Mshauri
wa masuala ya ulinzi katika Benki Kuu (BoT), Shaban Ndosi (39) amepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya
kujaribu kumuua ofisa wa Polisi.
Ndosi alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema.
Wakili wa Serikali, Janeth Kitali alidai kuwa Oktoba 21, 2014 katika eneo daraja la Salender karibu na mataa ya kuongoza magari, alijaribu kumuua askari Polisi, Koplo Salehe.
No comments:
Post a Comment