Habari
zilizotufikia zinasema kwamba watu wapatao zaidi ya 60 wanahofiwa kufariki
dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika
eneo la Changarawe, Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa muda mfupi uliopita.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu cha habari, basi hilo mali ya kampuni ya Majinja
lililokuwa likitokea mkoani Mbeya lilibamizwa na lori lililokuwa likitokea Dar
es Salaam na katika harakati za dereva wa lori hilo kukwepa shimo barabarani,
ndipo trela lake lilipoligonga basi hilo na kisha kupinduka na kulifunika
kabisa.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zinasema kwamba kwa zaidi ya saa nzima hakuna sauti yoyote
ya abiria iliyoweza kusikika na hivyo kuzua hofu kwamba huenda abiria wote
wamepoteza maisha.
Wakati
zoezi ya kuinua trela hilo zikiendelea, baadhi ya miili imeharibika vibaya huku
baadhi yao ikiwa imepasuka vichwa kiasi kutisha kutazama.
Hadi
chanzo chetu kinaondoka eneo la tukio, juhudi za kuondoa trela hilo zilikuwa
zikiendelea kujaribu kunusuru endapo kuna majeruhi wowote ndani ya basi hilo.
Trafiki
aliyekuwepo eneo la tukio ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema matumaini
ya kukuta abiria walio hai ni madogo mno hasa kwa kuzingatia jinsi basi hilo
lilivyopondeka vibaya sana.
Taarifa
zaidi endelea kuperuzi ziro99blog.
No comments:
Post a Comment