SERIKALI YAPIGA VITA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU


Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando amesema pamoja na utafiti wa chanjo ya Ukimwi kuwa katika hatua ya tatu, Serikali bado inajizatiti katika kuhakikisha maambukizi mapya yanapungua. 
Mmbando aliyasema hayo wakati wa kufungua mkutano wa kubadilishana uzoefu kuhusu mpango wa kupunguza Ukimwi(AIDSRelief) kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Self Rashid. 
Alisema kwa sasa, utafiti wa chanjo ya Ukimwi ambao uko katika hatua ya binadamu, unaweza kuleta matumiani mapya lakini bado Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa wakifanya kila liwezekano katika kupambana na ugonjwa huu. 
Mbando alishukuru Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Kupunguza makali ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi (VVU) na Ukimwi (PEPFAR), kwa kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya afya na matibabu nchini kote.

No comments: