Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa
wanyama pori mkoani hapa,
wamefanikiwa kuwakamata watu wawili kwa tuhuma
za kupatikana na meno ya tembo na ngozi ya chui.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Mkoani hapa,
tukio la kwanza ni la Januari 24 saa 6 mchana katika maeneo ya mbuga ya
wanyama ya Selous.
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Mwagi Doto,
ambapo alisema kuwa askari hao baada ya kumtilia shaka, walimfanyia
upekuzi na kumkuta na jino hilo la tembo, lenye thamani ya sh.mil 24.3.
Tukio la pili ni la Januari 25 saa 9 alasiri
katika kitongoji cha Pondamali kijiji cha Bwawani tarafa ya
Mang’ula wilayani Kilombero mkoani hapa, ambapo askari wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA), walimkamata Ally Abdalah (22), mkazi wa Bwawani
akiwa na ngozi ya chui.
Alisema watuhumiwa wote, wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment