MJAMZITO AFANYIWA KITU MBAYA NA WAPORAJI...

Mama mjamzito alifungwa kamba zilizokazwa vilivyo kwenye kiti nyumbani kwake huku akitishiwa kwa panga na ubao wa kuchezea soka la Kimarekani mbele ya mwanae wa kiume mwenye miaka mitatu.
Kundi hatari la wanaume lilimteka Victoria Ratheram mwenye miaka 28, na kumfunga kamba kwenye kiti katika chumba cha mtoto mtarajiwa huku wakisema wangemdhuru yeye na mbwa wake kama angekaidi walichomwambia.
Waporaji hao walifanya tukio hilo mjini Wollerton, jirani na Soko la Drayton, na  asubuhi hiyo hiyo kufanya shambulio jingine kwenye nyumba moja katika kijiji cha Shropshire.
Victoria alisema leo ameachiwa maumivu mwilini baada ya shambulio hilo lililotokea Alhamisi iliyopita majira ya saa 3 asubuhi, na hadi sasa hana amani nyumbani kwake.
Amesema: “Nilikuwa nyumbani kwangu na mwanangu wakati mume wangu amekwenda kazini.
“Nilikuwa najiandaa kutoka ndipo wanaume watatu wakaingia ndani kupitia mlango mkubwa huku wakiwa wameshikilia mapanga na kitu kilichoonekana nana kirungu cha polisi wa zamani.
“Walikuwa wanatisha na ilikuwa ikiogopesha. Nina ujauzito wa miezi nane. Nilikuwa na mwanangu wa miaka mitatu ndipo wakanifunga kwenye kiti cha jikoni katika chumba tulichokuwa tumekiandaa kwa ajili ya mtoto wangu mtarajiwa.
“Kwa bahati mwanangu hakuogopa, walimwambia kuwa wanacheza tu.”
Mama huyo aliokolewa baada ya binti wa jirani yake kufika nyumbani hapo na kumwita Victoria bila majibu. Ndipo alipoingia ndani na kumfungua kamba.
Victoria aliongeza: “Niliwasha gari na kutimka mimi na mwanangu kuelekea kwa mama kuona kama yuko salama na kwa bahati tukakuta polisi wameshafika.
Mwanamke huyo na mwanae walipelekwa hospitali baada ya kushambuliwa nyumbani kwao ambako jirani kuna kijana anayesubiri kufanyiwa upasuaji wa jipu kubwa mkononi mwake.
Waporaji hao waliiba laptop kadhaa na simu za mikononi kwenye nyumba hizo mbili, pamoja na gari aina ya Land Rover Discovery nyeusi ambalo walilitelekeza nje kidogo ya kijiji na kuchukua gari jingine.
Mwanamke huyo aliyejawa hofu na mume wake, James mwenye miaka 32 walikwenda kuchekiwa afya mtoto wao aliyeko tumboni Jumamosi iliyopita na wakapata ahueni kuambiwa wote wako salama.
Victoria amepinga ushauri wa kuwataka wahame kwenye nyumba hiyo akisema kwamba imewagharimu yeye na mumewe zaidi ya Pauni 200,000 za Uingereza kukarabati chumba cha motto atakayezaliwa.
“Sina amani nyumbani kwangu lakini siwezi kukubali waporaji hawa walifanye niikimbie nyumba yangu,” alisema.
“Sina mpango wa kuwaruhusu hawa jamaa wanifanye nikimbie nyumba yangu. Ni kwangu, sio kwao.”
Askari Upelelezi Pete Brophy, kutoka Kituo cha Polisi cha West Mercia alisema: “Bado nasaka ushahidi wa watu walioiba gari dogo la rangi ya shaba kijiji siku ya Alhamisi majira ya saa 12 alfajiri.
“Discovery nyeusi ilikutwa majira ya saa 3.30 asubuhi nje ya shamba la Wollerton jirani na kibao cha alama za barabarani kinachokataza mwendokasi zaidi ya maili 30 kwa saa.
Inaonesha watuhumiwa walikuwa na gari jingine likiwasubiri maeneo hayo ambalo inawezekana liliegeshwa usiku huo ama lilitelekezwa mapema zaidi.”
Diwani wa Hodnet katika Halmashauri ya Shropshire, Karen Calder ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho amesema tukio hilo ni la kushitusha mno.
“Hapo kabla hatujawahi kusikia matukio kama haya katika eneo hili. Ni kijiji kizuri na chenye amani. Sikumbuki kitu kama hiki kuwahi kutokea katika kijiji hiki.”

No comments: