Wednesday, April 30, 2014

PINDA AAGIZA MADENI YA WALIMU YALIPWE KABLA YA JUNI 30

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameiagiza Wizara ya Fedha kuhakikisha  madeni ya walimu yamelipwa hadi kufikia Juni 30 mwaka huu, ili Serikali isiingie na madeni katika Bajeti ijayo.
Mbali na madeni ya walimu, Pinda alitaka pia madeni ya makandarasi,  pembejeo na mengineo, kulipwa ifikapo Juni 30 kutokana na madeni kuchangia kutotekelezwa vizuri kwa Bajeti ya mwaka huu.
Pinda alisema hayo jana wakati wa kikao cha wabunge cha kupokea taarifa ya mfumo wa Bajeti kwa mwaka 2014/2015  na kutaka Wizara hiyo, kuhakikisha inalipa madeni haraka.
Alisema Bajeti iliyopita, ilikumbana na changamoto nyingi, lakini katika Bajeti ya sasa, wamejipanga kuhakikisha changamoto hizo hazijirudii na inatekelezeka, kama ilivyopangwa na kutaka wabunge kupitia maelezo ya Waziri na kuyachambua kwa makini.
“Bado Bajeti inategemea misaada kutoka nje na mikopo mpaka nchi itakapokuwa na uwezo wa kujitegemea kwani kila mwaka inapungua taratibu hasa baada ya gesi toka Mtwara kufika jijini Dar es Salaam na kuwa na umeme wa uhakika na viwanda vingi kuongeza uzalishaji,” alisema Pinda.
Pinda alisema  katika kukabiliana na tatizo la mapato yasiyokuwa na kodi na katika Serikali za Mitaa kutofikiwa malengo wameunda timu maalum ya kufanyia utafiti suala hilo kwa nini hayafikii malengo na kupitia kila halmashauri kila baada ya miezi mitatu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira alisema thamani ya wazi ya utekelezaji wa miradi ya Matokeo Makubwa Sasa, imeonesha mafanikio mazuri na kukubalika kwa utaratibu huo mpya.
Wasira alisema hayo wakati akiwasilisha Rasimu ya mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2014/2015 katika Bunge lililokaa kama kamati.
Alisema katika kilimo, wametoa mafunzo ya skimu za umwagiliaji kwa maofisa ugani 95 na wakulima 95.
Alisema katika nishati, wateja wapya 138,931 wameunganishiwa umeme dhidi ya lengo la kuunganisha wateja 150,000 kwa mwaka 2013/2014 na kupunguza upotevu wa umeme kutoka asilimia 21 hadi 19.

RAIS KIKWETE ATUMA RAMBIRAMBI AJALI YA BASI SINGIDA

Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Kone kutokana na vifo vya watu 19, wakiwemo polisi wanne na viongozi watatu wa Kijiji.
Watu hao walikufa katika ajali ya barabarani, iliyosababishwa na basi la Kampuni ya Sumry,  lenye Nambari ya Usajili T. 799 BTE, lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Utaho Wilaya ya Ikungi mkoani Singida baada ya kuwagonga watu  hao, waliokusanyika katika eneo,  ambako ajali nyingine ilikuwa imetokea.
Polisi waliopoteza maisha katika ajali hiyo, walikuwa wanatoa msaada katika ajali nyingine, iliyotokea katika eneo hilo, ambapo mwendesha baiskeli aligongwa na lori na kufariki papo hapo.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Ikulu, iliyotolewa jana, Rais alisema: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 19 wakiwemo askari Polisi wanne na Viongozi watatu wa Kijiji cha Utaho katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.  Vifo hivi vimetupotezea kama Taifa nguvu kazi muhimu kwa ujenzi wa nchi yetu na hakika vimeacha simanzi na huzuni kubwa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu”.
Rais Kikwete alimuomba  Kone, kumfikishia salamu zake za rambirambi na pole nyingi kwa watu wote, waliopotelewa na ndugu na jamaa zao, kutokana na ajali hiyo.
Aliwahakikishia wafiwa kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huo mkubwa.
“Ninamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema awawezeshe kupona haraka na kurejea katika hali zao za kawaida watu wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo ili waweze kupona haraka na kuungana tena na ndugu na jamaa zao”, alisema Rais Kikwete.

JAMII YATAKIWA KUPUNGUZA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Jamii imetakiwa kupambana na kupunguza matumizi ya  dawa za kulevya, ambazo zimekuwa zikiathiri nguvu kazi kwa vijana.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, wakati akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Ikulu, wakati akipokea mpango wa kazi wa robo Bajeti mwaka 2013-2014.
Alisema njia pekee ya kupambana na kupunguza matumizi ya  dawa za kulevya, ni jamii yenyewe kuhusishwa moja kwa moja ikiwemo kuanzisha nyumba zitakazotoa ushauri nasaha na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
“Naiomba jamii kujitokeza kwa wingi kushiriki moja kwa moja katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa vijana wetu ambao wameathirika vibaya,” alisema.
Alipongeza watu waliojitolea kuanzisha nyumba zinazotoa ushauri nasaha kwa vijana na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na kurekebisha tabia zao Unguja na Pemba.
Alisema mchango wa nyumba hizo ni mkubwa na mabadiliko makubwa yamejitokeza kwa vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya na kuacha moja kwa moja.
“Nimefurahishwa na mchango wa jamii kuanzisha nyumba za ushauri nasaha kwa vijana kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, ambapo faida zake tumeziona moja kwa moja kwa sasa,” alisema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Alhabib Fereji, alisema Wizara inaendelea na juhudi za kukabiliana na hatari ya matumizi ya dawa za kulevya kwa jamii.
Alizitaja juhudi hizo ikiwemo matayarisho ya Kanuni ya Sheria ya Dawa za Kulevya, ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia kudhibiti tatizo hilo kwa vitendo.
“Tupo katika mchakato wa kutayarisha Kanuni za kupambana na  dawa za kulevya ambazo kasi yake ni kubwa pamoja na matumizi yake kwa ujumla zaidi kwa vijana,” alisema.
Aidha alisema Wizara ipo katika hatua za kutayarisha muongozo kwa matumizi ya nyumba za kurekebisha tabia na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya maarufu kwa jina la Sober house  ambazo tangu kuanzishwa kwake zimeleta mabadiliko makubwa.
Alisema kuwepo kwa kanuni na muongozo wa nyumba hizo kwa kiasi kikubwa kutasaidia kuhakikisha tatizo la matumizi ya dawa za kulevya linapungua na nyumba hizo kuwepo kwa mujibu wa sheria.
'Serikali inaridhishwa sana na kuwepo kwa nyumba za kurekebisha tabia kwa vijana kuachana na matumizi ya dawa za kulevya maarufu sober ambazo zimesaidia vijana wengi kuacha matumizi ya dawa za kulevya' alisema Fereji.
Hata hivyo, Fereji alikiri kuwepo kwa changamoto ya bandari ambazo sio rasmi kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha uingizaji wa dawa za kulevya Zanzibar.
'Zanzibar hivi sasa zipo bandari bubu nyingi ambazo zinatumiwa kwa njia moja au  nyingine kuingiza dawa za kulevya na kusababisha taifa kuangamia' alisema Fereji.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza wakati wa kupitia mpango wa Bajeti ya 2014/2015 jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijadiliana jambo kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa  wakuu wa nchi za  Jumuiya ya Afrika Masharariki uliofanyika mjini Arusha jana. (Picha na Freddy Maro).

Wafuasi wa Shehe Ponda Issa Ponda wakipiga kelele nje ya mahakama jana baada ya kesi ya Shehe huyo kushindwa kusikilizwa.

Jaji wa Mahakama kuu Mhe.Njengafibili Mwaikugile akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu  katika ofisi za Mahakama kuu jijini Dar es Salaam wakati IGP alipokwenda kula kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza.Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil na kushoto ni  DCI Issaya Mngulu.

