Yaliwekwa kimiani jumla ya mabao 12 katika mchezo mmoja. Hii ilikuwa jana ambapo baada ya kukandamizwa 4-0, Arsenal iliweza kubadili matokeo na mwisho wa mchezo kuibuka na ushindi wa mabao 7-5 dhidi ya Reading katika mechi ya Kombe la Capital One na kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali. Mabao ya Arsenal yaliwekwa kimiani na Theo Walcott aliyefunga mabao matatu kwa namna ya kipekee (Dakika ya 45, 90 na 120) huku mengine yakifungwa na Giroud, Kocielyn na Marouane Chamakh aliyefunga mawili. Hakika ilikuwa mechi ya ajabu!!
Wednesday, October 31, 2012
MFANYABIASHARA SALIM ABRI ASAS ACHANGIA UJENZI WA MABWENI KILOLO...
![]() |
Mfanyabiashara Salim Abri (kulia) katika picha ya pamoja na viongozi mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo ya saruji. |
![]() |
Salim Abri (wa pili kulia) akikabidhi mifuko 200 ya saruji kusaidia ujenzi wa mabweni wilayani Kilolo. |
Akikabidhi msaada huo ofisini kwake, Asas ambaye pia ni Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa, alisema kuwa amelazimika kuchangia ujenzi huo wa mabweni ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Jakaya Kikwete katika kuinua kiwango cha elimu ambapo elimu imekuwa ikipewa kipaumbele zaidi.
Alisema kuwa mbali ya kuchangia ujenzi huo katika wilaya ya Kilolo pia ameshafanya hivyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na maeneo mengine ya mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa wilaya ya Kilolo kupitia kwa Mkuu wa Wilaya waliandika barua kwake kuomba kusaidiwa ujenzi wa Shule za Sekondari na mabweni katika wilaya hiyo ya Kilolo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita mbali ya kumpongeza Asas ambaye pia ni mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa mkoani Iringa, aliwaomba wadau zaidi wa elimu katika mkoa wa Iringa wakiwemo wafanyabiashara kujitokeza kuchangia maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo ya Kilolo.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa saruji hiyo itagawanywa mifuko 50 kwa shule nne za sekondari ambazo zinaendelea na ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike.
Alizitaja shule za sekondari ambazo zitanufaika na msaada huo kuwa ni Uhambingeto, Gangwa, Ukwega na Masisiwe.
LORI LAUA WATU WATATU HUKU MWINGINE AKINYONGA MTOTO NA KUJIUA...
Kamanda wa Polisi Dodoma, Zelothe Steven. |
Watu watano wamefariki dunia mkoani Dodoma kutokana na matukio mawili tofauti likiwemo la mwanamume kunyonga mtoto wake na kisha kujiua na ajali ya lori iliyosababisha vifo vya watu watatu na wengine 40 kujeruhiwa.
Akizungumzia matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Steven alisema kuwa, mkazi wa Bicha Wilaya ya Kondoa Michael Jerome (43) alimuua binti yake Filomina Michael mwenye umri wa miaka mitatu kwa kumnyonga na kipande cha kitenge chumbani kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia kitenge hicho hicho.
Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 29, mwaka huu saa nne asubuhi
kijijini hapo ambapo chanzo cha mauaji hayo kinadhaniwa kuwa ni mgogoro wa ndoa baina yake na mkewe ambaye walikuwa wametengana tangu mwaka jana na alikuwa akihitaji kufika nyumbani kwa wakwe zake kwa ajili ya kikao cha usuluhishi.
Hata hivyo kamanda Zelothe alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea
kufuatilia uchunguzi zaidi wa tukio hilo la kinyama.
Katika tukio la ajali Kamanda Zelothe alisema kuwa, watu watatu wamefariki dunia huku wengine 40 kujeruhiwa baada ya gari la Jeshi lenye namba T.5747 JW09 aina ya Iveco likitokea kwenye msiba Kondoa mkoani hapa kuelekea Jijini Dar es Salaam kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea juzi mchana katika Kijiji cha Zoisa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma kwenye barabara ya Dodoma Kiteto.
Alisema gari hilo mali ya JWTZ Kikosi cha 312 cha Lugalo Jijini Dar es Salaam lilipinduka kutokana na mwendo kasi wa dereva Koplo Selemani Shija (40) ambaye alishindwa kulimudu gari wakati likiwa kwenye mteremko na kupinduka.
Waliofariki katika ajali hiyo wametajwa kuwa ni Thomas Degela anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 38 hadi 40, Zinduna Khalfani anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30 ambao makazi yao hayafahamiki na Mariam Omary (24), mkazi wa Mondo Kondoa.
Kamanda Zelothe alisema kuwa katika ajali hiyo watu 34 walijeruhiwa akiwemo dereva wa gari hilo ambalo majeruhi watatu kutokana na hali zao kuwa mbaya walihamishiwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Maria Pascal (30), Pendo Pascal (33), Mkazi wa Jijini Dar es Salaam na Rajab Hassan (22), mkazi wa Manyoni Singida.
Kamanda Zelothe alisema majeruhi 25 wamelazwa katika hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Kongwa wakiendelea na matibabu.
Aliwataja watu hao kuwa ni Koplo Shija, Ayub Salum, Salum Kajelele, Akida Muhehe, Hamisi Bakari, Adam Ramadhani, John Pascal, Elisha Mahaki, Mohamed Hussein, Sikitu Abdallah, Zuhura Lameck, Rehema Idd (35) na Rukia Masudi.
Wengine ni Salma Ramadhani, Zuhura Abasi, Arafa Shabani, Stahimily Masudi, Hafsa Kijuu, Leah Jonas, Anastazia Pascal, Aliza Ally, Elizabeth Agustino, Hadija Ibrahim na Halima Hassan.
Pia majeruhi sita walitibiwa katika kituo cha afya cha Mkoka Wilaya ya Kongwa na kuruhusiwa ambao ni Husna Kavina, Asha Idd, Yassin idd, Nadia Muhagi, Mariam Daimeshi na Hussein Njenha.

POLISI WASHUSHA BENDERA YA KUNDI LA UAMSHO ZANZIBAR...
![]() |
Mmoja wa wafuasi wa Uamsho akionesha bendera ya kundi hilo. |
Baada ya kuchoshwa na vitendo vya kihuni vinavyofanywa visiwani hapa, Serikali imeamua kusafisha vigenge hivyo ikiwa ni pamoja na kushusha bendera za Jumuiya ya Uamsho zilizokuwa zikipepea katika maeneo mbalimbali mitaani mjini hapa.
Kazi hiyo inafanywa na Jeshi la Polisi ambalo limethibitisha kusaka vikundi hivyo vya kihuni ambavyo vimekuwa vikijipachika majina mbalimbali kwa kutumia mwavuli wa Jumuiya hiyo kufanya fujo.
Akizungumza kwa simu jana, Kamishna wa Polisi, Musa Ali Musa, alisema polisi wamekuwa wakifanya msako dhidi ya vigenge vya vijana wanaofanya uhalifu na kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.
“Jeshi la Polisi linachokifanya ni kutafuta vigenge vinavyofanya uhuni na kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria … tumeanza kuwabaini baada ya kutumia teknolojia kupitia video,” alisema Musa.
Alisema baadhi ya vijana wameanza kukamatwa baada ya picha zao kuonekana kwenye maandamano ya Jumuiya ya Uamsho wakiwa na mapanga huku wakitoa kauli za ‘Chinja! Chinja’!
“Polisi haifanyi kazi kwa kukiuka misingi ya haki za binadamu … tunawafuata wahusika wa fujo baada ya kuwatambua,” alisema Kamishna Musa.
Taarifa zilizopo zilisema zaidi ya bendera 50 ziliteremshwa katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya Bububu, Mboriborini na Daraja bovu.
Aidha, ulinzi mkali na msako vinaendelea katika maeneo kadhaa ya mji ikiwa ni pamoja na Bububu ambako aliuawa askari Said Abrahman kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana wakamjeruhi na kusababisha mauti yake.
Hivi karibuni, Jeshi la Polisi lilionesha picha za baadhi ya vijana wakiwa mstari wa mbele kwenye maandamano ya Jumuiya ya Uamsho, huku wakiwa na mapanga na Polisi kuomba msaada kwa wanaowajua kutoa taarifa ili kufikishwa kunakohusika.
Akihutubia Baraza la Iddi mjini hapa, Rais Ali Mohamed Sheni alisema uvumilivu wa Serikali sasa umefika kikomo na kuongeza kwamba vyombo vya Dola vitachukua hatua kali dhidi ya watakaobainika kuvunja sheria za nchi huku akisisitiza hakuna aliye juu ya sheria.
Jumuiya ya Uamsho imeingia katika matatizo na Serikali baada ya wafuasi wake wakiongozwa na Shekhe Farid Hadi Ahmed, kutokana na kufanya maandamano na vurugu.

WAZIRI WA NISHATI AIPIGA 'STOP' EWURA KUPANDISHA UMEME...
![]() |
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. |
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza Mamlaka ya Nishati na Maji nchini (EWURA), kutopandisha bei ya umeme kwa kuwa Serikali inalipa baadhi ya gharama za ufuaji umeme kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45, kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV Dar es Salaam juzi, Profesa Muhongo alisema badala ya kupandisha bei ya umeme, Serikali imeshusha gharama za kuunganisha umeme ili wananchi wengi wanufaike, kwani nishati hiyo si anasa bali ni huduma inayotakiwa.
“Hivi kama Serikali inatoa fedha za kuendesha mitambo ya kufua umeme, sasa Tanesco wanataka kupandisha bei ya umeme kwa mantiki gani, na wanazipeleka wapi hizo fedha?” Alihoji Waziri Muhongo.
Alifafanua kwamba Serikali inatoa fedha kufanya kazi hiyo kwenye mitambo ya kufua umeme nchini, hivyo hakuna sababu ya kupandisha bei ya umeme na kwamba hata madeni ya Tanesco ya mafuta ya mitambo hiyo yameanza kulipwa na Serikali.
Kuhusu mgao wa umeme, Profesa Muhongo alisema hakuna mgao wa umeme nchini na hautakuwapo na masuala ya umeme wa dharura pia hayatakuwepo tena na kusisitiza, kuna baadhi ya watu wanafurahia mgao kwa sababu binafsi zikiwamo za kisiasa na biashara.
“Niwaambie Watanzania, kwamba hakuna mgawo wa umeme na hautakuwapo, haya mambo ya umeme wa dharura nayo hayapo tena, ila kuna watu wanafurahia uwepo wa mgawo na hiyo ni kwa sababu zao binafsi zikiwamo siasa na biashara,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema Watanzania wamechoka kuishi maisha ya karne ya 16, ilhali wapo karne ya 21, ya Sayansi na Teknolojia na kusisitiza, kwamba ni lazima wananchi kwenye maeneo yote nchini wapate umeme ili kuleta maendeleo.
“Hatuwezi kuendelea kama nishati ya umeme haitafikia wananchi wengi, hivi sasa watumiaji wa nishati ya umeme nchi nzima ni asilimia 18.4 na vijijini ni asilimia 6.6, hii si sahihi ni lazima umeme usambae vijijini na nchi nzima,” alisema Profesa Muhongo.
Alitaka Watanzania wasiwe na hofu ya umeme, kwani mpango wa wizara kwa miaka mitano ijayo ni kuhakikisha ifikapo 2015, umeme utakaozalishwa utaongezeka hadi megawati 2,780 kutoka za sasa ambazo ni 1,438.24
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, hivi sasa matumizi ya umeme ya juu nchini ni megawati 830 na kiwango hicho cha matumizi hakijawahi kufikiwa kwa muda mrefu isipokuwa miezi miwili iliyopita ambapo yalifikia megawati 850.
Kuhusu kufikia lengo la kuzalisha megawati 2,780, alisema hilo linawezekana, kwa kuwa anaamini ana uwezo wa kulitekeleza na kwamba wizara anayoiongoza ni moja ya fani zake na tayari wameanza kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme.
“Umeme tunaotumia sasa asilimia 65, umetokana na gesi asilia na tunatarajia pia kuzalisha umeme kutokana na makaa ya mawe ya Ngaka,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema tatizo kubwa la awali la mgao wa umeme lilitokana na miundombinu ya Tanesco kuchoka na hujuma na wizi wa miundombinu ya shirika hilo.
Profesa Muhongo alisema hata kama umeme ungezalishwa mwingi usingesafirishwa, kwa kuwa miundombinu iliyopo imechoka, hivyo katika mpango wa miaka mitano wa wizara hiyo, miundombinu ni eneo mojawapo linalofanyiwa kazi.
Alisema, ikiwa umeme utakatika ghafla, alishaagiza mameneja wa Tanesco kwenye kanda mbalimbali nchini kuomba radhi Watanzania kupitia vyombo vya habari na kueleza kwa nini jambo hilo limetokea.
Aliongeza, kuwa kama kuna matengenezo yanafanyika kwenye maeneo fulani na inabidi umeme ukatwe, ni lazima taarifa zitolewe kwa wananchi kupitia vyombo vya habari zikielewa ni maeneo gani hayatakuwa na umeme na kwa muda gani na sababu zipi.
Akizungumzia uchimbaji mafuta, gesi na urani, Profesa Muhongo alisema kuna upotoshaji mkubwa kuhusu rasilimali hizo na kwamba upotoshaji unachochewa na watu waliohudhuria mafunzo ya wiki moja kuhusu gesi na urani.
“Wapo wapotoshaji wakubwa wanaojidai kuwa mabingwa wa gesi na urani, si kweli, wamehudhuria mafunzo ya wiki moja na kupewa vyeti vya mahudhurio, sisi hatushindani nao, tunatumia wataalamu wetu wenye vyeti vya kitaaluma,” alisema Profesa Muhongo.
Kuhusu kugawa vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi kwa wawekezaji, alisema si jambo geni kwenye sekta hiyo na tangu uhuru kuna mashimo 53 yaliyokwishachorongwa kwa ajili ya kuangalia kama kuna gesi au mafuta ardhini.
Alisema kitaaluma ni lazima utafiti wa mafuta au gesi ufanyike ikiwamo uchorongaji na kutaka wapotoshaji wanaosema wanajua masuala ya gesi na urani waache, kwa kuwa mambo haya yanaendeshwa kitaalamu.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), ni lazima lisukwe upya ili liendane na hali ya sasa na kuwa na kampuni ya kizalendo itakayofanya utafiti wa gesi na mafuta badala ya kuziachia kampuni binafsi za nje kufanya kazi hiyo.

MWANAMKE ABAKWA MARA MBILI KATIKA MATUKIO TOFAUTI USIKU MMOJA...
![]() |
KUSHOTO: Mtuhumiwa wa kwanza wa ubakaji, Yussuf. KULIA: Eneo ambapo tukio hilo la ubakaji lilifanyika. |
Mwanamke ambaye alikokotwa kwenye kichochoro na kubakwa akitoka matembezini usiku alikumbana na tukio lingine la kutisha kwa kubakwa na mwanaume mwingine wakati akijizoazoa baada ya shambulio la kwanza.
Mustafa Yussuf ndiye alikuwa wa kwanza kumbaka mwanamke huyo wakati akitembea katikati ya jiji la Manchester katika Sherehe za Mwaka Mpya, akipita kwenye maegesho ya magari yaliyoko Church Street na kumbaka karibu kabisa na barabara.
Baada ya shambulio hilo mwanaume huyo aliyekuwa na miaka 20 wakati huo akitoweka eneo la tukio, akimwacha mwanamke huyo bila msaada wowote.
Ni wakati huo ndipo, badala ya kumsaidia, mwanaume mwingine akamvamia mwanamke huyo na kuanza kumbaka tena.
Habari za matukio hayo mawili ya ubakaji zimebainika wakati Yussuf ambaye sasa ana miaka 21, mkazi wa Manchester, akihukumiwa kifungo cha miaka saba jela kutokana na shambulio hilo.
Alidai kufanya mapenzi na mwanamke huyo lakini akakanusha kumbaka.
Lakini Baraza katika Mahakama ya Manchester limetupilia mbali utetezi wake na kumtia hatiani.
Jaji Martin Steige, akitoa hukumu, alisema hana shaka kwamba Yussuf alifahamu kabisa kwamba mwanamke huyo alikuwa amelewa mno kiasi cha kutojitambua.
Mahakama ilielezwa kwamba mwanamke huyo 'mtu mzima' alikunywa kupita kiasi sababu ya matatizo yake ya kimapenzi, huku kamera za CCTV zikimuonesha akiwa hawezi kusimama.
Alizuiwa kuingia tena kwenye klabu ya usiku wakati alipotaka aruhusiwe kuingia akatafute begi lake dogo la mkononi alilopoteza ndani ya klabu hiyo.
Baada ya kubakwa mara mbili, mwanamke huyo alihitaji msaada kutoka kwa watu baki kuweza kufika nyumbani kwake na kwa masaa mawili hakuweza kabisa kukumbuka kilichomtokea.
Muathirika aliieleza mahakama kwamba maisha yake yamezimwa kufuatia shambulio hilo na ametengwa kwa hofu ya kutembea nje.
Jaji Steiger alisema: "Wakati fulani baada ya shambulio la kwanza alibakwa tena na mtu mwingine."
Mwanaume mwingine alikamatwa kufuatia shambulio la pili la ubakaji lakini akaachiwa bila kufunguliwa mashitaka yoyote.

Tuesday, October 30, 2012
TIMU YA AZAM YAMTIMUA TENA KOCHA WAKE...
![]() |
Kikosi cha timu ya soka ya Azam. |
Uongozi wa timu ya soka ya Azam umemtimua tena kocha wake Mserbia Boris Bujak ‘Buka’ kwa madai ya kutoridhishwa naye.
Mserbia huyo amefukuzwa ikiwa ni miezi mitatu tu tangu achukue jukumu la kuinoa timu hiyo kutoka kwa Muingereza Stewart Hall, ambaye naye alitimuliwa kwa tuhuma kama hizo baada ya kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la Kagame ambapo ilifungwa na Yanga mabao 2-0 Julai mwaka huu.
Habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa Azam zilizopatikana Dar es Salaam jana, zilisema, uongozi wa timu hiyo umeamua kumrudisha kocha wake Hall ambaye kwa sasa anaifundisha Sofapaka ya Kenya.
“Kocha Buka amefukuzwa hivi ninavyokwambia ameshalipwa haki zake zote na ameshakatiwa tiketi yake Ijumaa anaondoka, mechi zijazo timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Kally Ongala mpaka Hall atakapokuja… na hatachelewa kuja kwa maana Sofapaka hana mkataba,” alisema mtoa habari wetu.
Habari zaidi zinasema kuwa sababu ya Azam kumtimua kocha huyo ni kutoridhika na kiwango kinachooneshwa na timu tangu kupewa jukumua la kuinoa.
Timu hiyo mwishoni mwa wiki ilifungwa mabao 3-1 na Simba, katika mechi ya Ligi Kuu Bara na ushindi wa juzi wa Coastal Union umeishusha hadi nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 18.
“Lakini pia hata sisi wachezaji hatukumbali, hivyo wengine walikuwa na kamgomo baridi, hata katika mechi na Simba, kulikuwa na mzozo kwenye benchi, baadhi ya wachezaji wakilaumiana kufanya hujuma ili kocha aondolewe, wale ambao hawamkubali walicheza chini ya kiwango kwa makusudi,” alisema mtoa habari wetu.
Msemaji wa Azam, Jaffar Iddi hakuwa tayari kulizungumzia hilo kwa madai alikuwa hajafika ofisini mpaka saa tisa alasiri jana.
Mbali na kuiongoza Azam kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya Kombe la Kagame, Hall ambaye awali alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar, aliiongoza timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa mwaka huu baada ya kushika nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya Simba.

POLISI YAKAMATA MENO YA TEMBO YA SHILINGI BILIONI 2.1...
![]() |
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. |
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imekamata meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni 2.1, yakiwa katika viroba vilivyofunikwa na Bendera ya Taifa, na kuhifadhiwa katika nyumba eneo la Kimara Stop Over, Kinondoni.
Akizungumza ofisini kwake jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema baada ya kukamata nyara hizo za Serikali juzi saa 6.30 mchana, wataalamu wa Maliasili walifanya majumuisho na kubaini kuwa yalitokana na tembo 91 waliouawa.
Mbali na nyara hizo, pia walikamata watuhumiwa wanne wa uhalifu huo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.
Nyara hizo na mali zingine zinazodaiwa kuibwa na majambazi katika matukio mbalimbali Dar es Salaam, kwa mujibu wa Kova, zilikutwa ndani ya nyumba ya Peter Kami, raia wa Kenya anayeishi na mwanamke Mtanzania, Leonida Kabi.
Wengine waliokamatwa ndani ya nyumba hiyo ni Charles Wainaine (41) ambaye ni ndugu wa Leonida na dereva wa daladala, Polisi Simon (42).
“Tunawashukuru raia wema wanaoendelea kushirikiana nasi kupambana na uhalifu na tunawaomba waendelee hivyo hivyo, maana hata kukamata watu hawa, ndio wamefanikisha,” alisema Kova.
Idadi ya meno hayo ni 214 na yaliyokuwa katika viroba 12. Sambamba na men ohayo pia kulikutwa pembe 10 za ng’ombe zikiwa zimeshindiliwa chokaa na mifupa mitano ya tembo.
Alifafanua kuwa katika kubaini idadi ya tembo waliouawa, wataalamu wa Maliasili walifanya majumuisho ya kitaalamu ya meno na mifupa hiyo na kugundua kuwa na jumla ya kilo 450.6 ambazo ni sawa na tembo 91.
Kwa mujibu wa Kova, uchunguzi wa awali ulionesha kuwa watu hao ni wahalifu wazoefu katika matukio mbalimbali ya kijambazi pamoja na usafirishaji na umiliki wa nyara za Serikali.
Pia alidai kwamba walikuwa na mpango wa siri wa kusafirisha meno hayo kwa kutumia gari aina ya Toyota Coaster linaloendeshwa na Simon.
“Kulikuwa na mpango wa siri wa kusafirisha meno haya kwa kutumia Coaster (Toyota) ambapo wangeweka jeneza lililofunikwa Bendera ya Taifa kama vile wanasafirisha maiti ya mtu maarufu serikalini.
“Lengo lilikuwa kuhadaa vyombo vya Dola na Mamlaka husika; nyara hizi zingevushwa kwenda nje kupitia mpaka wa Tarakea, Rombo kwenda Kenya,” alisema Kova.
Alisema Leonida anashikiliwa kwa tuhuma zingine za kushawishi askari waliokamata mali hizo kupokea rushwa ya Sh milioni 15 kama kianzio na kuwaahidi nyingine siku inayofuata, baada ya benki kufunguliwa, ambapo askari hao walikataa na kuwapeleka kituoni.
Kova alisema uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini mtandao wa wizi wa nyara za Serikali nchini na nje ya nchi na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
“Hawa askari walishawishiwa kupokea rushwa lakini walikataa, nawapongeza sana na kuna zawadi ambazo nitawapa, kwa sababu wameonesha ujasiri wa hali ya juu na kutanguliza utaifa,” aliongeza Kova.
Katika tukio lingine, Polisi wakishirikiana na ulinzi shirikishi wamemkamata Swalish Rweyemamu (23) kwa tuhuma za wizi wa pikipiki na mali mbalimbali akiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa kujifanya abiria na kukodi pikipiki na baada ya kufika mbele, alimnyang’anya dereva wa pikipiki ya bodaboda baada ya kumtishia bastola bandia.
Kamanda Kova alisema walipomkamata mtuhumiwa na kumpekua, walikuta kitambulisho kilichotolewa na JWTZ cha namba (TPDF) DFF 7001 831 KJ na anuani S.L.P. 1992 Dar es Salaam.
Kitambulisho hicho kwa mujibu wa Kova kilitolewa Machi 13, 2008 kwa jina la MT. 84187 Ahmed Salum. Pia alikutwa na nguo za kiraia ambazo inadaiwa hubadilisha baada ya tukio.

FAO LA KUJITOA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII SASA RUKSA...
![]() |
Moja ya vikao vya Bunge mjini Dodoma. |
Baada ya wafanyakazi na baadhi ya wabunge kulalamikia Sheria ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2012 inayozuia mwanachama kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, Serikali imeridhia wafanyakazi kujitoa kwenye mifuko hiyo na kupewa mafao yao kama ilivyokuwa awali.
Chanzo cha habari kutoka serikalini, kimebainisha kuwa katika mkutano wa tisa wa Bunge la 10 unaanza leo, Serikali itawasilisha tamko lake la kuruhusu fao hilo la kujitoa.
Taarifa hizo zinabainisha, kuwa Tamko la Serikali litakalotolewa bungeni, litafuta barua ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA), Irene Isaka iliyobainisha kuwa Serikali imefuta fao hilo la kujitoa na kuzuia wanachama kuchukua mafao yao.
“Serikali imeona kisheria haiwezekani kuzuia mfanyakazi kujitoa kwenye mfuko wowote, hivyo imeamua kuwasilisha taarifa yake rasmi ya kufuta muswada wake iliokuwa iuwasilishe ambao ulionekana una upungufu na hivyo kuifuta barua ya SSRA,” kilisema chanzo cha habari.
Barua ya SSRA itakayofutwa na tamko hilo, iliyokwenda kwenye mifuko hiyo ya hifadhi za jamii, ilikataza wafanyakazi kupewa mafao wanapojitoa hadi watimize miaka 55 ya kustaafu kwa hiari au kwa lazima miaka 60.
Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja alipoulizwa juu ya taarifa za fao hilo kuwasilishwa bungeni alikataa kusema lolote, akidai taarifa za shughuli za Bunge zitatolewa leo kwa wabunge na waandishi wa habari na hapo ndipo itakapojulikana.
Hatua ya Serikali imekuja baada ya Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jafo (CCM), kuwasilisha hoja binafsi bungeni kutaka Bunge liazimie kuitaka Serikali iruhusu fao la kujitoa liendelee.
Hata hivyo, wabunge waliazimia mambo manane ikiwamo fao hilo la kuzuiwa kujitoa lirekebishwe pamoja na barua ya Mkurugenzi Mkuu wa SSRA kufutwa.
Mbali na hoja binafsi pia Jafo alitaka kuwasilisha muswada binafsi wa kutaka fao hilo lirejeshwe, lakini muswada huo ulikataliwa kwa sababu Azimio la Bunge lilishapitishwa na kamati inayohusika na masuala ya hifadhi ya jamii ndiyo ilitakiwa ipeleke muswada.
Hata hivyo Jumatano iliyopita, wabunge walipewa muswada wa Serikali wenye lengo la kuufanyia marekebisho Sheria ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2012 lakini marekebisho hayo yalihusu Mfuko wa Pensheni wa PPF pekee, kuruhusu wanachama kujitoa na kupewa mafao.
Mbunge Jafo aliliambia gazeti hili kwamba; “muswada huo tuliona una upungufu na hatukukubaliana nao, kwani ulikuwa unaletwa bila hati ya dharura, maana yake utasomwa kwa mara ya kwanza na baadaye Bunge lijalo utasomwa tena, lakini tumepanga kesho (leo) tupinge hilo.”
Hata hivyo, tayari Serikali imeonekana kubaini upungufu wa muswada huo na ndiyo maana inatarajia kueleza wabunge nia ya kupeleka tamko bungeni kuruhusu wafanyakazi kujitoa na kupewa mafao kama ilivyokuwa awali kabla ya aheria hiyo ya mwaka 2012.
Minja alisema jana kuwa Kamati ya Uongozi chini ya Mwenyekiti wake, Spika Anne Makinda imeshakaa na kupanga shughuli za Bunge na leo baada ya kipindi cha maswali na majibu, vikao vya kamati mbalimbali za Bunge na za vyama vya siasa zitakutana na baadaye wabunge wataelezwa ratiba ya shughuli za Mkutano wa Tisa wa Bunge la 10.

MKALI WA FILAMU YA 'BRING IT ON' AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI...
![]() |
Natina Reed (katikati) akiwajibika katika moja ya shoo za kundi la Blaque. |
Natina Reed, mwigizaji wa filamu ya "Bring It On" aliyoshirikiana na Lisa 'Left Eye' Lopes protégé, na mshirika wa kundi la R&B la Blaque, amefariki Ijumaa usiku mjini Atlanta baada ya kugongwa na gari, Polisi wa Gwinnett County wamethibitisha.
Natina, ambaye alikuwa na miaka 32 wakati akifikwa na mauti, alikuwa atimize miaka 33 juzi Jumapili.
Kwa mujibu wa Gwinnett, Sajenti Rich Long alitangaza kuwa amekufa katika Kituo cha Afya cha Gwinnett Saa 4:59 usiku.
Majira ya Saa 4:30 usiku wa Oktoba 26, dereva wa gari hilo alipiga simu kuelezea kwamba amemgonga mtembea kwa miguu.
Taarifa za awali zinaashiria kwamba Natina alikuwa kando ya barabara katika Barabara Kuu ya Lawrenceville karibu na Barabara ya Hamilton ndipo alipogongwa na gari. Dereva wa gari hilo anadhaniwa kuwa hana makosa na hakuna mashitaka yoyote yaliyofunguliwa mpaka sasa."
Dereva hue an abiria wake wanaaminika kuwa ndio mashuhuda pekee, na mamlaka zinahifadhi majina yao hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
Mshirika wa Blaque, Shamari Fears-De Voe, ametuma salamu za rambirambi kupitia mtandao wa Twitter. "Moyo wangu na roho vina uchungu mkubwa," aliandika. "Dada yangu, rafiki yangu mkubwa, nitakupenda siku zote."
Blaque, ilitoa albamu mbili, ya mwaka 1999 kujitambulisha na ile ya mwaka 2002 ya "Blaque Out." Mwaka 2000, walitokea kwenye filamu ya "Bring It On."
"Bring It On," film inayohusu viongozi we makundi pinzani, iliongozwa an Kirsten Dunst an Gabrielle Union, ambaye aliongoza timu zilizokuwa zikipingana. Natina na wenzake wa Blaque walikuwa sehemu ya wafuasi wa Union. Filamu hiyo iliingiza Dola za Marekani milioni 90 na kufuatiwa na mfululizo wa video nne. Filamu ya mwisho, "Bring It On: Fight To The Finish," iliingia mitaani mwaka 2009.
Agosti, Natina alijadili mipango ya Blaque kurejea kwenye gemu katika mahojiano na Website ya YouKnowIGotSoul. Julai, Blaque lilifanya onesho kwenye Tamasha la Muziki la First Annual Left Eye huko Decatur. Mshauri wa Natina, Lopes alikufa kwenye ajali ya gari mjini Honduras Aprili, 2002.
Natina ameacha mtoto wa kiume mwenye miaka 10, Tren Brown aliyezaa na Rapa wa Kundi la Dogg Pound, Kurupt.

WILL SMITH AKUMBUSHIA ENZI ZAKE ZA 1991...
Will Smith amempa
Gabrielle Union -- mtandao mzima wa intaneti -- zawadi bora zaidi
kuwahi kutolewa juzi usiku pale aliponyakua kipaza sauti kwenye sherehe
ya kutimiza miaka 40 mwanamitindo huyo wa zamani na kurap kama
alivyokuwa akifanya mwaka 1991.
Smith, pamoja na mkongwe Doug E. Fresh kwa upande wake walitumbuiza miondoko ya sauti bila midundo … na kisha kudondosha vitu vikali kama "Summertime na kibwagizo kutoka katika tamthiliya ya "Fresh Prince of Bel Air."
Smith alirudia kurekodi rap yake ya "Summertime" mwezi Juni na kuonjesha kidogo "Fresh Prince" katika kipindi cha "The Graham Norton Show" kinachorushwa na BBC mwezi Mei.
Hakika kuna vitu huwa havizeeki.

MAMA WA WHITNEY AMALIZA BIFU NA BOBBI KRISTINA...
![]() |
Bobbi Kristina (kushoto) na Cissy Houston. |
Bibi wa Bobbi Kristina, Cissy Houston amefuta mpango wake wa kutaka kuzuia fedha zilizoachwa na Whitney Houston mbali na Bobbi kwa miaka kadhaa, baada ya kuelezwa kwamba bibi huyo sasa amemaliza bifu na mjukuu wake huyo.
Imeelezwa, Cissy na Pat Houston (msimamizi mwenza wa mali za Whitney) walifungua madai ya kisheria kuomba kubadili utaratibu wa namna fedha za Whitney zitakavyogawanywa kwa Bobbi ambaye ana miaka 18, sababu wanafikiria 'ni nyingi mno, na mapema sana kufanya hivyo.'
Kama ilivyo, Bobbi alitakiwa kupokea fedha hizo zaidi ya Dola za Marekani milioni 20 kwa mikupuo mitatu tofauti … asilimia 10 wakati atakapotimiza miaka 21 (sawa na Dola milioni 2), chini ya asilimia 20 atakapotimiza miaka 25 (sawa na Dola milioni 4) na kiasi kilichobaki pale atakapotimiza miaka 30 (sawa na Dola milioni 16).
Sasa, imeelezwa … kesi hiyo imefutwa baada ya Bobbi na bibi yake Cissy wamefikia muafaka … na vyanzo vya habari vimesema mpango wa malipo uliokuwa umependekezwa na marehemu Whitney haujabadilika.
Imeelezwa kwamba wote, Bobbi na Cissy wameridhia mpango huo … na wanafurahia kuachana na kesi hiyo.

CHEKA TARATIBU...
Wakati ndege ya shirika moja kubwa ikiwa angani ndipo ikasikika sauti kutoka kwenye vipaza sauti ikisema, "Mimi ni Rubani Martin. Kwa niaba ya wafanyakazi wote napenda kuwakaribisha kwenye ndege yetu kutoka Dar es Salaam kuelekea Visiwa vya Comoro. Kwa sasa tuko umbali wa futi 35,000 kutoka usawa wa bahari katikati ya Bahari ya Hindi.
"Mkitazama dirishani upande wa kushoto mtagundua kwamba injini ya ndege inawaka moto.
"Na kama mkichungulia upande wa kulia mtagundua bawa limeanguka.
"Pia mkichungulia chini kwenye Bahari ya Hindi mtaweza kuona maboya madogo yakiwa na watu watatu wakiwapungia mikono.
"Hao ni mimi Rubani, msaidizi wangu na mmoja wa wahudumu. Ujumbe huu umerekodiwa tu. Nawatakia safari njema!" Kasheshe...

Monday, October 29, 2012
ANYWESHWA DAWA YA KUACHA WIZI, KISHA AFARIKI...
![]() |
Mmoja wa tembo katika Hifadhi ya Serengeti. |
Watu wawili wamekufa katika matukio tofauti, wilayani hapa, akiwamo aliyenyweshwa dawa ya kienyeji, baada ya kukiri kosa la wizi wa miwa ya mwanakijiji mwenzake, na mwingine kwa kuuawa na tembo wakati akifanya uwindaji haramu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Vyombo vya usalama wilayani hapa vimesema tukio la kwanza lilitokea Oktoba 24 saa 3 asubuhi katika kijiji cha Salama Kati, ambapo wachungaji wawili wa ng’ombe, Edwin Revocatus (19) na Mugisha Jackson (17) walituhumiwa kuiba miwa katika shamba la mwanakijiji mwenzao.
Ilielezwa kuwa mwenye shamba hilo, Warioba Makanga aliwakamata na kuwapeleka kwenye ofisi ya kijiji hicho ambako walikiri kosa na kuomba msamaha.
Ilidaiwa kuwa baada ya kutoka ofisini hapo, mwenye shamba hilo alitafuta mganga wa kienyeji kijiji jirani na mganga huyo kuja kuwanywesha dawa watuhumiwa hao, kama ishara ya kuapa kutorudia kosa na kuachana kabisa na wizi.
“Mganga huyo aliwanywesha dawa hiyo na baada ya kuinywa hali zao zilibadilika,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Aidha, ilielezwa kuwa baada ya kunywa dawa hiyo matumbo ya wafugaji hao yalijaa, na muda mfupi baadaye Revocatus alipoteza maisha huku Jackson akikimbizwa katika Kituo cha Afya Nyamuswa, ambako bado amelazwa.
Vyombo vya ulinzi na usalama wilayani hapa vilisema kutokana na hali hiyo, wananchi wa kijiji hicho walijichukulia sheria mkononi kwa kubomoa nyumba za mmiliki wa shamba hilo.
Aidha, ilielezwa kuwa watuhumiwa hao ambao ni Warioba Makanga na Makanga Makanga, baada ya tukio hilo walitoroka na wanatafutwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Katika tukio lingine la usiku wa Oktoba 24, katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Maduhu Baraka (55), mkazi wa kijiji cha Nyamatoke, wilayani hapa, aliuawa na tembo kwa kuchomwa na pembe tumboni wakati akifanya uwindaji haramu katika hifadhi hiyo.
Ilielezwa kuwa mwananchi huyo alikuwa akiwinda na wenzake ambao hawajajulikana na kwamba wenzake walikimbia baada ya mnyama huyo kumshambulia mwenzao.
Mmoja wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi wilayani Bunda ambaye hakutaka kutajwa kutokana na kwamba yeye si msemaji wa Jeshi hilo, alithibitisha kusikia matukio hayo lakini akasema hawezi kulitolea ufafanuzi.

WIVU WA MAPENZI WASABABISHA KUKATISHA UHAI KWA VISU...
Wakati mvuvi kutoka Kambi ya wavuvi ya Kakoma – Kilangawana katika Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Evod Luvanga (32), akidaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma kisu akimtuhumu kumdhalilisha kwa rafiki zake kumdhihaki kuwa mkewe ni mzinifu, mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam, amemchoma kisu na kumuua mchumba wake kwa sababu za kimapenzi.
Katika tukio la Sumbawanga, Luvanga anadaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma kisu ubavuni akimtuhumu kumdhalilisha mbele ya rafiki zake kwa kumdhihaki kuwa mkewe ni ‘mzinifu aliyekubuhu’.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha mauaji hayo yalitokea juzi katika kambi hiyo ya wavuvi usiku wa manane, ambako mtuhumiwa anadaiwa kumuua kwa kumchoma kisu ubavuni mkewe aitwaye Ales Mwanja (20) na kumsababishia umauti.
Kwa mujibu wa baadhi ya wavuvi kutoka kambi hiyo, walidai mtuhumiwa wivu dhidi ya mkewe ulikuwa ukiwaka kwa nguvu ndani yake, kwani alidai anampenda sana na hatakuwa tayari katika maisha yake kusikia ana mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine zaidi yake.
Inadaiwa kuwa kutokana na tabia yake hiyo ya kujigamba kumpenda sana mkewe, wenzake walianza kudhihaki iweje ampende kiasi hicho mkewe wakati ni ‘mzinifu’, hali iliyomkwaza mtuhumiwa ambaye aliahidi kuifanyia uchunguzi wa kina dhihaka hiyo.
“Kuanzia hapo tulimsikia mwenzetu huyu daima akilalamika kuwa mkwe si mwaminifu eti alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine hivyo aliapa ‘kumshughulikia’ ipasavyo ili wote wamkose,” alidai mmoja wa wavuvi hao.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, chanzo cha mauaji hayo ya kikatili ni wivu wa kimapenzi na kwamba Ales alifariki dunia muda mfupi baadaye kutokana na kuvuja damu nyingi.
Kamanda Mwaruanda alisema mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani.
Jijini Dar es Salaam, Fatuma Selemani (21) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, amemchoma kisu mchumba wake, Selemani Ramadhani (24) mkazi wa Magomeni Somanga, na kufariki dunia akipelekwa hospitali.
Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo juzi saa saba mchana kwa sababu za wivu wa kimapenzi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyela, Fatuma alimchoma kisu Ramadhani na kukimbilia kwa kaka yake aitwaye, Omary Matimbwa na kumwambia amemchoma kisu kifuani mchumba wake na anatoka damu kama maji.
Katika tukio jingine, Erasto Chalamila anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 30 hadi 40, mlinzi wa Kampuni ya Ultimate Security, mkazi wa Kinondoni Hananasif, amekutwa amekufa ndani ya chumba chake na mwili wake hauna jeraha lolote huku ukiwa umevimba ukitokwa na damu pia ukiwa na harufu kali.

