Watu watatu
wanaume wasiofahamika, wamekutwa wamekufa na kutelekezwa maeneo ya
Mjohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, huku miili yao ikionesha majeraha
maeneo tofauti pamoja na kuvuja damu nyingi puani.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela
(pichani) alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema ametuma maofisa wake eneo
la tukio na taarifa rasmi ataitoa itakapokamilika.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu hao wanakadiriwa
kuwa na umri wa kati ya miaka 28 na 32 wanadhaniwa ni wachimbaji wa madini ya
Tanzanite wa Mirerani mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa maeneo
ilipokutwa miili hiyo ambao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina
yao miili hiyo ilikutwa eneo jirani na
alipouawa bilionea wa madini ya Tanzanite mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya
aliyeuawa kupigwa risasi kifuani.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema askari kutoka
kituo cha Bomang'ombe walifika eneo la tukio majira ya saa 3:00 za asubuhi na
kufanya uchunguzi katika eneo la tukio na kisha wakaondoka na miili ya vijana
hao.
No comments:
Post a Comment