Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Agnes Kijazi amesema mvua iliyonyesha
Shinyanga na kusababisha maafa kwa jina la kitaalamu inajulikana kama ‘Tonado’,
ni mara ya kwanza kutokea hapa nchini.
Kijazi alisema katika
ofisi za mamlaka hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Wabunge ya Miundombinu,
jijini Dar es Salaam.
Alisema utabiri
waliokuwa wameutoa wa saa 24 ulionesha kutakuwa na mawingu mazito katika eneo
hilo, lakini hawakutarajia tonado kunyesha kwa kuwa sio mfumo wa
kawaida kwa
hapa nchini.
Kijazi alisema
kutokana na mabadiliko ya tabianchi kumekuwa kukiongezeka matukio ya hali mbaya
ya hewa hata ambayo awali yalikuwa hayatokei.
Alisema tonado,
kitaalamu ni mawingu mazito yenye unyevunyevu yanapozidi uzito yanaanguka
mabarafu, hivyo kutokana na mabadiliko hayo upepo mkali unaozunguka sio hali ya
kawaida katika maeneo ya tropiki.
“Inabidi
tahadhari ichukuliwe tunapoona mawingu mazito kuepusha maafa,” alisema.
No comments:
Post a Comment