Sunday, March 31, 2013

WALIOKUFA JENGO LILILOPOROMOKA DAR SASA WAFIKIA 22...

Jengo hilo lililokuwa na ghorofa 16 baada ya kuporomoka juzi.
Wakati Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linamshikilia mmiliki wa kampuni ya Lucky inayodaiwa kujenga ghorofa lililoanguka juzi, na kuhofiwa kuua watu zaidi ya 60 wakiwemo watoto wanne, maiti zaidi wameendelea kunasuliwa kutoka kwenye kifusi.

BINTI ABAKWA NDANI YA BASI AKITOKA 'SHOPINGI'...

Binti huyo alikuwa akitokea kwenye maduka haya.
Msichana mdogo amebakwa na wanaume wawili kwenye sehemu ya juu ya basi baada ya kutoka kwenye eneo lenye maduka mengi akiwa na rafiki yake.

JICHO LA TATU...


MACHANGUDOA WA KINYARWANDA WAKUTWA NA ARVs DODOMA...

Machangudoa wakiwa kazini.
Wanawake watatu raia wa Rwanda wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).

UHURU KENYATTA SASA RAIS HALALI WA KENYA...

Uhuru Kenyatta.
Mahakama Kuu ya Kenya imeamua kuwa Rais mteule Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza William Ruto, walichaguliwa kwa njia huru na ya haki katika uchaguzi uliofanyika Machi 4, mwaka huu.

CHEKA TARATIBU...

Jamaa kaomba kazi ya ulinzi. Akajibiwa kwamba aje na cheti chake. Pia lazima awe anajua kuongea Kiingereza. Jamaa akahoji: "Kwani hao wezi wanaokuja kuiba hawajui Kiswahili?" Kasheshe...

AJARIBU KUUA KWA KUMTEGEA SUMU MWANAME KWENYE VIATU...

Mtu mwenye miaka 40 amekamatwa nchini Japan kwa tuhuma za kujaribu kumuua mwanamke mmoja kwa kumwekea sumu ya tindikali ya Haidrofloriki kwenye viatu vyake.

Saturday, March 30, 2013

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA JENGO LILILOPOROMOKA DAR...

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA JENGO LILILOPOROMOKA DAR...

JAMBAZI ANYWA SUMU MAHAKAMANI AKIJARIBU KUJIUA...

Gereza la Mahabusu Harare ambako Muza alikuwa akishikiliwa kusubiri hukumu yake.
Jambazi wa kutumia silaha amekimbizwa hospitali nchini Zimbabwe baada ya kwa namna ya ajabu kujaribu kujiua mahakamani, imeripotiwa.

ALIYEMUUA PADRI EVARIST MUSHI AKAMATWA ZANZIBAR...

Marehemu Padri Evarist Mushi.
Jeshi la Polisi limesema anayedaiwa kuwa muuaji wa Padri Evarist Mushi amekamatwa na ametambuliwa na watu walioshuhudia tukio hilo.

WALIOGOMA BBC KUREJEA ENDAPO NELSON MANDELA ATAFARIKI DUNIA...

Waandishi na mafundi wa BBC wakitoka ofisini katika kutekeleza mgomo wao.
Viongozi wa chama wamesema wafanyakazi wa BBC waliogoma wanaweza kurejea kazini kwa ajili ya tukio la kifo cha Nelson Mandela - lakini wakasisitiza kwa kifo cha Baroness Thatcher hawawezi kuchukua hatua kama hiyo.

WATU 40 BADO WAHOFIWA KUFUNIKWA NA JENGO DAR...

Jengo hilo baada ya kuporomoka ambapo inahofiwa bado kuna watu 40 chini ya kifusi hiki.
Ni tukio la kusikitisha na kuhuzunisha baada ya jengo la ghorofa 16 lililokuwa likijengwa katika makutano ya barabara za Indira Gandhi na Morogoro jijini Dar es Salaam kuporomoka saa 2.30 asubuhi huku watu zaidi ya 40 wakihofiwa kufunikwa na kifusi.

JICHO LA TATU...


MTOTO WA MWANAMIELEKA MKONGWE AFARIKI DUNIA...

KUSHOTO: Reid Fliehr. KULIA: Mwanamieleka mkongwe, Ric Flair.
Mtoto wa kiume mwenye miaka 25 wa mwanamieleka mkongwe, Ric Flair amefariki dunia.

