CHEKA TARATIBU...

Jamaa wakati akirudi nyumbani akavamiwa na vibaka watatu maeneo ya Kinondoni Mkwajuni. Wale vibaka wakamwibia kila kitu na hakubahatika kuwaona. Moja kwa moja akaenda kuripoti kituo cha polisi kilichokuwa jirani. Haraka polisi wakatoka na kwenda eneo la tukio ambapo wakafanikiwa kuwakamata vijana kumi pale mtaani na kwenda nao kituoni. Kufika pale polisi wakamtaka jamaa awatambue waliomwibia. Jamaa akajibu, "Afande, kwa sura siwajui ila sauti naweza kuzikumbuka." Ikaamriwa wale vijana watamke chochote watakachooneshwa na polisi. Polisi akashika sigara na kuwataka mmoja mmoja asome. Baada ya vijana saba kupita bila tatizo ndipo ikafika kwa watatu wa mwisho. Wa8 akasoma, "Chigala." Akakamatwa. Wa9 kuona mwenzake kakamatwa akaona abadili, "Chipoti." Naye akakamatwa. Wa mwisho akaona hana ujanja, "Mi Chichomi." Aaah, naye ndani...

No comments: