Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini, Richard Ndassa amewaambia wakazi wa kata ya Ibihwa iliyopo Bahi mkoani Dodoma kuwa
gharama za kuunganishiwa huduma
ya umeme zimeshuka hadi Sh
177,000.
Aidha amewataka kama ikatokea wakatozwa
zaidi ya kiwango hicho, na watumishi wasio waaminifu basi wana haki ya
kuwafikisha mbele ya vyombo vya kisheria.
Ndassa alisema hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati
na Madini ilipotembelea wilaya ya Bahi kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme pamoja na kuzungumza
na wananchi.
“ Iwapo atatokea mtumishi na kuwatoza
gharama zaidi ya ile inayohitajika kulipwa kisheria, basi mna haki
ya kumfikisha Polisi ili
afunguliwe mashtaka,” alisema Ndassa.
Aidha aliendelea kusema kuwa wakati
umefika kwa Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya kukamilika kwa
miradi ya umeme, kwani umeme ndio kitovu cha ukuaji wa uchumi katika nchi yoyote.
“ Kuna
vijiji ambayo vimeshaanza
kunufaika na huduma ya umeme, nawasihi muanzishe viwanda vidogo vidogo vya kukoboa nafaka, kukamua mafuta ya alizeti ili kujiongezea kipato”,
alisema Ndassa.
Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya
wakazi wa kata hiyo, Mtendaji wa Kata, Jenipha
William alisema kuwa katika
utekelezaji wa miradi ya umeme ya REA
Awamu ya Pili pamekuwepo na
changamoto ya vijiji vingine kurukwa hali inayopelekea wananchi
wachache kupata umeme.
No comments:
Post a Comment