ATAMBA NA KICHWA CHA MWENZAKE MITAANI MWANZA...

Kamanda Ernest Mangu.
Mkazi mmoja wa eneo la Bugarika jijini Mwanza ameuawa na wananchi wenye hasira baada ya kufanya mauaji kwa mwenzake kwa kumtenganisha kichwa, kisha kuanza kutamba nacho mtaani.

Friday, March 29, 2013

GHOROFA LAPOROMOKA DAR, 60 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA...

Baadhi ya wasamaria na vikosi vya uokoaji wakitoa majeruhi na baadhi ya miili ya watu.
Kama ilivyo kawaida ya 'wabongo'! Umati wa watu ukikimbilia kwenye eneo la tukio bila tahadhari yoyote.
Habari zilizotufikia zinasema kwamba watu wapatao 60 wanahofiwa kupoteza maisha baada ya jengo walilokuwa wakiishi kuanguka mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo ambalo liko katika makutano ya Mtaa wa Indira Ghandhi na Morogoro, inaelezwa kwamba lilikuwa bado likiendelea kujengwa huku sehemu ya chini ikiwa imeanza kutumika kwa makazi ya watu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, maiti 14 zimeopolewa kutoka kwenye kifusi cha jengo hilo na zaidi ya majeruhi 30 wamekimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Inaaminika kwamba bado kuna watu walio hai ambao wamefukiwa na vifusi wakiwamo watoto wanafunzi wa madrassa za Kiislamu inayosemekana ilikuwa katika jengo hilo.
Vikosi vya ukoaji vinaendelea na zoezi la uokoaji huku taarifa za hivi punde zinasema kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi naye ameshafika eneo la tukio.
Taarifa zaidi zinasema kwamba kazi ya uokoaji inafanyika katika mazingira magumu kutokana na ukosefu wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi hiyo.
Habari zaidi endelea kuperuzi ziro99blog.

MZEE MANDELA YU TAABANI, WANANCHI WATAKIWA KUJIANDAA KWA LOLOTE...

Mzee Nelson Mandela.
Hali ya Mzee Nelson Mandela ilibadilika na kuwa mbaya sana usiku wa kuamkia leo, kiasi cha kumchochea Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kulitaka taifa hilo kujiandaa kwa taarifa zozote mbaya.

BABA AUA MTOTO WAKE NA KUMZIKA SEBULENI...

Kamanda Diwani Athumani.
Mtoto Debora Riziki (3), mkazi wa kitongoji cha Iponjola katika Kijiji cha Isange wilayani Rungwe, ameuawa na kufukiwa katika shimo ndani ya nyumba ya baba yake mzazi.

BILIONEA WA ARUSHA KUZIKWA KENYA KAMA ALIVYOAGIZA...

Nyaga Mawalla.
Mgogoro wa maziko ya Wakili Nyaga Mawalla, umeingia katika sura mpya, baada ya wakili wake, Fatuma Karume, kutoa wosia wake ambao ameelekeza azikwe Kenya.

MBUNGE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA KIHARUSI...

KUSHOTO: Marehemu Salim Hemed Khamis. KULIA: Baadhi ya wabunge na waandishi wa habari wakisaidia kumbeba Mbunge Salim mara baada ya kuanguka ghafla.
Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), amefariki dunia.
Mbunge huyo ambaye aliugua ghafla juzi, akiwa kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, amefikwa na umauti jana saa sita mchana; akiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambako alikuwa amelazwa.

MWALIMU ADAIWA KUSHAWISHI WANAFUNZI WA KIKE WAMTUMIE PICHA ZAO ZA UTUPU...

Mwalimu wa zamani wa sekondari ya juu anatuhumiwa kuwashawishi wanafunzi wa kike wenye umri mdogo kumtumia picha zao wakiwa watupu na kwa kuwa na mahusiano na msichana mwnye miaka 17.

JICHO LA TATU...


LOWASSA AONYA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI...

Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Edward Lowassa amewatahadharisha wabunge wa Afrika Mashariki kuwa Watanzania hawatawaelewa iwapo vikao vya Bunge vitaendelea kufanyika nje ya Mji wa Arusha ambako ni makao makuu ya jumuiya hiyo.

HATIMAYE MWIZI MZOEFU WA SIMU ZA MKONONI ATUPWA JELA MIEZI 20...

KUSHOTO: Calin-Lonel Rostas. KULIA: Rostas (aliyezungushiwa duara) akijiandaa kufanya wizi wake ndani ya mkahawa.
Kibaka wa Romania ambaye aliwalaghai wateja wa mkahawa kwa kutumia vipande vya karatasi zilizopangwa kama 'ngao' huku akiwaibia simu zao, ametupwa jela jana.

Thursday, March 28, 2013

MAHALI ATAKAPOZIKWA BILIONEA WA ARUSHA KUJULIKANA LEO...

Marehemu Nyaga Mawalla.
Familia ya marehemu Nyaga Mawalla, inatarajia kutoa taarifa rasmi ya wapi maziko ya bilionea huyo kijana, yatafanyika.

BABA WA GARY NA PHIL NEVILLE KORTINI KWA MADAI YA UBAKAJI...

Mzee Neville Neville (kushoto) akiwa na mwanae, Gary.
Nyota wa soka Gary na Phil Neville wanasemekana walipatwa na mshituko mkubwa usiku wa juzi baada ya baba yao kukamatwa kwa madai ya shambulio la aibu.
Neville Neville, mwenye miaka 63, alikuwa akishikiliwa mapema Jumamosi asubuhi baada ya mwanamke aliyejawa hofu kuwapigia simu polisi kufuatia madai ya tukio hilo.

JICHO LA TATU...

MIPANGO YA DK MWAKYEMBE YAGONGA UKUTA...

Dk Harrison Mwakyembe.
Utekelezaji wa mipango ya Wizara ya Uchukuzi, inayosimamiwa na Dk Harrison Mwakyembe, kwa mwaka huu wa fedha uliobakiza miezi mitatu kwisha, ni wazi umekwama.

WIFI YAKE WHITNEY HOUSTON ANUSURIKA KUJIUA...

Pat Houston.
Wifi yake Whitney Houston, Pat Houston amenusurika kujiua ... ama wanandugu kadhaa walidhani pale walipopiga simu ya dharura -- baada ya kugundua kutokuelewana kwa kiasi kikubwa.

PAPA AGOMEA IKULU, ALALA NA KULA VYUMBA VYA WAFANYAKZI...

Papa Francis I.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ameendelea kuwa kiongozi wa matukio yanayopingana na watangulizi wake, ambapo sasa amekataa kuhamia katika makazi ya kifahari ya Papa.

Wednesday, March 27, 2013

WASIOAMINI MATOKEO KIDATO CHA NNE 'WAKATWA MAINI'...

Mkurugenzi Mkuu wa NECTA, Dk Joyce Ndalichako.
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limeeleza kuwa mara nyingi ukataji rufaa na usahihishaji upya wa mitihani hiyo, matokeo yamekuwa hayabadiliki kutokana na umakini wa usahihishaji.

HOSPITALI NA SHULE ZA KANISA KATOLIKI KUWABEBA MASIKINI...

Mwalimu katika moja ya shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki akiwa darasani.
Tabia ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ya kuwa ni mtu asiyetabirika kiutawala, na aliyejitambulisha kuwa mtumishi kwa masikini, inatarajiwa kuleta neema kwa watoto wa masikini katika shule za Kanisa.

JICHO LA TATU...

AUA MWANAE KWA RISASI WAKATI AKISAFISHA BUNDUKI SEBULENI...

Mtoto Christopher Stanlane Jr.
Mtu mmoja wa North Carolina kwa bahati mbaya amempiga risasi na kumuua mtoto wake wa kiume mwenye miaka 10 wakati alipokuwa akisafisha bunduki yake kwenye sebule yao.

SASA MUME AWEZA KUMNASA KIBAO MKE MBELE YA KADHI...

Waislamu walipoandamana kushinikiza uwepo wa Mahalama ya Kadhi.
Upungufu uliopo katika Mahakama ya Kadhi Zanzibar, umesababisha Serikali kuamua kuifanyia marekebisho sheria iliyoanzisha Mahakama hiyo.

ATENGENEZA GARI LA AJABU KWA KUTUMIA MABAKI YA NDEGE...

JUU: Gari hilo likiendelea kuundwa kwenye karakana ya Jeff. CHINI: Gari hilo la ajabu likiwa tayari kwa mashindano. KULIA: Jeff Bloch akiwa ndani ya gari lake hilo la ajabu.
Unaweza tu kuiita Frankenplane.
Jeff Bloch ametengeneza gari ya mashindano ya mabati ya aluminium yenye macho yake juu ya anga - ni sehemu ya ndege ya Cessna 310 ya mwaka 1956 na sehemu ya gari aina ya Toyota minivan la mwaka 1987.

Tuesday, March 26, 2013

MWANDISHI WA NYIMBO KALI ZA KUNDI LA JACKSON 5, DIANA ROSS AFARIKI DUNIA...

KUSHOTO: Kundi la Jackson 5 enzi hizo. KULIA: Deke Richards.

Mwandishi na Prodyuza mkongwe wa nyimbo wa Motown, Deke Richards amefariki dunia kwa maradhi ya saratani kwenye hospitali ya wagonjwa mahututi katika jimbo la Washington. Alikuwa na umri wa miaka 68.
Richards, ambaye nina lake halisi ni Dennis Lussier, alifariki Jumapili kwenye nyumba ya wagonjwa ya Whatcom, msemaji wa Peace Health St Joseph Medical Center, Amy Cloud alithibitisha jana.
Richards amekuwa akipambana na saratani, kwa mujibu wa taarifa kutoka Universal Music.
Alikuwa kiongozi wa timu ya uandishi, mpangilio na utengenezaji muziki ya Motown inayofahamika kama The Corporation, ambayo ilikuwa chini ya waasisi wa Motown Records Berry Gordy, Alphonzo Mizell na Freddie Perren.
Richards alijikita kikamilifu katika kuandika na kutengeneza nyimbo nyingi zilizotamba za Jackson 5, kwa mujibu wa taarifa kutoka Universal Music.
Nyimbo hizo ni pamoja na vibao vikali vitatu vya mwanzo vya Jackson 5 - "I Want You Back," "ABC," na "The Love You Save."
Akizungumza baada ya kifo cha Michael Jackson mwaka 2009, Richards alisema kwamba Mfalme huyo wa Pop alikuwa na 'akili za kuzaliwa.'
Pia alishiriki kuandika nyimbo kama "Love Child" ya Diana Ross & The Supremes, vilevile wimbo binafsi wa Diana Ross wa "I'm Still Waiting."
Wasanii wengine ambao Richards alitengeneza au kuandika nyimbo zao ni pamoja na Bobby Darin, The Four Tops na Martha Reeves & the Vandellas.
Richards ameacha mke, Joan Lussier, kaka na wapwa zake wawili.
Mipango ya kufanya sherehe ya faragha ya familia kusherehekea maisha yake inaendelea.

MAZIKO YA BILIONEA WA ARUSHA SASA UTATA MTUPU...

Marehemu Nyaga Mawalla.
Maziko ya mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Nyaga Mawalla, yameingia katika utata baada ya familia kushindwa kuamua wapi mahali pa kuzikwa.

MTOTO ALIYEOA MAMA WA MIAKA 61 ADAI SASA ANAJISIKIA KUWA BABA...

KUSHOTO: Sanele akibusiana na mkewe, Helen siku ya harusi yao wiki mbili zilizopita. KULIA: Sanele na Helen walipata chakula cha usiku pamoja nyumbani kwa mkewe huyo.
Huku miguu yake ikining'inia juu ya sakafu na sehemu yake ya chakula cha mtoto, inaonekana kama anakula chakula cha usiku na bibi yake.

UTAFITI WAONESHA WATANZANIA HAWANA IMANI NA POLISI, WANASIASA...

Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa kazini.
Watanzania wamepoteza imani na wanasiasa, polisi na wafanyabiashara, huku wakiwakubali zaidi, viongozi wa dini, walimu, madaktari na wauguzi.

JICHO LA TATU...

ABIRIA WENYE UZITO MKUBWA KUPANDISHIWA NAULI KWENYE NDEGE...

Abiria wenye uzito mdogo sasa wanaweza kupewa punguzo kubwa la nauli.
Mpango wa kulipa kadri ya uzito ulionao kwenye ndege unaweza kuanza kutumika sababu watu wenye uzito mkubwa wanagharimu zaidi katika mafuta wakati wa kuruka, profesa mmoja amedai.

BANDARI KUBWA AFRIKA KUJENGWA BAGAMOYO...

Wavuvi wakiendelea na shughuli zao kwenye moja ya fukwe za Bagamoyo.
Ziara ya siku mbili ya Rais wa China, Xi Jinping iliyomalizika jana, imeacha neema kwa Watanzania, ikiwemo makubaliano ya kutoa mkopo usio na riba kwa ajili ya maendeleo.

Monday, March 25, 2013

HIVI NDIVYO TAIFA STARS ILIVYOPIGA HATUA KOMBE LA DUNIA 2014...

Skrini kubwa ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ilivyokuwa ikisomeka mara baada ya mechi kati ya Taifa Stars na Morocco ambapo vijana wa Tanzania walifanikiwa kupiga hatua nyingine kuweza kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya pili katika kundi lake ikiwa imejikusanyia pointi 6 nyuma ya Ivory Coast yenye pointi 7. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars.

MWALIMU WA KIUME AVAA NGUO ZA KIKE MKUTANONI DODOMA...

Moja ya mitaa ya mji wa Dodoma.

Katika hali ya kushangaza, mwalimu wa kiume katika shule ya msingi Chididimo Kata ya Zuzu katika Manispaa ya Dodoma (jina tunalo),  juzi alitinga mkutanoni akiwa amevalia sketi na blauzi ya kitenge huku akiwa amesuka nywele za bandia na kuzua gumzo mkutanoni hapo.

SHY-ROSE BHANJI AZIDI KUMKALIA KOONI SAMUEL SITTA...

Shy-Rose Bhanji.

Mmoja wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shy-Rose Bhanji amesema walishafanyiwa semina moja tu, iliyoandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na hivyo kulalamikiwa kuwa ni watoro, ni uonevu.

ALIYETUMIKIA MIAKA 23 JELA KIMAKOSA AACHIWA HURU, APATA MARADHI YA MOYO...

