AJALI ZILIZOHUSISHA KEMIKALI ZAUA WATU 14

Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), umesema mwaka jana kumetokea matukio ya ajali za kemikali 11 zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 14 na uharibifu wa tani zaidi ya 250 za kemikali.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele jana jijini Dar es salaam kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa madereva wanaoendesha magari yanayosafirisha kemikali ndani na nje ya nchi.
Profesa Manyele alisema lengo kuu la sheria hiyo ni kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika katika hali iliyo salama bila kuleta athari kwa watu na mazingira ambapo kabla ya kutungwa na kuanza utekelezaji wa sheria hiyo kemikali zilikuwa zinaingia nchini kiholela na kutumika bila kuwa na ufuatiliaji.

No comments: