Rais Jakaya
Kikwete ametuma salamu za pongezi kwa uteuzi uliofanywa na Baba
Mtakatifu, Papa Francis wa Padre Liberatus Sangu wa Jimbo la Sumbawanga kuwa
askofu wa jimbo Katoliki la Shinyanga.
Alituma salaam hizo kwa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania (TEC) na Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Mhashamu Baba
Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na kuomba salaam hizo afikishiwe Padre Sangu.
Askofu Mteule Liberatus Sangu aliyekuwa Ofisa
katika Idara ya Uenezaji wa Injili kwa Mataifa katika Makao Makuu ya Kanisa
Katoliki, Vatican, anatarajiwa kupewa Daraja la Uaskofu na kusimikwa rasmi kuwa
Askofu wa Jimbo la Shinyanga Aprili 12 mwaka huu.
Alisema, “Hii inadhihirisha wazi kutambuliwa
kwa mchango mkubwa wa Padre Sangu katika kuwatumikia kikamilifu Kondoo wa Bwana
hususan kupitia Idara nyeti ya Uenezaji wa Injili kwa Mataifa aliyokuwa
akiitumikia akiwa Vatican ambako ndiyo Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani.”
No comments:
Post a Comment