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATANO




MTIHANI MPYA KIDATO CHA NNE HUU HAPA, KUSAMBAZWA MEI 10

Wanafunzi wa Kidato cha Nne, watafanya mitihani miwili ya Taifa mwaka huu, baada ya kuongezwa mtihani wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), ambao utatumika kuwapima walivyojiandaa na Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Sekondari.
Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Paulina Mkonongo, alitangaza utaratibu huo jana na kufafanua kwamba lengo ni   kubaini wanaohitaji msaada kabla ya mtihani wa mwisho, ili kuboresha taaluma darasani. 
Kwa mujibu wa Paulina, mtihani huo wa BRN, utafanyika kwa masomo machache lakini yanayosomwa na wanafunzi wote ambayo ni Baiolojia, Hisabati, Kiswahili na Kiingereza.
Paulina alisema mtihani huo wa majaribio, tayari umeanza kuandaliwa na utasambazwa kwa maofisa Elimu nchini ifikapo Mei 10 mwaka huu, na barua kuhusu kufanyika kwa mtihani huo imeshatumwa kwa makatibu tawala wote, ili kuanza maandalizi.
Matokeo ya mtihani huo, yanatarajiwa kutumika kubaini mada ngumu kwa wanafunzi,  wanaohitaji msaada na kuwapa walimu mwanga kuhusu wapi wanafunzi hao wanahitaji msaada na lengo ni kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Tayari  tangu mwaka jana mikoa 12 ilianza kushiriki katika programu iliyohusisha mafunzo kwa walimu 4,064 wa masomo husika, na mikoa 13 iliyosalia itashiriki programu hiyo mwaka huu. 
Mafunzo ya walimu wa mikoa hiyo 13 kwa mujibu wa Paulina, yatafanyika Juni 2014 na programu ya mafunzo rekebishi kwa wanafunzi wenye upungufu, itaanza Julai mwaka huu kulingana na matokeo ya mtihani watakaofanya.
“Tutatoa mtihani wa majaribio kwa wanafunzi wa kidato cha nne, ili kubaini maeneo yenye wanafunzi wanaohitaji msaada zaidi na kutoa utaratibu wa mafunzo rekebishi na mafunzo kazini,  ili kuwajengea uwezo walimu wa kuwasaidia wanafunzi walioko kwenye hatari ya kutofanya vema,” alisema Paulina.
Hata hivyo, Paulina alisema katika utekelezaji utoaji wa mtihani huo, wanakabiliwa na changamoto ya kuwapatia mafunzo wakuu wa shule zisizo za serikali, kuchapisha kitabu cha mwongozo na ziara za wasimamizi wa elimu katika ngazi mbalimbali kutoa ushauri.
Tayari walimu wakuu 3,001 wa shule za Serikali wamepatiwa mafunzo na Taasisi ya Uongozi wa Elimu Bagamoyo (ADEM) katika maeneo yaliyoainishwa, huku kitabu hicho cha mwongozo kikiwekwa kwenye tovuti ya Wizara.
Paulina alisema mikakati endelevu iliyopo, inalenga kuendeleza mafunzo ya walimu kazini, ili kuwajengea uwezo kulingana na wakati na mahitaji ya mitaala.
Mbali na mafunzo hayo, pia wanalenga kuwajengea walimu tabia ya kutunga mitihani bora ya kupima mchakato wa ufundishaji, kubaini wanafunzi wanaohitaji kusaidiwa zaidi, kubaini mada ngumu na kutoa mafunzo rekebishi kwa wanafunzi.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde, alisema vitabu rekebishi vitaonesha wanafunzi waliofanya vizuri katika kila swali, waliojibu vibaya na swali lilikuwa likitaka nini.
Vitabu hivyo vitasaidia walimu na wanafunzi kubaini makosa mbalimbali yanayofanywa na watahiniwa wakati wa kujibu maswali na kutumia mbinu bora za kujibu maswali.
“Mwisho wa vitabu hivyo, kuna mada zilizofanywa vizuri na vibaya na jinsi ya kusaidia walimu wahakikishe wanafunzi wanafaulu mada hizo,” alisema.
Vitabu hivyo kwa shule za msingi vimetolewa vya masomo ya Kiswahili, Hisabati, Kiingereza, Sayansi na Maarifa ya Jamii kwa ajili ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2012 na 2013.
Kwa sekondari, vimetolewa kwa masomo ya Hisabati, Uraia, Historia, Jiografia, Kiswahili, Kiingereza, Baiolojia, Kemia na Fizikia kwa mwaka huo.
Dk Msonde alisema Baraza pia limepewa jukumu la kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu, ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za msingi na sekondari, na kuwajengea walimu na wanafunzi hali ya ushindani na kujitambua kama shule imepanda au imeshuka.
Makundi ya ufaulu yatapangwa kwa kutumia rangi za kijani kwa shule zenye ufaulu wa juu, njano kwa zenye ufaulu wa kati na nyekundu kwa shule zenye ufaulu wa chini kwa shule za msingi na sekondari.

AJINYONGA CHOONI BAADA YA KUMKUMBUKA MKEWE

Mkazi wa Mtoni Kijichi, Richard Kijazi (36) amekutwa amekufa kwa kujinyonga chooni na kuacha ujumbe kwamba amejiua kwa sababu ya kumkumbuka marehemu mkewe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema jana kuwa Kijazi alijiua juzi saa 11:15 jioni katika maeneo ya Mtoni Kijichi, Wilaya ya Temeke.
Alisema Kijazi alikutwa amejinyonga kwa kutumia kitambaa cha nguo alichokitundika kwenye kenchi ya choo ya nyumba anayoishi.
Ujumbe uliokutwa katika eneo hilo ulisomeka: “Hajahusika mtu yeyote kuhusu hili, nimemmiss Mama John wangu, nizikwe Dar es Salaam na Mchungaji Haule naomba ujumbe huu uheshimiwe.”
Kwa mujibu wa Kamanda Kiondo, uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mama John alifariki mwaka 2012 baada ya kuugua malaria na  tangu wakati huo Kijazi alikuwa akijaribu kujiua na kuokolewa na ndugu zake. Maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.
Katika tukio jingine, Kamanda Kiondo alisema, Mwendesha Pikipiki, Said Jongo (32) amekufa papo hapo baada ya kugongwa kwa nyuma na gari aina ya Toyota Coaster lenye namba T412 ATJ.
 Ajali hiyo ilitokea juzi saa 12:00 jioni katika Barabara ya Chamazi eneo la Charambe Magengeni, ambapo gari hilo likiendeshwa na mtu asiyefahamika akitoka Mabagala Rangi Tatu kwenda Chamazi,  liligonga kwa nyuma pikipiki yenye namba T281 CKY aina ya Fekon, iliyokuwa ikiendeshwa na Jongo.
Mwili wa Jongo umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na dereva wa gari hilo aliyekimbia baada ya ajali bado anatafutwa, gari liko katika Kituo cha Polisi Mbagala.
Katika tukio la tatu, mkazi wa Majohe aliyetambuliwa kwa jina la Erasmus Marshal (52), amekutwa amekufa chumbani kwake   huku mwili ukiwa umeanza kuharibika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema mwili wa Minangi ulikutwa juzi saa 7:00 mchana huko Majohe Kichangani ukiwa umekaa kitandani huku umefunikwa shuka na  mezani kwake kulikutwa mabaki ya chakula aina ya utumbo na soda ya Azam Malta.
Uchunguzi wa awali kwa mujibu wa Kamanda Minangi, umeonesha kuwa enzi za uhai wake alikuwa akiishi peke yake kwenye nyumba hiyo  na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

MLIBERIA ALIYEKAMATWA NA HEROIN ANYIMWA DHAMANA

Raia wa Liberia, Deocntee Togbah (28) anayekabiliwa na mashitaka ya kuingiza dawa za kulevya aina ya heroin, zenye thamani ya Sh milioni 38, amenyimwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alimnyima dhamana mshitakiwa huyo, kwa kuwa mashitaka yanayomkabili hayana dhamana na Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Kesi imefunguliwa katika Mahakama hiyo kwa hatua za awali na upelelezi ukikamilika, itahamishiwa Mahakama Kuu kuanza kusikilizwa.
Togbah anatuhumiwa Aprili 25, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,  aliingiza  gramu 862.3 za dawa hizo za kulevya zenye thamani ya Sh milioni 38.803.
Upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ili wakamilishe upelelezi.
Mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka yake na kurudishwa rumande hadi Mei 12, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

WANAWAKE 100 SALAMA DHIDI YA SARATANI YA KIZAZI

Zaidi ya wanawake 100 waliojitokeza kupima maambukizi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi katika Jukwaa la Familia Kitchen Party Gala, lililofanyika Dar es Salaam juzi, wamethibitika kutokuwa na ugonjwa huo.
Jukwaa hilo hufanyika katika mikoa mbalimbali chini ya ufadhili wa Shirika linalojishughulisha na masuala ya afya la PSI Tanzania kwa ushirikiano na Asasi ya Women in Balance ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia upimaji huo uliofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee juzi jioni, Meneja wa Mradi wa Uzazi wa Mpango wa PSI, Catheline Paul alisema zaidi ya wanawake 100 waliopima wamekutwa hawana maambukizi ya ugonjwa huo ambao ni tishio kwa wanawake nchini.
“Imekuwa ni bahati nzuri kwamba tofauti na Dodoma na Mwanza ambako karibu wanawake tisa walikutwa wana ugonjwa huo, leo kwa Dar es Salaam wanawake waliopima wamethibitika kuwa hawana maambukizi na wamepewa elimu ya kujikinga,” alisema Paul.
Awali, Mratibu wa Familia Kitchen Party Gala, Vida Mndolwa alisema hamasa ya wanawake kujitokeza kupima afya kupitia jukwaa hilo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hatua inayotoa matumaini ya kupungua kwa vifo vya akinamama kutokana na masuala ya uzazi.
Alisema kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwa mikoa ya Dodoma, Mwanza na Dar es Salaam, ni azma ya waandaaji kuona kuwa wanawake katika maeneo mengine nchini wanafikiwa ili kupewa elimu kuhusu afya ya uzazi, Ukimwi, malaria, ndoa, malezi ya watoto na ujasiriamali.
“Kama inavyofahamika kuwa ni vigumu kuweza kuwakusanya wanawake wengi kiasi hiki ili kuwafanyia vipimo vya afya zao, lakini kupitia jukwaa hili mwamko wao umekuwa ni mkubwa kwani pamoja na kupima afya wamekuwa wanapata burudani na kuzungumza masuala yanayohusu kujitambua na kujithamini,” alisema Mndolwa.
Mratibu wa Mawasiliano wa PSI, Mohammed Mziray alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Asasi ya Women in Balance katika kuendesha jukwaa hilo katika maeneo mbalimbali nchini baada ya majaribio ya awali katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Dar es Salaam kuonesha mafanikio makubwa.

WAKILI ADAI KESI YA MWALE ILIFUNGULIWA KIMAKOSA

Upande wa utetezi kwenye kesi ya wakili maarufu jijini hapa, Median Mwale na wenzake watatu  ya kutakatisha fedha haramu, umedai mashitaka hayo dhidi ya washitakiwa, yalifunguliwa kimakosa kabla ya sheria iliyowashitaki kutungwa.
Kutokana na hoja hiyo, wakili wa upande wa utetezi, Omary Iddi Omary  ameomba kesi hiyo ihamishiwe Mahakama Kuu kupata tafsiri ya kisheria.
Aidha, wakili huyo amelalamikia  kile alichodai ni ucheleweshaji wa makusudi wa kuanza, kusikilizwa kwa kesi unaofanywa na upande wa Serikali kwa kigezo kwamba upelelezi haujakamilika huku wateja wake wakiendelea kusota rumande kwa miaka mitatu sasa.
Alidai hayo jana mbele ya  Hakimu Mkazi Mfawidhi, Devota Kamuzora. Wakili  huyo anasaidiana na Mawakili, Mosses Mahuna na Modest Akida huku upande wa Serikali ukiwakilishwa na Wakili, Tumaini Kweka.
Alidai  kifungu kilichotumika kufungua mashtaka dhidi ya Mwale na wenzake, Elius Ndenjembi, Don Bosco Gichana na Bonifas Mimbwa wanaoshikiliwa kwa muda wa miaka mitatu sasa ni kile kilichofanyiwa mabadiliko Februari 24, 2012, wakati wateja wake wakiwa mahabusu, jambo alilodai kuwa ni kinyume cha sheria.
Omary ambaye aliwasilisha hoja nne tofauti akitaka Mahakama hiyo iwape idhini ya kwenda Mahakama Kuu, alisema hata shtaka lingine walilofunguliwa wateja wake, chini ya Sheria ya Uzuiaji Utakatishaji wa Fedha Haramu ya mwaka 2006, ina upungufu mkubwa kisheria na hivyo si halali.
Alisema  sheria hiyo iliwekwa kwenye Gazeti la Serikali Januari 12, 2006 kabla ya kusainiwa na Rais mwaka  2007, jambo alilodai kuwa linakwenda kinyume na Katiba ya nchi, inayoeleza utaratibu wa kutunga sheria kuwa mara baada ya muswada kupitishwa na Bunge hupelekwa kwa Rais ili aidhinishe kisha itangazwe kwenye gazeti la Serikali ndipo ianze kutumika.
“Mheshimiwa hakimu, kutokana na ukiukwaji wa taratibu hizo, inafanya sheria ya  Utakatishaji Fedha Haramu ya mwaka 2006 isiwepo, hii ina maana hata  washtakiwa  hawa wanashikiliwa kwa kutumia sheria ambayo haipo, hata kosa wanaloshtakiwa nalo halipo kwenye sheria za sasa.’’
Alidai; “ Katika mazingira hayo hakuna shaka kuwa hapa hakuna mashtaka sahihi, na hapa wameweka mtego fulani upande wa mashtaka lakini sisi tunasema tunataka kwenda Mahakama Kuu ili Mahakama hiyo iangalie suala hilo.”
Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka akijibu hoja hizo alidai hazina msingi kwa madai kuwa sheria hutumika baada ya kupitishwa na Bunge na kuwa imefuata michakato yote.
“Nafikiri wameleta malalamiko kwenye eneo lisilo sahihi, kwani hata kwa mujibu wa uanzishwaji wa Mahakama hii sidhani kama wewe ( Hakimu) unaweza kuamua mashauri ya Manyara, hii ni sawa na kumtuma mtoto akachukue chakula cha mlinzi,” alisema Wakili Kweka jambo lilomfanya Hakimu kuingilia kati na kumtaka afute kauli yake hiyo ya kumfananisha yeye na mlinzi.
Hata hivyo wakili huyo alisisitiza kuwa shauri hilo lipo mahakamani hapo kwa ajili ya kuahirishwa na kupangiwa tarehe nyingine kwa maelezo kuwa Mahakama hiyo haina nguvu kisheria kusikiliza shauri hilo.
“Upelelezi wa kesi hii ni kweli umechukua muda mrefu lakini ikumbukwe kuwa kesi hii ni ya kutakatisha fedha na hakuna sheria inayoweka mipaka ya lini upelelezi uishie ndio maana nimeomba tarehe nyingine lakini wenzangu wamekuja na hoja ya kupinga sheria iliyotumika kuwashtaki washtakiwa. ‘’
Wakili Mahuna alisema kuwa hata wao wanajua kuwa Mahakama hiyo, haina mamlaka kisheria kusikiliza shauri hilo, ndiyo maana wanaomba kupewa idhini kwenda Mahakama Kuu, wakapatiwe ufafanuzi wa kisheria juu ya yale wanayoyalalamikia.
“Tunasikitika kwa upande wa Serikali kila siku kuomba tarehe ya kesi kutajwa, kimsingi haturidhishwi na mwenendo huu, upande wa Jamhuri unatumia mamlaka yake vibaya, tunaomba leo watuambie ni lini hasa upelelezi utakamilika kwani hawaoneshi utayari na hawana hoja ya msingi zaidi ya kauli hiyo kila mara,” alisema Wakili Mahuna.
Hakimu Kamuzora alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili na atatoa uamuzi wa awali  Mei 12, mwaka huu.

WAFANYAKAZI STRABAG WAENDELEA NA MGOMO WAO

Wafanyakazi wa Kampuni ya ujenzi ya Strabag, wameingia siku ya pili ya mgomo wao huku wakishinikiza kulipwa marupurupu mbalimbali, wanayoyadai kwa zaidi ya miezi saba hadi sasa.
Awali, wakizungumza nje ya ofisi za kampuni hiyo zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam juzi, wafanyakazi hao wanaojenga barabara za mabasi yaendayo kasi chini ya Mradi wa DART, walisema walifikia hatua ya kugoma kwa madai ya kuona wanazungushwa kupewa marupurupu hayo huku wakihofu muda uliobaki kwa kampuni hiyo kabla ya kumaliza kazi yake.
“Marupurupu hayo yanayohusisha fedha za chakula, usafiri, matibabu ambayo jumla yake ni shilingi elfu sabini kwa kila mwezi yapo katika mkataba wa kazi na  mwanzoni tulikuwa tukilipwa lakini cha kushangaza baadaye yalisitishwa bila sababu zozote za msingi,” walisema wafanyakazi hao, ambao hata hivyo hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini.
Kwa mujibu  wao, muda wa kampuni hiyo kumaliza kazi ya ujenzi wa barabara hiyo, unaelekea ukingoni jambo linalowapa hofu ya kupewa malipo hayo huku kesi ya msingi iliyopo mahakamani ikiwa bado haijakwisha wala kujua  itakwisha lini huku wakidai kuendelea kuumizwa na majukumu mbalimbali ya kimaisha.
“Walikimbilia kufungua kesi katika Mahakama ya Kazi ya Kinondoni kutaka kuondolewa kwa malipo hayo, na hadi sasa ni miezi saba kesi bado  ipo mahakamani ikipigwa danadana hatujui lini itakwisha na kama unavyojua karibu wanamaliza kazi tuna hofu haki yetu kupotea,” walisema wafanyakazi hao.
Walisema wakati wao wakifanyiwa kitendo hicho, wafanyakazi wenzao kutoka nchi za Kenya,Kongo na India wanaendelea kulipwa marupurupu hayo kama kawaida huku wakidai kuwa hawaelewi kwa nini wanafanyiwa hivyo wakati kazi wanazozifanya wao zinalingana na wafanyakazi hao wa kigeni.
Wafanyakazi wakiwemo   madereva, waendeshaji wa mitambo, wasimamizi na makundi mengine walisema wanachotaka ni malipo yao bila kujua lini hatma ya kesi iliyotolewa itafikiwa vinginevyo  hawatokuwa tayari kurejea kazini.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana amewataka wafanyakazi hao kurejea kazini wakati suala lao likiendelea kushughulikiwa na mamlaka zinazohusika.
Akizungumza na mwandishi jana, alisema baada ya kupata taarifa hizo juzi, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, uongozi wa Strabag, viongozi wa wakala wa Barabara nchini (TANROADS) pamoja na viongozi wa Ofisi ya DART walikutana kuzungumzia suala hilo alilosema kuwa hata hivyo linahitaji busara kwa kuwa kesi yake bado ipo mahakamani.

KAMPUNI TISA ZA MAFUTA ZAFUTIWA LESENI

Bodi ya Wakurugenzi  ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imefuta leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa kampuni tisa,  zinazojihusisha na biashara hiyo hapa nchini.
Uamzi huo ulifanywa jana katika kikao  cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura,  Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa leseni hizo, kumetokana na ukiukaji wa sheria na kanuni za biashara hiyo.
Ngamlagosi katika taarifa yake, alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa leseni hizo na Ewura.
Kampuni zilizofutiwa leseni ni Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.
Mamlaka hiyo imeundwa chini ya sheria ya Ewura Sura Namba 414 ya Sheria za Tanzania.  Mamlaka hiyo ina majukumu ya kusimamia shughuli za udhibiti, kiufundi na kiuchumi  katika  sekta za Petroli, Umeme, Gasi Asili na Maji Safi na Maji Taka.

LHRC YATAKA CHOMBO KUDHIBITI MASHARTI YA KUKOPA

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeiomba Serikali iunde mamlaka ya kudhibiti taasisi za mikopo, kutoa riba nafuu na masharti rahisi, wananchi wa sekta zisizo rasmi waweze kunufaika.
Imeelezwa kwamba baadhi ya  taasisi, zimekuwa si rafiki kwa wajasiriamali kwa kulenga zaidi kufilisi mali za dhamana, huku zingine hazijasajiliwa kisheria na zimekuwa zikitapeli wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Flaviana Charles  aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia umuhimu wa serikali, kudhibiti taasisi za kukopesha fedha.
Alisema zaidi ya kesi 26 kwa mwaka zimeripotiwa katika ofisi zilizopo Arusha,  juu ya utapeli na ukiukwaji unaofanywa na taasisi za mikopo.
Alisema Serikali kupitia Wizara husika, iweke utaratibu mzuri wa kusajili vikundi vya wajasiriamali, ambao wamejikusanya, wapatiwe mikopo kiurahisi.
‘’Watunga sera wanatakiwa kutunga sera mahsusi zitakazoweka misingi kwa sekta zisizo rasmi  kwani hatuna sera inayozungumzia sekta hiyo ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wote,’’ alisema Charles.
Aliongeza kwa serikali za mitaa kupitia halmashauri, wapewe mamlaka kamili ya kuvitambua vikundi vya wajasiriamali na kuwapatia hati ya utambuzi  kupata mikopo katika taasisi za mikopo.
‘’Tukiyafanya hayo, Serikali itaboresha mazingira ya wananchi waliojiajiri katika sekta zisizo rasmi, itaruhusu wananchi wengi hasa vijana na wanawake ambao hawana ajira kuingia katika sekta hiyo na kuongeza pato la Taifa,’’ aliongeza.
Alifafanua kwamba LHRC imeanzisha Mradi wa Kazi na Staha kwa wananchi waliojiajiri katika sekta zisizo rasmi kuwezesha kupata tija katika shughuli zao.
Alisema katika mradi huo, wamefanikiwa kunufaisha vikundi 36, kati ya hivyo na vikundi 20 vya wanawake na 16 vya vijana, kutoka vikundi 620 vya akinamama na vikundi 175 vya vijana.
Alisema wameweza kuwajengea uwezo wajasiriamali hao kwa kuwajengea uelewa juu ya haki za binadamu, haki na wajibu, taratibu za kisheria katika usajili na leseni ya biashara.

MRADI WAPONGEZWA KWA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI

Serikali imepongeza juhudi zilizofanywa na Mradi wa Champion  katika  kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
Hayo yalisemwa jana na Mganga Mkuu wa Serikali, Donan Mmbando katika mkutano wa kufunga mradi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema mradi huo ulioanzishwa mwaka 2008, umekuwa ukiwasaidia wanaume kujihusisha katika kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
Alisema lengo ni kuongeza juhudi za kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo na utoaji wa elimu katika Kamati za Ukimwi katika ngazi zote.
“Kiwango cha maambukizi kimepungua kwa asilimia 18 mwaka 1988 hadi 5.1 kwa mwaka huu,” alisema Mmbando.
Alisema kazi kubwa wanayoifanya ni kuzuia maambukizi mapya,  kuhakikisha watu wote wanapata huduma na kuwasaidia wagonjwa katika upataji wa huduma.
Aidha alisema wamepata fursa ya kuzuia na kutibu kifua kikuu kwa waathirika na wameshirikiana na taasisi na asasi mbalimbali katika kuelimisha jamii.
Juhudi nyingine ni kutoa elimu kuhusu tohara kwa mikoa yenye maambukizi makubwa ya Ukimwi, utokomezaji wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Katika maoni yake, Mkuu wa Championi,  Jane Schueller alisema mradi  ulizinduliwa Februari 2008 na watu wa Marekani na kuungwa mkono na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Alisema watu 345,000 wamefikiwa na mradi wa kupambana na Ukimwi na Afya ya Uzazi na wengine  260,000 walifikiwa na mradi huo kwa kupewa elimu dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti  Ukimwi (Tacaids), Fatma Mrisho alisema mradi huo umeleta usawa wa jinsia katika jamii na kuhakikisha wanaume wanakuwa karibu katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

MFUKO WA SEKTA BINAFSI WAZINDULIWA

Rais Jakaya Kikwete amezindua mfuko wa sekta binafsi wa kuwezesha wawekezaji nchini katika kupata mtaji, utakaokuza biashara na kukuza uchumi nchini.
Mfuko huo unajulikana kama Mkoba, unalenga kutoa mitaji inayoanzia dola milioni moja hadi milioni 15.
Hafla ya uzinduzi huo, ilifanyika jana Dar es Salaam ambapo Rais Kikwete alisema ujio wa mfuko huo ni fursa kubwa itakayosaidia kutoa mitaji haswa kwa wajasiriamali wadogo . Iliandaliwa na Taasisi  Uongozi Institute na Mkoba.
Alisema nchi yoyote inayokua kiuchumi husaidiwa na sekta binafsi ambao hupatiwa mitaji yenye kukuza biashara zao katika mazingira yaliyo nafuu.
“Mashirika mengi ya sekta binafsi hutegemea sana mikopo kutoka katika taasisi za fedha ili kuboresha biashara zao ambayo riba yake huwa kubwa," alisema na kuongeza kuwa mkoba umekuja kwa wakati muafaka.
Alisema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika inayokua kiuchumi, jambo ambalo
linapanua wigo wa biashara pamoja na kuongeza  wawekezaji  kutoka nje ya nchi.
Rais Kikwete alisema kuingia kwa mkoba nchini, kunaleta ushindani katika kuzalisha bidhaa  na kuongeza masoko kwa biashara za ndani zitakazopelekea kukua kwa kampuni kwa kiwango kikubwa.
“Uwezo wa kupata fedha ni changamoto kubwa nchini kwa wajasiriamali wengi wadogo na kuja kwa mkoba ni njia madhubuti ya kukuza uchumi ambao kwa sasa umekuwa kwa asilimia saba,” alisema .
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoba, Dk Frannie Leautier alisema  mfuko huo utawezesha mitaji kwa wawekezaji na lengo kubwa ni kukuza uchumi kwa nchi za Afrika.
Alisema wajasiriamali wadogo na wa kati  wamekuwa wakizalisha ajira na kukuza uchumi ingawa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya mtaji.
“Ujio wa mkoba ni mahsusi kwa kuitoa pengo lililopo la kukua kibiashara kwa kuwa na wigo wa kupata mitaji kwani zipo baadhi ya biashara ambazo zinashindwa kukua kwa kukosa uwezo wa kifedha,” alisema Leautier.
Dk Frannie alisema mkoba inatarajia kuwa na dola milioni 300  ambazo zitawekezwa katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati, ubunifu ili kuwezesha maendeleo yenye kukuza uchumi.

MKUU WA WILAYA ILALA ATAKA WATENDAJI KUWA WAAMINIFU

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Raymond Mushi amewataka watendaji wa kata, mitaa na wenyeviti , kutanguliza mbele suala la uaminifu katika ukusanyaji kodi za majengo ili kuiwezesha wilaya hiyo kufikia Malengo ya Matokeo Makubwa  Sasa (BRN).
Mushi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi, alipofungua semina ya siku moja ya watendaji na wenyeviti hao kutoka Tarafa ya Ukonga, iliyokuwa na lengo la kuwapa elimu juu ya suala zima la ukusanyaji wa mapato hayo.
Alisema ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa asilimia mia moja yaliyowekwa na wilaya hiyo, kila mtendaji hana budi kujipima kutokana na utendaji wake hatua aliyosema pia itamsaidia kutoa elimu kwa wananchi wanaomzunguka katika eneo lake.
“Nyinyi kama viongozi  mnapaswa kujituma ili malengo yaweze kufikiwa na kubwa zaidi itakuwa vizuri kama mtaweka mbele suala la  uaminifu wakati wa ukusanyaji wa mapato hayo vinginevyo hakuna mafanikio yoyote yanayoweza kufikiwa,” alisema Mushi.
Aidha alisema malengo ya wilaya hiyo ni kuongoza katika maeneo mbalimbali dhidi ya wilaya zingine zote na hivyo kuwa mfano jambo alilosema litafanikiwa  kama viongozi hao watajituma na kuzingatia ushauri unaotolewa kwao.
“Tunataka wilaya yetu iwe ya mfano katika ulinzi na usalama ili watu waweze kuishi kwa amani, hivyo ili iwe salama ni vizuri kuwandaa watu kuanzia sasa kwa kuwa thamani ya mtu hupanuka kwa kuongeza upeo wake tuna kila sababu kutia mkazo katika suala hili la Matokeo Makubwa Sasa kielimu ili tufike huko,” aliongeza Mushi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Fedha kutoka wilaya hiyo, Stellah Mgumia aliwataka watendaji na wenyeviti hao kusimamia vyema suala zima la ukusanyaji wa mapato ili kuiwezesha wilaya hiyo kufikia malengo waliyojiwekea.
Alisema lengo la Serikali kurejesha suala la ukusanyaji kodi za majengo katika halmashauri, lilitokana na maombi yaliyokuwa yametolewa na halmashauri hizo, hivyo wanapaswa kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuonesha kwa vitendo dhamira yao ya kulitaka hilo.
Alisema ni jambo la fedheha kuiona baadhi ya mitaa inasuasua katika ukusanyaji wa kodi hizo, jambo alilosema linatia shaka kufikiwa kwa malengo waliyojiwekea.

RAIS KIKWETE AMTUMIA SALAMU MFALME WA UHOLANZI

Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za pongezi Mfalme wa Uholanzi, Willem Alexander kwa kutimiza umri wa miaka 47 jana.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mataifa, imemkariri Rais Kikwete akimhakikishia mfalme huyo kwamba uhusiano wa nchi yake na Tanzania utaendelea kuwepo.
“Ni furaha yangu, kwa niaba ya wananchi na Serikali ya Tanzania kukupongeza kwa kutimiza miaka 47,” alisema Rais Kikwete.
Aliendelea kusema, “wakati ukiendelea kusherehekea siku ya kuzaliwa kwako, nichukue nafasi hii kukueleza namna ninavyoridhishwa na uhusiano uliopo baina ya watu na nchi .”
Alimhakikishia kwamba Tanzania  itaendelea kufanya kazi naye pamoja na serikali yake kuimarisha uhusiano wa karibu na wa muda mrefu kwa faida ya pande zote.

