TCRA YAONYA KUHUSU MITANDAO YA BURE


Mamlaka ya Mawasilino Tanzania(TCRA), imehadharisha juu ya matumizi ya mitandao ya bure ‘WiFi’ katika maeneo ya halaiki kufanya miamala ya fedha.
Aidha Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Mawasiliano wa TCRA, Isaac Mruma alisema kitengo chake kinapokea malalamiko mengi kuhusu wizi wa kwenye simu.
Alishauri watu kutopenda kutumia mitandao hiyo ya bure maeneo ya halaiki kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, kwa kuwa ni miongoni mwa maeneo ambao watu wengi pia huibiwa fedha.
Alisisitiza umma kuepuka kutoa taarifa zao za fedha kwa kutumia simu. “Mfano unakuta mtu anakupigia ana kuuliza kuhusu akaunti zako za fedha za simu, umezaliwa mwaka gani au namba zako nne za mwisho kupiga ni zipi. Msikubali kutoa taarifa kama hizo kwa simu, kwa sababu wengi wameibiwa kwa kufanya hivyo,” alionya.

No comments: