BARUA YAMNASA MWALIMU WA KIKE MWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAFUNZI

Mwalimu mmoja huko Pennsylvania ameshitakiwa kwa kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanafunzi wa kiume kwa takribani mwaka mmoja, akidaiwa kupiga simu zinazodaiwa kufikia 509 na kijana mwenye umri wa miaka 16 na ujumbe wa maandishi 319.

Sarah O'Neill, mwenye miaka 35, mwalimu wa zamani wa somo la Kiingereza katika shule binafsi ya bweni ya wavulana ya Church Farm School mjini Exton, allinaswa na mfanyakazi mwenzake baada ya kutelekeza katika printa ya ofisini barua ya kimapenzi aliyomwandikia kijana huyo.
"Fikra kwamba ningeweza kuzama mno kwenye penzi vibaya hivi zilianza hata kabla ya mimi na wewe kuanza rasmi," Sarah anadaiwa kumwandikia kijana huyo, kwa mujibu wa chanzo cha habari.
"Ilikuwa ni wakati wa mapumziko marefu ya majira ya baridi kabla ya midomo yangu haijaumana na yako na nilistaajabu kama uliathirika kama ilivyokuwa kwangu."
Polisi wamesema wawili hao wamekiri kuwa uhusiano wao huo wa  kimapenzi na kwamba ulikuwa umedumu kwa miezi 10.
Mahusiano hayo ya kimapenzi yaliendelea hata baada ya Sarah kutakiwa kuacha kazi kufuatia kugundulika kwa barua hiyo.
Kijana huyo, ambaye sasa ana miaka 17, aliieleza polisi alianza kuonana na Sarah Januari, 2014.
Alisema kwanza walibusiana Motel 6 iliyoko mjini King of Prussia mnamo Februari, na kisha tena mnamo Machi wakati wa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa Sarah.
Kijana huyo anadai wapenzi hao walijiingiza katika ngono mara kadhaa kwenye hoteli hiyo, ndani ya gari la Sarah na kwenye maegesho ya magari.
Mlinzi aliieleza polisi kwamba aliwanasa mara tatu Sarah na kijana huyo wakiwa wamejifungia ndani ya chumba cha darasa huku wakiwa wamezima taa.
Wakati fulani soksi zake zilionekana zimechanika na wakati mwingine Sarah alisema alikuwa akimsaidia kijana huyo kupata kredit za ziada katika masomo yake, alisema mlinzi huyo.
Zaidi ya mamia ya simu hizo na ujumbe wa maandishi, polisi walisema wawili hao waliongea kwenye simu kwa jumla ya masaa 106 pamoja na kuwasiliana kwa njia ya baruapepe.
Mojawapo ya baruapepe hizo ni ile ambapo kijana huyo alimuuliza Sarah nguo alizopanga kuvaa.
Sarah akajibu; "Nitavalia nguo za kimahaba kwa ajili yako kama ukitaka nifanye hivyo. Kama chupi ya kubana sana au kutovaa kabisa. Lakini nimepitwa mno na wakati kwa mavazi kama hayo."
Kisha kijana huyo akatoweka eneo la shule hiyo mnamo Novemba, na ikaja kubainika alikuwa na Sarah.
Aliwaeleza polisi walikuwa katika Extended Stay America mjini Exton wakifanya mapenzi.
Kijana huyo alirejea shuleni hapo baada ya kupigiwa simu kadhaa kutoka kwa uongozi wa shule hiyo ya bweni ambayo ada yake ni dola za Marekani 35,000 kwa mwaka.
Uongozi wa Church Farm School ulikieleza chanzo cha habari kwamba Sarah aliajiriwa shuleni hapo kuanzia Septemba 2007 hadi Juni 2-14.
Alikamatwa kufuatia uchunguzi.
Sarah anashitakiwa kwa makosa manne ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa chini ya umri wa miaka 18.
Kwa sasa Sarah yuko nje kwa dhamana na kesi yake imepangwa kusikilizwa Februari 2, mwaka huu.

No comments: