DUME LINALOFANANA NA WHITNEY HOUSTON LAPAGAWISHA ULAYA...


Whitney Houston ni mlimbwende wa Kijerumani mwenye urefu wa futi 5'9"…angalau, kama unamwamini Piers Morgan.
Morgan alikuwa akizungumza na rapa LL Cool J kuhusu maisha ya Whitney Julai 6 katika mfululizo wa shoo zake kwenye televisheni ya CNN na kurushwa baadhi ya picha za mwimbaji kupamba mahojiano.
Tatizo ni kwamba, mwanamke katika picha hizo si Whitney …na wala si mwanamke, bali ni malkia nyota wa kulazimisha anayefahamika kwa jina la Ikenna Beney Amaechi.
Katika maongezi na Ikenna, jamaa mcheshi kutoka mjini Berlin alisema, "Nilikuwa nimekaa tu nyumbani na kwa mara ya kwanza sikuelewa, lakini mara ikanilipua kama bomu! Hakuwa Whitney …Nilikuwa mimi!"
Ikenna alisema amekuwa 'akicheza' kama Whitney kwa miaka 21 sasa (kama inavyoonekana kwenye video hapo juu) na picha hizo zilizotumika CNN zimetoka kwenye Onesho la Tuzo za Reel mwaka 2008 mjini Las Vegas, onesho lililokuwa maalumu kwa nyota wanaoigiza watu wengine.
Ikenna aliongeza, "Najisikia nimeheshimiwa mno kwamba nimefananishwa na Whitney Houston wa ukweli kwenye CNN."

2 comments:

Anonymous said...

generic xanax cheap xanax bars for sale - buy alprazolam .5 mg

Anonymous said...

buy viagra online order viagra by phone - where to buy viagra in stores