David Ranta (katikati) akitoka gerezani.
Mtu ambaye aliachiwa huru baada ya kutumikia miaka 23 jela kwa makosa ambayo hakufanya anasumbuliwa na shambulio kubwa la moyo siku moja baada ya kuachiwa kwake.
David Ranta alikimbizwa hospitali ya New York Ijumaa usiku ambako aligundulika kwamba mmoja wa mishipa yake ya damu kuwa umeziba kabisa na mwingine ukiwa umeziba kidogo.
Mwanasheria wa Ranta, Pierre Sussman, alisema kwamba mteja wake alipokea matibabu na atalazimika kufanyiwa upasuaji mwingine.
Mlevi wa dawa za kulevya asiye na ajira, Ranta alihukumiwa kifungo cha miaka 37 na nusu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Rabbi Chaskel Werzberger mjini Williamsburg mnamo Februari 8, 1990.
Ranta aliachiwa huru Alhamisi baada ya majaji kugeuza hatia yake, ambayo ilipatikana kwa ushahidi wa uongo na kuweka wazi kwamba ulipotoshwa na polisi.
Mtu huyo mpya huru alikuwa akiishi kwenye hoteli na familia yake kufuatia kuachiwa kwake huku akiingia katika maisha yake mapya baada ya kutumikia karibu robo ya karne ndani ya gereza lenye ulinzi mkali.
Ijumaa usiku, mtu huyo mwenye miaka 58 alihisi maumivu mgongoni mwake na mabegani na kuwa na joto kali, kwa mujibu wa Sussman.
Kwanza, wapendwa wa Ranta walifikiri alipatwa na shambulio la mchecheto, lakini muda mfupi baadaye wakabaini kwamba ni mbaya zaidi ya hayo.
"Kiasi cha miaka yake katika gereza ambayo David ametumikia ni kitu kikubwa," aliongeza Sussman.
Shuhuda mtoto, ambaye ushahidi wake ulimtupa mwanaume huyo miaka 23 jela kwa mauaji ya mwalimu wa New York ambayo hakutenda, amezungumzia jinsi polisi walivyomweleza kumtambua mtu ambaye ametuhumiwa kimakosa.
Menachem Lieberman alikuwa na umri wa miaka 13 wakati alipooneshwa mstari wa watuhumiwa wa mauaji ya mwalimu wa dini ya Kiyahudi Chaskel Werzberger katika wizi wa almasi ambao haukufanikiwa.
Uamuzi wake wa kuhifadhi taarifa yake ulisababisha kuachiwa kwa David Ranta aliyetiwa hatiani kimakosa kutoka katika gereza lenye ulinzi mkali juzi baada ya miaka 23 ya kufungiwa humo.
Ranta aliachiwa huru baada ya jaji kupindua hatia yake ambayo ilisukumwa na ushahidi wa kimakosa wa shuhuda na mstari uliotengenezwa na polisi.
Sasa akiishi Montreal, shahidi huyo mwenye miaka 36 juzi alieleza jinsi polisi walivyomweleza kumchagua Ranta wakisema lazima 'achague yule mwenye pua kubwa'.
Mlevi wa dawa za kulevya asiye na ajira Ranta alihukumiwa kifungo cha miaka 37 na nusu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mwalimu wa dini ya Kiyahudi Chaskel huko Williamsburg mnamo Februari 8, 1990.
Siku hiyo mtu mmopja alijaribu kuteka gari lenye almasi na pale iliposhindikana kuliteka gari la mwalimu wa dini ya Kiyahudi Chaskel - alimpiga risasi kisogoni na kumuua.
Mauaji hayo yamebwatisha jamii ya Kiyahudi ya Kihasidi mjini Brooklyn na kutaka adhabu kali kwa aliyehusika.
Akiwa bado mwanafunzi wakati huyo, Lieberman alikuwa mmoja wa mashuhuda wa kutoroka kwa mtu huyo na utambulisho chanya wa Ranta ulishuhudia akifungwa mwaka 1991.
Zaidi ya miaka aligundua kwamba chaguo lake ulishinikizwa na mwaka 2011 - miaka 20 baadaye - aliamua kushirikisha wengine mashaka yake yote hayo.
"Huku miaka ikisonga, nilikumbuka mtu fulani aliniambia," alisema. "Kadri nilivyokuwa nikiona taarifa za kuachiwa kwa watu wasio na hatia - nilianza kufikiria nyuma hukumu ambayo nilihusishwa," alifafanua.
"Sikumweleza yeyote katika hii dunia lakini nilivyokuwa nikiendelea kukua na kuona zaidi na zaidi ya hizi hatia za kimakosa hakika ilinisumbua. Miaka miwili iliyopita nikaamua lazima nilitoe kifuani kwangu.
"Mtu asiye na hatia alikuwa jela na sasa ameachiwa huru - sehemu ya huzuni ni kwamba muuaji hajahukumiwa. Najihisi nilipangwa kama mtoto na nilitaka tu kutekeleza sehemu yangu katika hukumu."
Mpelelezi katika kesi hiyo, Louis Scarcella bado anapinga makosa yoyote na anasema hakukuwa na jaribio lolote la kumkomoa Ranta.
Hatahivyo, matatizo mengine yaligunduliwa pale Kitengo cha Uadilifu wa Hatia kilipotazama kesi hiyo.
Karatasi ziligundulika kupotea na miongozo mingine ikionekana kuwa haikuchunguzwa.
Mtuhumiwa mkuu mwingine alikuwa mlevi wa dawa za kulevya Joseph Astin. Mkewe alichunguzwa mwaka 1996 alikiri mauaji shidi yake siku hiyo lakini alifariki miezi miwili baadaye.
Katika yote, hii ilishawishi mahakama hiyo kwamba ulikuwa muafaka wa kumwachia Ranta, baba wa watoto watatu mwenye miaka 58.
Ndugu, akiwamo binti yake mdogo ambaye alikuwa mtoto mchanga wakati alipohukumiwa kifungo, walibubujikwa machozi na kupiga kelele za furaha.
Mwalimu wa dini ya Kiyahudi, Chaskel alikuwa kipendwa mno na wafuasi wake wa jumuiya ya Brooklyn.
Maelfu ya watu walihudhuria mazishi yake, na Meya wa wakati huo David Dinkins alitangaza dau la Dola za Marekani 10,000 kwa yeyote aliyekuwa na taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa mtuhumiwa.
Wakati Ranta alipokamatwa, gari la polisi lililomchukua kumpeleka jela lilizingirwa na wati wakiimba, "Hukumu ya kifo!"

JICHO LA TATU...