TFDA YAKAMATA 'OFISA WAKE' BANDIAMamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na jeshi la polisi imemtia mbaroni mtu aliyejifanya ni ofisa mamlaka hiyo na kutumia mwanya huo kujihusisha na vitendo vya kitapeli katika maduka mbalimbali ya vyakula na vipodozi.
Aidha, pamoja na kutumia vitisho kujinufaisha huku akijua si mtumishi wa TFDA, mtu huyo anadaiwa pia alikuwa anatoa dtakabadhi bandia za mamlaka hiyo.
Mkaguzi Mkuu wa TFDA, Kanda ya Kaskazini ,Elia Nyeura, akizungumza kwenye maeneo yalikofanyika matukio hayo amesema kuwa  mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vitambulisho bandia ambavyo amevitengeneza mwenyewe na kughushi nembo ya TFDA.
Nyeura, amesema katika ukaguzi walioufanya nyumbani kwa mtuhumiwa eneo  Sekei, jijini Arusha, walimkuta ana Vitambulisho vyenye majina tofauti ,mihuri, nembo (logo) za TFDA, ana stakabadhi bandia ambavyo vyote ni bandia ,ambavyo amekuwa akivitumia kuwatapeli wafanyabiashara hao.
Katika kitambulisho cha kwanza anaitwa Obadia Andrew  Gama, na kitambulisho kingine anaitwa Laizer Evance ,vitambulisho hivyo vyenye nembo bandia ya TFDA,huwa anavitumia kutapeli wafanya biashara.

No comments: