Kampuni ya bia ya Serengeti imewatunuku vyeti
wahudumu wa baa 700, walioshiriki mafunzo ya kimataifa ya Diageo Master Academy
(MBA), yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapa wahudumu hao ujuzi wa kufanya kazi
kwa weledi.
Akitunuku vyeti hivyo kwa wahitimu hao jijini Dar
es Salaam jana, Mkuu wa Masoko wa Vinywaji Vikali, Stanley Samtu, alisema mafunzo hayo yatawawezesha wahitimu
hao kushiriki shindano la kitaifa na la kimataifa la Diaego Master Bar Academy.
“Tumewatunuku vyeti vya kimataifa vya MBA wahudumu
wa baa kutoka mikoa kumi nchini baada ya kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja,”
alisema.
Alisema mafunzo hayo yamewapatia ujuzi wa kuhudumia
wateja, kuchanganya bia, kujua wajibu wao na aina ya vinywaji vikiwemo vya
Barleys, Gordons, Grants, John Walker,
Guiness, Smirnoff na jamii zote za bia za Serengeti.
Alisema mafunzo hayo ya kimataifa kwa Afrika, yalianza kutolewa Februari 7, mwaka huu na kukamilika Machi 7
na yaliyolewa na wakufunzi kutoka Afrika Kusini.
“Mafunzo hayo yalifanyika katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha,
Morogoro na Mbeya,” alisema.
Kuanzia sasa wahitimu wote wameandikishwa katika
shindano la kimataifa la Diageo Master Bar Academy na watahitajika kujibu
maswali kwa njia ya simu ya mkononi.
Alisema shindano la kuwapata washindi kumi wa juu (top ten), litafanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
Aprili 2015 na kila mmoja atapatiwa
zawadi ya dola 1,000 (Sh milioni 1.7) za Marekani.
Alifafanua kuwa mshindi wa jumla, atapata tiketi ya
kushiriki shindano la kimataifa la ‘Diageo World Class’ litakalofanyika mwaka
huu Johannesburg, Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment