Kampuni ya Reli ya Kati (TRL) imepata mkopo wa Sh bilioni 12
kutoka Benki ya Maendeleo (TIB) kwa ajili ya kuongeza mtaji wa uendeshaji.
Makabidhiano ya mkopo huo yalifanyika jana kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Peter Noni na Mwenyekiti wa Bodi wa TRL,
Severine Kaombwe.
“Sisi kama TIB lazima
tushiriki katika uwekezaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ila sasa
tumeamua kuwasaidia TRL,” alisema Noni.
Mwenyekiti wa Bodi TRL, Kaombwe alisema mtaji huo utawasaidia kufanya kazi
bila tatizo. Alisema sasa wana vichwa sita ambavyo ni vizima na vinafanya kazi
na wanategemea kupata vichwa vingine viwili.
“Reli ni muhimu sana
na ni mahali ambapo serikali inapenda kuwekeza hivyo kwa mtaji huu mambo
yataenda vizuri,” alisema Kaombwe.
No comments:
Post a Comment