JE, WAJUA?

Mbunge wa Jimbo la Isimani, Mhe. William Lukuvi
Jina Isimani, Jimbo linaoongozwa na Mbunge wa CCM na Waziri Mhe. William Lukuvi limetokana na neno la Kiingereza! Imedaiwa na wenyeji kwamba enzi hizo za mwishoni za ukoloni palitokea kisa kimoja katika eneo hilo kati ya Mzungu na Mnyalu mwenyeji wa hapo. Inasemekana Mzungu huyo wakati wa ukoloni alikuwa akimiliki sehemu kubwa ya eneo hilo akitumia kama mashamba. Baada ya Uhuru mashamba yoye yakataifishwa na kugawiwa kwa wazawa. Miaka kadhaa kupita Mzungu akarejea na kukuta eneo lake linakaliwa na Wanyalu ndipo akaanzisha bonge la timbwili lililozaa jina hilo. Wakati wa mzozo Mzungu alikuwa akisisitiza kwa Kiingereza, "This Land is Mine!" (Akimaanisha eneo lile ni la kwake) huku mwanakijiji akidai la kwake. Baada ya kuamuliwa shauri hilo ndipo Kiongozi wa eneo hilo wakati huo akawa akilitambua kwa jina alilokuwa akitaja Mzungu, "Isimani". (Akimaanisha, Is Mine).

No comments: