Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, leo anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa 22 wa wataalamu wa wabunifu majengo na
wakadiriaji majenzi utakaofanyika kwa siku moja jijini Dar es Salaam.
Mbali na Mwinyi, alisema pia atakuwemo
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za
sekondari.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Msajili wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Jehad
Abdallah Jehad, alisema mkutano huo utakaohudhuriwa na washiriki wapatao 400,
mada kuu itakuwa sheria ya manunuzi namba 7 ya mwaka 2011 na athari zake katika
mazingira ya ujenzi.
Mwenyekiti wa AQRB, Ambwene Mwakyusa
alisema mategemeo yao ya baadaye katika mashindano hayo ni kuendelea
kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi hususani taaluma za ubunifu na
ukadiriaji majenzi ili kukidhi pengo la upungufu uliopo ambapo hadi kufika
mwaka 2025 wanataka kuwa na wataalamu wa aina hiyo walau 6,500 kutoka 1,000
waliopo sasa.
No comments:
Post a Comment