiwa upande wa Muungano ambao siyo kwao kwa asili. 
“Wanakuwa wageni na fursa walizokuwa wanazipata waendapo popote haiwi rahisi tena kuzipata. Katika mazingira hayo ni rahisi sana chuki kupandikizwa na watu waliokuwa ndugu mara moja watajikuta maadui.
“Aidha watu wanaweza kujikuta wakilazimika kurudi kwao kwa asili ama kwa kufukuzwa au kwa sababu ya mazingira kuwa magumu kiasi cha kuona bora waondoke. Watu hao wanaweza kulazimika kuondoka huku wakiacha nyuma kila kitu walichokichuma maishani,” aliasa Rais Kikwete.
Alionya kuwa changamoto hizo kubwa mbili za mfumo wa serikali tatu ambazo Tume imeziona, ni za kweli na si mambo ya kufikirika.
“Yale yaliyowakuta watu wenye asili ya Tanzania Bara ya kuchomewa moto biashara zao Zanzibar mwaka 2012 na watu wenye hisia kali za Uzanzibari, na kuwataka watu wa Bara waondoke Zanzibar, huenda yakawa madogo.
“Matukio ya namna hii yanaweza kutokea pande zote mbili na kusababisha maafa makubwa. Itaanza baina ya watu, baadaye itakuwa baina ya serikali zetu mbili na kufikisha nchi zetu mbili zilizokuwa ndugu na rafiki, kwa nusu karne, ghafla kuwa maadui wasioombana chumvi na wasiotakiana heri. Umoja wetu utatetereka na Muungano wetu unaweza kuvunjika. Kwa nini tufike huko?” Alihoji.
Kutokana na hoja na ushauri huo wenye maonyo, Rais Kikwete aliwataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kwa dhamana waliyopewa ya kuamua kwa niaba ya wananchi, kupima mambo hayo kwa umakini mkubwa ili wafanye uamuzi ulio sahihi.
“Tusije tukajutia uamuzi wetu tutakapoona watu wanafukuzana, wanauana na mali zao kuporwa. Na tukifikia hatua hiyo Muungano kusambaratika, halitakuwa jambo la ajabu. Kwa kweli unapoyatafakari haya, ni rahisi kuelewa kwa nini wazee wetu waasisi waliamua walivyoamua.
“Waliona mbali. Tusipuuze fikra zao na maono yao. Kuna hatari ya nchi yetu na watu wake kupoteza kila kitu tulichokijenga kwa miaka 50. Badala ya kujenga tunaweza kujikuta tumebomoa hata msingi katika nchi washirika. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1993 alituasa kuhusu hatari hiyo,” alisema.
Pia alikumbushia ushauri uliowahi kutolewa na kiongozi mmoja wa juu wa madhehebu ya dini nchini, ambaye Rais Kikwete alisema kiongozi huyo alimuuliza: “Hivi Serikali mbili zikiwa na matatizo jawabu ni kuongeza ya tatu? Si matatizo ndiyo yatazidi? Je, matatizo yakizielemea hizo Serikali tatu, si kila mtu atachukua njia yake? Mtakuwa mmepoteza kila kitu. Mimi nawashauri msichoke kutafuta majawabu kwa matatizo ya hizi mbili. Huko mnakotaka kwenda kuna hatari nyingi.”
Kutokana na ushauri huo wa kiongozi wa kidini, Rais Kikwete alisema pengine na ushauri huo wa mtu wa Mungu nao ni vyema kuupa nafasi na kuutafakari.
Baada ya kuwataka Watanzania kutilia maanani ushauri wa Rais kutokana na nguvu ya ushauri wake inayotoka kwa Mungu, Askofu Isuja pia aliasa kundi la wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa kuwataka kujipima kama wanatumia hekima katika kujadili na kuwapatia Watanzania Katiba mpya.
Alisema kutofautiana kifikra si kosa, ila pawepo na busara katika kuridhiana na kufikia hitimisho ambalo matokeo yake ni kuleta amani, umoja na ustahimilivu kwa Watanzania wote na si kama inavyoonekana hivi sasa.
Askofu Isuja alisema yeye ni Mtanzania na mtumishi wa watu, hivyo analojukumu la kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa kitu kimoja, wakisaidiana, kuheshimiana na kuvumiliana haswa pale panapotakiwa jambo la pamoja kama Watanzania.
Aliwataka viongozi wa kada mbalimbali hapa nchini, kuomba busara kutoka kwa Mungu, kama alivyofanya Suleimani aliyekuwa Mfalme wa Israel, ambaye alipopewa ufalme na Mungu, kitu cha kwanza alimwomba Mungu ampatie hekima ya kuamua mambo yote kwa haki.
Alisema, Watanzania ni wengi kiasi ambacho ni vigumu kwa kiongozi moja kutenda kwa usahihi hadi watu wote waridhike.
“Suleimani alilitambua hilo, na akaomba hekima ya Mungu ili  imwongoze kutenda kwa haki na kuamua kwa hekima,” alisema.

TAASISI YA KUFUNDISHA HISABATI YAJA, MKATABA KUSAINIWA AGOSTI 4

Serikali inatarajia kusaini makubaliano ya awali (MOU) na  Taasisi ya Masuala ya Sayansi ya Hesabu Afrika (AIMS), yatakayoiwezesha taasisi hiyo kuanzisha kampasi yake hapa nchini itakayofundisha na kuendeleza masomo ya  Hisabati na Sayansi. 
Katika taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylivia Temu, mkataba huo utasainiwa rasmi Agosti 4, mwaka huu.
Alisema kampasi hiyo itakuwa ya tano kuanzishwa na taasisi hiyo katika mataifa mbalimbali na itasaidia  kuandaa  wataalamu  wa  kuendeleza masomo  ya Hisabati na Sayansi nchini kwa njia tofauti, ikiwa  ni pamoja  na ufundishaji wa masomo hayo kwenye  ngazi  mbalimbali za elimu. 
“Kuanzishwa  kwa kampasi  hiyo  ni jitihada za  Rais Jakaya  Kikwete, aliyekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa AIMS, Profesa  Nell Turok, ambaye pia ni Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Taasisi ya  Perimetr  Institute  for  Theoretical  Physics, ambayo  ina uhusiano na AIMS,” alisema Profesa Temu.
Alisema Profesa Turok ni mzaliwa wa Afrika Kusini na ni mtoto wa Ben Turok, mpigania uhuru wa nchi hiyo ambaye ni mbunge na aliwahi kuishi Tanzania wakati wa utoto wake.
Kwa mujibu wa Profesa Temu, taasisi hiyo inayotoa shahada za utafiti kwa ngazi  mbalimbali, inalenga  kutoa wanafunzi  wenye uwezo  wa  kufanya  utafiti  wenye ubora  wa kiwango  cha juu  katika  masuala ya  sayansi.
Alibainisha kuwa AIMS imejikita  kutoa  mafunzo  katika ngazi ya Uzamili  kwenye sayansi  za Hisabati na hadi mwaka  2013, taasisi hiyo ilishaanzisha vituo  vinne Afrika  katika nchi za  Afrika Kusini, Ghana, Cameroon na Senegal.
“Serikali kwa kutambua umuhimu wa masomo ya Sayansi na mwitikio chanya uliopo sasa kwa wanafunzi kusoma masomo hayo, imeendelea kuimarisha miundombinu ya shule kwa kutoa fedha za ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa majengo ili wanafunzi wengi zaidi wasome masomo hayo,” alisema.
Serikali inafanya juhudi mbalimbali za kukabiliana na changamoto ya uhaba wa wataalamu katika fani za sayansi, kwa kujiwekea mkakati wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi aliyefaulu masomo ya Sayansi, anapangiwa taasisi ya masomo ya Sayansi.

KAMPUNI ZATAMANI KUINGIA UBIA NA ATCL

Kampuni kubwa za ndege zimeonesha nia ya kuja nchini kuingia ubia na Kampuni ya Ndege nchini (ATCL) kuongeza ufanisi na ushindani wa biashara katika usafirishaji wa anga.
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amewahakikishia wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kuwa ndani ya miezi mitatu ijayo kuanzia sasa, ATCL itakuwa imebadilishwa katika uendeshaji wake.
Alisema hivi karibuni anatarajia kwenda nchini Marekani ambako pamoja na mambo mengine, atapata fursa ya kufanya mazungumzo na mwekezaji wa nchini humo ambaye ameonesha nia ya kufahamu kuwekeza katika usafiri wa anga.
“Katika kipindi kirefu ATCL, imepitia katika misukosuko mingi ikiwemo wizi, ubabaishaji, rushwa lakini baada ya kurekebisha hesabu ya mizania mashirika mengi ya kimataifa yanataka kuwekeza katika ATCL ili kuleta ushindani katika usafiri wa anga,” alisema Dk Mwakyembe.
Alikuwa akizungumza na wafanyakazi wa TCAA mwishoni mwa wiki ambapo pia alizindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo itakayofanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mujibu wa sheria.
Akijibu swali la mmoja wa wafanyakazi, Mtesigwa Maugo aliyetaka kufahamu kuhusu uboreshaji na usimamizi wa usafiri wa anga, Dk Mwakyembe alisema wawekezaji kutoka Marekani na Oman wameonesha dhamira ya kuja nchini kuingia ubia na ATCL.
Waziri Mwakyembe aliahidi kutatua kero  ya muda mrefu ya wafanyakazi wa TCAA  na wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA)  kutakiwa kulipa Sh  50, 000 kwa mwaka kama tozo ya magari yao yanapoingia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere (JNIA).
Dk Mwakyembe alimwelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, kumpelekea kwa maandishi malalamiko yote ya wafanyakazi ayatafutie ufumbuzi na kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa tija na ufanisi mkubwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Charles Chacha alisema Sekta ya Usafiri wa Anga nchini haijakua. Alitoa mfano wa mashirika ya ndege nchini kuwa hayajaweza kushindana na mashirika mengine ya kimataifa.
Alitaja changamoto inayoikabili  mamlaka kwa sasa kuwa ni ya usimamizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa wanataaluma hasa wakaguzi.
Hata hivyo alisema juhudi zinachukuliwa  kurekebisha kasoro zilizojitokeza; ikiwa ni pamoja na kuajiri kwa mikataba ya muda mfupi wakaguzi waliostaafu na wengine kutoka katika sekta hiyo.

JICHO LA TATU