Zabuni ya ujenzi wa
barabara za juu jijini Dar es Salaam inatarajiwa kutangazwa mwezi ujao.
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alitoa taarifa hiyo wakati
wa hafla ambayo serikali ya Japan ilitia saini mkataba wa kusaidia serikali
fedha za ununuzi wa magari ya kubebea wagonjwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili na mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti wilayani Chato.
Ingawa Magufuli hakuzungumzia undani wa mchakato huo, alisema taratibu zinaendela vizuri kwa ajili
ya ujenzi huo.
“Tunatarajia kutangaza tenda ya ujenzi wa barabara za juu
mapema mwezi wa tatu mwaka huu,” alisema
Magufuli.
Ujenzi wa barabara za juu jijini Dar es Salaam, ulifikwa na
serikali ikiwa ni hatua mojawapo ya kupunguza tatizo la msongamano wa magari,
unaosababisha foleni kubwa na adha kwa wananchi.
Barabara za juu zinatarajiwa kujengwa katika eneo la Tazara
na eneo la Ubungo.
No comments:
Post a Comment