BREAKING NEWS!!! ZAIDI YA WATU 60 WAFARIKI AJALI YA MABASI MUSOMA

        HABARI KAMILI ZILIZOTHIBITISHWA:       

Abiria 36 wamekufa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili katika eneo la Sabasaba, wilayani Butiama katika mkoa wa Mara .

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Phillip Kalanji alithibitisha kutokea kwa ajali  mkoani Mara, akisema ilitokea saa 5 asubuhi ikihusisha magari matatu, yakiwemo mabasi yaliyogongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Nissan Terrano lililogongwa na kutumbukia mtoni.

Akizungumza na mwandishi kwa njia ya simu kutoka Butiama, alisema taarifa ya vifo 36 na majeruhi 79 zilikuwa za awali kwa kuwa walikuwa wanaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo ya mabasi kugongana katikati ya daraja.

Aliyataja mabasi yaliyogongana ni Scania lenye namba za usajili T 736 AWJ mali ya kampuni ya Mwanza Coach lililokuwa linatokea Musoma kwenda Mwanza na jingine aina ya Zoutong, lenye namba za usajili T 677 CYC mali ya kampuni ya J4 Express lililokuwa linatokea Mwanza kwenda Musoma. Gari dogo lililogongwa aina ya Nissan Terrano lina namba za usajili T 332 AKK.

“Kwa ujumla, hizi ni taarifa za awali, tunakwenda kwenye kutambua chanzo cha ajali, idadi ya abiria waliokufa katika kila gari na pia kuwatambua. Kwa ujumla ni ajali mbaya,” alisema Kamanda Kalanji.
***********************************
***********************************
Watu zaidi ya 60 wamefariki dunia baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso Musoma, mkoani Mara muda mfupi uliopita.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imesababishwa na  uzembe mkubwa wa madereva wa mabasi hayo kwa kutoheshimu sheria za barabarani.
Ajali hiyo imehusisha mabasi ya J4 lililokuwa likitokea Mwanza na basi la Mwanza Coach lililokuwa likitokea Musoma.
Akielezea chanzo cha ajali hiyo, mmoja wa mashuhuda ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema ajali hiyo ilitokea eneo ambapo kuna daraja huku kukiwa na bango kubwa linalosomeka Single Lane (yaani Njia Moja).
Alisema basi la J4 likiwa nyuma ya gari dogo aina ya Toyota LandCruiser lilijaribu kulipita gari hilo dogo bila kuchukua tahadhari yoyote ndipo ghafla likakutana na basi la Mwanza Coach lililokuwa likisubiria magari ya upande wa pili yaishe, ndipo likapoteza uelekeo na kujibamiza na kusababisha maafa hayo makubwa.
Taarifa ambazo badi hazijathibitishwa na mamlaka husika, zinasema zaidi ya maiti 60 zimenasuliwa kutoka kwenye mabaki ya mabasi hayo na kwamba haijafahamika kama kuna yeyote aliyedhurika kutoka kwenye gari hilo dogo.
"Kwakweli hali ni mbaya sana eneo la tukio, yaani miili ya watu imeharibika vibaya sana na damu imetapakaa kila kona," alisema mmoja wa mashuhuda hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo hakuweza kupatikana mara moja, ila habari za uhakika ni kwamba miili ya marehemu na majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa kwenye hospitali ya mkoa wa Mara na zahanati za jirani na eneo la tukio.
Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu wote na kuwapa nafuu majeruhi wote wa ajali hiyo.
Endelea kuperuzi ziro99blog kwa taarifa zaidi.

No comments: