Baadhi ya wanafunzi wakifanya mtihani wa Kidato cha Nne. |
Wakati jamii ikitafuta suluhisho la kushuka kwa elimu nchini na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya mwaka jana, baadhi ya walimu wamebainika kupongezana kutokana na matokeo hayo.
Walimu hao wamekuwa wakitumiana ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu, wakionesha kushabikia hali hiyo, huku wakiitaka jamii kusubiri pia matokeo yajayo ya aina hiyo hiyo.
“Ukibishana na mpishi, jiandae kula chakula kibichi, matokeo ya darasa la saba, kidato cha pili na cha nne, yanatokana na kumsema vibaya mpishi, eti hajui kupika, ni mtu zandiki na dhaifu kwenye Taifa hili wala hahitaji maslahi bora.
“Huu ni mwanzo tu, haya tuone mwakani. Wapi maendeleo ya mtu yatapatikana pasipo mtu anayeitwa mwalimu?” Moja ya ujumbe wa simu ambao umeenezwa kwa walimu wengi nchini ulisomeka.
Kutokana na hali hiyo inayoonesha kupotoka kwa walimu hao, Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA), katika mikoa ya Rukwa na Katavi, ulilazimika kukutana juzi kujadili hali hiyo na matokeo mabaya ya kidato cha nne.
Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Katibu wa Tahosa Rukwa na Katavi, Jenus Kasunga, alisema wamelazimika kulaani vitendo vya baadhi ya walimu hao.
Alisema walimu hao wamekuwa wakitumiana ujumbe mfupi wa simu, wakipongezana kwa matokeo mabaya ya wanafunzi wa kidato cha nne na cha pili.
“Mwalimu ni mzazi na mdau mkubwa wa elimu, hapaswi kuchekelea kufanya vibaya kwa wanafunzi wake, hata kama Serikali itakuwa haimtimizii mahitaji yake muhimu,” alisema Kasunga.
Kasunga alisema Tahosa katika kikao hicho, ilibaini sababu zinazochangia kufeli kwa wanafunzi kuwa ni pamoja na maslahi duni ya walimu.
Nyingine alisema ni upungufu wa walimu, utitiri wa vitabu vya kiada, kushuka kwa nidhamu ya wanafunzi, migongano ya watunga sera na Baraza la Mitihani na muundo wa shule za kata kuchukua wanafunzi wa eneo moja kusikoleta ushindani kitaaluma.
Aliitaka Serikali kusikiliza maoni ya walimu ambao wanaishi na wanafunzi kwa muda mrefu, ili kufahamu undani wa changamoto walizonazo na kufafuta mbinu za kuzitatua ili wasiendelee kukata tamaa.
Hata hivyo, wakati walimu hao wakitaka kujinufaisha kutokana na matokeo hayo mabaya ya sekondari, tathmini inaonesha kuwa waliofeli si wanafunzi wa shule za Serikali tu, ambazo walimu wao ndio waliokuwa wakishabikia.
Katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, hata shule zinazofahamika kuwa na historia ya kufaulisha vizuri kama vile seminari, shule za watu binafsi, za mashirika ya dini na sekondari kongwe za Serikali, ambazo hazina matatizo kama sekondari za kata, nazo hazikupata mafanikio kama ilivyo kawaida yao.
Shule hizo nazo zilishuhudia idadi ya vijana waliopata daraja la kwanza, la pili na la tatu ikipungua wakati waliopata daraja la nne na waliofeli ikiongezeka.
Kwa mfano kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kumi bora, kilikuwa cha juu katika mtihani wa mwaka 2010, ambao matokeo yalitangazwa mwaka 2011, ambapo wanafunzi 10 bora wote walifaulu daraja la kwanza la alama saba kwa maana ya kupata alama A katika masomo saba yaliyotumika kuwapima.
Hali ilibadilika kuanzia mwaka 2011, kwa matokeo yaliyotangazwa 2012, ambapo kati ya wanafunzi 10 bora, wanane ndio walipata daraja la kwanza la alama saba na wawili walipata daraja la kwanza la alama nane.
Katika mtihani wa mwaka jana, ambao matokeo yake yalitangazwa mwaka huu na kushitua Taifa, kati ya wanafunzi 10 bora, watatu walipata daraja la kwanza kwa alama tisa, watatu alama 10 na wawili alama 11.
Katika matokeo hayo, hakuna mwanafunzi aliyepata alama saba, jambo lililodhihirisha kuwa kushuka kwa elimu, hakukutokea shule za kata na Serikali tu, bali hata shule zilizozoeleka kutoa wanafunzi bora za seminari na shule binafsi, zilipata anguko la elimu.

No comments:
Post a Comment