Friday, May 31, 2013
Thursday, May 30, 2013
Wednesday, May 29, 2013
Tuesday, May 28, 2013
TRENI YA MWAKYEMBE 'YAONDOKA' NA MAISHA YA MCHUMI DAR...
![]() |
Gari hilo baada ya ajali, Dar es Salaam jana. |
Mchumi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Elias Kitundu (39) amekufa papo hapo huku mkewe Agness Msoka (37) na mtoto wao Samson Kitundu (17) wakijeruhiwa, baada ya gari lao kugonga ‘treni ya Mwakyembe’ jana alfajiri eneo la Moshi Baa Ilala, Dar es Salaam.
BENKI NNE ZAIDI ZAJITOKEZA KUKOPESHA NYUMBA WANANCHI...
Benki nne nchini zimeingia mkataba wa kukopesha nyumba zinazojengwa na kuuzwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) hivyo kufanya idadi ya benki zinazotoa huduma hiyo kufikia 12.
Monday, May 27, 2013
CHEKA TARATIBU...
Baada ya kumaliza maombi, Mchungaji akawaambia waumini wake wafumbe macho. Akainama na kuingiza mkono kwenye kapu la sadaka na kuiba pesa. Wakati akiinuka akakutana macho kwa macho na mzee mmoja aliyekuwa akiingia kanisani. Mchungaji akasema: "HERI YAKE YULE ASIYESEMA KUHUSU ALIYOYASHUHUDIA KWA MACHO YAKE…" Yule mzee akadakia: "…KWA MAANA ATAPATA MGAWO WAKE BAADA YA MISA KWISHA!" Duh...
Sunday, May 26, 2013
HILI NDILO BAO LA ARJEN ROBBEN LILILOIPA BAYERN MUNICH UBINGWA WA ULAYA 2013...
Mabingwa wa soka nchini Ujerumani, Bayern Munich usiku wa kuamkia leo imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwachapa Borussia Dortmund mabao 2-1 katika mechi ya fainali iliyowakutanisha miamba hao wawili wa Ujerumani kwenye Uwanja wa Wembley, nchini Uingereza. Hiyo ilikuwa fainali ya pili kwa Bayern Munich katika kipindi cha miaka mitatu, ambapo ilishuhudia mchezaji mwenye kasi ya ajabu Arjen Robben akiwapa raha mashabiki wake hao kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 90 ya mchezo, baada ya kuwasononesha katika fainali zilizopita dhidi ya Chelsea. Katika fainali zilizopita, Robben alikosa penalti ambayo ilikuja kuigharibu timu hiyo kwa kukosa ubingwa.
Saturday, May 25, 2013
BRITISH AIRWAYS YATUA KWA DHARURA BAADA YA KULIPUKA INJINI ANGANI...
![]() |
KUSHOTO: Moshi ukifuka kwenye moja ya injini za ndege hiyo angani. KULIA: Mafundi wakiichunguza injini hiyo mara baada ya kutua Uwanja wa Heathrow. |
Abiria mmoja ameelezea jinsi 'moto mkubwa'
ulivyokuwa ukionekana kutoka ndani ya ndege ya British Airways kabla kwa
namna ya ajabu kulazimisha kutua kwa dharura kwenye Uwanja wa Heathrow
jana.
Friday, May 24, 2013
SHEHA AJERUHIWA BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR...
![]() |
Sheha Mohammed Omar Said `Kidevu’. |
Matukio ya kujichukulia sheria mkononi yameendelea kujitokeza hapa, na juzi jioni Sheha wa Shehia (Kata) ya Tomondo Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Mohammed Omar Said `Kidevu’ alivamiwa na watu wasiojulikana na kisha kummwagia tindikali ambayo imemjeruhi vibaya sehemu ya kifua na jicho la kulia.
WATU 91 WATIWA MBARONI KWA VURUGU ZA GESI MTWARA...
![]() |
Wananchi wakiandamana muda mfupi kabla ya kuzuka vurugu hizo mkoani Mtwara. |
Serikali imelaani vikali vurugu zilizotokea Mtwara juzi na imeapa kuwasaka waasisi wa vurugu hizo ndani na nje ya Mtwara na ndani na nje ya nchi ili waliohusika kupanga, kushawishi, kuandaa na kutekeleza vurugu hizo wafikishwe kwenye mkono wa sheria.
Thursday, May 23, 2013
Wednesday, May 22, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)