MACHANGUDOA WALIPWA MAGUNIA YA MPUNGA BAADA YA NGONO...

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Ally Rufunga.
Wazee wenye familia katika Kata ya Bulige wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, wamedaiwa kufanya biashara ya kubadilisha magunia ya mpunga kwa ngono kutoka kwa wanawake wanaouza miili wakati wa msimu wa mavuno.
Kutokana na kushamiri kwa biashara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Ally Rufunga amewaonya wazee hao kuwa ataanzisha msako wa kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.
Akizungumza na viongozi wa kata hiyo iliyokithiri kwa biashara hiyo, Dk Rufunga alisema kuwa wakulima wenye tabia kama hiyo ni bora waiache, kwa kuwa watakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya makosa ya jinai mahakamani.
Alisema kuwa wengi wanaofanya biashara hiyo katika kata hiyo ni wazee wenye familia zao, hali ambayo alisema ni laana kubwa kwa wakazi wa kata hiyo.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyekuwa katika ziara ya siku nne wilayani hapa kuhamasisha kilimo, alisema kuwa wazee hao wamekuwa wakiwatuma watoto kubeba magunia na kuyapeleka walipo wanawake hao mchana huku wao wakienda usiku.
“Ni laana kubwa kwa mzee kumuonesha sehemu za siri binti yake tena mwenye umri mdogo, kwani hamuwezi kuwafuata wazee wenzenu?”Alihoji Mkuu huyo wa Mkoa.
Dk Rufunga aliitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya,  kuhakikisha watu wanaofanya biashara hiyo wanakamatwa mara moja, kwani wanasababisha chakula katika familia kupungua kutokana na vitendo vya ngono.
Alisema wasichana hao hutoka katika Mji wa Kahama wakati na mavuno hujipatia magunia zaidi ya 100 kwa kutumia biashara hiyo haramu.
Hata hivyo,  alisema udhibiti wa biashara hiyo  inayoongeza maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwi Kahama, utasaidia wazee hao.
“Biashara hiyo pia ina masharti yake ambayo kwa kuvaa mpira  kuna idadi ya magunia yake ya mpunga na kutovaa pia kuna idadi ya magunia yake, hii ni balaa kubwa katika kata hii,” alionya
Rufunga.

No comments: