Polisi mkoani Kagera, wanamshikilia mkazi wa wilaya ya
Misenyi mwenye umri wa miaka 19 kwa tuhuma za kumbaka dada yake mwenye umri wa miaka 15 (majina yanahifadhiwa)
na kumpa ujauzito.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi alisema binti huyo alitakiwa kujiunga na masomo ya sekondari katika Shule ya Sekondari Kagera ya wilayani Misenyi.

Alisema
wazazi wa watoto hao walimuona binti yao akiwa na mabadiliko ambayo
yaliwashitua na kuchukua uamuzi wa kumpeleka katika Kituo cha Afya kupima
ujazuzito.
“Baada
ya kufanyiwa vipimo iligundulika kuwa ana ujauzito wa miezi minne, ndipo wakaja
kwetu kutoa taarifa na kwa sasa tumemkamata mtuhumiwa na muda wowote
atafikishwa mahakamani.
“Mtoto
huyo amekiri mwenyewe baada ya kufanya naye mahojiano kuwa ni kaka yake
aliyempatia ujauzito na kwamba alikuwa anambaka siku za nyuma,” alisema Kamanda
Olomi.
No comments:
Post a Comment