Jamaa mmoja kaingia baa akiwa tayari kapendeza ile mbaya kwa lugha nyingine matingasi. Moja kwa moja kaelekea kaunta na bila kupoteza wakati akaagizia wiski. Mhudumu kwa upole kabisa akamfuata na kumwambia hawezi kumpa pombe zaidi kwakuwa amelewa sana. Msaada pekee anaoweza kumpa ni kumuitia teksi impeleke nyumbani. Jamaa kwa dharau akamtazama mhudumu na kisha kutoka nje. Lakini baada ya dakika tano jamaa akarudi tena na kukaa kwenye kiti kingine na kuagiza wiski. Mhudumu yule yule akamfuata na kumweleza tena kuwa hawezi kumpa pombe na msaada pekee ni kumuitia teksi tu. Jamaa akacheka kwa dharau na kutoka nje. Jamaa akarudi tena baada ya dakika kumi lakini sasa kupitia mlango wa nyuma ya baa na kukaa kiti cha pembeni kisha akaagiza wiski. Kwa bahati mbaya mhudumu yule yule akamfuata na kumkumbusha kwamba alishamkatalia mara mbili kumpa pombe ila msaada pekee kwa sasa ni kumuitia teksi ama polisi wamsaidie. Hapo ndipo yule mlevi akaruka na kusema kwa sautin ya juu, “Ebo! Kwani wewe unafanya kazi kwenye baa ngapi usiku mmoja?” Duh, ulevi kweli noma…
No comments:
Post a Comment