LAKE OIL YATOA MISAADA KWA HOSPITALI TATU

Kampuni ya Lake Oil imetoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya  milioni 11.3  katika hospitali tatu za halmashauri za manispaa  za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Msaada huo kwa hospitali za Mwananyamala (Kinondoni), Amana (Ilala) na Temeke, unalenga kupunguza changamoto za utoaji huduma za afya katika hospitali za umma nchini.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vya kujifungulia kwa wajawazito, viti vya kubebea na kukalia wagonjwa, mashine za kupima shinikizo la damu na taa za uchunguzi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Ackim Mwaikasu alisema msaada huo umetolewa wakati muafaka ikizingatiwa kwamba hospitali husika zinakabiliwa na ukosefu wa vifaa mbalimbali.
“Ni kutokana na ukweli huo ndio maana tunaona msaada wa Kampuni ya Lake Oil umefika kwa wakati mwafaka na tungependa kampuni nyingine pia ziige mfano huu,” alisema Mwaikasu.
Meneja wa Lake Oil, Khaled Mohamed, alisema kampuni yake inaamini msaada huo utasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na sababu nyingine zinazoweza kuzuilika.
“Tumegundua kuwa vifo vingi katika hospitali zetu vinatokana na sababu ambazo tunaweza kuzizuia...kama kampuni, tunafanya biashara na watu na furaha yetu ni pale tunapochangia katika kuboresha afya ya jamii inayotuzunguka,” alisema Mohamed.
Alieleza kwamba hospitali hizo zilichaguliwa kutokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hupata huduma za afya katika hospitali hizo.
Kampuni hiyo ilisajiliwa nchini mwaka 2005 na kuanza shughuli za uuzaji mafuta  jijini Dar es Salaam Machi, 2006. Hivi sasa ina vituo 73 vya kuuzia mafuta nchini.

RONALDO BREAKS RECORD AS BRILLIANT REAL SCORE FOUR TO REACH FINAL

Real Madrid booked their place in the Champions League final with a hugely impressive 4-0 victory against Bayern Munich.
Three first-half goals shocked the home side, who were constantly at risk from counter-attacks and set-pieces, unable to defend with confidence.
Sergio Ramos scored twice, the first coming from a simple Luka Modric corner, with no Bayern player marking him. A few minutes later, he and Real had their second when Pepe glanced on Angel Di Maria's cross, and the Spain defender was lurking to fire past Manuel Neuer again.
Cristiano Ronaldo then scored his 15th of his Champions League campaign - a record - by sweeping home a shot at the near post after a textbook counter.
In the second half, Real were content to sit back and absorb any pressure, as Bayern had to score at least five goals to progress.
Despite a couple of chances for Arjen Robben and Franck Ribery (who was lucky not to see red for a slap on Daneiel Carvajal which went unnoticed), Real never seemed troubled.
Ronaldo waited until the last minute to add a clever second, firing a free kick under the wall. This was a hugely disappointing display by Bayern, and Real should now consider themselves favourites for the final in Benfica.

KEY EVENTS
 16' - RAMOS GOAL! (Bayern 0-1 Real): Luka Modric curls out a corner from the right, and Sergio Ramos is allowed to leap, unmarked, to the ball at the back post and thunder a header past Manuel Neuer.
20' - RAMOS GOAL! (Bayern 0-2 Real): Toni Kroos fouls Bale on the right wing. Di Maria curls in a left-footed cross, flicked on by Pepe, and Sergio Ramos is running behind to fire in his second header.
34' - RONALDO GOAL! (Bayern 0-3 Real): Karim Benzema sends the ball forward to Gareth Bale, who takes a few touches to the edge of the box. He slides a pass left for Ronaldo, sprinting to his left, who slots a shot past Neuer at the near post.
37' - RONALDO VOLLEY! Neuer heads away a long ball. It comes to Ronaldo on the left wing, and his volley from 40 yards bounces just in front of goal and wide.
38' - ALONSO BOOKED! OUT OF THE FINAL! Xabi Alonso's lunge on Bastian Schweinsteiger, 30 yards from goal and in front of plenty of Real players, is met with a yellow card, which means he misses the final.
57' - ROBBEN SHOT - The ball is worked to Arjen Robben on the edge of the box, and he curls a shot a fraction wide.
60' - RIBERY CHANCE - Franck Ribery engineers a gap in the Real defence, bursts through and fires in a shot at Casillas' near post that he saves well.
90' - RONALDO GOAL! (Bayern 0-3 Real): Ronaldo sizes up a free kick to the left of the D, and sends a low shot underneath the jumping wall, leaving Neuer rooted to the spot.

KEY STATS
Real Madrid are on course to win their 10th Champions League.
Cristiano Ronaldo scored his 15th and 16th Champions League goal this season alone, and has 57 in total for the competition.
This is the first Champions League final Real have reached since 2002.
Bayern Munich had gone nine Champions League games undefeated before two consecutive defeats to Real Madrid.
Real Madrid had just 31% possession.

TALKING POINT
Is this Real Madrid's year? For such an illustrious and well-backed side, Real Madrid have failed to convert financial dominance into European trophies of late. They are now just one game from their 10th Champions League (or European Cup) success. Despite Carlo Ancelotti's apparent disquiet in the job, this is Ronaldo's and his best chance at winning another Champions League after so many years without victory.

MAN OF THE MATCH
Sergio Ramos (Real Madrid): He managed to stay on the pitch in a high profile match without a booking or sending off, which is always a surprise, and he also scored the first crucial two goals to settle the tie. Ronaldo, Bale and Di Maria all excelled on the counter-attack, but Ramos' defending provided a platform for those attacks.

PLAYER RATINGS
Bayern Munich: Neuer 5, Dante 5, Boateng 5, Lahm 6, Alaba 6, Schweinsteiger 5, Kroos 5, Ribery 6, Robben 6, Muller 5, Mandzukic 5. Subs: Martinez 5, Pizzaro 6, Gotze 6.
Real Madrid: Casillas 6, Pepe 7, Ramos 8, Coentrao 6, Carvajal 6, Alonso 7, Modric 6, Bale 7, Ronaldo 8, Di Maria 7, Benzema 6. Subs: Varane 6, Casemiro 6, Isco 6.

TERRY FIT TO FACE ATLETICO TODAY, CECH RULED OUT

Chelsea manager Jose Mourinho has confirmed Petr Cech is not in contention to play today's Champions League semi-final second leg with Atletico Madrid, but has confirmed that captain John Terry will feature.
Cech took part in training on the eve of the contest a week after being ruled out for the season by Mourinho with a dislocated shoulder sustained in the first leg.
The stopper departed after 20 minutes of last Tuesday's first leg after he punched the ball from underneath his own crossbar, with David Luiz pushing Raul Garcia into the Chelsea goalkeeper, who hit the ground with a thud and was replaced by Mark Schwarzer.
It was later revealed that he had dislocated his shoulder.
At the time, Jose Mourinho said: "Petr Cech's season over. Don't ask me technically, but season over.”
However, it appeared that the keeper may recover in time after taking part in training ahead of Wednesday’s match, but Mourinho insisted his number one trained alongside injured personnel, suspended players and those fully fit to show solidarity.
"Everybody's ready and he's ready and that's the message we wanted to give," the Portuguese said.
"Everybody was on the pitch.
"It's a very important match for our group. Everybody's together, everybody wants to help, everybody wants to play.
"His condition doesn't allow him to play, but the message from him and the group."
Terry limped off after turning his ankle in the second half of the 0-0 first-leg draw in Madrid and Mourinho said at the time that he was unlikely to play again this season.
Yet Terry, who missed Sunday's 2-0 Premier League win against Liverpool, trained on Tuesday and is fit.
"He is ready and he will start," Mourinho said at his pre-match news conference.
Eden Hazard, who went off after 17 minutes of their quarter-final, second leg against Paris St Germain, is also available, leaving Mourinho to decide whether or not he will start.
Goalkeeper Petr Cech, who dislocated his shoulder last week, is not fit, even though he trained yesterday.
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani akihojiwa na waandishi wa habari katika hafla ya kuhamsidha jamii kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa sikoseli 'seli mundu' iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Ugonjwa  wa sikoseli hurithiwa kutoka kwa wazazi wote wawili wenye vinasaba vya ugonjwa huo.

Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus juzi usiku.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB, Teddy Mapunda akizungumza wakati alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu  vivutio  vya utalii vya Tanzania katika kongamano la biashara na uwekezaji jijini Abuja, Nigeria juzi.

Katibu Mkuu,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Sazi Salula (katikati) akifungua rasmi kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kilichofanyika Karimjee jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu katibu Mkuu  Eng. Angerina Madete, na wa kwanza kushoto Katibu wa Baraza Bw. Isaya Kisiri.

Tuesday, April 29, 2014

ARSENAL CLOSE IN ON TOP FOUR WITH WIN OVER NEWCASTLE

Arsenal are now four points clear of Everton in the final Champions League spot after a 3-0 victory over Newcastle at the Emirates Stadium.
Newcastle, who had manager Alan Pardew back on the touchline after his seven-game ban for headbutting Hull City’s David Meyler, were outplayed by a patient Arsenal side for whom Santi Cazorla, Aaron Ramsey and Mesut Ozil shone.
The opening goal came after 26 minutes when Laurent Koscielny barged Moussa Sissoko out of the way to prod home Cazorla’s chipped free-kick past Tim Krul.
Arsenal doubled their lead through Ozil’s tap-in at the far post on 42 minutes after Krul had twice denied Olivier Giroud with blocks from point-blank range.
Giroud then completed the scoring midway through the second half with a bullet header at the near post from Ozil’s driven cross.
The Gunners next face West Brom at the Emirates on Sunday knowing a win, or a defeat for fifth-placed Everton at home to Manchester City on Saturday, will ensure their qualification for the Champions League for a 17th successive time.
For Newcastle, it is a sixth consecutive defeat, their worst run for 27 years, and the supporters held up banners at the end calling for their manager Pardew to be sacked.

KEY MOMENTS
16’ - CHANCE! Ozil volleys wide from a Krul punch but the referee had already ruled that Koscielny had fouled the Dutchman.
25’ - GOAL! (Arsenal 1-0 Newcastle): Arsenal lead 1-0. Cazorla's free-kick bounces in the box and Sissoko fails to deal with the run of Koscielny, who pokes home from close range.
28’ - SAVE! Debuchy concedes a corner, Arsenal's fifth of the game so far. Podolski's header from Cazorla's corner is brilliantly saved one-handed by Krul.
41’ - GOAL! (Arsenal 2-0 Newcastle): Mesut Ozil makes it 2-0 with a tap-in after Krul brilliantly keeps out two efforts from Giroud at the near post.
45+2’ - SAVE! Great save from Krul to deny Cazorla from close range.
65’ - GOAL! (Arsenal 3-0 Newcastle): Giroud gets his 21st goal of the season, heading Ozil's cross to the near post past Krul. Nice little pass by Ramsey in the build-up to release the German.
87’ - CHANCE! Monreal gets in round the back but is denied by Krul, then Podolski's follow-up ends up on the roof of the net.

KEY STATS
The Magpies have lost nine of their last 10 Premier League games at Arsenal.
Newcastle remain in the top-half of the table despite losing ten of their last 13 Premier League matches.

TALKING POINT
Will Pardew get the sack? Probably. Newcastle have been awful recently, and David Moyes is available...

MAN OF THE MATCH
Mesut Ozil (Arsenal): The German scored one and set up another with a superb performance in the middle of the park that brought back memories of his coruscating early season form. But a humdrum Monday night at home to Newcastle is one thing - Gunners’ fans will be looking for more from their 25-year-old playmaker in the big games next season.

PLAYER RATINGS
Arsenal: Szczesny 7, Sagna 7, Mertesacker, 7 Koscielny 7, Monreal 7, Arteta 7, Ramsey 8, Ozil 9, Cazorla 8, Podolski 7, Giroud 7. Subs: Rosicky 7, Flamini 7,Sanogo 7.
Newcastle: Krul 7, Debuchy 6, Williamson 6, Coloccini 6, Dummett 6, Gosling 5, Anita 5, Tiote 6, Gouffran 6, Sissoko 6; Remy 6. Subs: Yanga-Mbiwa 6, Armstrong 6, Shola Ameobi 6.

JICHO LA TATU


IMF YASISITIZA UTHABITI BRN KUPUNGUZA UMASIKINI

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limesema Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) iwapo utatekelezwa kikamilifu  katika sekta kadhaa, utasaidia upatikanaji wa ajira na kupunguza umasikini nchini.
Shirika hilo limebainisha katika ripoti yake kuwa, ukuaji wa uchumi wa Tanzania utasaidia  kuondoa  umasikini pale kutakapokuwa na sera madhubuti zitakazochochea kuboresha sekta ya kilimo pamoja na kujenga viwanda vitakavyopunguza tatizo la ajira nchini.
Ripoti hiyo ya IMF ya uchumi kwa nchi za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara, imesisitiza kuwa ili Tanzania iweze kuwakwamua  watu wake katika lindi la umasikini, ni lazima iwekeze zaidi kwenye elimu kwa kuhakikisha kuwa inakuwa na sera nzuri zitazosaidia kuboresha sekta hiyo, ikiwa ni pamoja na miundombinu yake.
Ofisa Mkazi wa IMF nchini, Thomas Baunsgaard akiwasilisha ripoti hiyo  katika mkutano ulioandaliwa na Asasi ya Utafiti wa Uchumi (REPOA), alisema  uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia saba, lakini hata hivyo kukua huko hakujasaidia kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi wake.
Akichangia kwenye ripoti hiyo, Profesa Ibrahim Lipumba alisema  ripoti hiyo inasaidia Tanzania kubuni sera za kuboresha uchumi wake na akashauri misamaha mingi ya kodi iondolewe kwani inachangia upotevu wa asilimia tano ya pato la taifa kwa mwaka.
Mkurugenzi wa Utafiti wa REPOA, Dk Donald Mmari alisema matumizi ya Serikali ni makubwa kuliko kiasi kinachokusanywa, jambo ambalo alisema linachangia kuwepo kwa mfumuko wa bei na hivyo kuwaathiri wafanyakazi.

IDA YAPIGA JEKI UJENZI WA RELI YA KATI

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia imeidhinisha msaada wa dola za Marekani milioni 300 kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo (IDA) kwa ajili ya kuongeza nguvu jitihada za Serikali katika mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya reli.
Katika mradi huo, Tanzania inatarajia kujenga reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam-Isaka pamoja na kuimarisha wakala zinazosimamia reli nchini humo, ikiwa ni sehemu ya mradi wa korido ya Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Philipe Dongier, mradi huo ni muhimu kwa Tanzania kutokana na ukweli kuwa nchi hiyo, imebarikiwa hasa eneo ilipo, madini, maliasili za kilimo, utalii na umuhimu wake katika usafiri wa maji hasa kwa nchi zisizozungukwa na maji.
“Sifa hizi zinaipatia fursa Tanzania ya kujiwekea maendeleo mazuri ya kutoa huduma kupitia miundombinu ya kisasa, tuna hamasa kubwa ya kuisaidia juhudi za Serikali katika kujenga upya mfumo wa kisasa wa miundombinu ya reli,” alisema Dongier.
Alisema mradi huo, pia unatarajiwa kuimarisha soko la mazao ya kilimo, kutengeneza ajira, kuisogeza karibu Tanzania na nchi za jirani kwa kuimarisha shughuli za kijamii na kiuchumi lakini pia kuboresha usafiri huo ambao ni tegemeo la wananchi hasa wenye kipato cha chini.
Akizungumzia fedha hizo zilizoidhinishwa, mkurugenzi huyo alisema zitasaidia katika  mradi huo kuanzia ujenzi wake hadi uendeshaji wa treni, kuboresha uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam na vituo vya treni.
“Fedha hizi zitaboresha njia za treni kuwa za kisasa, kujenga vituo vya treni kwa mtindo wa kisasa, kukarabati na kujenga upya maeneo ya madaraja,” alisisitiza.
Alisema kutokana na hali ya sasa ya miundombinu nchini humo na maeneo mengi ya Afrika Mashariki, shughuli za kiuchumi zimekuwa zikisuasua na kusababisha usafirishaji wa bidhaa kuwa wa gharama kubwa baina ya Tanzania na nchi jirani kama vile Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Uganda.
Kwa upande wake, kiongozi wa timu ya benki hiyo maalumu kwa ajili ya mradi huo, Henry des Longchamps, mradi huo utasaidia kuboresha na kuunganisha mawasiliano ya usafiri muhimu kwa Tanzania na nchi za jirani na kutengeneza ushindani wa kibiashara na nchi nyingine za jirani zenye miundombinu bora.

MFUKO WA PPF WAWAITA WASTAAFU KUHAKIKI TAARIFA

Mfuko wa Pensheni wa PPF  wamewaomba wastaafu ambao taarifa zao  hazijahakikiwa wafike katika ofisi yoyote ya PPF kuhakiki taarifa zao kabla ya Mei  3, mwaka huu.
Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele, alisema jana kuwa  Sh bilioni 18 zimekuwa zinalipwa na mfuko huo kwa wastaafu kwa miezi mitatu.
Aliongeza kuwa mfuko huo unahakiki wastaafu wake ambao walikuwa hawajahakikiwa katika mpango wa uhakiki  uliofanyika Mei hadi Agosti, mwaka 2013.
Hivyo alisema uhakiki wa taarifa za wastaafu unafanyika katika ofisi za makao makuu, ofisi za kanda pamoja na ofisi ndogo za mfuko na nyaraka zinazohitajika katika uhakiki huo ni  kitambulisho cha benki, picha ndogo  ya rangi, barua ya Serikali ya mtaa anapotoka, kitambulisho cha Taifa/kadi ya kupiga kura au  leseni ya udereva.
Alisema madhumuni ya kuhakiki wastaafu hao ni kukusanya taarifa za sasa za wastaafu kama vile namba za simu; hivyo kuwa na taarifa  sahihi kwa wastaafu wote na kupata mrejesho kuhusu huduma katika ulipaji mafao.

WATAALAMU WAZEMBE WA MIFUGO KUSHUGHULIKIWA

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani amesema Serikali haitasita kumchukulia hatua za kisheria mtaalamu  wa mifugo, ambaye eneo lake litabainika kukabiliwa na ukiukwaji wa sheria ya ustawi wa wanyama.
Pia, amelaumu baadhi ya mamlaka za Serikali ikiwemo mahakama na taasisi za wanyamapori, zinazokamata mifugo na kuifungia kwenye maeneo yasiyostahili bila maji wala malisho mpaka kufa.
Aidha, amesema wakati mwingine hupiga mifugo risasi, kuwalazimisha wamiliki kulipa faini, jambo alilosema ni ukatili dhidi ya wanyama.
Dk Kamani ameagiza wasimamizi wa sheria na watoa huduma za wanyama, kusimamia ipasavyo kanuni za ustawi wa wanyama kazi, usafirishaji, uchinjaji na ufugaji wa mifugo kwa ujumla.
Alisema katika kuimarisha ustawi huo, wizara yake itaendelea kuhimiza elimu ya ustawi wa wanyama iingizwe kwenye mtaala wa shahada ya kwanza ya udaktari wa mifugo.
Alisema hayo Dar es Salaam  jana, alipokuwa akihutubia wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo katika sherehe za 14 za Siku ya Veterinari Duniani kwenye viwanja vya wizara hiyo.
“Aidha nawahimiza wataalamu wote wa afya ya mifugo wakishirikiana na wakaguzi wa ustawi wa wanyama kuhakikisha Sheria ya Ustawi wa Wanyama Sura ya 154, ya mwaka 2008 na kanuni zake  zinasimamiwa,” alisema.
Alisisitiza, “ikumbukwe kwamba wanyama hawana utashi kama binadamu, hivyo ni unyama uliokithiri kumtesa mnyama kwa kosa lililotendwa na binadamu.”
Akifafanua zaidi, alisema sheria haitasika kuchukua mkondo wake kwa mtu yeyote atakayepatikana akivunja sheria hiyo kwa makusudi na hata kumfutia usajili mtaalamu ikibainika eneo lake la kazi kuna ukiukwaji wa sheria na wanyama wanateswa.
Wakati huo huo, alikemea tabia ya watu kusafirisha kuku wakiwainamisha vichwa chini, kuwapiga mifugo.
Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania, Profesa Dominick Kambarage alisema sekta ya mifugo ni muhimu kwa ustawi wa jamii na wataendelea kusimamia utoaji bora wa huduma.

CCM YAZINDUA SHINA MARYLAND NCHINI MAREKANI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba amezindua shina la chama hicho Maryland, Marekani.
Uzinduzi huo ulifanyika juzi, ikiwa ni mwendelezo wa kuhakikisha wanachama wa chama hicho, wanakuwa katika mfumo mmoja wa kichama.
Akizungumza na Watanzania waliofika kwenye uzinduzi huo, Mwigulu alisisitiza umuhimu wa wana CCM, kujenga mazingira ya umoja na mshikamano, ikizingatiwa wako mbali na nyumbani.
"Umoja wenu ndio ngao yenu kwa hapa Marekani, naomba sana mshiriki kwenye Jumuiya zenu na mshiriki kwenye shughuli za pamoja zikiwamo hizi za kisiasa,” alisema.
Mwigulu alisema, “Haitakuwa vyema kufunga mashina na matawi ya CCM. Tutumie mashina haya kutuimarisha zaidi.”
 Aliwaelezea juu ya mchakato wa kutengeneza Katiba mpya, akisema kukosekana kwa utashi kwa viongozi wa kisiasa, kunasababisha katiba kutopatikana au kuchelewa kupatikana.
Aliomba Watanzania walioko nje ya nchi, kuacha kushabikia mambo yasiyokuwa na tija kwa taifa, kwa kuwa yatasababisha utengano.

VODACOM TANZANIA WAENDA 'PEMBEZONI' MWA NCHI

Kampuni ya Vodacom Tanzania imechaguliwa kuwa moja ya watoa huduma za mawasiliano watakaotoa mawasiliano ya simu vijijini na mijini ambayo awali haikupewa kipaumbele.
Katika kufanikisha hilo, kampuni hiyo imesema inatarajia kufikia wakazi takribani milioni moja wa maeneo husika.
Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jana kwa vyombo vya habari, imemkariri Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza kisema wameshinda zabuni ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu kwa vijiji 466 katika kata 73 ambazo zina wakazi takribani 1,000,000.
“Haya ni mafanikio makubwa kwetu sisi kuendelea kuwatumikia watanzania kwani inaonesha jinsi  mtandao wetu unaaminika. Vodacom  ipo mstari wa mbele kushirikiana na serikali pamoja na taasisi za kimataifa kuhakikisha wateja wake wanafikiwa kila pembe ya nchi,” alisema.
Alisema nchi bado ina uhitaji mkubwa wa huduma za mawasiliano na ni jukumu lao kuwahudumia.
Zabuni hiyo ilitolewa na  mfuko wa kimataifa wa kutoa huduma za mawasiliano (UCSAF) ikiwa ni sehemu ya mpango wa miundombinu ya mawasiliano Tanzania na mfumo wa kielektroniki wa serikali  (RCIP-Tanzania) ambao umefadhiliwa na  taasisi ya kimataifa ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini  makubaliano hayo kwa kampuni za simu za mkononi ambazo zimeshinda zabuni za kutoa huduma za kimawasiliano vjijini,  Mtendaji Mkuu na Meneja wa Mfuko wa UCSAF, Peter Ulanga alisema walitangaza zabuni hiyo kwa kata 152 ambapo zitawafikia watu takribani 1,600,000.
Kwa mujibu wa Ulanga, mshindi wa zabuni hiyo amepatikana kwa kufuata taratibu zote kwani kulikuwa na fursa sawa kwa kila kampuni.
UCSAF ilianzishwa kwa lengo la kukuza upatikanaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani kote.

JWTZ WAKABIDHIWA VITABU KWA AJILI YA MAKTABA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma.
Alikabidhi vitabu hivyo  jana Dar es Salaam kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange na kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo cha Kijeshi kilichopo Monduli, mkoani Arusha.
Maktaba hiyo ilianzishwa na  Kikwete  alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita.
"Lazima mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu lakini na mimi nitaendelea kutafuta vitabu niwaletee ili kujijengea uwezo maktaba yetu ya Monduli,Ó alisema.
Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Mwamunyange amemshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha Jeshi la Ulinzi  la Wananchi Tanzania kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi.

MASHARTI YA THELUTHI MBILI KUKWAMISHA KATIBA MPYA

Hofu ya kutopatikana kwa Katiba mpya, baada ya changamoto zilizojitokeza wakati wa awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu la Katiba, sasa ni dhahiri.
Hofu hiyo inaonekana katika mahojiano maalumu kati ya waandishi wa HabariLEO na Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahaya Khamis Hamad.
Katika mazungumzo kuhusu nini anafikiri kinafaa kufuatwa kwa sasa baada ya hekaheka ya awamu ya kwanza, Katibu huyo alipendekeza Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ifanyiwe marekebisho.
Katibu huyo katika mazungumzo, amesema kama msimamo wa wajumbe wa Bunge hilo waliojiundia kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), utaendelea kuwa kama ulivyo, mchakato wa kupata Katiba mpya kwa Sheria iliyopo, unaweza kuganda.
Kutokana na hali hiyo, amependekeza kwa maoni yake binafsi kwamba ni vyema Serikali ifikirie kubadilisha Sheria hiyo kwa kurekebisha masharti yanayotaka kila kifungu cha Katiba hiyo, kipite baada ya kupigiwa kura na zitakazounga mkono za theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar.
Kwa mujibu wa kifungu cha 26(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ili Katiba inayopendekezwa ipitishwe katika Bunge Maalum la Katiba, itahitaji kuungwa  mkono kwa wingi wa theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge Maalum kutoka  Tanzania Bara, na theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka Tanzania Zanzibar.
Hata hivyo Katibu huyo alisema ipo haja kwa Serikali kurekebisha kifungu hicho, kwa kuwa kama wajumbe wa Ukawa waliosusia vikao vya Bunge hilo na kutoka nje Aprili 16 mwaka huu wataendeleza msimamo wao, Katiba itaganda.
“Kubadili theluthi mbili mimi siwezi kulisemea maana ni kazi ya Serikali, lakini ni vizuri likaangaliwa, hatuwezi kuganda kwa mbili ya tatu (thelithi mbili),” alisema Katibu huyo.
Alisema wajumbe hao wa Ukawa wengi ni wa vyama vya siasa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar na wanashirikisha pia baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 wasiozidi 25.
Hata hivyo alisema: “Bado tunaendelea kuwaomba wajumbe waliotoka bungeni waje tufikie mwisho wa jambo hili kwa maslahi ya Taifa.”
Alipendekeza marekebisho ya Sheria yafanyike, na badala ya kusema theluthi mbili ya akidi ya wajumbe wote, ni bora iseme theluthi mbili ya wajumbe waliohudhuria vikao wakati uamuzi ukifanyika.
Hata hivyo, mabadiliko ya Sheria hiyo yatalazimisha kufanyike mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, kwa kuwa imezuia baadhi ya vipengele visifanyiwe uamuzi, isipokuwa uamuzi huo uungwe mkono na idadi ya kura ya theluthi mbili ya wabunge kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wabunge kutoka Zanzibar.
Zuio hilo lipo katika Orodha ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na limetajwa katika Ibara 98 (1) (b)  kwa kuorodhesha mambo ambayo mabadiliko yake yatahitaji masharti hayo.
Mambo hayo ni kuwapo kwa Jamuhuri ya Muungano, kuwapo kwa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, madaraka ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano, kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano, madaraka ya Serikali ya Zanzibar, Mahakama Kuu ya Zanzibar na Orodha ya Mambo ya Muungano. 
Pamoja na Bunge Maalumu kuendelea kutafuta suluhu ili wajumbe hao wa Ukawa warejee bungeni, Katibu huyo wa Bunge Maalumu, aliweka wazi namna wajumbe hao walivyokuwa na msimamo mgumu wa kuendelea kususia Bunge Maalumu.
Kuhusu kikao cha Kamati ya Uongozi kilichokaa Alhamisi iliyopita, Katibu alisema pamoja na mambo mengine kilipokea taarifa ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta ya kwenda Zanzibar kukutana na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Ukawa kutafuta suluhu ili wajumbe hao warejee.
Viongozi wa Mapinduzi Zanzibar aliokutana nao Sitta ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu, Amani Abeid Karume na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad.
Kwa mujibu wa Katibu huyo, ziara ya Sitta visiwani humo aliyoifanya Jumatatu ya wiki iliyopita, ililenga kutafuta suluhu ya wajumbe waliotoka bungeni kurejea tena, lakini viongozi wa Ukawa kutoka vyama mbalimbali vya siasa, ambao pia ni wajumbe wa Bunge hilo na wasio wajumbe, waligoma ombi la Sitta kuwataka warejee mpaka wapate ridhaa ya vyama vyao.
“Mwenyekiti alikwenda Zanzibar kukutana nao (Ukawa) na wajumbe hao walisema hawawezi kuzungumza na Sitta kuhusu kurudi mpaka wapate uamuzi wa vyama vyao, baadhi ya viongozi aliwapigia simu lakini walipokea wasaidizi wao na alipowaambia wahusika wakipata ujumbe wake wampigie, hakuna aliyepiga,” alieleza Katibu.
Alisema wajumbe wengine Sitta aliwatumia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, akiwaomba waongee naye lakini hawakujibu.
Hata hivyo Katibu alisema bado Sitta ana matumaini kwamba watarejea na anaendelea na juhudi za kutafuta mapatano.
Ingawa Ukawa hawakutaka kupokea simu wala kujibu ujumbe mfupi wa maneno waliotumiwa na Sitta, lakini baadhi yao walionekana kurejea kufuata posho kimya kimya bungeni humo na idadi yao imeelezwa kuwa ni zaidi ya 10.  Hata hivyo hawakupewa posho za kuanzia Aprili 19 hadi 26.
Katibu alipoombwa kuwataja majina, aligoma kutoa  kwa kile alichoeleza kuwa ni kwa matumizi ya ofisi pekee kwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo.
Alisema hoja iliyotolewa na Mjumbe Said Mkumba   kwamba Ukawa walirejea kuchukua posho, ilitawaliwa na hofu na kujisemea tu, kutokana na ukweli kwamba, wajumbe hao walipaswa kuchukua posho zao za vikao za mpaka Aprili 18.
Aprili 17 baada ya wajumbe wa Ukawa kutoka nje ya Bunge, mjumbe Mkumba alikaririwa bungeni akidai kuwa Ukawa walirejea na wameonekana kwa mhasibu wakidai posho zao zote, jambo lililoelezwa na Katibu kuwa halikuwa sahihi lakini liliwalazimu kubadilisha utaratibu.
“Kutokana na tukio la Ukawa, ingawa wamo wachache walibaki bungeni, ilibidi tuzingatie utaratibu wa mtu aliyefika kwenye kikao ndio anasaini na kulipwa, ama la akiwa na dharura, alete maelezo ya Mwenyekiti kuhusu dhahura yake,” alisema Hamad na kuongeza kuwa walifanya hivyo baada ya kubaini baadhi ya Ukawa waliotoka, walirejea kuchukua posho.
Kuhusu nyongeza ya siku 60, Katibu alisema ipo kwa mujibu wa sheria baada ya mabadiliko yaliyofanyika Februari mwaka huu kuondoa kipengele cha nyongeza ya ukomo wa siku 20 baada ya siku 70 kumalizika.
Kifungu hicho ni 28 (4) kinachotoa mamlaka kwa Mwenyekiti na Makamu wake kuongeza siku kwa ridhaa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, bila kuathiri kifungu cha 28 (3) kinachoeleza siku 70 za awali.

MAMENEJA WA BENKI YA BARCLAYS WATIWA MBARONI KWA WIZI

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watuhumiwa 13, wakiwamo mameneja wawili wa Benki ya Barclays kwa tuhuma za kuhusika na wizi katika benki hiyo katika tawi la Kinondoni.
Mameneja hao ni Alune Kasililika maarufu kama Mollel (28), mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa tawi hilo na Neema Bandari maarufu kama Bachu (28) ambaye ni Meneja Operesheni wa tawi hilo.
Kamishna wa Kanda hiyo, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa hao wanahusishwa katika ujambazi uliotokea Aprili 15, mwaka huu saa 3:30 asubuhi.
Alidai katika siku ya tukio hilo, watu wenye silaha aina ya SMG na bastola waliingia katika benki hiyo na kupora Sh milioni 390.22, dola za Marekani 55,000, Euro 2,150 na Pauni 50.
"Majambazi hao waliwatishia kwa silaha watumishi wa benki hiyo na kuwaweka chini ya ulinzi na hatimaye kutoroka na fedha hizo kwa kutumia pikipiki aina ya Fekon," alisema.
Alidai awali watuhumiwa hao walifika katika benki hiyo wakiwa na magari mawili moja aina ya Opa lenye namba T421 BQV ambayo imekamatwa.
Kwa mujibu wa madai ya Kova, uchunguzi wa kina ulibaini kuwa Alune alishirikiana na Neema pamoja na watuhumiwa wengine kufanikisha tukio hilo, huku ikigundulika kuwa robo tatu ya fedha zote zilizoibwa zilichukuliwa kabla ya tukio hilo.
"Siku hiyo ya tukio ilikuwa ni utekelezaji ili kukamilisha njama zao, hawa walisakwa na vikosi mbalimbali maalumu ikiwa ni pamoja na Kikosi Maalumu ambacho ni kwa ajili ya kuzuia na kupambana na wizi katika mabenki jijini Dar es Salaam," alisema.
Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Fredrick Lazaro (19), Kakamiye Julius (31), Iddi Nguvu (32), Sezary Massawe maarufu kama Msolopa, Boniface Ndaro maarufu kama Muumba (29), Erasmus Mroto maarufu kama Menyee (38), Deo Olomy (32), Mohamed Athumani (31), Joseph Mkoi (33), Lucy Amos maarufu kama Macha (30) na Grace Amon (39).
Alisema baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa, baadhi yao wamekiri kuhusika na wizi huo na walipopekuliwa walikutwa na fedha kidogo ambazo ni sehemu ya mgawo waliopata baada ya tukio hilo.
"Kabla ya tukio lile, imebainika kulikuwa na vikao mbalimbali vya maandalizi ya kufanikisha tukio hilo kabla ya siku hiyo.
"Matukio kama haya yanatudhalilisha, yanatoa picha kwamba Jeshi la Polisi na serikali tumeshindwa kuzuia uhalifu wa aina hii lakini kumbe ni kazi iliyofanyika ndani," alisema Kamanda Kova.
Alisema bado upelelezi unaendelea, hivyo wananchi waendelee kushirikiana na Polisi ili watuhumiwa wengine wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.
Katika hatua nyingine, Kova alisema kwa sasa wataanza kuwachukulia hatua wamiliki wa hoteli zenye mabwawa ya kuogelea ambayo hayana uangalizi wakati watu wakiogelea.
Hatua hiyo inatokana na tukio la watoto watatu kufa wakati wakiogelea katika bwawa la kuogelea kwenye Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Jangwani, tukio ambalo ni la juzi saa 11:00 jioni.
Alisema mtoa taarifa David Mboka (44) alisema akiwa hotelini hapo kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake, Derrick Mboka (1) aligundua watoto hao ambao ni Ndimbuni Bahati (9), Eva Nicholous (9) na Janeth Zacharia (10) wametumbukia katika bwawa hilo.
"Matukio ya aina hii tunaanza kuyafanyia kazi na tunaanza na huyu, pia tunatoa onyo kwa wamiliki wengine ambao wana mabwawa ya kuogelea kuwa makini na maeneo hayo kwa kutoruhusu watoto kukaribia maeneo hayo," alisema Kova.

Monday, April 28, 2014

TUCTA KUPIGANIA 'PAYE' ISHUKE KUTOKA ASILIMIA 13 HADI 9

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), limeazimia kuendelea kupigania kushushwa kwa Kodi ya Mshahara (PAYE) kutoka asilimia 13 inayokatwa hivi sasa hadi asilimia tisa, ili   mfanyakazi apate ahueni ya maisha.
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya, alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya Mei Mosi  yatakayoambatana na wiki ya wafanyakazi itakayoanza rasmi leo.
Maadhimisho ya Mei Mosi yatafanyika nchini kesho kutwa ambapo kitaifa yatafanyikia jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.
Mgaya alisema mbali na kupunguzwa kwa kodi, Tucta inayo mambo mengine mawili inayopanga kupigania ili ujumbe ufike serikalini na kupatiwa suluhu.
Suala la pili alitaja kuwa ni kila mfanyakazi kupatiwa malipo mazuri awapo kazini, jambo alilosema wamekuwa wakiliomba mara kwa mara na hadi sasa halijakamilika.
“Kila mfanyakazi ni mstaafu mtarajiwa, hivyo ni vyema waajiri waandaliwe malipo mazuri, ili mfanyakazi atakapostaafu awe na kiwango cha maisha kitakachomsaidia katika maisha yake,” alisema Mgaya.
Pia wamejipanga kupigania mifuko ya pensheni, ilipe kiwango sawa cha kiinua mgongo tofauti na sasa ambapo baadhi ya mifuko inalipa kiwango kidogo na mingine inalipa kiwango kikubwa.
 “Ifikie wakati sasa kusiwepo na utitiri wa mifuko, bali ivunjwe na kubaki miwili yaani wa binafsi na wa umma ambayo mengine yanabakia yakijitangaza tu,” alisema Mgaya.
Mgaya alilitaja jambo lingine kuwa ni fidia kwa wafanyakazi ambapo alishauri kuundwe kwa mfuko ambao utawezesha mfanyakazi atakayeumia kazini, kulipwa fidia ambayo  itamsaidia.
Kuhusu mabadiliko ambayo yametokea tangu maadhimisho yaliyopita ya Mei Mosi, Mgaya alisema ni kupungua kwa kodi kutoka asilima 14 kwenda 13 ambayo alisisitiza kwamba  wafanyakazi wanaomba sasa ifikie asilimia tisa.
Mwandishi alimtafuta Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka na Naibu wake, Makongoro Mahanga, wazungumzie mpango huo wa Tucta, lakini simu zao ziliita bila majibu.