Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kuendelea kushuka
kwa bei ya mafuta bei ambazo zinaanza kutumika Jumatano hii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka
hiyo, Ewura imesema katika bei hizo mpya, sasa mafuta ya petroli imeshuka kwa
Sh 116 kwa lita moja, dizeli Sh 145 na
mafuta ya taa Sh 134 kwa lita moja.
Katika taarifa hiyo imesema kwamba bei za sasa
ni Sh 1,652 kwa lita moja ya petroli, Sh 1,563 kwa lita moja ya dizeli na Sh
1,523 kwa lita moja ya mafuta ya taa bei ambazo zinaanza rasmi leo.
Kwa mujibu wa EWURA, punguzo hilo la bei
linaonesha kwamba hakuna mkoa ambao utauza nishati hiyo kwa Sh 2,000 na hivyo
kutoa unafuu mkubwa katika mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na unafuu wa
usafirishaji wa bidhaa.
Wananchi watakaonunua kwa bei ya juu nishati
hiyo ni wa Uvinza mkoani Kigoma ambao watanunua kwa Sh 1,895 kwa lita moja ya
petroli, Sh 1,806 kwa dizeli na Sh 1,766 kwa mafuta ya taa.
Ewura imesema hata hivyo bei hizo hazijashuka
sana kutokana na kuendelea kushuka thamani ya shilingi ambayo kuanzia Desemba
mwaka jana imeshuka kwa asilimia 8.
No comments:
Post a Comment