Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP mstaafu Said Mwema, amepewa Shahada ya Uzamivu (PHD) ya heshima iliyotolewa
na Chuo Kikuu cha Omega Global cha Afrika ya Kusini.
Mwema amepewa heshima hiyo, baada ya chuo
hicho kutambua juhudi ya kazi nzuri na uadilifu aliouonesha katika kipindi
chake cha utumishi kwa Taifa.
Akizungumza katika dhifa hiyo Dar es
Salaam jana, Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, aliyehudhuria alisema
kiongozi bora ni yule anayekubalika kwa wenzake pamoja na jamii inayomzunguka.
“Kiongozi mzuri ni yule anayekubalika na
wenzake pamoja na jamii yote inayomzunguka. Leo hii tupo hapa kwa sababu ya
kazi nzuri aliyoifanya IGP mstaafu Said
Mwema, kazi yake nzuri Mungu ameiona, sisi tumeiona na hata wenzetu wa chuo
hiki cha Omega pia wameiona na kutambua,” alisema.
Alisema uadilifu wa Mwema umewezesha
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi, kupunguza vitendo vya kihalifu
kwa kiasi kikubwa.
Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Omega Global
University, Professa Vusumuzi Sibiya, alisema huu ni wakati wa kutambua kazi
nzuri ya kiongozi sio kusubiri hadi akifa.
“Tunatambua kazi yake ya uadilifu na
jinsi alivyolitumikia si tuTaifa lenu bali hata sisi kwetu Afrika ya Kusini
tunajivunia kazi yake maana taifa letu tunaiona Tanzania kama mzazi,” alisema
Sibiya.
No comments:
Post a Comment