Mkazi
wa kijiji cha Ibosa, kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini, Amelia Richard (50)
anatuhumiwa kumuua mwanamke mwenzake kwa kummwagia mafuta ya taa na kumchoma
moto baada ya kumfumania na mumewe.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry
Mwaibambe alitaja tukio hilo ni la Februari 15, mwaka huu saa 3 usiku katika
kijiji cha Ibosa kata ya Nyakata Bukoba vijijini.
Alimtaja
aliyeuawa ni Pelagia Martin (46)
aliyeunguzwa mwili mzima. Kamanda alisema mwanamke huyo alicheleweshwa
kufikishwa Hospitali ya Mkoa hadi kesho yake; Februari 16 baada ya wanafamilia
kuomba wayamalize bila kwenda Polisi.
Makubaliano
ya wanafamilia hao yalitokana na kile kilichoonekana kwamba Amelia alimfumania Pelagia akiwa na
mumewe, Richard Bulebo (57) ndani ya
nyumba yao.
Kwa
mujibu wa Kamanda, Februari 16 walipoona hali ya majeruhi inazidi kuwa mbaya,
ndipo walifika katika Kituo cha Polisi mjini Kati wakiomba msaada.
Polisi
walimpeleka majeruhi huyo Hospitali ya Mkoa lakini alifariki kabla ya kupatiwa
matibabu. Polisi inamshikilia Amelia na Bulebo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji
hayo.
No comments:
Post a Comment