Kampuni ya
Microsoft imezindua simu tatu aina ya Nokia Lumia zilizounganishwa na mfumo wa kisasa wa teknolojia ya uendeshaji
wa simu wa Windows Phone 8.1.
Simu
hizo ni Nokia Lumia 530, Nokia Lumia 630 na Nokia Lumia 930 ambazo mfumo huo
unawapa watumiaji na wataalamu wa masuala ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (Tehama) kujitengenezea bidhaa mbalimbali kupitia Window Phone
8.1.
Meneja
wa bidhaa wa Microsoft, Kingori Gitahi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam
wakati wa uzinduzi wa simu hizo.
Alisema
kupitia bidhaa hizo mtumiaji atakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kutumia huduma
za mawasiliano ya moja kwa moja kwa njia ya simu kama Skype na zile za Microsoft Office hasa
katika masuala ya biashara.
Aliongeza
kuwa simu hizo zina uwezo wa kutumia laini mbili kama wateja wengi wanavyopenda
na kwamba watumiaji wa simu za mkononi za Tigo, Airtel na Vodacom watapata muda
wa maongezi wa bure na vifurushi vya mtandao.
No comments:
Post a Comment