Upelelezi wa kesi ya kutotii
amri halali ya polisi na kufanya mkusanyiko usio halali inayowakabili wafuasi
30 wa Chama cha Wananchi (CUF) haujakamilika.
Wakili wa Serikali Joseph
Maugo alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Emilius Mchauru wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Hakimu Mchauru aliahirisha
kesi hiyo hadi Februari 26, mwaka huu itakapotajwa kwa ajili ya kuangalia kama
upelelezi umekamilika.
Washitakiwa wanadaiwa Januari 27, mwaka huu , wilaya ya Temeke,
washitakiwa wote walikula njama ya kufanya kitendo cha uhalifu.
Katika mashitaka
yanayowakabili mshitakiwa wa kwanza hadi wa 28, wanadaiwa siku hiyo katika
ofisi za CUF, karibu na Hospitali ya Temeke, bila halali walifanya mkusanyiko
kwa nia ya kufanya maandamano yasiyo halali kwenda viwanja vya Mbagala Zakhem.
Aidha, washitakiwa wanadaiwa
siku hiyo katika eneo la Mtoni Mtongani, Temeke, waligoma bila kujali tangazo
halali lililotolewa na Polisi la kuzuia
kukusanyika na kuandamana isivyo halali.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka,
washitakiwa hao ni Shabani Ngurangwa, Shabani Tano au Kasakwa, Shabani Polomo,
Juma Mattar, Mohammed Kirungi , Athumani Ngumwai, Shaweji Mohamed, Abdul Juma
,Hassan Saidi , Hemed Joho , Mohamed Mbarouk
na Issa Hassani.
Wengine ni Allan Ally, Kaisi
Kaisi , Abdina Abdina, Allawi Msenga, Mohamed Mtutuma, Salehe Ally, Abdi
Hatibu, Bakari Malija, Abdallah Ally , Said Mohamed, Salimu Mwafisi, Saleh
Rashid, Abdallah Said, Rehema Kawambwa, Salma Ndewa, Athumani Said, Dickson
Leason na Nurdin Msati.
No comments:
Post a Comment