MABABU WAWILI WAMBAKA MJUKUU WAO WA MIAKA 11 DAR...
![]() |
Kamanda Charles Kenyela. |
Mtoto wa miaka 11 aliyekuwa anasoma Darasa la Sita katika Shule ya Msingi ya Mbezi wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, amedaiwa kubakwa na babu zake wawili wenye umri wa zaidi ya miaka 50.
Kutokana na hali hiyo, mama wa mtoto huyo (wote majina tunayo), anatishiwa maisha na ndugu wa mwanamume aliyezaa naye baada ya kutoa siri za kubakwa kwa mtoto huyo.
Mama huyo amedai kutaka kugeuziwa kesi baada ya kushitaki polisi vitendo vya ubakaji alivyofanyiwa mwanawe na babu zake wawili wa upande wa baba anaodai wana umri zaidi ya miaka 50 kwa nyakati tofauti, Julai na mapema mwezi huu (Oktoba).
Akizungumza jana, mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kufanyiwa vitendo hivyo na babu zake wawili, mkazi wa Mbezi, Malamba Mawili, Dar es Salaam, alidai mwanawe alibakwa na alipoamua kuchukua hatua polisi, sasa anatishiwa na ndugu wa mwanamume.
“Mwanamume niliyezaa naye mtoto huyo (jina tunalo) tuliachana, mwezi mmoja uliopita akaja kumfanyia uhamisho mtoto kwenda Gongo la Mboto anakoishi kwa vile mtoto ana zaidi ya miaka saba, sikukataa niliposikia japo hakunishirikisha, lakini tangu amemhamisha mpaka leo shule hajaanza,” alisema mama huyo na kuongeza:
“Wiki mbili zilizopita, nilipigiwa simu na baba wa mtoto wangu kuwa mtoto ametoroka, nikaenda na tukatoa taarifa Kituo cha Polisi Gongo la Mboto, niliporudi nyumbani kesho yake, wakanipigia amepatikana kwa babu yake mdogo katika familia ya babu mzaa baba yake, wakiniomba niende tukaongee maana kuna jambo limetokea.”
Mama huyo alisema alipokwenda, alikuta kuna kikao cha ndugu wa mwanamume na walianza kumwomba radhi wakimueleza kuwa mtoto alitoroka baada ya kuingiliwa kimwili na babu ndugu wa familia (jina tunalo) na walimtaka wamalize suala hilo kifamilia.
“Mtoto alipohojiwa alikiri kweli kubakwa na babu huyo na walisisitiza nisamehe huku wakimtaja Mungu, lakini mimi nikasema hilo ni kosa la jinai, tulipotoka nikaenda Polisi Mbezi kwa Yusuf ili mtoto ahojiwe na kisha hospitali ya Serikali ya Mbezi kumpima mwanangu,” alidai mama huyo.
Alisema vipimo vya hospitali vilihakikisha kweli mtoto alibakwa, lakini akawa hana ujauzito wala Ukimwi na mtoto alipohojiwa polisi, alikiri kubakwa na kueleza kuwa vitendo hivyo alikuwa akifanyiwa pia na babu mdogo wa mwisho kwa babu yake Julai mwaka huu.
“Kinachonisikitisha ni kwamba, yule mgambo aliyenisaidia kuwapata watuhumiwa hadi kuwafikisha polisi, sasa amekamatwa na watuhumiwa wapo huru, kama haitoshi, ndugu wa mwanamume wananitumia ujumbe wa simu wa kunitishia kuwa watahakikisha wananigeuzia kesi, naomba Serikali inisaidie katika hili,” alilalamika mama huyo.
Alisema pia Polisi wamekuwa wakimpiga danadana kuhusu suala hilo akiwafuata kuulizia hivyo kutokana na vitisho vya ndugu wa mwanamume wanaodai watamshikisha adabu kwa kuwa ameidhalilisha familia yao kushitaki suala hilo polisi wakati wangelimaliza kifamilia, anaishi kwa wasiwasi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alipoulizwa jana kuhusu tukio hilo, alisema hana taarifa, lakini alisema Polisi inawezekana wanafanya upelelezi ndio maana hawana jibu la moja kwa moja kwa mama huyo kiasi cha kuona anazungushwa na kumuomba aende ofisini kwake leo.
“Naomba kama anahisi anazungushwa au kuonewa, aje ofisini kwangu kesho (leo), unajua kesi kama hizi zinahitaji upelelezi, pande zote mbili lazima watafute ukweli, siwezi kusema sana maana sijafikishiwa tukio hili kwangu ila kama anaona mambo hayaendi aje,” alisema Kenyela.
Baba mzazi wa mtoto huyo alipotafutwa kwa simu ya mkononi, namba yake ilikuwa ikiita bila kupokewa na baadaye mtu mwingine alizungumza na mwandishi, kumweleza kuwa simu ya baba huyo ni mbovu.

CHADEMA NA CCM WAINGIA VITANI TENA ARUSHA...
![]() |
Kamanda wa Polisi Arusha, Liberatus Sabas. |
Hali tete ilijitokeza jana katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Daraja Mbili jijini Arusha, baada ya makada wawili wa CCM na Chadema kudaiwa kufyatua risasi hewani.
Makada hao ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nasari na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) Wilaya ya Arusha, God Mwalusamba.
Wakati Nasari akikanusha madai hayo na kumtupia mpira Mwalusamba, kada huyo wa CCM alikuwa akiandikisha maelezo yake jana jioni katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha; wakati Nasari na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wakisakwa na Polisi kutokana na tukio hilo.
Kata 19 nchini ikiwamo ya Daraja Mbili, jana zilikuwa zikifanya Uchaguzi Mdogo wa madiwani kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo za waliokuwa wakishikilia nyadhifa hizo kufariki dunia.
Nasari anadaiwa kuwafyatulia risasi hewani mfululizo na kufanya wananchi waliokuwa wakienda katika kituo cha Shule ya Sekondari ya Felix Mrema kupigia kura, kutawanyika hovyo, hali iliyozua tafrani na vurugu kubwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na wafuasi zaidi ya 10 wa Chadema kukamatwa huku Nasari na Lema wakisakwa baada ya kutoroka kutokana na vurugu hizo.
Waliokamatwa ni Efraim Mmasi, Nicholaus Andrew maarufu ‘Ringo’, Makenzi, mwingine aliyefahamika kwa jina la Snoka na wengine ambao hawakufahamika majina yao mara moja.
Nasari anadaiwa kuanzisha vurugu hizo akiongozana na Lema ambapo kijana wa CCM, Kabwelwa Mturuka alijeruhiwa mkononi kwa kukatwa na panga na mfuasi wa Chadema.
Pia vurugu hizo zilisababisha kushambuliwa kwa kipigo na kuporwa kwa simu ya mkononi na fedha za Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha, Martin Munis na wafuasi hao wa Chadema na tukio hilo limeripotiwa polisi na kupewa namba AR/RB/13624/2012 ya shambulio la kudhuru mwili.
Vurugu hizo zilitokea eneo la Mtaa wa ‘Alinyanya’ jirani na Ofisi ya Mtendaji Kata ya Daraja Mbili baada ya wafuasi wa Chadema kufika katika eneo hilo wakiwa na silaha hizo na kuwazingira wananchi ambao wengi wao walikuwa wafuasi wa CCM walipokuwa wakienda kupiga kura katika kituo hicho.
Kabla ya vurugu hizo, alifika Lema akiwa ndani ya gari aina ya Noah akiwa na Nasari na baadhi ya wafuasi wao ambapo kabla ya gari hilo kusimama, Nasari alishuka na baada ya muda mfupi walifika wafuasi wengine wakiwa katika gari jingine aina ya Toyota Land Cruiser VX mali ya Lema.
Imeelezwa kuwa lengo la kuwazingira wananchi hao ni ili kuwatisha wasipige kura kwa kuhofia vurugu ambapo hata hivyo zimeonekana kuathiri kwa kiasi upigaji kura, huku likishuhudiwa na askari Polisi waliokuwa wamesimama nje la lango la kuingilia shuleni hapo.
Kutokana na kuwapo kwa umati mkubwa wa wananchi, wengi wao wakiwa wafuasi wa CCM, Nasari anadaiwa kutoa bastola yake na kufyatua risasi tatu hewani, jambo ambalo liliwashitua wananchi wakiwamo wafuasi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Alinyanya, Omar Sheikh.
Kutokana na kudhibitiwa, Nasari, Lema pamoja na wafuasi wao walipanda katika magari yao na kisha kuondoka na kuelekea katika ofisi yao ya chama na kuanza kuzungumza na wafuasi wao.
Akizungumzia tukio hilo, Sheikh alisema kutokana na vurugu hizo, wananchi wengi waliingiwa na woga wa kwenda katika vituo vya kupiga kura, hali iliyosababisha kuomba msaada wa kusindikizwa.
Kwa upande wake, Mwalusamba ilibidi apige risasi nne hewani baada ya kudaiwa kuzingirwa kwa silaha za jadi na wafuasi wa Chadema.
Tukio hilo lilizuka saa 5 asubuhi pale wafuasi wa Chadema wakiwa na silaha za jadi, panga, sime, marungu na fimbo, walipowazingira wanachama wa CCM kwa madai kuwa walikuwa na shahada za ziada.
Akizungumzia tukio hilo, mwanachama wa UVCCM, Ramadhani Mkulu ambaye shati lake lote lililowa damu alidai kupigwa risasi hewani na Mwalusamba kuliwaokoa kukatwa mapanga na vijana wa Chadema.
Mkulu alidai mwenzao Kabwele Mturuka amekatwa mkono na panga na wengine kujeruhiwa vibaya.
“Baada ya kuona hali hiyo ikiwa mbaya sana, Mwalusamba alipiga risasi nne hewani, risasi zilizosaidia kwa asilimia kubwa kutuliza jazba, lakini hali ilikuwa tete na kama Mwalusamba asingepiga risasi maafa yangekuwa makubwa zaidi,” alidai Mkulu ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa.
Mwalusamba hakupatikana kueleza tukio hilo kwani alikuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha akitoa maelezo ya kupiga risasi hewani na tukio zima kwa ujumla.
“Si unaniona niko hapa Polisi….subiri kidogo kaka nikitoka hapa ntakutafuta na kukupa taarifa rasmi juu ya hiki ninachoandika hapa,” alisema Mkulu akiwa kituoni hapo.
Kwa upande wake, Nasari alisema yeye hawezi kuwa mpuuzi kiasi cha kupiga hovyo hovyo kwani “sasa nimekua na nina majukumu mengi katika jimbo.”
Alikiri kuwapo katika Kata ya Daraja Mbili, lakini aliyepiga risasi ni Mwalusamba. “Mimi sijapiga risasi kaka, nina akili timamu…siwezi kuwa na akili mbovu kiasi hicho. Mtu aliyepiga risasi ni Mwalusamba,” alidai.
Uchaguzi huo wa Daraja Mbili ulitokana na kifo cha aliyekuwa Diwani wa CCM, Bashir Msangi na ulihusisha vyama vya CCM, Chadema, NCCR- Mageuzi, TLP na CUF. Wakati tukienda mitamboni, matokeo ya awali yalionesha kuwa CCM ilikuwa imeachwa nyuma na Chadema katika vituo vyote 39.

Mchungaji wa kanisa moja baada ya kukagua jengo la kanisa lake akagundua kuna ulazima wa kupaka rangi tena. Kesho yake akaenda mjini kununua galoni moja ya rangi akurudi kanisani na kuanza kazi ya kupaka rangi. Baada ya kumaliza upande mmoja akagundua amebakiwa na nusu galoni tu. Akaamua kuchakachua kwa kuchanganya na mafuta ya taa ili iweze kutosha pande tatu zilizobaki. Kweli akafanikiwa. Usiku mvua kubwa sana ikanyesha na alipoamka asubuhi kukagua kazi aliyofanya jana yake akagundua rangi imeondoka kwenye kuta zile tatu. Mchungaji akatazama juu na kuanza kulia, "Jamani sasa nitafanyaje?" Ghafla sauti ikajibu kutoka juu, "Rudia kupaka rangi na usijaribu tena kuchakachua!" Duh...
MWANAMKE ALIYEUPONDA UISLAMU SASA ADAI UMEMLETEA UPENDO NA FURAHA...
![]() |
KUSHOTO: Heather kabla ya kuingia katika Uislamu. KULIA: Heather akiwa na watoto wake. |
Kusilimu kwake kutoka msichana wa Ibiza hadi kuwa Muislamu wa kuvaa hijab ndani ya kipindi cha miezi mitatu kunaweza kuibua mshangao, na anakiri kwamba rafiki zake wanaweza kudhani ni moja ya kufifia kwake.
Lakini mwalimu aliye mafunzoni Heather Matthews mwenye miaka 27, anasema Uislamu umemletea 'upendo na furaha' ambayo hakuweza kuipata katika maisha yake ya zamani.
Heather, mama wa watoto wawili, alijiunga kwenye imani hiyo mpya wiki nne zilizopita, miezi miwili baada ya kurejea kutoka mapumzikoni huko Ibiza. Na anasema kwamba picha zake za zamani zilizopigwa katika safari hiyo zinaonesha yote yaliyo mabaya pamoja na picha cha urembo za Magharibi.
Alisema: "Nilifikiri nilihitaji kuchukua hatua na kuvaa katika njia nitakayojihisi vizuri mwenyewe. Naona wasichana sasa na kufikiri kuhusu taswira gani wanayoonesha kwa watu wengine, hasa wanaume.
"Ni juu ya kujiheshimu mwenyewe. Kama unavaa na kujiweka katika njia fulani, kisahihi au kimakosa, utachukuliwa katika njia hiyo hiyo.
"Uislamu umenifundisha kuhusu upendo halisi, si hamaki na tamaa. Ninaweza pia kuona maana katika ndoa iliyopangiliwa."
Uchunguzi uliofanywa na kundi la imani zaidi la Faith Matters umegundua idadi ya Waislamu waliosilimu nchini Uingereza sasa imevuka 100,000, ikiwa ni mara mbili zaidi katika kipindi cha miaka kumi.
Ripoti imekadiria karibu ya theluthi mbili ya watu wapya waliosilimu kuwa ni wanawake, wakiwa na wastani wa umri wa miaka 27 kama alivyo Heather.
Safari yake katika kusilimu ilianzia pale alipojaribu kumshawishi mumewe wa zamani Jerrome, ambaye alihamia Uislamu, kwamba dini hiyo haikuwa sahihi. Alikuwa 'na mashaka mno' kuhusu imani hiyo, na kuanza kusoma kuhusu dini hiyo ili kuzipa nguvu hoja zake.
Ingawa walikuja kutengana mwaka jana, aliendelea kujifunza kuhusu Uislamu, na kujitambulisha zaidi na zaidi kuhusu hilo. Kisha, wiki nne zilizopita, alimaliza mchakato wa 'kurejea'. Alisema: "Nilipitia maadhimisho ya 'Shahadah' ya kusilimu kuwa Muislamu kwa kurudia azimio la imani mbele ya Imam katika kituo cha kukuza imani kilichopo karibu na eneo langu.
"Nilikuwa na dada zangu kashaa wa Kiislamu pamoja nami na walininunulia hijab na vitabu vya Kiislamu kusherehekea. Ilishangaza sana."
Lakini anakiri kwamba marafiki zake wamepatwa na mshituko kwa kusilimu kwake katika dini ambayo inaaminika kuwa inawakandamiza wanawake.
"Watu wamekuwa wakijiuliza "Oh, hii ni hatua nyingine katika kufifia kwa Heather". Si kweli. Ni kile nilichokuwa nikitafuta katika kipindi chote nilichokuwa nikijaza maisha yangu kwa shauku ya kupanua maarifa," alisema.
Heather, mkazi wa Preston, amekuwa akikabiliana na wakati mgumu kutoka kwa familia yake. Lakini ni msukumo kutoka kwa wapitanjia kwamba ameshangaza sana hasa muonekano wa ushungi wake kichwani.
"Hakuna wanaume wanaojaribu kunitongoza. Ni ujingwa wa kuchukiza. Pale ninapovaa ushungi ninaweza kucheka na watu bila wao kufikiri ni kujitongozesha," alisema.
"Nimekubaliana kabisa na taratibu za Kiislamu kwa kutofanya mapenzi na mtu ambaye hujafunga naye ndoa na kulinda urembo wako kwa mumeo. Hivyo nafikiri mpenzi wangu ajaye atatakiwa kuwa aliyejifunza Uislamu ili kuelewa.
"Ni rahisi kwangu sasa kusema haya, kwa jicho pembe, kuwa nilifanya makosa, lakini nafikiri nilipotezwa na marafiki ambao wazazi wangu walidhani wananifaa, kujifunza kuwapenda kupitia kwanza urafiki."
Heather ameacha kabisa pombe, huku akikazania mlo unaoruhusiwa na imani hiyo na amepanga kufunga mwezi wa Ramadhani. Anacho kitabu cha Qur'an kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza ambacho anakisoma kila siku, na anataka kujifunza Kiarabu ili kuweza kuswali sala mara tano kwa siku.
Lakini amesema hatalazimisha Uislamu kwa binti zake wawili - Ellah mwenye miaka mitano na Halle mwenye miaka miwili, aliozaa katika ndoa yake na Jerrome.
"Watu wanafikiri nitakandamizwa lakini niko imara, najiamini na mwanamke huru," alisema. "Najua mimi ni mmoja wa watu ambao hawakufikiriwa kuingia katika Uislamu.
"Inanishangaza. Lakini nimefanya kwa upendo na furaha na imebadili kabisa maisha yangu."

Sunday, October 28, 2012
UMAARUFU WA MSANII LULU ULIANZIA HUKU...
Pamoja na filamu nyingine kadhaa alizocheza, lakini hapa Msanii
Elizabeth Michael maarufu kama Lulu aling'ara zaidi akicheza kama binti
wa Senga katika filamu ya Wema ambayo iliingia mitaani mwaka 2006.
Wakati sasa Lulu akikabiliwa na mashitaka ya kumuua msanii mwenzake,
Steven Kanumba, filamu hii aliyocheza akiwa bado binti mbichi kabisa
inaendelea kutesa kwenye vituo vikubwa vya kimataifa kama DStv kupitia
Chaneli ya Africa Magic Swahili (158).Tumewaletea kipande hiki kama
utambulisho wa kipengele kipya cha "TUMETOKA MBALI" kitakachoanza
kukujia kupitia blogu hii siku chache zijazo!
P. DIDDY AONEKANA AKIDUNDA MITAANI BAADA YA AJALI MBAYA...
![]() |
P. Diddy akivuka barabara katika moja ya mitaa ya mjini Los Angeles. |
Licha ya kupata majeraha kadhaa katika ajali mbaya ya gari Jumatano iliyopita, mwimbaji Sean Combs 'Diddy' ameonekana akiranda kwenye mitaa ya Los Angeles juzi huku akionekana mwenye afya njema.
Kama ilivyoripotiwa, Diddy alihusika kwenye ajali mbaya ya gari huko Beverly Hills, na kwa mujibu wa mwakilishi wake, gwiji huyo wa rap alipata majeraha katika shingo, mbavu na mgongoni.
Diddy alikuwa akiendeshwa ndipo gari lake SUV lilipogongana na gari jingine. Baada ya ajali hiyo, Diddy alipatwa na mshituko na hivyo kulazimika kulala chini kwenye majani.
Cha kushukuru ni kwamba anaendelea vema kwa sasa.

Jamaa mmoja baada ya kukurupushwa kwenye fumanizi akatoka mbio huku bila nguo hata moja na kudandia daladala lililokuwa mbele yake. Wakati akijiweka sawa, akagundua kondakta alikuwa akimkodolea macho kwa mshangao. Jamaa kwa ukali akasema, "Unashangaa nini sasa?" Kondakta akajibu kwa upole, "Sikushangai Bro, ila najiuliza utakuwa umeweka wapi nauli!" Kasheshe...
MSICHANA ALIYEMUUA MPENZI WAKE KATIKA AJALI YA KIZEMBE AFUNGWA JELA...
![]() |
KUSHOTO: Mabaki ya gari baada ya ajali. KULIA: Eleanor Coleman. |
Kijana aliyemuua rafiki yake kwenye ajali ya gari kufuatia usiku mzima wa sherehe ya sanamu amesema 'hatajisamehe mwenyewe' wakati akihukumiwa kifungo juzi.
Eleanor Coleman mwenye miaka 19, alikuwa katumia dawa za kurusha akili na bangi wakati akisherehekea na rafiki zake katikati ya mji wa Norwich huku wakiwa wamevalia nguo za vituko.
Lakini wakati akiendesha gari kuelekea nyumbani majira ya Saa 11 alfajiri gari lake aina ya Fiat Punto liliserereka kando ya barabara na kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limeegeshwa pembeni.
Gari hilo liliwaka moto na dereva wa lori Peter Jolly akafanikiwa kuokoa maisha ya Eleanor kwa kumburuta nje ya gari lake kabla ya kulipuka.
Aliomba msaada kwa wapita njia, ambao waliweza kuwatoa abiria wengine kutoka kwenye gari hilo lililoharibika vibaya, mahakama ilielezwa.
Lakini abiria aliyekuwa ameketi katika kiti cha mbele Ellie Tweed mwenye miaka 18, alinaswa ndani ya gari hilo lililokuwa likiwaka moto na kufa, Mahakama ya Norwich ilielezwa.
Eleanor alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela juzi baada ya kukiri kusababisha kifo kutokana na uendeshaji wake wa kizembe.
Jaji Peter Jacobs alisema: "Ulikuwa na uchovu na hukuwa na uwezo wa kuendesha gari kabisa.
"Utajutia hili kwa kipindi chote kilichobakia cha maisha yako."
Ajali hiyo ya kutisha iliyokea Novemba 11, mwaka jana kwenye Barabara ya A47 huko Runham, karibu na Great Yarmouth, Suffolk.
Eleanor, ambaye alikuwa 'akijirusha' mjini Norwich, alipata majeraha kadhaa kichwani na hana kumbukumbu yoyote ya kilichotokea.
Vipimo vimeonesha kwamba alikuwa amevuta bangi ingawa hakukuwa na uthibitisho kwamba ndivyo vilivyochangia kusababisha ajali hiyo.
Haikufahamika kilichosababisha ajali hiyo lakini abiria wengine watatu walipata majeraha makubwa na wote waliokuwa wamekaa kiti cha nyuma hakuwa wamefunga mikanda.
Barua iliyoandikwa na Eleanor, ambayo ilikabidhiwa kwa Jaji na kusomwa kwa sauti mahakamani hapo ilisema: "Najichukia mwenyewe kwa kila kitu kilichotokea na kamwe ziwezi kujisamehe mwenyewe."
Eleanor alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela na kufungiw kuendesha gari kwa kipingi cha miaka mitatu.
Pia aliamriwa kurudia mtihani wa udereva kabla ya kuruhusiwa kurejea tena barabarani.

JUMBA ALIMOFIA MICHAEL JACKSON LAPATA MNUNUZI...
Jumba ambamo Mfalme wa Pop duniani, Michael Jackson alifia sasa iko mnadani na unakaribiwa kufungwa ... imefahamika ... na mnunuzi alikuwa na wasiwasi, anahamia humo wiki chache zijazo kabla ya tarehe iliyopangwa ya mnada huo kufungwa.
Mnunuzi huyo ni Steven Mayer, mwekezaji tajiri mno wa benki.
Vyanzo vya habari vimesema bei ya kununulia ilikuwa kati ya Dola za Marekani milioni 17 na milioni 20 ... ilikuwa imeorodheshwa kuuzwa kwa karibu Dola za Marekani milioni 24.
Na hii inavutia mno ... kwa sababu fulani muuzaji kumruhusu Mayer kuingia kabla ya kufungwa mnada ... jambo ambalo linadhaniwa na madalali wakongwe kuwa ni hatari kubwa mno.

Saturday, October 27, 2012
FAMILIA YA RAIA WA UGANDA YAVUNA MAMILIONI KITAPELI UINGEREZA...
![]() |
KUTOKA JUU: Lamulah, Albert na Jordan. KULIA: Mahakama ambako kesi hiyo inasikilizwa. |
Familia ya walaghai wa Kiafrika imeiba kiasi kisichopungua Pauni za Uingereza milioni 4 kutoka kwa walipakodi katika kipindi cha miaka 20.
Mmoja alitengeneza vitambulisho feki kwa watoto zaidi ya 100 ili kufaidi utaratibu wa mfumo wa mafao.
Pia alidai kuwa na virusi vya ukimwi na kuhitaji dawa za gharama kubwa mno - lakini badla yake alizisarifisha kinyemela kwenda nchini Uganda kwa ajili ya kuziuza kwa faida kubwa.
Mahakama ilielezwa kwamba usafirishaji dawa hizo kwa miaka mingi uliwagharimu walipakodi zaidi ya Pauni za Uingereza milioni 2.
Zaidi ya Pauni za Uingereza 154,000 zililipwa kwa ajili ya elimu kwa 'familia', ambapo Pauni za Uingereza 37,000 ni kwa ajili ya kozi moja tu ya elimu ya juu.
Ulaghai unaohusiana na gharama za malazi na kodi ya pango la maghorofa uligharimu Pauni za Uingereza 650,000, na kiwango kikubwa cha mafao ya familia kinachofikia Pauni za Uingereza 900,000.
Kwa kipindi cha wiki sita cha usikilizwaji kesi yao, baraza la mahakama lilielezwa jinsi kundi 'lililoungana kuandaa, kutumia na kunyonya' utambulisho feki kwa lengo la kutekeleza ulaghai wa kuduwaza.
Mchunguzi mmoja alilieleza gazeti la Daily Mail: "Balaa ni, walikuwa na vitambulisho vingi mno kwamba inaweza isifahamike hasa kiasi gani walichovuna kutoka kwenye mfumo wa mafao na nchi hii katika kipindi hicho kirefu."
Mwendesha mashitaka Paul Raudnitz alisema: "Mkono wa ulaghai huu umefika mbali na kwa mapana kwa miaka mingi sana. Kila mshitakiwa kwa mara tofauti alishiriki njama hizo."
Alisema 'mshiriki mkuu' Ruth Nabuguzi mwenye miaka 49, 'ametumia vitambulisho kadhaa ... vingi kiasi kwamba idadi ya vitambulisho haiwezi kufahamika'.
Nabuguzi, mwenye asili ya kutoka Uganda, alidai dawa za Ukimwi zilizogharimu Pauni za Uingereza 2,280,000. Pia alipokea Pauni za Uingereza 500,000 kwa ajili ya mafao ya nyumba kutoka Halmashauri ya Newham huko mashariki mwa London, Mahakama ya Croydon ilielezwa.
Nabuguzi aliingia Uingereza mwaka 1991 na kuomba hifadhi ya ukimbizi yake mwenyewe na ya watoto wanne aliowaacha nchini Uganda.
Miaka mitatu baadaye, alitumia jina la Jane Namusisi kuomba tena hifadhi ya ukimbizi sambamba na ya watoto wawili zaidi. Mwaka 1999 akitumia jina la Pauline Zalwango, aliomba tena hifadhi safari hii akiwa na watoto wengine watatu.
Anaaminika amekuwa akisafiri mara kwa mara kwenda Uganda na kuweza kununua nyumba takribani tatu ndani na maeneo mbalimbali katika mji mkuu Kampala.
Dennis Kyeyune mwenye miaka 29, anadhaniwa kuwa ni mtoto wa Nabuguzi. Polisi walikuta begi jeusi kubwa la kubebea nguo nyumbani kwake mashariki mwa London likiwa limefichwa kwenye paa na mkoba wenye nyaraka bandia, ulioelezewa kama 'hifadhi ya ulaghai wa vitambulisho'.
Wafuasi wengine wa genge hilo ni pamoja na Jordan Sebutemba mwenye miaka 26, ambaye anadhaniwa kuwa ni binti wa Nabuguzi; Albert Kaidi, mshirika wa zamani wa Sebutemba ambaye anadhaniwa kuwa na asili ya Rwanda; na Lamulah Sekiziyuvu mwenye miaka 36, mshirika wa zamani wa Kyeyune na Kaidi.
Kyeyune, Sebutemba, Kaidi na Sekiziyuvu walipatikana na hatia ya makosa mbalimbali ya ulaghai juzi.
Watahukumiwa wiki ijayo sambamba na Nabuguzi na Betty Tibakawa mwenye miaka 21, Lina Katongola mwenye miaka 29, Mathy Matumba mwenye miaka 50, na Eddie Carlos Semcenda mwenye miaka 30.

