Patricia Lefranc akibusiwa na binti yake Laetitia mara baada ya kutoka mahakamani ambako Richard Remes alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Alikuwa mwanamke anayevutia akiwa na miaka zaidi ya 40, lakini sasa Patricia Lefranc anajitambulisha kama 'dudu la kutisha' baada ya shambulio la kumwagiwa tindikali.
Mama huyo wa watoto watatu, Laetitia mwenye miaka 28, Marie, 18, na Joey, 13, alimwagiwa tindikali mara kadhaa na mpenzi waliyetengana naye Richard Remes mwaka 2009, ameongea hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu shambulio hilo la kutisha ambalo limemwachia ulemavu wa kudumu na hofu kubwa maishani mwake.
Katika tukio hilo, pua yake na kope ziliyeyushwa na tindikali na pia alipoteza kidole, upofu kwenye jicho lake la kushoto na ukiziwi kwenye sikio lake moja. Hakika alikaribia kabisa mauti, ambapo athari ya tindikali hiyo ilikaribia kufika kwenye moyo na mapafu lakini katika hali ya kushangaza vimelea kwenye matiti yake vikafifiisha nguvu hiyo ya tindikali.
Mama huyo ambaye amefanyiwa upasuaji mara 86, akiwa na miaka 48 sasa amekuwa akipata maumivu ya mara kwa mara lakini anasema hamu ya kuja kuwaona wanawe wana furaha na kufunga ndoa ndio siri kubwa inayomfanya aendelee kuishi.
Katika mahojiano na Jarida la Closer mara baada ya mpenzi wake huyo wa zamani kuhukumiwa kifungo Machi 22, Patricia amesema: "Amenifanya nionekane dudu la kutisha. Siku nyingine huwa nalia tu.
"Watu wananikwepa kutokana na muonekano wangu. Ni kifungo cha maisha kwangu, kwanini na yeye hakupewa kifungo kama hicho."
Patricia, ambaye hapo kabla alifanya kazi ya utunzaji nyumba, alikutana na Remes mwenye miaka 57, kwa mara ya kwanza mjini Brussels Desemba 2008.
Remes amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kujaribu kuua. Katika utetezi wake, aliendelea kusisitiza kwamba hakujua kama tindikali aliyommwagia kama ingeweza kuleta madhara makubwa hivyo.

No comments:
Post a Comment