Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeiagiza Bodi ya Korosho Tanzania,
kuandika barua inayoeleza hatua walizochukua katika kurudisha nyumba iliyouzwa
kwa Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka (CCM).
Akitoa
agizo hilo, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kamati yake haijaridhishwa
na namna nyumba hiyo ilivyouzwa.
Zitto
aliitaka Bodi hiyo kuhakikisha inapeleka barua yenye taarifa na lazima iifikie
kamati leo saa 6, ikieleza mchakato, taratibu na hatua waliyofikia katika
kushughulikia suala hilo.
Taarifa
ya CAG inaonesha nyumba ya Bodi ya Korosho iliyopo katikati ya jiji la Dar es
Salaam, iliuzwa kwa Koka kwa thamani ya Sh milioni 300 na iliyokuwa Bodi ya
Kilimo, ambayo kwa sasa haipo.
Pia,
Zitto aliiagiza Bodi hiyo kuhakikisha wanatafuta hati za nyumba na viwanja
vyake na kila hatua wanayofuatilia watoe taarifa kwa kamati.
Aidha,
PAC imeitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha mapato ya nje yanayopatikana kutokana
na kuuza korosho, wayatumie kuongeza thamani ya zao hilo ikiwamo kufufua
viwanda.
No comments:
Post a Comment