Friday, October 26, 2012
TUNAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA IDD EL HAJJ...
Mhariri na timu yake nzima ya ziro99blog tunawatakia Waislamu wote kote duniani na Watanzania kwa ujumla heri na fanaka katika kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hajj. Tunawasihi Waislamu wote kusherehekea Sikukuu hii kwa amani na utulivu wa hali ya juu ili kuenzi matendo mema aliyotufundisha Mtume Muhammad (S.A.W). -Mhariri
WALIMU WAKATA RUFAA KUPINGA KUSITISHWA MGOMO WAO...
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, kupinga uamuzi wa kusitisha mgomo uliotolewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, kwa madai ulikuwa batili.
Katika rufaa hiyo iliyowasilishwa juzi mahakamani hapo na Wakili wake, Gabriel Mnyele, CWT inadai kuwa uamuzi huo uliotolewa na Jaji Sophia Wambura haukufuata sheria.
Mnyele anadai Jaji alikosea kisheria kuamuru mgomo huo usitishwe kwa madai ulikuwa batili na pia alikosea kisheria kuamuru taarifa ya kwanza ya kuzuia mgomo ilikuwa mbaya kisheria kwa sababu ilitolewa siku za mwisho wa wiki.
Jaji Wambura pia anadaiwa kukosea kuamuru kwamba mgomo ulipaswa kuwa na kikomo na alikosea kusema upigaji kura wa wanachama wa kuunga mkono haukufanyika kihalali.
Katika hati hiyo ya kukata rufaa, Mnyele alidai Jaji Wambura alikosea kisheria kuwaamuru wakata rufaa kulipa fidia bila uthibitisho.
Katika uamuzi huo unaokatiwa rufaa, Jaji Wambura aliamuru chama hicho kusitisha mgomo, kulipa hasara kwa wanafunzi iliyosababishwa na mgomo huo, ikiwa ni pamoja na kufidia muda wa masomo waliyokosa wakati wa mgomo.
Jaji Wambura alisema sheria ilikiukwa na chama hicho kutoa notisi ya siku 48 Ijumaa na kuanza mgomo Jumatatu asubuhi, huku wakijua siku za mwisho wa wiki hakuna kazi serikalini.
Aidha, alisema walitangaza mgomo wakati kesi ikiwa mahakamani, hivyo pamoja na kuwapo upigaji kura kwa wanachama wake kukubali au kukataa mgomo huo, bado haikuwa sahihi. Alisema pia kulikuwa na kasoro, kwa kuwa hawakueleza kisheria ni mgomo wa aina gani na ukomo wake.

SHEKHE FARID WA UAMSHO KULA IDD EL HAJJ GEREZANI...
![]() |
Wafuasi wa Uamsho wakitoka mahakamani huku wakiwa chini ya ulinzi mkali. |
Mahakama ya Vuga mjini Unguja, imetupilia mbali ombi la dhamana kwa kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Shekhe Farid Hadi Ahmed na wenzake sita na hivyo kuwafanya kusherehekea Sikukuu ya Idd el-Hajj katika gereza kuu la Kinua Miguu mjini hapa.
Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazzi anayesikiliza kesi hiyo alitangaza uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe 8 mwezi ujao, kwa sababu mbili; kubwa ikiwemo hakimu aliyesikiliza kesi hiyo awali hakuwa na mamlaka ya kusililza kesi hiyo.
Aidha Mrajisi Kazzi alisema watuhumiwa wamenyimwa dhamana kwa sababu za usalama kwa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Awali watuhumiwa hao walisomewa mashtaka matatu mbele ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Raya Mselem ikiwemo mwaka huu kushawishi kufanya fujo na vurugu.
Aidha tarehe 26 Mei hadi Oktoba 17 huko Lumumba pamoja na Fuoni mjini hapa waliendesha mhadhara wakitoa maneno ya kashfa yenye kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
Mwendesha mashtaka Raya alisoma shtaka la tatu ikiwa kula nyama za kujificha kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed na kusababisha mtaharuki mkubwa kwa wananchi kulikopelekea kuzuka kwa fujo na vurugu zilizosababisha uharibifu mkubwa wa mali za wananchi kinyume na sheria kifungu 399 sheria nambari 6 ya mwaka 2004.
Mapema wakili wanaowatetea watuhumiwa na viongozi wa jumuiya ya uamsho Abdalla Juma na Salum Toufiq walilazimika kuondoka katika mahakama hiyo kwa madai kwamba wamekuwa
wakihangaishwa na kukosa mawasiliano na taarifa kamili kutoka kwa wateja wao.
Awali wananchi wengi pamoja na waandishi wa habari walifika katika mahakama ya Mwanakwerekwe ambayo awali ilisikiliza kesi hiyo, lakini kumbe watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya Vuga mjini hapa.

DALADALA YA TRENI DAR KUANZA RASMI JUMATATU IJAYO...
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe amesema kuwa usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam utaanza Jumatatu wiki ijayo.
Akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Kampuni ya Reliu (TRL), Dk Mwakyembe alisema siku hiyo saa 12 asubuhi atafanya uzinduzi mdogo wa usafiri huo na baadaye watamwomba Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufanya uzinduzi mkubwa wa mpango huo ambao umebuniwa na uongozi wa wizara hiyo.
Waziri huyo alisema kutokana na juhudi zilizofanywa na wafanyakazi wazalendo wa TRL wamefanikiwa kutengeneza na kukarabati mabehewa na injini za kampuni ambazo zilikuwa mbovu na hivyo kuwezesha usafiri huo uweze kuanza siku hiyo ya Jumatatu.
"Napenda kuwashukuru wafanyakazi kwani licha ya kutokuwepo bajeti ya mpango huu na ndani ya muda mfupi baada ya kuwaombeni kufanya kazi hii ya kukarabati mabehewa na injini mbovu, mmefanya hivyo na tarehe 29 mwezi huu tutazindua usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam," alisema Mwakyembe.
Usafiri huo unaanza baada ya kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa 14 na injini 2 hivyo kuwezesha mpango huo ambao unalenga kupunguza kero ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam.
Kwa kuanzia usafiri huo utakuwa kati ya Ubungo hadi Stesheni na baadaye utafuata maeneo mengine ambako kuna reli ya Kati na ile ya Tazara.
Waziri huyo pia alisema Serikali kwa kutambua umuhimu wa TRL ndio maana imetenga fedha kwa ajili ya kukarabati miundombinu za kampuni hiyo ili kuweza kuinua uchumi wa nchi.
Alisema ili kufanikisha hilo, Serikali imetenga Sh bilioni 104 kwa ajili ya kufanya ukarabati na ununuzi wa vitendea kazi na akaeleza kuwa miongoni mwa kazi zitakazofanywa kwa fedha hiyo ni ukarabati wa injini tatu, behewa 22 za abiria, mabehewa ya mizigo 125 na kununua mabehewa mengine ya mizigo 274 na behewa za breki 43.
Alisema Sh bilioni 18.9 kati ya hizo zitatumika kukarabati karakana mbalimbali za kampuni hizo zilizoko Dar es Salaam na mikoani.
Alisema Sh bilioni 8.1 zimetengwa kwa ajili ya kukodisha vichwa kutoka nje ya nchi, lakini akasema kuwa wamechukua sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kufanya ukarabati wa injini na mabehewa ambayo yatakuwa yanatoa usafiri kwa treni itakayokuwa inatoa huduma jijini Dar es Salaam.
"Zimebaki Sh bilioni 5.1 kwa ajili ya kukodi vichwa kutoka nje ya nchi, lakini hawa ambao tumewaomba kutukodishia wanaamini kuwa sisi ni vichwa vya wendawazimu nadhani hatutaweza kukodi tena hivyo vichwa badala yake tuwawezeshe wafanyakazi wetu wakarabati hivi vilivyopo," alisema waziri huyo.
Dk Mwakyembe alisema wakodishaji hao wametoa bei ya Sh milioni 3 kwa siku kwa ajili ya kukodisha kichwa kimoja, gharama ambazo ni kubwa kuliko zile ambazo Rites ambao ni wawekezaji wa zamani ndani ya TRL ambao walikuwa wanakodisha kichwa kimoja kwa Sh
milioni moja kwa siku.
"Huu ni uwendawazimu kuendelea kukodi vichwa hivi na kama wanang'ang'ania nawasihi achaneni nao na tufufue vichwa vilivyopo kwa kutumia hiyo pesa iliyopo," alisema Dk Mwakyembe.
Pamoja na mafanikio hayo, Dk Mwakyembe amewaeleza wafanyakazi hao kuwa ndani ya TRL kuna tabia mbaya ya wizi na udokozi pamoja na hujuma mbalimbali mambo ambayo alisema yanamtia kichefuchefu.
Mtendaji Mkuu wa TRL, Kipallo Kisamfu alikiri kuwa mafuta ndio yanachukua kiasi kikubwa cha fedha kwani hesabu zinaonesha kuwa asilimia 70 ya matumizi ya TRL yanaenda kwenye mafuta kila mwezi.
Aliahidi kuwa watafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kusaka mitaji ya maendeleo kwa kampuni hiyo ambayo kwa sasa inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 baada ya kuondolewa wawekezaji wa Rites kutoka India.

Subscribe to:
Posts (Atom)