Hospitali ya
upasuaji wa moyo ya Apollo iliyopo India, inatarajia kufungua tawi lake Jijini Dar es Salaam mwezi ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, daktari
mwakilishi kutokea hospitali hiyo, Hari Prasad alisema kuwa lengo la ufunguzi
wa hospitali hiyo ni kusogeza huduma za hospitali hiyo karibu zaidi na
wananchi.
Alisema Watanzania wengi wamekuwa wakienda kuzifuata
huduma za hospitali hiyo nchini India ambapo wamekuwa wakilazimika kuingia
gharama kubwa.
Alisema gharama za usafiri wa ndege, maradhi na
nyinginezo zimekuwa ni kikwazo pia kwa Watanzania wa hali ya chini kujipatia
huduma hiyo.
"Huduma zitakuwa zikitolewa hapa Dar es Salaam na
kuna eneo maalumu ambapo ujenzi utaanza na lengo ni kuwasaidia wananchi wa
kawaida kujipatia huduma za afya kwa ukaribu zaidi," alisema daktari huyo
wa Hospitali ya Apollo yenye uzoefu wa miaka 31 katika upasuaji wa moyo.
Alisema
kuwa itashughulikia magonjwa ya saratani, kisukari na magonjwa yanahusu
matatizo ya figo.
No comments:
Post a Comment